Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Membe ndiye mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM mwaka huu ni suala la muda tuDisclaimer;
Mtoa ushauri huu ni mwana CCM anayeamini katika demokrasia. Anaamini CCM imara itatokana na uwepo wa upinzani bora kwa kuwa CCM itapata kioo cha kujitazama, na kufa kwa upinzani kutasababisha CCM isiwe na pa kujipimia na hivyo ubora wake kuyumba.Kama Simba ikipotea kabisa, hatuwezi kuwa na Yanga tunayoijua leo, bali tutakuwa na kitu kingine kabisa.
Hivyo ushauri huu haulengi kusaidia vyama vya upinzani kushinda kiti cha urais Tanzania bara kwa kuwa hilo kwa sasa haliwezekani (kutokana na sababu mbalimbali) lakini angalau kusaida vyama hivyo kubaki kwenye ramani baada ya uchaguzi wa oktoba.
================
‘Facts nne (4) za wazi sana (Hizi ukiona mtu anabisha ni kwa kuwa tu anatumia uhuru wake wa kidemokrasia. Ni kama mtu anavyoweza kubisha kuwa dunia sio duara)
Kwanza, kwa hali ilivyo kuna dalili za wazi sana kwa CHADEMA kupoteza karibu viti vyote vya ubunge bara, na Zbar hawana dalili ya kupata kiti hata kimoja.(ili kuepuka kutanua sana mjadala hatutajadili sababu moja moja kwa kuwa zipo wazi sana tayari)
Pili, ACT wana dalili ya kutopata kiti hata kimoja bara lakini kupata viti kadhaa Zbar
Tatu, kwa upande wa urais bara, Rais Magufuli ana uhakika wa kishinda kwa 99%. Kwa sababu ambazo pia ziko wazi sana. na
Nne, Vyama vya upinzani vyenye ushawishi kiasi kwa bara kwa sasa ni CHADEMA na ACT, wengine ushawishi wao uko chini sana.
Kwa nini CHADEMA wamsimamishe Membe na ACT wasisimamishe mgombea?
Kwanza, Lissu ndie mpinzani pekee anayeweza kum challenge rais Magufuli kwa kiasi fulani, japo pia hawezi kumshinda kwa sababu mbalimbali. Kwa bahati mbaya lisu yuko ulaya na ndege haziruki kutoka ulaya kwa sasa. Kwa hiyo upo uwezekano ukafika wakati wa kuchukua fomu na Lissu kakwama ulaya.
Pili, kuhusu mbowe; kwa tukio lililotokea Dodoma, iwe maelezo yaliyotolewa kwa upande wa polisi ndio kweli au maelezo yaliyotolewa upande wa Mbowe ndio kweli; tukio kama lile kutokea kwenye kipindi hiki linamfanya Mbowe kuonekana hayuko serious vyakutosha na hivyo sio ‘presidential material’.
Tatu , kuhusu Msigwa; Kwa tukio la kumsingizia mzee Kinana kuwa anaua tembo (huku akijua ametunga tu kichwani kwake kwa hila) na asiombe msamaha kwa miaka na miaka hadi ahukumiwe mahakamani huku akijua anasababisha usumbufu usio wa lazima, linamfanya asiwe ‘presidential material’.
Nne, kuhusu Nyalandu; huyu kalelewa na CCM, kawa waziri wa muda mrefu na hana ushawishi wa kutosha kwenye level ya urais Tanzania bara.
Tano, Kuhusu Zitto; kwa sababu mbalimbali kiwango chake cha kuaminika kimepungua kwa sababu mbalimbali. Hivyo, akigombea urais hawezi kupata hata 10% ya kura. Aidha, hataungwa mkono na CHADEMA, na ndani ya ACT hakuna mtu mwingine ambaye ni ‘presidential material’ kwa Tanzania bara anayeweza kuwa na ushawishi zaidi ya Zitto.
Kwa nini Membe?
Kwa sababu ukimuacha Lisu, upande wa vyama vya upinzani hakuna mtu mwingine Tanzania bara mwenye haiba ya urais inayomkaribia Membe. Kwa mantiki hiyo, ijapokuwa Membe hatamshinda Rais Magufuli; angalau atasaidia CHADEMA kujipatia % fulani la kura ambayo itasaidia waendelee kupata ruzuku japo kidogo na uwepo wao uendelee kuonekana.Ikombukwe hapo tayari watakuwa washapoteza viti karibu vyote vya ubunge!
