Uchaguzi 2020 Ushauri kunusuru upinzani ‘kidharura’: CHADEMA msimamisheni Membe, ACT msiweke mgombea bara; Haitawapa ushindi ila itawasaidia kuendelea ku 'savaivu'

Membe ndiye mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM mwaka huu ni suala la muda tu
 
Ushauri ungetolewa kuwe na tume huru ya uchaguzi tu, Magu atashindwa hata na mwanasiasa yeyote asie na jina wa upinzani.
Magu, hajui kujieleza, hana busara ya uongozi, mipango yake ya uchumi imeshindwa vibaya, ubabe usio na akili n.k
Mkuu, kuna vitu unaweza kuwa unatamani viwe na kuna vile inavyowezekana kuwa. Kwa mfano , unaweza kutamani kuwa Tajiri mwenye Akiba ya 1B kwenye account yako lakini kinachowezekana ni kupata hela ya mhogo tu. Sasa hatusemi unachotamani ni kibaya, tatizo unatamani bila kuzingatia kinachowezekana kulingana na mazingira yako.
 
Ushauri wake umekaa kimatako zaidi
 
Halafu uchaguzi ukipata warudi ccm
Kwani hilo likifanyika, itakuwa ndio mara ya kwanza? anyway ni ushauri tu, ushauri sio amri. Na sisi wengine ni vidagaa tu, kwa hiyo wakati mwingine mawazo yetu ni kama mapovu ziwani.
 
Nimeshangaa. Halaf anae toa ushauri ni mwana ccm?
Like seriously?
Mm si mwanasiasa lakin huyu jamaa anawaona wapinzani kama watoto fulani wa hovyo.
Ungejibu hoja zilizotolewa ingependeza zaidi kuliko kulaumu tu kijumla jumla. Kwa mujibu wa Mzee Kikwete, hoja huwa hazipigwi rungu.
 
Hatutaki yale ya 2015,chadema ikimsimamisha mgombea wake itaaminika zaidi hata uchaguzi wakishindwa wana mda mzuri kujiandaa 2025 ,kuliko watu kutoka ccm
 
CDM wameshafunga zoezi la kutia nia toka 15th June 2020,(Kosa la kiufundi) kumchukua Membe leo au kesho litatoa tafsiri ya kutapata tu.

ACT wao bado mlango wazi kwa Membe ila CDM kumuunga mkono Membe akiwa ACT na wao kutokuweka mgombea hawawezi (Ubinafsi)

Bora wakomae ni ubunge zaidi!
 
Hapa wataangalia nani kaweka mgombea wapi, kama ACT wakimsimamisha Seif Zanzibar, itakuwa zamu ya CDM kumsimamisha mgombea wao Bara, hakuna ubinafsi wala nini.

Unless itokee wagombea wa ACT wawe na nguvu pande zote, which is very rare.
 
Hapa cha muhimu tujue kitu kimoja, huko "kumsingizia" alikutambua muda gani,
Mkuu, 'voluntary actions' zote mtu anakuwa anazitambua kabla hata ya kuzifanya. Kwa hiyo wakati mtu anafanya, anakuwa alishatambua tayari. Kwa mfano, wewe ulijua unachotaka kukiandika hapa kabla ya kukiandika. ukiamua kupiga mtu ngumi, unakuwa unajua kwamba sasa unarusha ngumi kabla ya kurusha.

kitu unachoweza kujitetea kuwa hukujua au ulichelewa kujua ni 'involuntary actions' au vitu usivyokuwa na ujuzi navyo wakutosha, au madhara unayosababisha kwa mwingine bila kukusudia. Na hili nafikiri liko wazi na hata mhusika analijua vyema. Na nadhani kuna vitu hatupaswi kuvitetea maana tunapovitetea tunawapa confidence wahusika kuvifanya tena na tena, na ni kwa mantiki hiyo tumekuwa tukisema, mambo mengi yakutatanisha yanayofanywa na baadhi ya wanasiasa, yanafanywa kwa sababu nyuma yao wapo wanaowatetea mambo hayo.
 

Hata mimi kidogo nimemshangaa sana huyu mwana CCM kutoa ushauri kama huu...

