Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Soma vizuri concept ya VAT!Nimesema tra waweke mfumo mzuri wa kuwafanya viwanda ndio wawe walipaji wa VAT Kwa kuwa wao ndio wanamiliki chain ya tangu uzalishaji Hadi mtumiaji wa mwisho.
Ni vyema ungeboresha HOJA Badala ya kupinga tu bila fikra.
Ukiingalia kwa uzuri hii VAT ni jini tuNi hivi.
Kiwanda cha maji kikinunua maji kwa shilingi 200 kwa lita, na kuya purify na kuyaweka kwenye chupa kwa gharama shilingi 800 kwa lita, kitalipia VAT hiyo "value added" ya shilingi 800 kwa lita. Ndiyo value iliyokuwa added kwenye maji ya shilingi 200 (ku purify na kuweka kwenye chupa).
Maji hayo yakiuzwa kwa shilingi 1200 kwa muuzaji barabarani, ambaye na yeye anayaweka kwenye friji, kwa gharama ya shilingi 200 kwa chupa, muuza maji naye atailipia hiyo value ya kupooza maji kwa sh 200 kwa lita kwenye friji kodi, hiyo ndiyo "value" aliyo add.
Ndiyo maana inaitwa "Value Added Tax".
Sasa, unatakaje mwenye kiwanda alipie kodi Value Added ya muuzaji kuweka maji kwenye friji, ambayo ni value iliyowekwa na muuzaji, wakati mwenye kiwanda hahusiki na hiyo value added ?
Mantiki ya HOJA hujaielewa,Soma vizuri concept ya VAT!
Value Added Tax!
Kuna productz zinaenda hadi mizunguko kumi ndo unaingia kuliwa.. ..hiyo mizunguko inatoa nafasi ya ongezeko la thamani...na mikunjo ya kodi ya Ongezeko la Thamani bado inaandamana na huo mzunguko.....au mkunjo...!
VAT haifi...inaendelea kuongezeka kadiri inavyopita kwenye Ongezeko la Thamani...!
Kwa hivo wazo la kukusanya VAT kwenye Viwanda haliwezekani na wala nature ya hiyo kodi haiko hivo!
Kwani mwenye kiwanda Ananua wapi Malighafi?
Na anaponunua VAT yake itaokotwaje?
Elimu
Elimu
Elimu!
VAT ni ujinga. Marekani tumeikataa.Ukiingalia kwa uzuri hii VAT ni jini tu
Imekataliwa Kwa grounds zipi?VAT ni ujinga. Marekani tumeikataa.
Weka kimahesabu kabisaSina hakika kodi ninayo imaanisha mimi inaitwaje ila nitakupa mfano
Pepsi garama zao zote za kutengeneza soda moja ni Sh 250 wanajumlisha na faida yao sh 100 soda inakua 350
Serikali inaweka sh 100 kwenye kila soda, hapo soda hadi inatoka kiwandani inakua inauzwa (garama na faida)350 + 100(kodi) jumla 450
Soda itapita kwa muuzaji wa jumla kisha reja reja
Mushi Wa jumla atainunua soda sh450 ataongeza garama zake na faida sh 100 inakua 550 bei ya kumuuzia wa reja reja
Mangi duka reja reja nayeye akinunua 550 ataongeza 150 garama na faida na bei itakua 700 ambayo atainunua Mayu kukata kiu
Soda ikimaliza mzunguko makusanyo ya kodi yatakua hivi
Pepsi kwanza ataipa serikali ile 100 iliyowekwa kwenye kila soda
Halafu tena Pepsi italipa 18% ya faida aliyoweka kwenye soda
Mushi muuza jumla TRA atalipia 18% ya faida yake
Na Mangi duka atalipa asilimi 18% ya faida yake
Kwa mlolongo huo kuna kodi imewekwa direct na serikali sh 100 na kuna kodi 18% watalipa wafanyabishara kulingana na faida
Sijui nimeeleweka
Unamaanisha 100 tayari kiwanda kimeilipa na imo kwenye Bei ya soda.Sina hakika kodi ninayo imaanisha mimi inaitwaje ila nitakupa mfano
Pepsi garama zao zote za kutengeneza soda moja ni Sh 250 wanajumlisha na faida yao sh 100 soda inakua 350
Serikali inaweka sh 100 kwenye kila soda, hapo soda hadi inatoka kiwandani inakua inauzwa (garama na faida)350 + 100(kodi) jumla 450
Soda itapita kwa muuzaji wa jumla kisha reja reja
Mushi Wa jumla atainunua soda sh450 ataongeza garama zake na faida sh 100 inakua 550 bei ya kumuuzia wa reja reja
Mangi duka reja reja nayeye akinunua 550 ataongeza 150 garama na faida na bei itakua 700 ambayo atainunua Mayu kukata kiu
Soda ikimaliza mzunguko makusanyo ya kodi yatakua hivi
Pepsi kwanza ataipa serikali ile 100 iliyowekwa kwenye kila soda
Halafu tena Pepsi italipa 18% ya faida aliyoweka kwenye soda
Mushi muuza jumla TRA atalipia 18% ya faida yake
Na Mangi duka atalipa asilimi 18% ya faida yake
Kwa mlolongo huo kuna kodi imewekwa direct na serikali sh 100 na kuna kodi 18% watalipa wafanyabishara kulingana na faida
Sijui nimeeleweka
Marekani kuna ugatuzi mkubwa sana wa mamlaka kutoka serikali kuu kwenda serikali za chini za majimbo na wilaya, mpaka za miji.Imekataliwa Kwa grounds zipi?
