Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

Wana JF habari za Jumapili!

Naamini na ntaendelea kuamini kuwa JF ni kisima cha hekima na ushauri na ndio maana naleta kwenu ombi la ushauri juu ya uaanzishaji wa duka la vivywaji vya jumla.

Kimsingi eneo nilipo linauhitaji wa duka la vinywaji vya jumla, baada ya kugundua hilo nimeona nipate ushauri namna ambavyo naweza kuanzisha duka hilo
Kwa haraka haraka eneo (Location) kwa ajili ya biashara hiyo ipo na ni centre nzuri tu.

Mwenye uzoefu namna ambavyo naweza kuanza biashara hiyo, kiasi cha mtaji , vinywaji kipaumblele, namna ambavyo naweza ku-link na depo za makapuni ya vinywaji hasa kwa mkoa wa (Arusha) kwa ajili ya ununuzi na la msingi kabisa upatikaji wa cret kwa ajili ya kuanzia, namna ya ununuzi wa pombe kali yaani gin, grands, wine na jamii zake.

Kwa mawazo na uwezo wangu nilitaka nianze na cred 100 za beer, 100 za soda, kuhusu vinywaji vikali ntaomba kushauriwa zaidi!

Nashukuru kwa ushauri ambao utatolewa!!

Karibuni kwa ushauri.
Umefikia wapi mkuu
 
Japokua nimechelewa sana kuiona post yako lakini kama bado ujaanza nitaweza kukushauri baadhi ya vitu. Mimi nauzoefu wa zaidi ya miaka kumi kwenye hiyo biashara lakini ni kwa Dar es salaam.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Kwanza lazima nijue unamtaji kiasi gani, pili biashara ya makreti itakusumbua kama mtaji wako nimdogo kwani kreti 100 huwezi kua agent Bali utanunua kwama agent na faida itakua ndogo. Ila ushauri wangu deal na box tu kama mtaji ni mdogo.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Kwanza lazima nijue unamtaji kiasi gani, pili biashara ya makreti itakusumbua kama mtaji wako nimdogo kwani kreti 100 huwezi kua agent Bali utanunua kwama agent na faida itakua ndogo. Ila ushauri wangu deal na box tu kama mtaji nimdogo.

Kaka nahitaji ufahamu kidogo wa biashara hii u naweza nisaidia.
 
Habarini wana jukwaa,

Jamani mwenzenu nawaza kufanya biashara ya vinywaji ila sijajua vinywaji gani vinafaida na vinauzika haraka hapa.

Nipo kwenye mchakato wa kutafuta mtaji angalau milioni 1, sasa wataalam wa biashara niambie ni vinywaji gani vitauzika sana kwa wanywaji?
 
Uko wapi na je location uliyopo ikoje? Washindani wako wakoje na mitaji yao ikoje? Vp hali ya upatikanaji wa umeme hapo ulipo fanya utafiti wa hivyo vitu kwanza
 
Nina mdogo wangu anafanya, yeye yupo Kijitonyama na anafanya jumla. Mtaji wake ulikuwa 13 Million, na anamauzo sasa kwa wastani wa million 1 kwa siku, na faida yake ni 40,000 wastani kwa siku. Ukiangalia kwa karibu utaona faida ni 4% ya mapato baada ya kutoa gharama za uendeshaji, hii (razor skin margin) ni faida ndogo sana na hatari zake ni kwamba ukienda kwenye mtikisiko wowote ule biashara inakufa. Ukiangalia urudishaji wa mtaji utaona kwamba anarudisha 10% kwa mwaka hii inaweza chukua muda mrefu sana yeye kurudisha pesa yake.

Ushauri wangu ni kwamba hii biashara inaitaji uangalizi wa hali ya juu sababu ya mzunguko wake wa fedha ni mwingi lakini faida yake ni ndogo sana. Kama unaweza tazama biashara angalia yoyote yenye 10-15% faida baada ya kuondoa gharama za uendeshaji. Biashara hii nafananisha na upigaji tofali zote hizi maumivu makali.

Habari mkuu,niliwahi kupitia nyuzi fulani huko nyuma juu ya biashara ya soda kwa ujumla,vipi mdogo wako alieendelea maana nilikaa kimya kusubiri mrejesho wa mtu aliyekuwa ameeomba ushauri kama alijaribu au aliibadilisha maamuzi hakurejea,hebu nifahamishe anaendeleaje jamaa yako? na ikibidi ningependa kupata mawasiliano naye maana nina pesa kiasi fulani nafikiria kuifanya hiyo biashara.
 
Tafadhali kama unauwelewa au unafanya biashara ya kuuza vinywaji kwa bei ya jumla nahitaji msaada wako, vinywaji kama maji, juice, soda n.k mtaji niliokuwa nao ni 1.5m naomba kujua inalipa vipi hii biashara, msaada ndugu zangu au je kwa mtaji tajwa hapo juu naweza fanya biashara gani nikaishi hapa mjini bila kudhalilika

Nakaribisha ushauri, mchango, maoni n.k
 
mkuu nakushauri ungenunua boda boda tu halafu chukua 50 kwa wiki itakulipa sana. sidhani kama biashara ya vinywaji utapata faida hiyo
 
Back
Top Bottom