Uchaguzi 2020 Ushauri kunusuru upinzani ‘kidharura’: CHADEMA msimamisheni Membe, ACT msiweke mgombea bara; Haitawapa ushindi ila itawasaidia kuendelea ku 'savaivu'

Mfano, ikatokea huko CHADEMA wenyewe wakamkata jina Lissu, halafu mtu akajenga hoja kuwa CHADEMA ni CCM B? mtu huyo atakuwa yuko sahihi, au na yeye atakuwa anajaribu kuleta 'confusion?'

Wakati fulani kuna watu wanatamani vitu, halafu wanadhani wanavyovitamani ndivyo vilivyo lakini kumbe vilivyo katika uhalisia wake ni tofauti kabisa. Pamoja na kutamani, ni muhumu kuangalia vitu katika jicho pana zaidi.
 
Hebu acha kuandika UPUUZI!!! Umekosa ya maana ya kuandika? Tangu lini umekuwa mshauri wa vyama vya siasa Nchini!?
😳😳😳😳

 
Hebu acha kuandika UPUUZI!!! Umekosa ya maana ya kuandika? Tangu lini umekuwa mshauri wa vyama vya siasa Nchini!?
😳😳😳😳
Sio kwamba ndio demokrasia? au demokrasia wewe unaielewa tofauti? au wewe huamini kwenye demokrasia na uhuru wa watu? demokrasia ni kutoa mawazo ya maana kama yako na kuvumilia wanaotoa mawazo ya kipuuzi kama yangu. Ukitaka wote watoe mawazo kama yako 'kwa kuwa ndio ya maana' huo ni udikteta.
 
Hatima ya Tanzania ipo mikononi mwa Mungu sio ccm wala tume wakati ukifika umsfika
 

1. Ndugu, hujakatazwa kuandika kutoa maoni yako kama ambavyo wengine hatujafungwa breki pia....

2. Lakini pia ni heri yako wewe umejiweka wazi kabisa kuwa ni mwana CCM unayewashauri mazuri CHADEMA. Hilo nalo halina ubaya, lakini tunaujadili ushauri wako huo...

3. Kwa upande wangu, mimi siyo mwanachama wa CCM wala wa CHADEMA. Ila naunga mkono mabadiliko ya uongozi wa taifa hili kutoka CCM na kwenda chama kingine. Binafsi, naamini CHADEMA wanaweza kutupa uongozi makini. Kwa hiyo mimi ni mpenzi na shabiki wa chama hiki. Ninakiunga mkono....

4. Hii mbinu yenu ikifanikiwa na ikatokea kweli CHADEMA wakafanya kosa hilo la si tu kumkata Tundu Lissu bali kuwatupa wagombea wanachama wao watiifu na waaminifu wote waliotia nia na kumkaribisha mgeni toka CCM kama ulivyopendekeza, itakuwa ni wao kwa sababu, binadamu yeyote mwisho wa siku huwa ni lazima achague mojawapo ya options nyingi zilizo mbele yake; DEATH or LIFE; WRONG or RIGHT...

5. Ukichagua KOSA au KIFO, basi unatakiwa kuyaishi matokeo ya kile ulichokichagua. Ukichagua KOSA lenye madhara hasi kwako hautakuwa tu umesababisha CONFUSION bali tayari utakuwa uko CONFUSED na hata wakiitwa CCM "B", ni sawa kwa maana watakuwa wanastahili kwa sababu wamependa wenyewe iwe hivyo kutokana na uchaguzi wao.....!!

6. Ndiyo maana sisi wengine, tunawaambia WASIFANYE MAKOSA HAYA ya kufuata ushauri wako. Wanao watu tayari waliokwisha tia nia. Waende na hao hadi mwisho. Nchi hii ya Tanzania na watu wake ni mali ya Mungu muumba. Kama huu ndiyo mwisho wa utawala wa CCM na Mungu akaamua hivyo, basi yeye (Mungu) ndiye atasimamia mabadiliko haya. Na kwa mantiki hii kumbe basi, hata Peter Msigwa anaweza kuwa Rais bora kabisa wa nchi hii. Ni kwa sababu Mungu hapangiwi cha kufanya. Yeye hufanya kwa namna yake mwenyewe. Huweza kuvitumia vitu vinyonge kabisa kwa ajili ya utukufu wake na kuviaibisha vile vinavyoonekana vyenye nguvu na heshima..!!
 
Kwa aina ya upinzani tulionao wa skendo na kupinga kila kitu ni bora ufe ila tuimarishe na tutoe uhuru wa kutosha kwa vyombo vya habari na taasisi za kiraia za haki za binadamu ziweze kuikosoa na kuisurubu serikali bila uoga
 
mkuu Kitaturu kwa nini unadhani kwenye mazingira ya Tanzania ya sasa, CHADEMA inaweza kuongoza nchi vizuri kuliko CCM? au unaamini tu kama Imani zingine? yaani kama mtu anavyoweza kuamini tu kwamba mtoni kuna majini usiku! au kuna viashiria flani ambavyo unavitumia kufikia hitimisho hilo?
 

Sijui hata una maana gani kwanza kuniuliza swali hili. Labda naweza kuelewa unakoelekea...

Nitakujibu hivi:

Na wewe kwanini huamini kuwa CHADEMA ama ACT Wazalendo ama NCCR Mageuzi ama chama kingine chochote hakiwezi kuongoza nchi hii?

Mimi "NAAMINI" kwa sababu nina "IMANI" . Na wewe una "UNAOGOPA" kwa sababu umejengwa juu ya "HOFU" ya mabadiliko....

