Ushauri: Kuongeza Tax base, Rais na Wabunge walipe Kodi

Hili la wabunge walipe kodi nasema hapana, hawa wanazo familia mbili mbili za kutunza, yaani Dodoma na jimboni kwake na mwisho hawatakiwa kuwa na mawazo ya siku ya mshahara ili waweze kututumikia vizuri.
Hii ni poverty mentality. Si kazi ya mbunge kututua changamoto za kifedha za wananchi. Mbunge anaweza kuhamasisha na kuchangia fedha katika miradi jimboni kwake. Jamii ielimishwe kuwa si kazi ya mbunge kugawa hela
 
Hiyo kodi wanalipa. Msikilize Kibajaji hapo.

Halafu, milioni 360 kwa mwezi katika hesabu za kuendesha nchi ni hela ndogo sana.

Hatuwezi kuendelea kwa kubana matumizi na kutoza kodi viongozi (ambao ni wachache sana ukiwalinganisha na mamilini ya wananchi) kama uzalishaji haujaongezeka.

Nchi inaendelea kwa mamilioni ya watu kuongeza uzalishaji na kulipa kodi.

Ingawa kubana matumizi mabaya ya viongozi ni kitu muhinu, nchi haiendelei kwa kubana matumizi ya viongozi bila mkakati wa kuongeza uzalishaji kwa mamilioni ya wananchi.
Kodi hukusanywa chache kwa kila mtu, hizo chache ndizo zinafanya ziwe nyingi, senti moja hufanya shilingi.
 
Sawa.

Sasa ukikusanya kodi ya senti moja kwa kila mtu, wakati huduma za kijamii zinagharimu shilingi mia moja kwa kila mtu, huoni kwamba hapo hiyo kodi haitatosha kulipia hizo huduma za jamii?

Huoni kwamba hapo patahitajika kuongeza uchumi ili kila mtu apate kipato kikubwa zaidi na kulipa kodi ya shilingi mia moja ili kulipia hizo huduma za jamii?

This is simple math.
 
Tatizo sio Makusanyo, Kodi tunalipa na wengi wanakamuliwa even beyond their means...., Issue ya muhimu kabisa ni matumizi ya hio Kodi hakuna Value for Money..., Kama watu wangeona Kodi zao zinatumika ipasavyo na hazivujwi basi wangekuwa hata wanakumbushia iwapo wakisahaulika...
 
wabunge wapo wangapi?
Ukichukua idadi yao ukazidisha na kiwango cha kodi utapata sh ngapi?

#Tatizo la kusomesha ngwini wengi linaharibu Taifa tujikite kwenye sayansi kupitia mkopo wa Samia
 
Kumbe rais halipi kodi?
mbona yule jamaa mwijaku anagalagala na suti mavumbini akimsifu rais kwa kutoa mabilion
mi nkajua anaupiga mwingi kwa kulipa kodi kubwa sana kuliko raia wote!!
Ina maana halipi hata senti moja?
Halipo hata bili ya maji. Na hayakatiki,

Sasa mkilalamika daslam hakuna maji, anashangaa!!
 
Tatizo sio Makusanyo, Kodi tunalipa na wengi wanakamuliwa even beyond their means...., Issue ya muhimu kabisa ni matumizi ya hio Kodi hakuna Value for Money..., Kama watu wangeona Kodi zao zinatumika ipasavyo na hazivujwi basi wangekuwa hata wanakumbushia iwapo wakisahaulika...
Mbali na matumizi,

Ni UKWELI ulio wazi kuwa tax Base Iko chini, sababu mojawapo ni viongozi wakuu wamesamehewa ,hawalipi Kodi,

Sasa kusisitiza wananchi wengine walipe Kodi ilhali Yeye halipi, huoni mitihani huo?
 
Hiyo kodi wanalipa. Msikilize Kibajaji hapo.

Halafu, milioni 360 kwa mwezi katika hesabu za kuendesha nchi ni hela ndogo sana.

