Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

kwa bei ya jumla faida yake ni kidogo sana .niliwahi kufanya hii biashara coca kwa jumla walikua wananiletea kwa 11000 na pepsi kwa 10900 mimi nauza 11500.faida kama 500.maji uhai carton ilikua 2500 yale litre 1 .mimi nauza 2800,faida kama 300 hivi.angalau kipindi hicho kodi ya TRA tulikua tunapeta.bor tafuta sehemu kuna watu wengi unatafuta deepfreezer na vijana wako wanakimbiza kwa rejareja.ukifungua kuuza jumla jiandae na TRA wa magu hawajui kama bidhaa yako unapata faida ya 10,hata pipi mashine ya EFD itakuhusu
Mkuu kwa ujumla wake faida inaonekana au ndio yaleyale
 
Kubwa na la muhimu kuwa msimamizi wa biashara yako.

love thé love or hâte thé love.....
 
Umeandika yote sawa ila umesahau moja
11. Tafuta wahudumu wenye chura za kutosha.
 
Ni dhahiri kwamba wajasiriamali wengi wamekuwa wakijiuliza ni njia gani wazitumie katika kuanzisha,kukuza ama kuboresha biashara zao za kuuza vinywaji ili wapate kunufaika na faida kubwa.
Kama wewe pia ni mmojawapo kati ya wajasiriamali wanaotafuta mafanikio makubwa kwa kufanya biashara ya namna hii utakuwa umewahi kujiuliza maswali kama haya;

· Je, mtaji wa biashara hii (bar) ni kiasi gani?
· Mbona baa ya huyu inalingana na ile kwa mwonekano lakini yule anamafanikio zaidi kuliko huyu?
· Nitapajaje wateja wengi kila siku?
Majibu ya maswali yako yote ya kwanini na kivipi ni rahisi tu, zifuatazo ni mbinu zinazoweza kukuwezesha kufanikiwa sana katika biashara yako ya vinywaji au 'BAR'.

1.Fanya Maandalizi ya awali {Weka nia na malengo ya biashara yako (Ni vema Ukiandika)}
Ili kufanikiwa katika biashara hii kama ilivyo katika biashara nyingine yoyote,kitu cha kwanza kufanya ni kuweka nia na malengo au matarajio yako baada ya muda fulani. Kwa mfano, lengo lako la kwanza linaweza kuwa baada ya miezi sita, biashara hii iwe imekuzalishia faida kubwa inayoweza kutosha kuwa kama mtaji wa kufungua biashara nyingine n.k.
Ni lazima pia kuainisha mahitaji yote yanayohitajika kuanzisha biashara yako ikiwemo gharama ya ujenzi, malipo ya wahudumu (kwa miezi sita ya mwanzo), jinsi ya kufanya malipo, Gharama za bidhaa (vinywaji), friji, vyombo na samani za kukalia wateja.
Umakini wa hali ya juu unahitajika katika kufanya upembuzi yakinifu wa gharama za mahitaji ya biashara na muda wa kutosha pia unahitajika ili kupata bei sahihi.

2.Jiandae kiuchumi
Baada ya kufanya maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kufahamu kiasi cha pesa kinachohitajika ili kuanda biashara bila mawaa yoyote, sasa unaweza kujiandaa kiuchumi kwa kukusanya taratibu na kudunduliza pesa kwa ajili ya kufungua biashara (bar). Kama pesa ipo tayari ni vema kuihifadhi vyema na kuhakikisha haiingiliani na matumizi mengine.

3.Chunguza eneo unalohitaji kufanyia biashara
Eneo unalohitaji kuweka bar yako linanakiwa kuwa sehemu ambayo imezungukwa na wahitaji wa aina ya vinywaji unavyotaka kuuza. Kwamfano, eneo liwe sehemu ambayo ni rahisi watu kuhitaji kuja kupumzika baada ya kazi au kukutana na marafiki na sio karibu na Makanisa wala Misikiti au eneo lolote ambapo unaweza kuwakera watu wenye misimamo tofauti ya kiimani.

4.Jenga Bar yako kwa jinsi ya kumvutia macho ya mteja (kistarehe)
Wateja wengi hupenda bar yenye mandhari mazuri ya kuvutia macho ikiwa ni pamoja na usafi wake na mpangilio wa counter, maeneo/vyumba vya kunywea na sehemu za starehe nyingine kama 'pool table' na Muziki/Tv. Vyoo pia vinatakiwa kuwa visafi muda wote ili kuvutia wateja kuendelea kuja katika bar yako kila watakapohitaji kunywa.

5.Ajiri wahudumu wenye mwonekano na lugha nzuri ya biashara
Kufanikiwa kwa Biashara kunategemea sana mahusiano kati ya wateja na watoaji wa huduma. Wahudumu wa Bar yako wanatakiwa kuwa wenye mwonekano na lugha nzuri kwa wateja, wasafi,wakarimu na wasiowahi kukasirika wakati wa kuwahudumia wateja. Wahudumu wenye sifa zilizotajwa hapo juu wanafaa na ndio hitaji la wateja wako wengi kama si wote.