Maana yake anawaambia CHADEMA wafanye makosa ya mwaka 2015 kisha wawe "a talk of the town once again"...

This guy is not serious at all. Hii ni mbinu ya " system" kutaka kuleta "distraction" upande wa ngome ya wapinzani wa CCM....

Na CHADEMA walivyo wa ajabu, wanaweza kuingia wazima wazima kwenye mtego huu ulio wazi kabisa hata kwa kipofu.....

Mimi naelewa kwa hakika kabisa TUNDU LISSU is a real threat to CCM and Magufuli in particular....

CCM hawangependa by all means possible mgombea wao Magufuli apambane kwenye jukwaa la kampeni na Tundu Lissu and the reason is very well known....

Kuzuia hili, harakati kama za watu kama huyu mleta mada zilizovikwa mwavuli wa "kwa nia njema, nashauri", zitafanyika sana only to cause confusions in their main opponent camp....
 
Kwa wapenda demokrasia, udumavu au kufa kwa vyama vya siasa sio jambo la kufurahisha, kwa sababu hilo likitokea litapelekea siasa kupoa sana.

Hapa umekuja kurudia maoni ya kawaida kabisa ya wanaccm wengine, ila ww tofauti yako na wao umetumia font tofauti. Anzisha chama kisha mchukue Membe awe mgombea ili mpate ruzuku kuzuia upinzani usife. Ccm watatangazwa washindi sio kwa sababu wako imara, bali ni kwakuwa tuna rais mwenye kiburi cha madaraka, na anayatumia madaraka yake kunajisi box la kura kwa faida ya chama chake. Siwashauri wapinzani wa kweli kushiriki uchaguzi huu kwa tume hii isiyo huru ya uchaguzi. Hamna lililo nje ya ukweli huu.
 
Crap
[emoji240][emoji205][emoji240][emoji205][emoji200]
 
Siwashauri wapinzani wa kweli kushiriki uchaguzi huu kwa tume hii isiyo huru ya uchaguzi. Hamna lililo nje ya ukweli huu.
Mkuu, hilo suala la tume limekuwa likizungumzwa sana miaka na miaka hatua zilizochukuliwa na ambazo hazikuchukuliwa na kwamba nani kafanya nini wote tunajua, unaamini kabisa kwamba kuna tume tofauti itakayosimamia uchaguzi tofauti na iliyopo? Unaamini kabisa kwamba kinachoitwa tume mpya ambayo haijaweza kuwepo miaka yote ambayo imeanza kuzungumziwa, inaweza kuwepo sasa ndani ya mwezi mmoja? unaamini hao unaowaambia wasishiriki uchaguzi hawatashiriki? na huoni wasiposhiriki wengine watashiriki na wasioshiriki watakuwa ndio wanapotea hivyo?

Kuna kitu ambacho huwa tunakisema mara kwa mara, vile mtu anavyoweza kutamani iwe 'Wishful thoughts' na vile inavyowezekana kuwa ' Possibilities'

Ni sawa na tunatamani tuwe na viongozi flani hivi wenye sifa flani flani hivi, lakini swali ambalo huwa wengine tunauliza, watu hao tunao kwenye jamii yetu? kwama hatuna, kwa nini tufikiri tutawapata kwenye vyama? au tunatamani tu, bila kuangalia uwezekano?

Na mwisho kushinda uchaguzi ni jambo moja, jambo la pili ni haiba ya anayeshinda. Ndio maana kwenye uzi wa msingi tumejaribu kugusia kidogo suala la haiba.
 
Kwani hilo likifanyika, itakuwa ndio mara ya kwanza? anyway ni ushauri tu, ushauri sio amri. Na sisi wengine ni vidagaa tu, kwa hiyo wakati mwingine mawazo yetu ni kama mapovu ziwani.
Mawazo yako siyo kabisa . Bila unafki wahamiaji wameisumbua sana Cdm. Unakuwa na wabunge ndumilakuwili , wa nini hasa ?!.

Iteue tu wana Cdm hata kama watashindwa. After all uchaguzi huu umeshaharibiwa na system
 

Acha siasa za kitoto dogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…