Unashauri nini kifanyike ili mambo yawe tofauti, ukizingatia hali halisi ilivyo?
Watu wengi wana focus kwenye mambo ya juu juu, hawaangalii matatizo ya msingi.
Watu wanapenda sana kulaumu vi9ngozi, bila ya juangakia matatizo ya jamii kiujumla na kukubali kuwa hata hao viongozi wametoka katika janii yetu hii hii na hata matatizo yao kimsingi ni natatizo ya jamii yetu.
Utamaduni wetu kama taifa inabidi ubadilike. Inabidi watu wachukue ownership zaidi kwenye mambo ya kuendesha nchi. Hilo ni jambo la msingi kabisa. Sasa hivi watu wengi wamesha give up hawajaki wala hawafuatilii.
Watu wakichukua ownership katika mambo ya kuendesha nchi, jambo ambalo kwa sasa kuna wengi hawalifuatilii, watagundua kuwa kuna mambo mengi hawayaelewi, wamewaachia viongozi tu, na hapo ndipo viongozi wanapowapiga.
Wakigundua kuwa kuna mambo mengi hawayaelewi, kama wana nia thabiti kuiendeleza nchi yao, watajifunza zaidi na kuungana zaidi kuelewa mambo, ku lobby ili kupata uhuru zaidi na habari zaidi, kuwafanya viongizi wawe wanawajibika zaidi, kufanya mfumo uwe na checks and balances nyingi zaidi.
Eventually utapata maendeleo ya polepole yatakayoleta critical mass ya kuwafanya viongizi wasiwe mabwana wa wananchi, wawe kile kinachoitwa "servant leaders" zaidi.
Ukiangalia hii process, hii ni bottom up approach, wananchi wana ji organize wenyewe kuwawajibisha viongozi na kuleta uwajibikaji.
Tatizo sasa hivi wananchi wengi hawako involved, hawana elimu, hawana taarifa, hawana organization, wamebaki kutegemea viongozi wawahurumie na kuwafanyia kazi yao wananchi, viongozi wawaletee maendeleo.
Viongozi wenyewe wana matatizo kibao, wanapata "development fatigue", wana focus kwenye self preservation yao kisiasa ambayo inaweza hata kupingana na maendeleo.
Essentially viongozi wana uamuzi wa kuwaletea watu maendeleo makubwa ya kiuchumi na kielimu halafu viongozi watolewe madarakani kwa kuwa watu watakuwa wameamka sana, au viongozi kuwapa watu maendeleo kiduchu ya kupigia kampeni za kisiasa tu, halafu viongozi wabakie madarakani.
They choose the latter.