Ushauri; Kuna dada nampenda sana lakini hayuko tayari kuwa na mimi

Ja Mara

Member
Joined
Aug 19, 2021
Posts
44
Reaction score
44
Habari Wana JF,

Mimi ni kijana wa miaka 24 Kiukweli nashindwa Kumdanganya Mwanamke nina mapenzi ya dhati kwa mtu ninaempenda kweli. Ni mara ya pili naingia kwenye Mausiano baada ya nilie kuwanae kuniwekea masharti kwenye chakula cha mwili baada ya kumvumilia kwa miezi tisa.

Kazi ipo kwa huyu wa sasa,
Kuna Mdada nilikutananae katika kuwasiliana kwetu nilimwambia kilichopo moyoni, baada ya wiki moja nilikutananae kumwonyesha hisia zangu uso kwa uso. Ambapo alinieleza kuwa na yeye awezi kumdanganya mwanaume akipenda amependa. mungu ni mwema Alifunguka na kuniambia ananipenda, Lakini kwenye mazungumzo alinieleza historia yake ya mausiano yuko Kama mimi aliumwizwa na "X" wake. kwakuwa wote tuko Single tumekutana tunapendana Baasi moyoni nilifrai saana nikatambua jukumu langu kubwa kama mwanaume ni kumfanya aweze kumsahau "X" wake .

Nilijitahidi kweli kumjali kilichotokea juzi Tarehe 17.02.2022 usiku saa 09:45 nilikuta Kaniblock kwenye call na kuniachia text zifuatazo

"Jina langu.., am really sorry 😔. Sitaki Kukuumiza kwa Upendo wako me sitaki mpenzi moyo wangu bado unamaumivu."
"Am sorry Sitaki kukupotezea muda kwako sina hisia za mapezi tena."

Moyo wangu ulisinyaa ghafla kama hini lililo mwagiwa gongo. nilitoka nyumbani mda uleule na kupanda pikipiki kwenda mtaani kwao anapoishi na kujaribu kuulizia watu wa pale anapokaa sikufanikiwa kwa kweli kwakuwa siku ile sikupata nafasi ya kujua nyumba anayokaa kinyooonge nilirudi nyumbani. but nyuma aliniaidi kuwa tarehe 27.02.2022 Atanipatia Zawadi ya Valentine day nami nilimwaidi hiyo siku atapata zawadi kutoka kwa valentine boy wake ambae ni mimi.

Dah nifanye nini?? mwenzenu nampenda ya Kikwelii
 
Hizo sms alizokutumia ni kama mwandiko wa demu wangu juzi nilimchatisha kisha jana akaja ghetto
Kama ni mnene wa wastani, anaishi mabibo na mdogo wake basi ni demu wangu
 
Siyo kakuambia ukweli
 
Hii habari yako ipeleke Facebook, mimi siwezi kushauri huu utoto, bado unakuwa utajifunza mengi. Amua utakachoamua dogo..
 
Mapenzi hayalazimishwi hatk Mwache aende!! Utampata mwingine wakukupenda najua saisa hivi unaona haiwezekani Ila jipe muda dogo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…