Funguka tafadhali.
Mara zote GT unatakiwa kufikiri nje ya box.Soma vizuri concept ya VAT!
Value Added Tax!
Kuna productz zinaenda hadi mizunguko kumi ndo unaingia kuliwa.. ..hiyo mizunguko inatoa nafasi ya ongezeko la thamani...na mikunjo ya kodi ya Ongezeko la Thamani bado inaandamana na huo mzunguko.....au mkunjo...!
VAT haifi...inaendelea kuongezeka kadiri inavyopita kwenye Ongezeko la Thamani...!
Kwa hivo wazo la kukusanya VAT kwenye Viwanda haliwezekani na wala nature ya hiyo kodi haiko hivo!
Kwani mwenye kiwanda Ananua wapi Malighafi?
Na anaponunua VAT yake itaokotwaje?
Elimu
Elimu
Elimu!
Serikali ya majimbo kumbe itatusaidia!!Marekani kuna ugatuzi mkubwa sana wa mamlaka kutoka serikali kuu kwenda serikali za chini za majimbo na wilaya, mpaka za miji.
Hawa watu wanaamini sana katika local governments, watu wajipangie kodi zao nyingi wao wenyewe.
Sasa katika mfumo huo ambao una serikali za majimbo 50 (plus DC and territories), serikali za wilaya (counties) zaidi ya 3,000, na serikali za miji maelfu, ambazo nyingi zina maoni tofauti na hata kupingana kifalsafa kuhusu mambo ya kodi, ni vigumu kuwa na VAT moja ya kitaifa.
Hata Tanzania tukiwa na mfumo wa majimbo na ugatuzi wa madaraka kwenda serikali za mitaa, hizi kodi nyingi wananchi watakuwa na nafasi kubwa ya kuzipinga na ku,iondoa, au kuzibadilisha ziwe na manufaa kwao zaidi.
Sana tu, watu hawaelewi hivi vitu.Serikali ya majimbo kumbe itatusaidia!!
Hajiulizi kwanini nyumba za watumishi wa TRA Zina sefu/ kasiki za kutunzia pesa za RUSHWA!!Wewe umekakariri elimu ya mkoloni
Tunataka watu wanaotumia akili ya kuja na solution sio kutuletea theory walizo kariri za mazingira ya wazungu.
Kwa sasa suala la kukusanya VAT kwa mazingira yetu halitekelezeki kwa sababu
1. Wafanya biashara waliowengi hawana elimu (darasa la saba)
2. Wakusanyaji wanatumia ujinga wa wafanya biashara kujinufaisha
3. Rushwa kwenye kila hatua
Lazima tuje na njia rafiki itakayo endana na mazingira yetu; hiyo ulityo soma inaendana na mazingira ya Wazungu ambapo factor nilizotaja hapo juu kwao hazipo
Mazingira ya wazungu. Kwamba kuna standard ya waAfrika na standard ya kizungu? Vipi utafuata mfumo watu waliotumia wakafanikiwa au wwwe utakuja na wa kwako mpya ambao ni unproven na untested?Tunataka watu wanaotumia akili ya kuja na solution sio kutuletea theory walizo kariri za mazingira ya wazungu ambayo ni tofauti kabisa na ya kwetu;
Kwa sasa suala la kukusanya VAT kwa mazingira yetu halitekelezeki kwa sababu;
1. Wafanya biashara wetu waliowengi hawana elimu (darasa la saba)
2. Wakusanyaji wanatumia ujinga wa wafanya biashara kujinufaisha
3. Mifumo ya manual ya ufuatiliaji wa kodi ambapo hutumia gharama kubwa na kuleta usumbufu kwa wafanya biashara
4. . Rushwa kwenye kila hatua
Tatizo la elimu yetu tangu chekechea inafundisha watu kukariri, haifundishi watu kutumia akili ili kutatua changamoto; ndio sababu kila mtu hata Doctor anawazia kuajiriwa.....
