Ushauri: Kodi ya VAT ikusanywe direct toka viwandani kupunguza upotevu wa mapato

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom,

Wote tunafahamu kuwa uagizaji wa mafuta Kwa Mfano, Huwa mafuta yanapopakuliwa Kutoka kwenye meli, Huwa Lita zinafahamika na Kodi ya Serikali Huwa tayari inajulikana.

Kiwanda Cha kuuza maji Cha Kilimanjaro Kwa Mfano, TRA wakiweka mfumo wa kujua Lita kiasi Gani zinazalishwa Kwa siku, mwezi Hadi mwaka, wanao uwezo Kwa kudai Kodi ya ongezeko la thamani VAT Toka kiwandani direct, kwanini wasuburi maji yaendelee kwenye vioski na deports ambazo nyingi hazina, au haxitoi EFD?

Viwanda vya kuzalisha cement, vinywaji, CHUMA ambavyo Bei zake zinafahamika, nk nk, Serikali Ina uwezo wa kukaa na wazalishaji na kukubaliana nao Ili wao ndio wawe wanalipa vat direct bila kusubiri Hadi muuzaji wa mwisho ndiye abanwe kulipa vat.

Hawa wauzaji wa mwisho, wabanwe kulipa Kodi ya mapato pekee, lakini VAT ikusanywe na kiwanda na kiwanda kiwasilishe VAT hiyo direct Kwa Serikali.

FAIDA YA SERIKALI KIKUSANYA VAT KUTOKA KWA KIWANDA DIRECT NI:

1. KUPUNGUZA UKWEPAJI KODI
Wauza maji na wafanyabiashara wauzao bidhaa za viwandani, wanaotembeza juani, hawana EFD hao ndio wauzaji wakubwa wa wauzaji wa depot's kubwa ambazo hushiriki kuhujumu mapato Kwa kutotoa risiti hivyo kupunguza uwasilishaji wa vat hivyo kupotea Kwa mapato.

2. KUPUNGUZA RUSHWA

Utaratibu huu wa makadirio mawilayani inaongeza tu gharama na kutengeneza mwanya wa RUSHWA Kwa watumishi wa TRA. Kodi ya VAT ikikusanywa direct itamsaidia kuondoa RUSHWA maana itakuwa Rahisi kuwadhibiti viwanda.

3. GHARAMA YA KUKUSANYA KODI ITAPUNGUA

Kukusanya Kodi ya VAT direct Toka Kwa kiwanda automatically kutapunguza Mzigo wa Serikali kuajiri wafanyakazi kufuatilia Kodi, au utapunguza KAZI Kwa watumishi hivyo kujikita na shughuli zingine Kwa ufanisi zaidi.

4. MAPATO YA SERIKALI YATAONGEZEKA

Kuminya mianya ya RUSHWA na upotevu wa mapato, automatically kutaipa Serikali mapato ya kutosha, hivyo kusababisha mapato ya Serikali kuongezeka.

Karibuni Kwa maoni na maboresho ya HOJA hapo juu 🙏

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
 
naonekana mwanafunzi wa PoliSci na inaonekana bado hujamaliza.unatozaje kodi bidhaa ambayo huna uhakika kitafika kwa 'mlaji'
Nimesema tra waweke mfumo mzuri wa kuwafanya viwanda ndio wawe walipaji wa VAT Kwa kuwa wao ndio wanamiliki chain ya tangu uzalishaji Hadi mtumiaji wa mwisho.

Ni vyema ungeboresha HOJA Badala ya kupinga tu bila fikra.
 
unaonekana mwanafunzi wa PoliSci na inaonekana bado hujamaliza.unatozaje kodi bidhaa ambayo huna uhakika kitafika kwa 'mlaji'
HOJA yangu ililenga viwanda ambavyo Bei ya kununua na kuuza Hadi Kwa end consumer inafahamika,

Kwa Mfano maji, Bei inajulikana mwanzo mwisho.

