Uchaguzi 2020 Ushauri kunusuru upinzani ‘kidharura’: CHADEMA msimamisheni Membe, ACT msiweke mgombea bara; Haitawapa ushindi ila itawasaidia kuendelea ku 'savaivu'

Uchaguzi 2020 Ushauri kunusuru upinzani ‘kidharura’: CHADEMA msimamisheni Membe, ACT msiweke mgombea bara; Haitawapa ushindi ila itawasaidia kuendelea ku 'savaivu'

Nashukuru umenielewa na ndio maana ukajibu.

Mara ya mwisho nimeitwa baby baada ya kumbanjua demu mmoja mkali usiku kucha, today is the second time

Thanks sweetie
Kumbe demu wangu una demu, huwa namuita baby "niliemkaza".

Don't waste my time next time, usinilazimishe kuwa na akili ndogo kama zako, niletee mwingine kwenye kundi lenu.
 
Hatusemi kwamba Vyama vya upinzani havitaweza kuongoza bali tunasema ufanisi wao utakuwa wa chini sana ukilinganisha na wa CCM. Hili hatusemi tu kwa kuwa tunataka kusema bali kwa viashiria vya wazi sana. Nitatoa mifano michache;

Kwa mfano, tunaona kwenye vyama hivyo, vinashindwa ku control vitu vidogo sana vilivyo ndani ya uwezo wao. Kwa mfano Chadema kwa zaidi ya miaka 20, imeshindwa angalau tu kujenga ofisi ya makao makuu, sasa jiulize kama hilo tu limewashinda, kwa nini tudhani wataweza kuongoza nchi kwa ufanisi zaidi ya CCM?

Kwenye vyama vya upinzani havina dola ila kuna viongozi wanang'ang'ania madarakani, kwa nini tudhani wakiwa na dola hawatang'ang'ania?

Kuna viongozi wametoka huko wakahamia ccm na wakapewa madaraka mbalimbali serikalini, ufanisi wao, hekima na burasa zao tunaziona, na hiyo ndio reflection ya ambavyo ingekuwa ikiwa vyama walikotoka vingekuwa madarakani.

Kwa hiyo hatusemi haviwezi, tunachosema vitakuwa na ufanisi wa chini kuliko CCM kutokana na evidence zilizopo na kwa mantiki hiyo ndio maana tunafikiri bado CCM ni 'comparatively better' hadi sasa na pamoja na vyama hivyo kushauriwa sana kujifanyia maboresho ya ndani ili angalau hata vifikie level ya ccm, bado havijaweza kufanya hivyo.

Azizi Mussa, wewe nadhani una tatizo lako binafsi....

Unatetea jambo hili kwa hoja dhaifu sana zilizo ktk msingi wa HOFU tu. Nimelieleza hili kwa ufasaha hapo juu post #50. Unaweza kurudia kusoma tena....

Labda nikuulize jambo moja. Suppose tungekuwa na mfumo wa wagombea huru (wasio na vyama vya siasa). Akagombea Urais na kushinda. Huyu atawezaje kuongoza serikali?

Sijui wewe utajibu nini. Lakini jibu rahisi ni hili. Tanzania ina watu zaidi ya 55,000,000. Ashindweje mtu huyu kuunda serikali huku taifa likiwa na hazina ya human resources ya zaidi ya milioni 55??....Sijui kama unanielewa...

Hapa hata ndugu John Pombe Magufuli yumo kwenye namba hii ya watu milioni 55 na katika serikali mpya anaweza jikuta ameukwaa uwaziri wa miundonbinu au samaki kwa sababu ya uzoefu na uwezo wake wa kukariri kilometa za barabara na idadi ya samaki na dagaa majini....

Nimefafanua jambo hili vizuri hapo juu ktk post #50, kwamba, mifumo ya kidola na kiutumishi ya nchi iko yoyote static. Yenyewe haiathiriwi na nani ni Rais ama chama gani kimeshinda urais....