Tukitaka kufaniliwa lazima tuje na njia rafiki itakayo endana na mazingira yetu; hiyo uliyo soma inaendana na mazingira ya Wazungu ambapo changamoto nilizotaja hapo juu hazipo kwao ...
Huo mfumo ni failure kwetu.Mazingira ya wazungu. Kwamba kuna standard ya waAfrika na standard ya kizungu? Vipi utafuata mfumo watu waliotumia wakafanikiwa au wwwe utakuja na wa kwako mpya ambao ni unproven na untested?
NAUNGA MKONO HOJASalaam, Shalom,
Wote tunafahamu kuwa uagizaji wa mafuta Kwa Mfano, Huwa mafuta yanapopakuliwa Kutoka kwenye meli, Huwa Lita zinafahamika na Kodi ya Serikali Huwa tayari inajulikana.
Kiwanda Cha kuuza maji Cha Kilimanjaro Kwa Mfano, TRA wakiweka mfumo wa kujua Lita kiasi Gani zinazalishwa Kwa siku, mwezi Hadi mwaka, wanao uwezo Kwa kudai Kodi ya ongezeko la thamani VAT Toka kiwandani direct, kwanini wasuburi maji yaendelee kwenye vioski na deports ambazo nyingi hazina, au haxitoi EFD?
Viwanda vya kuzalisha cement, vinywaji, CHUMA ambavyo Bei zake zinafahamika, nk nk, Serikali Ina uwezo wa kukaa na wazalishaji na kukubaliana nao Ili wao ndio wawe wanalipa vat direct bila kusubiri Hadi muuzaji wa mwisho ndiye abanwe kulipa vat.
Hawa wauzaji wa mwisho, wabanwe kulipa Kodi ya mapato pekee, lakini VAT ikusanywe na kiwanda na kiwanda kiwasilishe VAT hiyo direct Kwa Serikali.
FAIDA YA SERIKALI KIKUSANYA VAT KUTOKA KWA KIWANDA DIRECT NI:
1. KUPUNGUZA UKWEPAJI KODI
Wauza maji na wafanyabiashara wauzao bidhaa za viwandani, wanaotembeza juani, hawana EFD hao ndio wauzaji wakubwa wa wauzaji wa depot's kubwa ambazo hushiriki kuhujumu mapato Kwa kutotoa risiti hivyo kupunguza uwasilishaji wa vat hivyo kupotea Kwa mapato.
2. KUPUNGUZA RUSHWA
Utaratibu huu wa makadirio mawilayani inaongeza tu gharama na kutengeneza mwanya wa RUSHWA Kwa watumishi wa TRA. Kodi ya VAT ikikusanywa direct itamsaidia kuondoa RUSHWA maana itakuwa Rahisi kuwadhibiti viwanda.
3. GHARAMA YA KUKUSANYA KODI ITAPUNGUA
Kukusanya Kodi ya VAT direct Toka Kwa kiwanda automatically kutapunguza Mzigo wa Serikali kuajiri wafanyakazi kufuatilia Kodi, au utapunguza KAZI Kwa watumishi hivyo kujikita na shughuli zingine Kwa ufanisi zaidi.
4. MAPATO YA SERIKALI YATAONGEZEKA
Kuminya mianya ya RUSHWA na upotevu wa mapato, automatically kutaipa Serikali mapato ya kutosha, hivyo kusababisha mapato ya Serikali kuongezeka.
Karibuni Kwa maoni na maboresho ya HOJA hapo juu 🙏
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Mkuu VAT haina uhusiano na added value on a productMzalishaji wa kiwandani atachajiwaje kodi ya value ambayo ataongeza muuzaji wa mwisho?
Unaelewa kwamba muuzaji wa mwisho naye anaongeza value?
Hujaelewa wapi huo mfano wa muuzaji wa mwisho kuongeza value ya maji kwa kuyaweka kwenye friji na kuyapoza?
Hii ni njia sahihi ya kukusanya hiyo kodi na kuandoa double taxation na kila muuzaji atairejea kupitiaa bei ya bidhaa husika hadi mraji wa mwisho. Tukumbuke kuwa VAT ni kodi ya mraji ambao ni mtu wa mwisho.Mzalishaji wa kiwandani atachajiwaje kodi ya value ambayo ataongeza muuzaji wa mwisho?
Unaelewa kwamba muuzaji wa mwisho naye anaongeza value?
Hujaelewa wapi huo mfano wa muuzaji wa mwisho kuongeza value ya maji kwa kuyaweka kwenye friji na kuyapoza?
Amekulisha matango pori huyo, USA nzima haina kodi ya VATSerikali ya majimbo kumbe itatusaidia!!