Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

Mkuu natamani sana kukushauri ila Imani yangu hailuhusu kuuza au kutumia hizo bidhaa, worry out wajasiliamali watapitia tu uzi wako!
 
Bw.Daffa unamaanisha kua hata kutoa ushauri imani yako haikuruhusu?

Waweza kuanzisha biahsara yoyote mahari popote ili mladi tu kuna watu wanao hitaji huduma zako, kingile labda inabidi ujiulize ze ni watu wangapi wanao hitaji huduma yako? Pili je wako tayali kununua/kulipa kiasi gani kupata kile wanachohitaji?. maana biashara ya wine inahitaji uvumilivu sanaaa haiko kama biahsara zingine
 
Last edited by a moderator:

[USER=156619]Bw.Daffa
unamaanisha kua hata kutoa ushauri imani yako haikuruhusu?

Waweza kuanzisha biahsara yoyote mahari popote ili mladi tu kuna watu wanao hitaji huduma zako, kingile labda inabidi ujiulize ze ni watu wangapi wanao hitaji huduma yako? Pili je wako tayali kununua/kulipa kiasi gani kupata kile wanachohitaji?. maana biashara ya wine inahitaji uvumilivu sanaaa haiko kama biahsara zingine
/QUOTE]

Mkuu jaribu tu kunielewa sina nia mbaya,so long kuna vitu kadhaa umevitaja kama kiwango cha uhitaji na uwezo wa kununua(level of demand and quantity demanded as well as purchasing power) Labda niseme kwamba moja ya factor yenye nguvu kwenye hiyo biashara yako ni Mahali(Location where business is found) hii ni kwa sababu kuna maeneo unaweza kuinga hata kwenye migigoro na watu wanaokuzunguka(kwa sababu za kiimani au kistaarabu) pamoja nakukosa soko kabisa:Zingatia hilo Mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Bw.Daffa unamaanisha kua hata kutoa ushauri imani yako haikuruhusu????????????????

waweza kuanzisha biahsara yoyote mahari popote ili mladi tu kuna watu wanao hitaji huduma zako, kingile labda inabidi ujiulize ze ni watu wangapi wanao hitaji huduma yako???????? pili je wako tayali kununua/kulipa kiasi gani kupata kile wanachohitaji?. maana biashara ya wine inahitaji uvumilivu sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa haiko kama biahsara zingine

Mkuu niliko bold unafikiri ni kwa nini?
 
Mkuu jaribu tu kunielewa sina nia mbaya,so long kuna vitu kadhaa umevitaja kama kiwango cha uhitaji na uwezo wa kununua(level of demand and quantity demanded as well as purchasing power) Labda niseme kwamba moja ya factor yenye nguvu kwenye hiyo biashara yako ni Mahali(Location where business is found) hii ni kwa sababu kuna maeneo unaweza kuinga hata kwenye migigoro na watu wanaokuzunguka(kwa sababu za kiimani au kistaarabu) pamoja nakukosa soko kabisa:Zingatia hilo Mkuu.

Asante kwa ushauri

Ila mategemeo yangu sio kuweka na eneo la watu kunywea hapo. Ni kwa wanunuzi wa Jumla na kwa wateja wa wa reja reja wa majumbani. Unanunua unaondoka nayo
 
Biashara ya wine nijuavyo mimi sio fast moving kwa baadhi ya maeneo kama vinywaji vingine. Ukiweka bia za jumla walau utauza kwa kutegemea na grocery na bar zilizopo eneo husika ila uwe na mtaji wa kueleweka uweze kuweka varieties za kutosha sio mteja anakuja mara aina hii imeisha hizo siweki nk
 
Asante my kaka Mkirua..
 
Last edited by a moderator:
Hongera kwa kuwa na wazo.Ukianza ni note nitakuunganisha kwa kampuni wanayoweza kununua kutoka kwako wanakulipa in 35 days.Watakupa hata confirmed orders hata kama ni kidogo lakini average kama za laki 2 kwa mwezi . Kwa kujua tu,kwanini kwenye makao mapya na si penye wateja wa wines na spirits.
 
Thax mkuu. I Will keep in touch

Swali lako: nachoweza kusema ni kwasababu 1. hakuna huduma hiyo maeneo hayo ingawa watu wenye uwezo na uhitaji wapo 2. ndiko ninakoishi, na nitaweza kufanya ufuatiliaji kwa urahisi.
 