Ingawa ni kweli kwamba Membe bado anaiwazia CCM, lakini ni kweli pia kwamba kwa sasa hana uwezekano tena wa kugombea kupitia CCM. Sasa kwa kuwa tatizo la Tanzania sio CCM kama chama bali mtu mmoja mmoja, CHADEMA wakimtumia Membe ili awabusti sio jambo baya kwa kuwa ana haiba chanya zaidi ukilinganisha na wengine wengi waliotajwa hapo juu.
Kwa upande wa ACT, viti kadhaa watakavyopata Zbar, vitawasaidia kuendelea kuonekana na kupata ka - ruzuku kidogo katakako wasaidia ku ‘savaivu’.
Najua wapo watakaobisha, kutukana, na kubeza ushauri huu, ila ushauri huu unazingatia zaidi ‘facts’ ziwe za kuvutia au za kuudhi. Ni hiari ya wahusika kuufuata na wapate namna yenye uafadhali ya kuendelea ku ‘savaivu’ kwenye kipindi cha 2021 -2025, au wapuuze halafu wawe kama TLP, NLD n.k Kama watapuuza na kufikia hatua hiyo, CCM itakosa pakujitizama hiyo nayo utendaji wake unaweza kuathirika kwa namna hasi na kwa kuwa kitakuwa ndicho chama kinachounda serikali, taifa nalo linaweza kukabiliwa na changamoto kadha wa kadha ambazo pengine zingeepukika kwa kufuata ushauri huu.
Kuna wazo kwamba CCM inaweza ikaamua kuwaachia vyama vya upinzani viti kadhaa kwa makusudi ili viendelee kuwepo. Hiyo ni kweli lakini sishauri vyama vya upinzani kutegemea favor kutoka CCM. Wanaweza wasipewe hiyo favor na ikawagharimu sana.
Mtu anaweza kusema kwa nini vyama vya upinzani visipewe ushauri utakaowawezesha kushinda? Jibu ni kwamba ushauri huo walishapewa sana na kuelezwa kwamba pamoja na changamoto za nje zinazowakabili, changamoto kubwa zinazowakwamisha ziko ndani ya vyama vyao wenyewe. Kwa bahati mbaya hilo hawajaliamini hadi sasa na kwa kuwa hawajaliamini na wanadhani changamoto zinazowakabili ni ‘100% external’; hawajachukua hatua na muda uliobaki ni mfupi mno ambao hauwezi kuwatosha tena. Ndio maana ushauri unaowezekana kwa sasa anagalau ni ule wa kuwawezesha waendelee ku ‘savaivu’ lakini sio kushinda.
Tunawashukuru sana kwa kuelewa.
Mkuu, kuna vitu unaweza kuwa unatamani viwe na kuna vile inavyowezekana kuwa. Kwa mfano , unaweza kutamani kuwa Tajiri mwenye Akiba ya 1B kwenye account yako lakini kinachowezekana ni kupata hela ya mhogo tu. Sasa hatusemi unachotamani ni kibaya, tatizo unatamani bila kuzingatia kinachowezekana kulingana na mazingira yako.Ushauri ungetolewa kuwe na tume huru ya uchaguzi tu, Magu atashindwa hata na mwanasiasa yeyote asie na jina wa upinzani.
Magu, hajui kujieleza, hana busara ya uongozi, mipango yake ya uchumi imeshindwa vibaya, ubabe usio na akili n.k
Ushauri wake umekaa kimatako zaidiUshauri wako mwana ccm umekaa ki ccm ccm! Yaani CHADEMA imsimamishe Membe ambaye yupo ccm!? Au unafikiri CDM ni kama wale TLP sijui NLD waliotangaza kumpitisha stone awe mgombea wao?
Unamkandia Nyalandu kuwa kalelewa ccm huku ukimpigia chapuo Membe ambaye si tu kalelewa ccm, bali bado yupo ccm!
Kwani hilo likifanyika, itakuwa ndio mara ya kwanza? anyway ni ushauri tu, ushauri sio amri. Na sisi wengine ni vidagaa tu, kwa hiyo wakati mwingine mawazo yetu ni kama mapovu ziwani.