Cement,Bei inafahamika point A to Z.

Nondo nk nk nk.

Ningependa kuona wachangiaji wakiboresha HOJA Kwa maslah mapana ya nchi yetu nzuri TANZANIA.
 
VAT imemlenga mtumiaji wa mwisho. We sema Serikali ihakikishe bidhaa zinazozalishwa viwandani na imports zitozwe VAT na zitolewe risiti na asiuziwe mtu mzigo bila kuonyesha min stock ya mzigo uliopita ufanane na VAT anayodai. Hawa wa juu wakinunua kwa risiti hawana option zaidi ya kuuza kwa risiti maana wasipofanya hivyo watakuwa na mzigo wasiokuwa nao na kushindwa kufanya manunuzi. Shida hawa wa juu wanauza bila risiti, anayeununua hawezi kubali kuuza kwa risiti.
 
Wewe umenielewa vizuri.

Bidhaa za viwandani vitozwe VAT,

Retailer anunue Mzigo Ukiwa umeshatozwa VAT Toka kiwandani,

Tukifanya hivyo, Serikali haitahangaika kutafuta muuzaji wa huko chini akusanye vat on behalf of the Gvt.

Mawazo yetu yakiboreshwa, Serikali itakusanywa mapato na kupunguza utegemezi.
 
Unaelewa VAT ni nini?
 
Wamiliki huko juu ni kama imekuwa shida kuwadhibiti. Ukishawadhibiti hao wakauza kwa risiti wanaofuata hawana option maana walishalipa VAT lazima watataka waiamishe kwa mwingine kupitia mauzo. Wimbo wa ukiuza toa risiti utakuwa si common.
 
Ni hivi.

Kiwanda cha maji kikinunua maji kwa shilingi 200 kwa lita, na kuya purify na kuyaweka kwenye chupa kwa gharama shilingi 800 kwa lita, kitalipia VAT hiyo "value added" ya shilingi 800 kwa lita. Ndiyo value iliyokuwa added kwenye maji ya shilingi 200 (ku purify na kuweka kwenye chupa).

Maji hayo yakiuzwa kwa shilingi 1200 kwa muuzaji barabarani, ambaye na yeye anayaweka kwenye friji, kwa gharama ya shilingi 200 kwa chupa, muuza maji naye atailipia hiyo value ya kupooza maji kwa sh 200 kwa lita kwenye friji kodi, hiyo ndiyo "value" aliyo add.

Ndiyo maana inaitwa "Value Added Tax".

Sasa, unatakaje mwenye kiwanda alipie kodi Value Added ya muuzaji kuweka maji kwenye friji, ambayo ni value iliyowekwa na muuzaji, wakati mwenye kiwanda hahusiki na hiyo value added ?
 
Salaam, Shalom,

Wote tunafahamu kuwa uagizaji wa mafuta Kwa Mfano, Huwa mafuta yanapopakuliwa Kutoka kwenye meli, Huwa Lita zinafahamika na Kodi ya Serikali Huwa tayari inajulikana.

Kiwanda Cha kuuza maji Cha Kilimanjaro Kwa Mfano, TRA wakiweka mfumo wa kujua Lita kiasi Gani zinazalishwa Kwa siku, mwezi Hadi mwaka, wanao uwezo Kwa kudai Kodi ya ongezeko la thamani VAT Toka kiwandani direct, kwanini wasuburi maji yaendelee kwenye vioski na deports ambazo nyingi hazina, au haxitoi EFD?

Viwanda vya kuzalisha cement, vinywaji, CHUMA ambavyo Bei zake zinafahamika, nk nk, Serikali Ina uwezo wa kukaa na wazalishaji na kukubaliana nao Ili wao ndio wawe wanalipa vat direct bila kusubiri Hadi muuzaji wa mwisho ndiye abanwe kulipa vat.

