Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

Umefikia wapi mkuu
 
Japokua nimechelewa sana kuiona post yako lakini kama bado ujaanza nitaweza kukushauri baadhi ya vitu. Mimi nauzoefu wa zaidi ya miaka kumi kwenye hiyo biashara lakini ni kwa Dar es salaam.
 
Reactions: ram
Kwanza lazima nijue unamtaji kiasi gani, pili biashara ya makreti itakusumbua kama mtaji wako nimdogo kwani kreti 100 huwezi kua agent Bali utanunua kwama agent na faida itakua ndogo. Ila ushauri wangu deal na box tu kama mtaji ni mdogo.
 
Reactions: ram
Kwanza lazima nijue unamtaji kiasi gani, pili biashara ya makreti itakusumbua kama mtaji wako nimdogo kwani kreti 100 huwezi kua agent Bali utanunua kwama agent na faida itakua ndogo. Ila ushauri wangu deal na box tu kama mtaji nimdogo.

Kaka nahitaji ufahamu kidogo wa biashara hii u naweza nisaidia.
 
Habarini wana jukwaa,

Jamani mwenzenu nawaza kufanya biashara ya vinywaji ila sijajua vinywaji gani vinafaida na vinauzika haraka hapa.

Nipo kwenye mchakato wa kutafuta mtaji angalau milioni 1, sasa wataalam wa biashara niambie ni vinywaji gani vitauzika sana kwa wanywaji?
 
Uko wapi na je location uliyopo ikoje? Washindani wako wakoje na mitaji yao ikoje? Vp hali ya upatikanaji wa umeme hapo ulipo fanya utafiti wa hivyo vitu kwanza
 

Habari mkuu,niliwahi kupitia nyuzi fulani huko nyuma juu ya biashara ya soda kwa ujumla,vipi mdogo wako alieendelea maana nilikaa kimya kusubiri mrejesho wa mtu aliyekuwa ameeomba ushauri kama alijaribu au aliibadilisha maamuzi hakurejea,hebu nifahamishe anaendeleaje jamaa yako? na ikibidi ningependa kupata mawasiliano naye maana nina pesa kiasi fulani nafikiria kuifanya hiyo biashara.
 
Tafadhali kama unauwelewa au unafanya biashara ya kuuza vinywaji kwa bei ya jumla nahitaji msaada wako, vinywaji kama maji, juice, soda n.k mtaji niliokuwa nao ni 1.5m naomba kujua inalipa vipi hii biashara, msaada ndugu zangu au je kwa mtaji tajwa hapo juu naweza fanya biashara gani nikaishi hapa mjini bila kudhalilika

Nakaribisha ushauri, mchango, maoni n.k
 
mkuu nakushauri ungenunua boda boda tu halafu chukua 50 kwa wiki itakulipa sana. sidhani kama biashara ya vinywaji utapata faida hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…