Ungejibu hoja zilizotolewa ingependeza zaidi kuliko kulaumu tu kijumla jumla. Kwa mujibu wa Mzee Kikwete, hoja huwa hazipigwi rungu.Nimeshangaa. Halaf anae toa ushauri ni mwana ccm?
Like seriously?
Mm si mwanasiasa lakin huyu jamaa anawaona wapinzani kama watoto fulani wa hovyo.
Kuhusu Mbowe, je ikitolewa CCTV Camera ikaonesha tofauti na unavyofikiri utaendelea kuwa huu nsimamo wako?
Msigwa kukosea akaomba samahani sio dhambi, ni nani asiekosea huko ulipo?
Kuliko Membe apewe hiyo nafasi bora apewe yeyote aliejitokeza kuchukua form Chadema.
Kwani Lowasa hakuwa mwana CCM 2015?Duh...!.
Yaani wapinzani wamsimamishe mwana CCM kuwa mgombea wao!. Hii kali!.
P
Hapa wataangalia nani kaweka mgombea wapi, kama ACT wakimsimamisha Seif Zanzibar, itakuwa zamu ya CDM kumsimamisha mgombea wao Bara, hakuna ubinafsi wala nini.CDM wameshafunga zoezi la kutia nia toka 15th June 2020,(Kosa la kiufundi) kumchukua Membe leo au kesho litatoa tafsiri ya kutapata tu.
ACT wao bado mlango wazi kwa Membe ila CDM kumuunga mkono Membe akiwa ACT na wao kutokuweka mgombea hawawezi (Ubinafsi)
Bora wakomae ni ubunge zaidi!
Mkuu, 'voluntary actions' zote mtu anakuwa anazitambua kabla hata ya kuzifanya. Kwa hiyo wakati mtu anafanya, anakuwa alishatambua tayari. Kwa mfano, wewe ulijua unachotaka kukiandika hapa kabla ya kukiandika. ukiamua kupiga mtu ngumi, unakuwa unajua kwamba sasa unarusha ngumi kabla ya kurusha.Hapa cha muhimu tujue kitu kimoja, huko "kumsingizia" alikutambua muda gani,
Dharau ya hali ya juu kabisaDuh...!.
Yaani wapinzani wamsimamishe mwana CCM kuwa mgombea wao!. Hii kali!.
P
Hapana Mkuu Aziz Mussa, nimesoma kwa makini hoja zako zote ziko very logical isipokuwa hili la Membe.
Membe ni mwana CCM, japo ilitamkwa kuwa emefukuzwa ila mpaka kesho hajapewa barua rasmi ya kufukuzwa na hajatamka kuacha CCM, sasa why wapinzani wawaze kusimamisha mtu ambae wala sio mwanachama wao?.
P
Kwa wapenda demokrasia, udumavu au kufa kwa vyama vya siasa sio jambo la kufurahisha, kwa sababu hilo likitokea litapelekea siasa kupoa sana.
Alijitoa CCM na kujiunga Chadema. Membe bado ni CCM, hajajitoa na hawezi kujitoa.Kwani Lowasa hakuwa mwana CCM 2015?
CrapDisclaimer;
Mtoa ushauri huu ni mwana CCM anayeamini katika demokrasia. Anaamini CCM imara itatokana na uwepo wa upinzani bora kwa kuwa CCM itapata kioo cha kujitazama, na kufa kwa upinzani kutasababisha CCM isiwe na pa kujipimia na hivyo ubora wake kuyumba.Kama Simba ikipotea kabisa, hatuwezi kuwa na Yanga tunayoijua leo, bali tutakuwa na kitu kingine kabisa.
Hivyo ushauri huu haulengi kusaidia vyama vya upinzani kushinda kiti cha urais Tanzania bara kwa kuwa hilo kwa sasa haliwezekani (kutokana na sababu mbalimbali) lakini angalau kusaida vyama hivyo kubaki kwenye ramani baada ya uchaguzi wa oktoba.