Ndugu zangu salam. Napenda kujua ni mtaji kiasi gani unahitajika kuanzisha biashara tajwa hapo juu ya vinywaji baridi kwa jumla kama maji ya kunywa, soda na juice za azam. Asanteni
 
Ndugu zangu salam. Napenda kujua ni mtaji kiasi gani unahitajika kuanzisha biashara tajwa hapo juu ya vinywaji baridi kwa jumla kama maji ya kunywa, soda na juice za azam. Asanteni

Mbona beer hujaiweka kwenye list mkuu au dhambi?
 
Sio dhambi mkuu but target yangu ni kuanza kwanza na vinywaji baridi then mbeleni nitaweka na bia.
 
Habarini wapendwa.

Mi nimeajiriwa ila sijaridhika kabisa mie kukaa ofsini. Siku zote ninawaza kuanzisha biashara yangu mwenyewe.

Sijawahi kufanya biashara ya aina yoyote ile ila tu nilipokuwa s/msingi nilikuwa namsaidia baba kuuza duka la rejareja.

Nimekaa muda mwingi nikifikiria nifanye nini pale ambapo baba alikua na duka lake. Mwisho wa yote ndo akili yangu inaniambia niwe nasupply vinywaji vyote kwa wafanyabiashara katika lile eneo ambalo babangu ana duka pale, yaani niwauzie maji, soda zote pamoja na vinywaji vingine vyote (alcoholic and non alcoholic drinks) kwani wengi wao huwa wanavifuata mjini isipokuwa soda ambapo wanaletewa na kampuni husika.

Nichouliza ni kwamba, nitafanyaje niwe napata vinywaji hivyo kutoka kampuni husika wawe wananiletea mimi halafu mimi niwauzie wafanya biashara wengine ambao watakuwa wanauza reja reja?

NB: sina usafiri wa aina yoyote ule ambao labda utanisaidia kusafirisha vitu hivyo kutoka mjini kuja pale ambapo nitakuwa nafanyia biashara.
 
Tatizo la Watanzania huwa hawajielezi vizuri, mi nashindwa kukusaidia. Sema upo wapi? Una mtaji wa shilingi ngapi? unataka ufanye biashara eneo gani? Unataka vinywaji vya kampuni gani?
 
Tatizo la Watanzania huwa hawajielezi vizuri, mi nashindwa kukusaidia. Sema upo wapi? Una mtaji wa shilingi ngapi? Nataka ufanye biashara eneo gani? unataka vinywaji vya kampuni gani?

Mbona anaeleweka, ameuliza Afanye utaratibu gani ili awe analetewa vinywaji husika mfano maji au alcol drinks
so ungetumia nafasi hii kueleza kile unachokijua!
 
Msaada kwa mtu yeyote anaye jua Biashara hii ya Vinywaji vikali na Luxury (mf. wisk na wine) Naomba anieleweshe kwa kina.Mimi nipo hapa Dar na mtaji wa million 5.

Vitu ninavyohitaji kufahaumu kwa kina ni:-

1. Mtaji wa kuanzisha duka la biasahara hii (initial capital.
2. Mazingira yanayo faa kwa Bisahara hii, je ni karibu na bar kama ninavyofikilia mm?
3. Mahali zinako patikana bidhaa kwa urahisi na kwa bei nafuu
4. Utaratibu wa kupata leseni wa hii biashara pamoja na gharama zake
5. Ni bidhaa zipi zinakua na wateja sana hasa zinazofaa kwa kuanzia biashara?
6. Faida na Changamoto zake.
7. Nini ushauri wako kuhusiana na wazo hili na bishara hii?

Natumaini wenye kufahamu zaidi juu ya bishara hii na ni serious people watanisaidia mawazo bora na kujibu maswali hayo hapo juu. Nitashukuru kwa ushirikiano wako.
 
Tatizo la wtanzania huwa hawajielezi vizuri, mi nashindwa kukusaidia. sema upo wapi?, una mtaji wa shilingi ngapi? unataka ufanye biashara eneo gani? unataka vinywaji vya kampuni gani?

Wewe ndio hujamuelewa.
 
Hahahaha, jamaa anampiga mkwala eti hajaeleweka, aisee kazi kweli

Jamaa wazo zuri na pia nampongeza kwa kujitambua kwamba mali ya Baba ni ya ukoo ila yako ni ya kizazi chako.

