Ushauri: Kodi ya VAT ikusanywe direct toka viwandani kupunguza upotevu wa mapato

Nimesema tra waweke mfumo mzuri wa kuwafanya viwanda ndio wawe walipaji wa VAT Kwa kuwa wao ndio wanamiliki chain ya tangu uzalishaji Hadi mtumiaji wa mwisho.

Ni vyema ungeboresha HOJA Badala ya kupinga tu bila fikra.
Soma vizuri concept ya VAT!

Value Added Tax!

Kuna productz zinaenda hadi mizunguko kumi ndo unaingia kuliwa.. ..hiyo mizunguko inatoa nafasi ya ongezeko la thamani...na mikunjo ya kodi ya Ongezeko la Thamani bado inaandamana na huo mzunguko.....au mkunjo...!

VAT haifi...inaendelea kuongezeka kadiri inavyopita kwenye Ongezeko la Thamani...!

Kwa hivo wazo la kukusanya VAT kwenye Viwanda haliwezekani na wala nature ya hiyo kodi haiko hivo!

Kwani mwenye kiwanda Ananua wapi Malighafi?

Na anaponunua VAT yake itaokotwaje?

Elimu
Elimu
Elimu!
 
Ukiingalia kwa uzuri hii VAT ni jini tu
 
Mantiki ya HOJA hujaielewa,

Rudia tena na tena kusoma.
 
Weka kimahesabu kabisa
 
Unamaanisha 100 tayari kiwanda kimeilipa na imo kwenye Bei ya soda.

Sasa kwann Serikali isiidai Moja Kwa moja Kutoka kiwandani,

Au kwanini Serikali usiweke sh 200 kwenye Bei Ili ije kuidai direct Toka Kwa kiwanda?

Hapo ndipo kwenye chanzo Cha tatizo🤔
 
Imekataliwa Kwa grounds zipi?

Funguka tafadhali.
Marekani kuna ugatuzi mkubwa sana wa mamlaka kutoka serikali kuu kwenda serikali za chini za majimbo na wilaya, mpaka za miji.

Hawa watu wanaamini sana katika local governments, watu wajipangie kodi zao nyingi wao wenyewe.

Sasa katika mfumo huo ambao una serikali za majimbo 50 (plus DC and territories), serikali za wilaya (counties) zaidi ya 3,000, na serikali za miji maelfu, ambazo nyingi zina maoni tofauti na hata kupingana kifalsafa kuhusu mambo ya kodi, ni vigumu kuwa na VAT moja ya kitaifa.

Hata Tanzania tukiwa na mfumo wa majimbo na ugatuzi wa madaraka kwenda serikali za chini/mitaa, hizi kodi nyingi wananchi watakuwa na nafasi kubwa ya kuzipinga na ku,iondoa, au kuzibadilisha ziwe na manufaa kwao zaidi.
 
Mara zote GT unatakiwa kufikiri nje ya box.

Tukifanya hivyo, tutaweza kutatua matatizo am Ayo viongozi wetu wameshindwa yatatua.
 
Serikali ya majimbo kumbe itatusaidia!!
 
Serikali ya majimbo kumbe itatusaidia!!
Sana tu, watu hawaelewi hivi vitu.

Zitasaidia kupinga sera za kijinga kutoka serikali kuu.

Na wananchi wataamua kama gavana wa jimbo analeta ujinga, wanamtoa kwenye kura. Gavana anakuwa si mteule wa rais, anakuwa anachaguliwa na wananchi.
 
Hajiulizi kwanini nyumba za watumishi wa TRA Zina sefu/ kasiki za kutunzia pesa za RUSHWA!!

Mtumishi anakutwa na 7 bn, huo mfumo wa Kodi corrupt upitiwe UPYA.
 
Mazingira ya wazungu. Kwamba kuna standard ya waAfrika na standard ya kizungu? Vipi utafuata mfumo watu waliotumia wakafanikiwa au wwwe utakuja na wa kwako mpya ambao ni unproven na untested?
 
Mazingira ya wazungu. Kwamba kuna standard ya waAfrika na standard ya kizungu? Vipi utafuata mfumo watu waliotumia wakafanikiwa au wwwe utakuja na wa kwako mpya ambao ni unproven na untested?
Huo mfumo ni failure kwetu.

Watanzania wangapi Wana account bank na wanapitishia mzunguko wao bank na kutunza kumbukumbu za matumizi ya biashara zao Kwa ajili ya return?

Inawezekana vipi mtu mwenye mtaji wa ml 5 kwenye biashara yake kuajiri muhasibu wa kupeleka return Kila mwezi?

Huoni mfumo huu upo kuwatajirisha watumishi wa TRA?

Mfumo wa Kodi ni copy na paste, kwetu Hauna reality,

Tukae chini tuufumue,tuuboreshe Ili tusonge mbele.
 
NAUNGA MKONO HOJA
 
Mkuu VAT haina uhusiano na added value on a product
 
Hii ni njia sahihi ya kukusanya hiyo kodi na kuandoa double taxation na kila muuzaji atairejea kupitiaa bei ya bidhaa husika hadi mraji wa mwisho. Tukumbuke kuwa VAT ni kodi ya mraji ambao ni mtu wa mwisho.
Aidha njia hii itaogeza wigo wa kodi na kuleta usawa wa mazingira kwa wafanyabiashara wote. Kwa sasa hali ilivyo bidhaa za wafanyabishara walio na usajili wa VAT ziko juu kuliko za wasio na usajiri. Mazingira haya yanaleta pool and push factor na kwa hulka ya binadamu ya kutaka unafuu, wananunua kwa wafanyabiashara wasio na usajiri wa VAT. Mazingira hayo yanawafanyawale waliosajiria VAT kuingia kwenye majadiliano na wanunuzi ili wapunguziwe bei kama watakubali kutopewa risiti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…