Vhukua CBR600 itakufaa sana, hakikisha unavaa safety gears kwa kila safari unayotoka hata kama sio mbali.
Kuhusu uendeshaji, utazingatia tu kwamba hiyo ni sport bike, ina nguvu kubwa tofauti na bike ya kawaida. Anza kwa kuiendesha mdogomdogo usivuke speed 60kph kwa muda wa week moja, alafu baada ya hapo utaanza kuongeza speed mdogo mdogo kadri unavyozidi kuielewa na kuizoea bike.
Katika mwezi mmoja tu wa mwanzo utaweza kuifahamu na kuielewa vizuri bike yako, kuanzia torque, balance kwenye corner na namna inavyo react unaposhika brakes n.k
Usiogope mkuu, ni jitihada na umakini tu.