6.Hakiki hesabu za mauzo ya kila siku
Unatakiwa kufanya hesabu za mauzo yanayokusanywa kila siku na kufahamu aina za vinywaji vilivyonunuliwa (kila aina kwa idadi yake). Uhakiki wa hesabu za mauzo ya kila siku yatakupa wastani wa mauzo ya kawaida kila siku, kwa wiki,mwezi na mwaka. Yanakupa pia uwezo wa kukadiria mauzo ya chini kabisa (minimum) na mauzo ya juu kabisa (maximum) kwa siku. Hii inakusaidia wewe kuweka malengo na faida unayoipata katika biashara yako.
Ni vizuri kuweka rekodi ya kila mauzo kwa maandishi ili kurahisisha tathmini yoyote inayoweza kufanywa kwa minajili ya kuboresha biashara.

7.Chunguza vitu wanavyopenda na vinavyowachukiza wateja wako
Ni rahisi kufahamu wateja wanapenda nini na wanachukia nini. Kwa upande wa vinywaji,ni wazi kuwa vile vinywaji vinavyowahi kuisha kuliko vingine ndivyo vinapendwa na wateja na inabidi viwepo vingi vya kutosha. Kuhusu ubora wa huduma, unaweza kuongea na wateja wako (wenye busara) moja kwa moja ili kutoa kero zao ili zile zinazorekebishika zirekebishwe maramoja ili kuepuka kupoteza wateja ambao ndio muhimiri wa biashara yako.

8.Epuka urafiki na mikopo kazini
Hii inawahusu wote, wewe mwenye bar, meneja na wahudumu. Biashara nyingi zinakufa au hazizai matunda tarajiwa kutokana na urafiki na mikopo mingi. Katika bar yako ni vema ifahamike kwa wote kuwa Ofa na mikopo isiyo na ulazima sio njia sahihi za uendeshaji wa biashara. Weka taratibu za wazi kuhusu kukata kwenye posho,malipo au mshahara ya mfanyakazi yeyote ambaye kwa uzembe wake mwenyewe au makusudi amesababisha upungufu katika mauzo ya kawaida ya kila siku.

9.Ubunifu na upekee katika biashara ya 'Bar' ni muhimu
Jitahidi kuwa na ubunifu wa pekee ili kufanya biashara yako kuwa tofauti na wengine. Kwa mfano, unaweza kuandaa tamasha dogo la muziki, urembo au vichekesho katika bar yako ambapo kiingilio chake ni kununua ki/vinywaji tu. Huu au ubunifu mwingine wowote utakukuzia biashara yako kwa kasi kubwa kama utakuwa makini kuwa utekelezaji wa ubunifu usigharimu zaidi ya faida unayoweza kupata.

10.Pokea ushauri na maoni kutoka kwa watu wengine
Unatakiwa kuacha masikio yako wazi kwa ajili ya kupokea kila wazo litakalolenga uboreshaji wa biashara yako wa Bar kutoka kwa wazoefu wa biashara ya namna hii au hata washauri wengine. Kuwa makini pia katika kutekeleza ushauri unaopewa kwani si wote wanaokupa uashauri wanakutakia mema katika mafanikio yako na wala si wote wanaokutakia mabaya katika biashara yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kati ya watu weledi wasio wachoyo wa mawazo ambao nimewahi kukutana nao naweza kudeclare leo nimeongeza mmoja muhimu. Stay blessed mkuu

Hakikisha baada ya mwezi, unaingiza mzigo mpya wa wahudumu wenye sifa ulizotaja na wengine wawe tayari kwenda the extra mile na wateja wao!
 
Habari Jf, naomba kuelekezwa haya kuhusiana na biashara ya kuuza soda za jumla

Ni mtaji kiasi gani unahitajika ili niweze kufungua biashara hii ya kuuza soda kwa jumla?

Depot hii nahitaji iwe ya kawaida, yaani kiwango cha chini kabisa nitenge kiwango gani cha milions
Lakini pia, ningependa kufahamu ni changamoto, faida na hasara katika biashara hii

Hatua zipi nahitaji kuzipitia niweze kuunganishwa na makampuni ya soda eg pepsi

Chupa na kreti nazipata vp and kwa kuanzia natakiwa niwe na mzigo wa kreti ngapi?
 
Kuna Uzi upo humu was hayo mambo utafute

Mpe anae kupa
 
Wakuu naomba kuunganishwa na wadau wanaofanya kazi katika kampuni za vinywaji baridi (non alcohol) kama vile mo, azam, Sayona, Masafi, Afya,

Pia naomba kama mtu anauzoefu na biashara husika aniambie magumu na mazur yaliyoko kwa hiyo biashara tajwa hapo juu
 
Iyo biashara iyo tafuta sehemu yenye mzunguko mkubwa ndo utaiweza na kama utajitahidi usiuze vinywaj pekee uza bidhaa zote za azam au mo la sivyo loss, haina faida kabisa kile kitin cha maji faida yake mia mbili,
 
Well said mi nilifanyaga utafiti nikaligundua hilo, usione MTU kazungukwa vinywaji ukafikiri anapiga hela kumbee
 
Back
Top Bottom