================
‘Facts nne (4) za wazi sana (Hizi ukiona mtu anabisha ni kwa kuwa tu anatumia uhuru wake wa kidemokrasia. Ni kama mtu anavyoweza kubisha kuwa dunia sio duara)
Kwanza, kwa hali ilivyo kuna dalili za wazi sana kwa CHADEMA kupoteza karibu viti vyote vya ubunge bara, na Zbar hawana dalili ya kupata kiti hata kimoja.(ili kuepuka kutanua sana mjadala hatutajadili sababu moja moja kwa kuwa zipo wazi sana tayari)
Pili, ACT wana dalili ya kutopata kiti hata kimoja bara lakini kupata viti kadhaa Zbar
Tatu, kwa upande wa urais bara, Rais Magufuli ana uhakika wa kishinda kwa 99%. Kwa sababu ambazo pia ziko wazi sana. na
Nne, Vyama vya upinzani vyenye ushawishi kiasi kwa bara kwa sasa ni CHADEMA na ACT, wengine ushawishi wao uko chini sana.
Kwa nini CHADEMA wamsimamishe Membe na ACT wasisimamishe mgombea?
Kwanza, Lissu ndie mpinzani pekee anayeweza kum challenge rais Magufuli kwa kiasi fulani, japo pia hawezi kumshinda kwa sababu mbalimbali. Kwa bahati mbaya lisu yuko ulaya na ndege haziruki kutoka ulaya kwa sasa. Kwa hiyo upo uwezekano ukafika wakati wa kuchukua fomu na Lissu kakwama ulaya.
Pili, kuhusu mbowe; kwa tukio lililotokea Dodoma, iwe maelezo yaliyotolewa kwa upande wa polisi ndio kweli au maelezo yaliyotolewa upande wa Mbowe ndio kweli; tukio kama lile kutokea kwenye kipindi hiki linamfanya Mbowe kuonekana hayuko serious vyakutosha na hivyo sio ‘presidential material’.
Tatu , kuhusu Msigwa; Kwa tukio la kumsingizia mzee Kinana kuwa anaua tembo (huku akijua ametunga tu kichwani kwake kwa hila) na asiombe msamaha kwa miaka na miaka hadi ahukumiwe mahakamani huku akijua anasababisha usumbufu usio wa lazima, linamfanya asiwe ‘presidential material’.
Nne, kuhusu Nyalandu; huyu kalelewa na CCM, kawa waziri wa muda mrefu na hana ushawishi wa kutosha kwenye level ya urais Tanzania bara.
Tano, Kuhusu Zitto; kwa sababu mbalimbali kiwango chake cha kuaminika kimepungua kwa sababu mbalimbali. Hivyo, akigombea urais hawezi kupata hata 10% ya kura. Aidha, hataungwa mkono na CHADEMA, na ndani ya ACT hakuna mtu mwingine ambaye ni ‘presidential material’ kwa Tanzania bara anayeweza kuwa na ushawishi zaidi ya Zitto.
Kwa nini Membe?
Kwa sababu ukimuacha Lisu, upande wa vyama vya upinzani hakuna mtu mwingine Tanzania bara mwenye haiba ya urais inayomkaribia Membe. Kwa mantiki hiyo, ijapokuwa Membe hatamshinda Rais Magufuli; angalau atasaidia CHADEMA kujipatia % fulani la kura ambayo itasaidia waendelee kupata ruzuku japo kidogo na uwepo wao uendelee kuonekana.Ikombukwe hapo tayari watakuwa washapoteza viti karibu vyote vya ubunge!
Ingawa ni kweli kwamba Membe bado anaiwazia CCM, lakini ni kweli pia kwamba kwa sasa hana uwezekano tena wa kugombea kupitia CCM. Sasa kwa kuwa tatizo la Tanzania sio CCM kama chama bali mtu mmoja mmoja, CHADEMA wakimtumia Membe ili awabusti sio jambo baya kwa kuwa ana haiba chanya zaidi ukilinganisha na wengine wengi waliotajwa hapo juu.
Kwa upande wa ACT, viti kadhaa watakavyopata Zbar, vitawasaidia kuendelea kuonekana na kupata ka - ruzuku kidogo katakako wasaidia ku ‘savaivu’.
Najua wapo watakaobisha, kutukana, na kubeza ushauri huu, ila ushauri huu unazingatia zaidi ‘facts’ ziwe za kuvutia au za kuudhi. Ni hiari ya wahusika kuufuata na wapate namna yenye uafadhali ya kuendelea ku ‘savaivu’ kwenye kipindi cha 2021 -2025, au wapuuze halafu wawe kama TLP, NLD n.k Kama watapuuza na kufikia hatua hiyo, CCM itakosa pakujitizama hiyo nayo utendaji wake unaweza kuathirika kwa namna hasi na kwa kuwa kitakuwa ndicho chama kinachounda serikali, taifa nalo linaweza kukabiliwa na changamoto kadha wa kadha ambazo pengine zingeepukika kwa kufuata ushauri huu.