Na ofcoz ni kwa sababu tu umeizoea CCM. Na kwa kweli nikikuuliza kwanini unadhani CCM ni vyema kuendelea kuongoza nchi hii, naamini sababu zitakuwa ni zilezile zilizo katika msingi wa "HOFU" yako/yenu. Hamuwezi kuwa sababu nyingine zozote za maana...

And may be you might be right kwa sbb ndivyo mlivyo...

Ninyi mtakuwa mmesahau kitu kimoja ama viwili;

MOSI; CHADEMA ni chama cha siasa kama kilivyo CCM. Kina watu mamilioni wanachama na wapenzi kama ilivyo kwa ama pengine kuliko CCM. Sasa kwanini kishindwe kuongoza nchi?

PILI; hakuna wakati uliokuwa mgumu na wenye changamoto lukuki kama wakati nchi hii inapata Uhuru mwaka 1961 na waafrika tunachukua jukumu la kujitawala wenyewe toka kwa mzungu mwingireza...

Wapo waliokuwa na HOFU na MASWALI yaliyojaa mashaka na kutojiamini kama haya yako unayoniuliza mimi leo. Lakini hali ilikuwaje? Ndivyo hivi tupo hapa leo, ndivyo hivi tulivyo leo....

Sasa leo unaniuliza swali hili ktk nyakati hizi?

Kwani ugumu uko wapi? Kama tumeweza kuongozwa na Magufuli maana yake anyone from any where anaweza kuongoza nchi hii....

Dola (kwa maana ya Jeshi, Polisi, magereza, TISS, mahakama nk ) haibadiliki, ni walewale. Wao hawajali chama gani kimeunda serikali. Watafanya kazi na awaye yeyote...

Kinachobadilika kwa vyombo hivi baada ya serikali mpya kuingia madarakani na wakipenda kufanya hivyo ni MUUNDO na MIFUMO ya uendeshaji vyombo hivi, basi hakuna kingine....

Yaani kuongoza nchi yenye katiba hata MGOMBEA HURU asiye na chama chochote cha siasa akishinda anaweza kuunda serikali na nchi ikaenda kwa uzuri na ubora kabisa kuliko hivi ilivyo chini ya CCM....
 
Umemjibu vzr mnooo..sidhni Kama ataendelea na huu mjadala...aisee ubarikiwe sana
 
Hatusemi kwamba Vyama vya upinzani havitaweza kuongoza bali tunasema ufanisi wao utakuwa wa chini sana ukilinganisha na wa CCM. Hili hatusemi tu kwa kuwa tunataka kusema bali kwa viashiria vya wazi sana. Nitatoa mifano michache;

Kwa mfano, tunaona kwenye vyama hivyo, vinashindwa ku control vitu vidogo sana vilivyo ndani ya uwezo wao. Kwa mfano Chadema kwa zaidi ya miaka 20, imeshindwa angalau tu kujenga ofisi ya makao makuu, sasa jiulize kama hilo tu limewashinda, kwa nini tudhani wataweza kuongoza nchi kwa ufanisi zaidi ya CCM?

Kwenye vyama vya upinzani havina dola ila kuna viongozi wanang'ang'ania madarakani, kwa nini tudhani wakiwa na dola hawatang'ang'ania?

Kuna viongozi wametoka huko wakahamia ccm na wakapewa madaraka mbalimbali serikalini, ufanisi wao, hekima na burasa zao tunaziona, na hiyo ndio reflection ya ambavyo ingekuwa ikiwa vyama walikotoka vingekuwa madarakani.

Kwa hiyo hatusemi haviwezi, tunachosema vitakuwa na ufanisi wa chini kuliko CCM kutokana na evidence zilizopo na kwa mantiki hiyo ndio maana tunafikiri bado CCM ni 'comparatively better' hadi sasa na pamoja na vyama hivyo kushauriwa sana kujifanyia maboresho ya ndani ili angalau hata vifikie level ya ccm, bado havijaweza kufanya hivyo.
 
Kitaturu kakujibu vzr mnooo..sikutegemea Kama ungelisongesha...yaani kamaliza kila kitu
 
Acha kuonyesha UJUHA wako hadharani kwa akili ya KUFIKIRIKA. Hivi ccm ina UFANISI upi kwenye sekta gani?

Miaka 60 madarakani na Watanzania hatuna chochote kile cha kujivunia si elimu, afya, ajira, uchumi, kufaidika na rasilimali za nchi. Hovyo hovyo mwanzo mwisho halafu unadai ccm ina ufanisi! 😳😳😳

Umetumia vigezo gani kupima ufanisi wa vyama vya upinzani ambavyo havijawahi kushika madaraka? Au UMEKURUPUKA tu na dhana yako POTOFU!?

 
Hapa cha msingi ni kutambua anachofanya (kumsema Kinana) kilikuja wakati gani, usitake kunilazimisha niamini Msigwa alijua anakosea toka mwanzo, hiyo itabaki kuwa ni siri yake mwenyewe. Ninachoamini mimi ni kwamba Msigwa alijua kakosea baada ya mahakama kupinga utetezi wake, ndio akatakiwa kuomba samahani, na ndicho alichofanya.
 
Usituletee uchuro CDM haiingii chaka.
Kama umetumwa waambie sikuwakuta!!
 
Look how single minded your loh! Unawaza ngono tu!
My brain is complex baby, you don't even know what you are talking about, stay away from me.

Halafu, it's; you are, not your, wacha kiherehere.
 
My brain is complex baby, you don't even know what you are talking about, stay away from me.

Halafu, it's; you are, not your, wacha kiherehere.
Nashukuru umenielewa na ndio maana ukajibu.

Mara ya mwisho nimeitwa baby baada ya kumbanjua demu mmoja mkali usiku kucha, today is the second time

Thanks sweetie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…