Wazoefu watakuja,ila mie nakushauri yafuatayo

Ufuatiliaji

-Kwanza bei zinatofautiana, mkoa na mkoa. Sasa wewe tembelea Bohari za bidhaa hizo, na kila mkoa na wilaya nchi hii Bohari za bidhaa hizo zipo. Wao watakupa bei ya jumla.

Usambazaji na usafiri
-Kuna taratibu mbili hapa,kuna wale wafanyabiashara wanaofikia kiwango cha kusambaziwa bidhaa,na hii huwa inategemea na mtaji wako na mzunguuko wao wa biashara. Wale wenye mzunguuko mkubwa na mtaji mkubwa kiasi huwa wanapelekewa bure kabisa. Na wapo wale ambao mtaji ni mdogo sana inabidi wajitegemee usafiri.
Muhim tafuta eneo lenye mzunguuko mzuri.

Uhakiki
Sasa nakushauri kwanza kabisa tembelea makampuni hayo,na ninakushauri bora uende moja kwa moja na sio kutumia kuuliza mawakala,maana kule moja kwa moja utapewa hadi ushauri wa kina,sasa utaamua usubiri mtaji ukue au la.

Mwanzo
Ili biashara unayoanza ili uone faidi yake lazima uwe na mtaji wa kiasi cha kati kwa maisha ya kawaida.Ukianza na mtaji mdogo wote utaishi kwenye usafiri na kulipa kodi. Mie niliwahi kwenda kwa Bakhresa moja kwa moja headoffice yao,nilipewa Data za maana,mpaka nikasema kweli kuuliza nje kwa watu wa kawaida unakosa mengi ukienda sehem husika unapata kila kitu. Kwanza wanakupa moyo sana na kukupa mbinu na njia zote bila longolongo.Maana nilienda kwa issues za ICE cream.

Mwisho
Kwa ufupi subiri waje wachambuzi humu, halafu chukua ushauri kisha nenda sehem husika moja kwa moja.
Usikatishwe tamaa kimaisha ndugu yangu, na wala usitume mtu nenda mwenyewe, maana kamahuna moyo unaweza kurudia mlangoni.

Kuna siku nilienda sehem kuuliza utaratibu nikakuta mtu anachukua order ya mzigo wa Fuso nne, basi mie nilitamani kukimbia. Lakini kumbe kila mtu na uwezo wake hata hao wa Fuso nne walianza kwa mzigo wa mdogo tu wa kubeba kwenye Carry.

Maisha lazima ujitoe na kujenga imani kwamba mwenye kumi alianza na moja, basi hapo huwezi kumuogopa mtu yoyote au tajiri yoyote kama ukiamini hivyo.
 
Nina mdogo wangu anafanya, yeye yupo Kijitonyama na anafanya jumla. Mtaji wake ulikuwa 13 Million, na anamauzo sasa kwa wastani wa million 1 kwa siku, na faida yake ni 40,000 wastani kwa siku. Ukiangalia kwa karibu utaona faida ni 4% ya mapato baada ya kutoa gharama za uendeshaji, hii (razor skin margin) ni faida ndogo sana na hatari zake ni kwamba ukienda kwenye mtikisiko wowote ule biashara inakufa. Ukiangalia urudishaji wa mtaji utaona kwamba anarudisha 10% kwa mwaka hii inaweza chukua muda mrefu sana yeye kurudisha pesa yake.

Ushauri wangu ni kwamba hii biashara inaitaji uangalizi wa hali ya juu sababu ya mzunguko wake wa fedha ni mwingi lakini faida yake ni ndogo sana. Kama unaweza tazama biashara angalia yoyote yenye 10-15% faida baada ya kuondoa gharama za uendeshaji. Biashara hii nafananisha na upigaji tofali zote hizi maumivu makali.
 
Ukiangalia urudishaji wa mtaji utaona kwamba anarudisha 10% kwa mwaka hii inaweza chukua muda mrefu sana yeye kurudisha pesa yake.

Mkuu hapo Mbona kama umetereza? Kama mtaji wake ulikuwa 13M na anapata faida 40,000 kila siku ina maana hiyo ni 12M kwa mwaka (40,000 Mara siku 300 za mwaka), sasa inakuaje unasema anarudisha 10% kwa mwaka? Au mimi ndio sijaelewa?
 
Back
Top Bottom