Ushauri: Kuongeza Tax base, Rais na Wabunge walipe Kodi

Ushauri: Kuongeza Tax base, Rais na Wabunge walipe Kodi

Inakera mama mtu mzima asiyelipa kodi eti anasimama na kuhimiza Watanzania walipe kodi, anataka nani alipe kodi ilhali yeye mwenyewe na wafuasi wake hawalipi kodi?
 
Boda na guta na Bajaj za abiria nowadays wanalipa Kodi ya mapato, 150,000 Kwa mwaka kama sikosei.

Kuhusu winga, msisitizo uongezwe, wasajili ofisi walipe Kodi, wabadilishiwe Jina Toka kuitwa winga Hadi "Commission Agents".
Nyie kina ChoiceVariable na FaizaFoxy hawa boda na guta ni katika hao milioni 2 waliosemwa wanalipa kodi??
 
Mbali na matumizi,

Ni UKWELI ulio wazi kuwa tax Base Iko chini, sababu mojawapo ni viongozi wakuu wamesamehewa ,hawalipi Kodi,

Sasa kusisitiza wananchi wengine walipe Kodi ilhali Yeye halipi, huoni mitihani huo?
Kama pakacha linavuja hauangaiki kuongeza maji kwa kazi kwanza unaziba pakacha...

Hivi Makosanyo ya kila Halmashauri, makusanyo ya VAT, Matozo ya kwenye Mafuta na kila Bidhaa, Makusanyo kwenye Simu, Halmashauri kuanzia Service Levy Taka sijui na kitu gani, bakuli linalotembezwa kila siku, mapato ya Utalii, Mapato kwenye Madini mengine tunayo pekee duniani (Tanzanite) yamefanya vitu gani vya maana na kuonekana ?

Kwahio ukiongeza kabla ya kuziba pakacha ni kuongezea mirija walambaji tena bora Kodi zingepunguzwa ili hawa wananchi wanaoumia kutokana na bidhaa / huduma kupanda bei kutokana na matozo wangepata ahueni...
 
Boda na guta na Bajaj za abiria nowadays wanalipa Kodi ya mapato, 150,000 Kwa mwaka kama sikosei.

Kuhusu winga, msisitizo uongezwe, wasajili ofisi walipe Kodi, wabadilishiwe Jina Toka kuitwa winga Hadi "Commission Agents".
Aisee badala ya kuja na Sera za kuwatoa vijana kitaa na kupata ujira kwa kufanya kazi productive tunataka kazi hizo kuzifanya halali kabisa.., Yaani kuanzia Top mpaka chini nchi hii ni Wachuuzi na Madalali tufauti ni kinachouzika..., kule wanauza nchi na Commanding Heights huku wanauza bidhaa za wachina na other junks...
 
Hili la wabunge walipe kodi nasema hapana, hawa wanazo familia mbili mbili za kutunza, yaani Dodoma na jimboni kwake na mwisho hawatakiwa kuwa na mawazo ya siku ya mshahara ili waweze kututumikia vizuri.
Point ya kijinga kabisa. Wako pale kutumikia wananchi period. Other thing ni control yao wenyewe
Walipe kodi kama wafanyakazi wengine wa serikali
 
Salaam, Shalom!!

Akiongelea Suala la Kodi, Mh Rais amesema kuwa tax Base ya nchini petu ni chini ya milioni mbili.

Hili limefika hapa Kwa sababu nyingi ambazo tumekuwa tukizipigia kelele Kila kukicha,

Kwa kuwa kiongozi wetu amedhamiria kuongeza Tax base Ili wengi zaidi wapate hamasa ya kulipa Kodi, ninamshauri yafuatayo:

1. Kiongozi wetu Mh Rais SSH aelekeze hazina Ili mshahara wake utajwe hadharani na ukatwe Kodi na posho zote zikatwe Kodi.

2. Wabunge mishahara Yao ikatwe Kodi na posho zao zikatwe Kodi.

Si vyema watunga Sheria na sera za Kodi nchini wasamehewe kulipa Kodi ilhali viongozi wa juu Wachache hawalipi Kodi, hii Si HAKI.