Hawa wauzaji wa mwisho, wabanwe kulipa Kodi ya mapato pekee, lakini VAT ikusanywe na kiwanda na kiwanda kiwasilishe VAT hiyo direct Kwa Serikali.

FAIDA YA SERIKALI KIKUSANYA VAT KUTOKA KWA KIWANDA DIRECT NI:

1. KUPUNGUZA UKWEPAJI KODI
Wauza maji na wafanyabiashara wauzao bidhaa za viwandani, wanaotembeza juani, hawana EFD hao ndio wauzaji wakubwa wa wauzaji wa depot's kubwa ambazo hushiriki kuhujumu mapato Kwa kutotoa risiti hivyo kupunguza uwasilishaji wa vat hivyo kupotea Kwa mapato.

2. KUPUNGUZA RUSHWA
Utaratibu huu wa makadirio mawilayani inaongeza tu gharama na kutengeneza mwanya wa RUSHWA Kwa watumishi wa TRA. Kodi ya VAT ikikusanywa direct itamsaidia kuondoa RUSHWA maana itakuwa Rahisi kuwadhibiti viwanda.

3. GHARAMA YA KUKUSANYA KODI ITAPUNGUA
Kukusanya Kodi ya VAT direct Toka Kwa kiwanda automatically kutapunguza Mzigo wa Serikali kuajiri wafanyakazi kufuatilia Kodi, au utapunguza KAZI Kwa watumishi hivyo kujikita na shughuli zingine Kwa ufanisi zaidi.

4. MAPATO YA SERIKALI YATAONGEZEKA
Kuminya mianya ya RUSHWA na upotevu wa mapato, automatically kutaipa Serikali mapato ya kutosha, hivyo kusababisha mapato ya Serikali kuongezeka.

Karibuni Kwa maoni na maboresho ya HOJA hapo juu 🙏

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
 
Ni hivi.

Kiwanda cha maji kikinunua maji kwa shilingi 200 kwa lita, na kuya purify na kuyaweka kwenye chupa kwa gharama shilingi 800 kwa lita, kitalipia VAT hiyo "value added" ya shilingi 800 kwa lita. Ndiyo value iliyokuwa added kwenye maji ya shilingi 200 (ku purify na kuweka kwenye chupa).

Maji hayo yakiuzwa kwa shilingi 1200 kwa muuzaji barabarani, ambaye na yeye anayaweka kwenye friji, kwa gharama ya shilingi 200 kwa chupa, muuza maji naye atailipia hiyo value ya kupooza maji kwa sh 200 kwa lita kwenye friji kodi, hiyo ndiyo "value" aliyo add.

Ndiyo maana inaitwa "Value Added Tax".

Sasa, unatakaje mwenye kiwanda alipie kodi Value Added ya muuzaji kuweka maji kwenye friji, ambayo ni value iliyowekwa na muuzaji, wakati mwenye kiwanda hahusiki na hiyo value added ?
Naelewa vizuri ulichoandika,

Ninachomaanisha ni kuwa, Kwa bidhaa ambazo Bei inafahamika Toka uzalishaji Hadi muuzaji wa mwisho soko la ndani,

Ikiwa Bei ya kiwandani Moshi ni sh 800, na Sirali mwisho wa Nchi yanauzwa 1500,

Serikali ije na mfumo ambao Mzalishaji kiwandani atachajiwa Kodi ambayo ataiwasilisha serikalini Kwa kuongeza Bei kwenye bidhaa hiyo.

Sijui unanielewa?
 
Mzalishaji wa kiwandani atachajiwaje kodi ya value ambayo ataongeza muuzaji wa mwisho?

Unaelewa kwamba muuzaji wa mwisho naye anaongeza value?

Hujaelewa wapi huo mfano wa muuzaji wa mwisho kuongeza value ya maji kwa kuyaweka kwenye friji na kuyapoza?
 
Back
Top Bottom