Kuna wazo kwamba CCM inaweza ikaamua kuwaachia vyama vya upinzani viti kadhaa kwa makusudi ili viendelee kuwepo. Hiyo ni kweli lakini sishauri vyama vya upinzani kutegemea favor kutoka CCM. Wanaweza wasipewe hiyo favor na ikawagharimu sana.
Mtu anaweza kusema kwa nini vyama vya upinzani visipewe ushauri utakaowawezesha kushinda? Jibu ni kwamba ushauri huo walishapewa sana na kuelezwa kwamba pamoja na changamoto za nje zinazowakabili, changamoto kubwa zinazowakwamisha ziko ndani ya vyama vyao wenyewe. Kwa bahati mbaya hilo hawajaliamini hadi sasa na kwa kuwa hawajaliamini na wanadhani changamoto zinazowakabili ni ‘100% external’; hawajachukua hatua na muda uliobaki ni mfupi mno ambao hauwezi kuwatosha tena. Ndio maana ushauri unaowezekana kwa sasa anagalau ni ule wa kuwawezesha waendelee ku ‘savaivu’ lakini sio kushinda.
Tunawashukuru sana kwa kuelewa.
Mkuu, hilo suala la tume limekuwa likizungumzwa sana miaka na miaka hatua zilizochukuliwa na ambazo hazikuchukuliwa na kwamba nani kafanya nini wote tunajua, unaamini kabisa kwamba kuna tume tofauti itakayosimamia uchaguzi tofauti na iliyopo? Unaamini kabisa kwamba kinachoitwa tume mpya ambayo haijaweza kuwepo miaka yote ambayo imeanza kuzungumziwa, inaweza kuwepo sasa ndani ya mwezi mmoja? unaamini hao unaowaambia wasishiriki uchaguzi hawatashiriki? na huoni wasiposhiriki wengine watashiriki na wasioshiriki watakuwa ndio wanapotea hivyo?Siwashauri wapinzani wa kweli kushiriki uchaguzi huu kwa tume hii isiyo huru ya uchaguzi. Hamna lililo nje ya ukweli huu.
Mawazo yako siyo kabisa . Bila unafki wahamiaji wameisumbua sana Cdm. Unakuwa na wabunge ndumilakuwili , wa nini hasa ?!.Kwani hilo likifanyika, itakuwa ndio mara ya kwanza? anyway ni ushauri tu, ushauri sio amri. Na sisi wengine ni vidagaa tu, kwa hiyo wakati mwingine mawazo yetu ni kama mapovu ziwani.
Mkuu, hilo suala la tume limekuwa likizungumzwa sana miaka na miaka hatua zilizochukuliwa na ambazo hazikuchukuliwa na kwamba nani kafanya nini wote tunajua, unaamini kabisa kwamba kuna tume tofauti itakayosimamia uchaguzi tofauti na iliyopo? Unaamini kabisa kwamba kinachoitwa tume mpya ambayo haijaweza kuwepo miaka yote ambayo imeanza kuzungumziwa, inaweza kuwepo sasa ndani ya mwezi mmoja? unaamini hao unaowaambia wasishiriki uchaguzi hawatashiriki? na huoni wasiposhiriki wengine watashiriki na wasioshiriki watakuwa ndio wanapotea hivyo?
Kuna kitu ambacho huwa tunakisema mara kwa mara, vile mtu anavyoweza kutamani iwe 'Wishful thoughts' na vile inavyowezekana kuwa ' Possibilities'
Ni sawa na tunatamani tuwe na viongozi flani hivi wenye sifa flani flani hivi, lakini swali ambalo huwa wengine tunauliza, watu hao tunao kwenye jamii yetu? kwama hatuna, kwa nini tufikiri tutawapata kwenye vyama? au tunatamani tu, bila kuangalia uwezekano?
Na mwisho kushinda uchaguzi ni jambo moja, jambo la pili ni haiba ya anayeshinda. Ndio maana kwenye uzi wa msingi tumejaribu kugusia kidogo suala la haiba.