Yakifanyika hayo, wote tutakuwa sawa mbele ya Sheria na tulipe Kodi na wote tuhisi uchungu wa kulipa Kodi Ili pia tuzisimamie vizuri.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Ukitembea sehemu nyingi ya miji ya Tanzania,wapo watu wanabiashara mabarazani,na wengine wamekaa hapo kwenye vibaraza,kumbe wana biashara kubwa sana,bidhaa zao zinakaa kwenye vyumba,mteja akitaka wanakwenda kumtolea,utakuta wanauza perfume za kujaza wao wenyewe kwenye chupa,na wanauza kwa jumla,wanauza rangi za kupaka kwenye mikeka kwa jumla na kusafirisha mikoani,hii nimeona Tanga,karibu na soko la Ngamiani.wapo wanaouza kamba za mkonge,utaona kaweka meza,utamdharau,kumbe wanauza jumla hizo bidhaa,wapo wanaokata mipira ya kufungia bidhaa kwenye pikipiki na baiskeli,hawa pia wanauza jumla na reja reja,hawatoi risiti,karibu na Soko la ngamiani,na bidhaa mbalimbali,wapo pia wanaouza bidhaa barabarani kwa wenye magari,wakati gari zimesimama kwenye mataa kama vile Dar.,hawa ukipata habari zao,unaambiwa wamejenga majumba ya kifahari,mawili mpaka matatu,hawalipi kodi ya aina yoyote mafundi simu kaweka kimeza barazani,hawalipi kodi wala kutoa risiti,na wenhine wanauza mpaka vifaa vya simu na simu,hapo hapo. ,serekali,ingewafatilia watu kama hawa.
 
Salaam, Shalom!!

Akiongelea Suala la Kodi, Mh Rais amesema kuwa tax Base ya nchini petu ni chini ya milioni mbili.

Hili limefika hapa Kwa sababu nyingi ambazo tumekuwa tukizipigia kelele Kila kukicha,

Kwa kuwa kiongozi wetu amedhamiria kuongeza Tax base Ili wengi zaidi wapate hamasa ya kulipa Kodi, ninamshauri yafuatayo:

1. Kiongozi wetu Mh Rais SSH aelekeze hazina Ili mshahara wake utajwe hadharani na ukatwe Kodi na posho zote zikatwe Kodi.

2. Wabunge mishahara Yao ikatwe Kodi na posho zao zikatwe Kodi.

Si vyema watunga Sheria na sera za Kodi nchini wasamehewe kulipa Kodi ilhali viongozi wa juu Wachache hawalipi Kodi, hii Si HAKI.

Yakifanyika hayo, wote tutakuwa sawa mbele ya Sheria na tulipe Kodi na wote tuhisi uchungu wa kulipa Kodi Ili pia tuzisimamie vizuri.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Naunga mkono hoja
 
Point ya kijinga kabisa. Wako pale kutumikia wananchi period. Other thing ni control yao wenyewe
Walipe kodi kama wafanyakazi wengine wa serikali
Mimi na Lucas Mwashambwa ni chawa wa chura kiziwi, na ni watanzania damudamu hatupendi kupewa haki zetu, sisi ni wanyonge.
 
Rais wa Tangangika, makamu wa rais, waziri mkuu, rais wa Znz, makamu wa kwanza na wa pili wa rais Znz, spika wa bunge na naibu spika, jaji mkuu, marais marais wastaafu wa Tanganyika na Znz hao wote wanahudumiwa na serikali na hawalipi kodi, wanapewa huduma ya usafiri bure, huduma ya afya bure, malazi na chakula bure.
 
Hili la wabunge walipe kodi nasema hapana, hawa wanazo familia mbili mbili za kutunza, yaani Dodoma na jimboni kwake na mwisho hawatakiwa kuwa na mawazo ya siku ya mshahara ili waweze kututumikia vizuri.
Yaani wewe sijui unaishi karne ya ngapi. Wafanyakazi wengi wanaofanya kazi migodini hawaishi na familia zao huko migodini maana yake wanazo familia zaidi ya moja lakini wanalipa kodi iweje Mbunge anayesinzia Bungeni na kuamshwa kwa kugonga meza ndo aonekane ana majukumu ya familia nyingi? Watumishi wangapi wanafanya kazi dodoma na familia zao zipo Dar, Moro, Mwanza na kwingineko lakini wanalipa kodi, Mbunge na Rais wao ni nani hadi wasilipe kodi? Kama kodi ni damu nchi, Rais na chawa wake walipe kodi pia.
 
