Ushauri kuhusu uchaguzi wa godoro bora

Ushauri kuhusu uchaguzi wa godoro bora

Wakubwa,nipo kwenye mchakato wa kununua godoro zuri. Baada ya kufuatilia kwa kina nikagundua godoro la Spring la Tanfoam ndio the best. Sasa baada ya kufika kwa wakala kununua,nimekuta kuna godoro lingine premium,halina spring lakini linanesa sana na bei yake ni juu kidogo kuliko la Spring. Nimegundua nahitaji kupata uzoefu kwa watumiaji kabla sijajunua. Karibuni kushare experience.
Upo wapi mkuu?
 
Godoro langu lilinesa nesa siku ya kwanza kulalia ila baada ya hapo ni majanga na limekuwa ulimi kinoma .Nliambiwa ni tanform nkatoa 150k,kuja kusoma vizuri limeandikwa Dodoma sijui nn...kuwa makini mkuu usiuziwe fyamba
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]gogoro n kuanzia laki nne kwenda mbele

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Tanform Walinipigia Wakaniambia Popote Ulipo Tanzania Wana Mawakala Wao
Unachofanya Unawasiliana Arusha Unapewa Ya Kiwandani Unaelekezwa Ulipo Na Wakala Wao Unabeba
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mkuu chukua godoro Dodoma hutajuta, nafikiri ina lifetime guarantee maana mimi nimetumia zaidi ya miaka 15 na hayaonyeshi dalili ya kuchakaa.
Dodoma ndo best miaka buku.
 
Mkuu chukua godoro Dodoma hutajuta, nafikiri ina lifetime guarantee maana mimi nimetumia zaidi ya miaka 15 na hayaonyeshi dalili ya kuchakaa.
Inategemea na Dodoma upi
 
Hilo godoro la tanfoam la spring silielewagi kabisa.

Yaani unalala kama unaelea vile na zile spring zinaumiza pia.
 
Back
Top Bottom