Kinachoweza kubadilika ni kidogo ni miundo tu ya taasisi hizi ili kuweza ku - accomodate Sera na mipango ya aliyeshinda....

Kumbuka jambo hili pia, kwamba, wanaotawala nchi ni WANANCHI mwenyewe kupitia kwa mtu aliyewashawishi kwa sera na mipango yake ya atafanya nini iwapo atachaguliwa ktk uchaguzi wowote...

Tukieelewa dhana hii ya demokrasia na kuifanyia kazi kwa uaminifu sawasawa na inavyotakiwa na kuachana na UONGO na UKIRITIMBA tunaolishwa na vyama vya siasa, nchi hii itapiga hatua za haraka sana za maendeleo ya KIJAMII na KIUCHUMI kuliko ilivyo sasa....
 
Disclaimer;

Mtoa ushauri huu ni mwana CCM anayeamini katika demokrasia. Anaamini CCM imara itatokana na uwepo wa upinzani bora kwa kuwa CCM itapata kioo cha kujitazama, na kufa kwa upinzani kutasababisha CCM isiwe na pa kujipimia na hivyo ubora wake kuyumba.Kama Simba ikipotea kabisa, hatuwezi kuwa na Yanga tunayoijua leo, bali tutakuwa na kitu kingine kabisa.

Hivyo ushauri huu haulengi kusaidia vyama vya upinzani kushinda kiti cha urais Tanzania bara kwa kuwa hilo kwa sasa haliwezekani (kutokana na sababu mbalimbali) lakini angalau kusaida vyama hivyo kubaki kwenye ramani baada ya uchaguzi wa oktoba.

================
‘Facts nne (4) za wazi sana (Hizi ukiona mtu anabisha ni kwa kuwa tu anatumia uhuru wake wa kidemokrasia. Ni kama mtu anavyoweza kubisha kuwa dunia sio duara)

Kwanza, kwa hali ilivyo kuna dalili za wazi sana kwa CHADEMA kupoteza karibu viti vyote vya ubunge bara, na Zbar hawana dalili ya kupata kiti hata kimoja.(ili kuepuka kutanua sana mjadala hatutajadili sababu moja moja kwa kuwa zipo wazi sana tayari)

Pili, ACT wana dalili ya kutopata kiti hata kimoja bara lakini kupata viti kadhaa Zbar

Tatu, kwa upande wa urais bara, Rais Magufuli ana uhakika wa kishinda kwa 99%. Kwa sababu ambazo pia ziko wazi sana. na

Nne, Vyama vya upinzani vyenye ushawishi kiasi kwa bara kwa sasa ni CHADEMA na ACT, wengine ushawishi wao uko chini sana.

Kwa nini CHADEMA wamsimamishe Membe na ACT wasisimamishe mgombea?

Kwanza, Lissu ndie mpinzani pekee anayeweza kum challenge rais Magufuli kwa kiasi fulani, japo pia hawezi kumshinda kwa sababu mbalimbali. Kwa bahati mbaya lisu yuko ulaya na ndege haziruki kutoka ulaya kwa sasa. Kwa hiyo upo uwezekano ukafika wakati wa kuchukua fomu na Lissu kakwama ulaya.

Pili, kuhusu mbowe; kwa tukio lililotokea Dodoma, iwe maelezo yaliyotolewa kwa upande wa polisi ndio kweli au maelezo yaliyotolewa upande wa Mbowe ndio kweli; tukio kama lile kutokea kwenye kipindi hiki linamfanya Mbowe kuonekana hayuko serious vyakutosha na hivyo sio ‘presidential material’.

Tatu , kuhusu Msigwa; Kwa tukio la kumsingizia mzee Kinana kuwa anaua tembo (huku akijua ametunga tu kichwani kwake kwa hila) na asiombe msamaha kwa miaka na miaka hadi ahukumiwe mahakamani huku akijua anasababisha usumbufu usio wa lazima, linamfanya asiwe ‘presidential material’.