Aisee badala ya kuja na Sera za kuwatoa vijana kitaa na kupata ujira kwa kufanya kazi productive tunataka kazi hizo kuzifanya halali kabisa.., Yaani kuanzia Top mpaka chini nchi hii ni Wachuuzi na Madalali tufauti ni kinachouzika..., kule wanauza nchi na Commanding Heights huku wanauza bidhaa za wachina na other junks...
Huku hata madalali wa nyumba na viwanja hawajasajili makampuni wanaitwa winga,

Wakati Nchi za wenzetu huwezi pata nyumba bila kuwatumia hao agents, wamesajili kampuni kabisa na wanalipa Kodi.

Ndicho nilichomaanisha.
 
Huku hata madalali wa nyumba na viwanja hawajasajili makampuni wanaitwa winga,
Huku hakuna formal sectors watu ni wabangaizaji na wanafanya hivyo ili mradi mkono uende kinywani hand to mouth, hili taifa kila kitu kinakwenda kama Pwagu na Pwaguzi
Wakati Nchi za wenzetu huwezi pata nyumba bila kuwatumia hao agents, wamesajili kampuni kabisa na wanalipa Kodi.

Ndicho nilichomaanisha.
Hizo nchi za wenzetu kipato cha mtu na disposable income yao ipo vipi..., haya mambo ukisema kuwe na official agents wachache watakwenda (ingawa hata sasa wapo ila premium customers wanaoogopa kuibiwa ndio wanakwenda) hawa wa uswazi chumba cha laki mbili huende kwa formal agent alipie kodi, na overheads kadhaa..., chumba hicho kitabadilika kuwa laki tatu wakati mshahara ujira wa mtu wachache wanachezea hio...

My point being kwanza tuzibe pakacha hata tukiongeza makusanyo maradufu yote yanaishia kwenye matumbo ya walamba asali.....

Better still badala ya kujikita kukamua tuwaze Sera za kuweza kuongeza lishe ya hao wanaokamuliwa...
 
Salaam, Shalom!!

Akiongelea Suala la Kodi, Mh Rais amesema kuwa tax Base ya nchini petu ni chini ya milioni mbili.

Kwa kuwa kiongozi wetu amedhamiria kuongeza Tax base Ili wengi zaidi wapate hamasa ya kulipa Kodi, ninamshauri yafuatayo:

1. Kiongozi wetu Mh Rais SSH aelekeze hazina Ili mshahara wake utajwe hadharani na ukatwe Kodi na posho zote zikatwe Kodi.

Si vyema watunga Sheria na sera za Kodi nchini wasamehewe kulipa Kodi ilhali viongozi wa juu Wachache hawalipi Kodi, hii Si HAKI.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Naunga mkono hoja Kuepuka Double Standards ya Kodi, Nashauri Rais Uongezwe Mshahara, Ili Alipe Kodi, Wote Tulipe Kodi!
na Big Up, TRA Kutumia Media Kuelimisha Umma Elimu ya Kodi na Umuhimu wa Kodi Kila Mtu Alipe Kodi. Je Wajua Viongozi Wetu Wakuu Hawalipi Kodi?. Kwanini?!
p
 
Mbunge mwingine alitaja mshahara wa wabunge na alisema hawalipi Kodi!!! Akaitwa kuhojiwa na viongozi wake
Watanzania wengi hawana nidhamu katika maneno, hawaweki tofauti kati ya "wabunge hawalipi kodi" na "wabunge wanalipa kodi ndogo".

Kibajaji kasema wanalipwa mshahara wa milioni 4.6 na wanalipa kodi ya milioni 1.2.

Kasema hivyo kwenye press conference akionesha na salary slip yake.

Na hakuna mtu aliyemkanusha.

Huko kwenye marupurupu hata mimi nishalipwa marupurupu yasiyolipiwa kodi, Tanzania na USA.
 
Back
Top Bottom