Nne, kuhusu Nyalandu; huyu kalelewa na CCM, kawa waziri wa muda mrefu na hana ushawishi wa kutosha kwenye level ya urais Tanzania bara.

Tano, Kuhusu Zitto; kwa sababu mbalimbali kiwango chake cha kuaminika kimepungua kwa sababu mbalimbali. Hivyo, akigombea urais hawezi kupata hata 10% ya kura. Aidha, hataungwa mkono na CHADEMA, na ndani ya ACT hakuna mtu mwingine ambaye ni ‘presidential material’ kwa Tanzania bara anayeweza kuwa na ushawishi zaidi ya Zitto.

Kwa nini Membe?

Kwa sababu ukimuacha Lisu, upande wa vyama vya upinzani hakuna mtu mwingine Tanzania bara mwenye haiba ya urais inayomkaribia Membe. Kwa mantiki hiyo, ijapokuwa Membe hatamshinda Rais Magufuli; angalau atasaidia CHADEMA kujipatia % fulani la kura ambayo itasaidia waendelee kupata ruzuku japo kidogo na uwepo wao uendelee kuonekana.Ikombukwe hapo tayari watakuwa washapoteza viti karibu vyote vya ubunge!

Ingawa ni kweli kwamba Membe bado anaiwazia CCM, lakini ni kweli pia kwamba kwa sasa hana uwezekano tena wa kugombea kupitia CCM. Sasa kwa kuwa tatizo la Tanzania sio CCM kama chama bali mtu mmoja mmoja, CHADEMA wakimtumia Membe ili awabusti sio jambo baya kwa kuwa ana haiba chanya zaidi ukilinganisha na wengine wengi waliotajwa hapo juu.

Kwa upande wa ACT, viti kadhaa watakavyopata Zbar, vitawasaidia kuendelea kuonekana na kupata ka - ruzuku kidogo katakako wasaidia ku ‘savaivu’.

Najua wapo watakaobisha, kutukana, na kubeza ushauri huu, ila ushauri huu unazingatia zaidi ‘facts’ ziwe za kuvutia au za kuudhi. Ni hiari ya wahusika kuufuata na wapate namna yenye uafadhali ya kuendelea ku ‘savaivu’ kwenye kipindi cha 2021 -2025, au wapuuze halafu wawe kama TLP, NLD n.k Kama watapuuza na kufikia hatua hiyo, CCM itakosa pakujitizama hiyo nayo utendaji wake unaweza kuathirika kwa namna hasi na kwa kuwa kitakuwa ndicho chama kinachounda serikali, taifa nalo linaweza kukabiliwa na changamoto kadha wa kadha ambazo pengine zingeepukika kwa kufuata ushauri huu.

Kuna wazo kwamba CCM inaweza ikaamua kuwaachia vyama vya upinzani viti kadhaa kwa makusudi ili viendelee kuwepo. Hiyo ni kweli lakini sishauri vyama vya upinzani kutegemea favor kutoka CCM. Wanaweza wasipewe hiyo favor na ikawagharimu sana.

Mtu anaweza kusema kwa nini vyama vya upinzani visipewe ushauri utakaowawezesha kushinda? Jibu ni kwamba ushauri huo walishapewa sana na kuelezwa kwamba pamoja na changamoto za nje zinazowakabili, changamoto kubwa zinazowakwamisha ziko ndani ya vyama vyao wenyewe. Kwa bahati mbaya hilo hawajaliamini hadi sasa na kwa kuwa hawajaliamini na wanadhani changamoto zinazowakabili ni ‘100% external’; hawajachukua hatua na muda uliobaki ni mfupi mno ambao hauwezi kuwatosha tena. Ndio maana ushauri unaowezekana kwa sasa anagalau ni ule wa kuwawezesha waendelee ku ‘savaivu’ lakini sio kushinda.

Tunawashukuru sana kwa kuelewa.
Membe ni mgombea Urais kupitia CCM, ni suala la muda tu.
 
Back
Top Bottom