Hatuwezi kuendelea kwa kubana matumizi na kutoza kodi viongozi (ambao ni wachache sana ukiwalinganisha na mamilini ya wananchi) kama uzalishaji haujaongezeka.

Nchi inaendelea kwa mamilioni ya watu kuongeza uzalishaji na kulipa kodi.

Ingawa kubana matumizi mabaya ya viongozi ni kitu muhinu, nchi haiendelei kwa kubana matumizi ya viongozi bila mkakati wa kuongeza uzalishaji kwa mamilioni ya wananchi.
Inabidi vyote kwa pamoja vifanyike. Kodi ni lazima iwe jumuishi hata hao viongozi waone umuhimu wa kupitisha sera zinazokuza uchumi.

Vinginenvyo huwezi kuwa unamtungia mtu kitu ambacho wewe hakikugusi. Kila mtu alipe kodi, kama kunufaika wanamalupulupu mengi hakuna anayepinga kwa kiongozi kupewa.

Milioni 360 haiwezi kuwa hela ndogo kamwe. Hizo fedha zikielekezwa sehemu moja zinaenda kuleta mabadiliko makubwa na kuacha alama.
 
wabunge wapo wangapi?
Ukichukua idadi yao ukazidisha na kiwango cha kodi utapata sh ngapi?

#Tatizo la kusomesha ngwini wengi linaharibu Taifa tujikite kwenye sayansi kupitia mkopo wa Samia
HOJA Si wangapi,

HOJA hapa ni

1. Wanalipa au hawalipi?

2. Na wanalipwa Bei Gani hao Wachache mishahara na marupurupu?

3. Na ikiwa hawalipi, wanawasaidia ndugu na jamaa zao kukwepa Kodi wangapi?

Karibu 🙏
 
Salaam, Shalom!!

Akiongelea Suala la Kodi, Mh Rais amesema kuwa tax Base ya nchini petu ni chini ya milioni mbili.

Hili limefika hapa Kwa sababu nyingi ambazo tumekkuwa tukizipigia kelele Kila kukicha,

Kwa kuwa kiongozi wetu amedhamiria kuongeza Tax base Ili wengi zaidi wapate hamasa ya kulipa Kodi, ninamshauri yafuatayo:

1. Kiongozi wetu Mh Rais SSH aelekeze hazina Ili mshahara wake utajwe hadharani na ukatwe Kodi na posho zote zikatwe Kodi.

2. Wabunge mishahara Yao ukatwe Kodi na posho zao zikatwe Kodi.

Si vyema watunga Sheria na sera za Kodi nchini wasamehewe kulipa Kodi ilhali viongozi wa juu Wachache hawalipi Kodi, hii Si HAKI.

Yakifanyika hayo, wote tutakuwa sawa mbele ya Sheria na tulipe Kodi na wote tuhisi uchungu wa kulipa Kodi Ili pia tuzisimamie vizuri.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Kabisa kabisa. Kinachouma, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kujiona miungu mitu huku wakiishi kwa kodi tunazolipa!
 
Salaam, Shalom!!

Akiongelea Suala la Kodi, Mh Rais amesema kuwa tax Base ya nchini petu ni chini ya milioni mbili.

Hili limefika hapa Kwa sababu nyingi ambazo tumekkuwa tukizipigia kelele Kila kukicha,

Kwa kuwa kiongozi wetu amedhamiria kuongeza Tax base Ili wengi zaidi wapate hamasa ya kulipa Kodi, ninamshauri yafuatayo:

1. Kiongozi wetu Mh Rais SSH aelekeze hazina Ili mshahara wake utajwe hadharani na ukatwe Kodi na posho zote zikatwe Kodi.

2. Wabunge mishahara Yao ukatwe Kodi na posho zao zikatwe Kodi.

Si vyema watunga Sheria na sera za Kodi nchini wasamehewe kulipa Kodi ilhali viongozi wa juu Wachache hawalipi Kodi, hii Si HAKI.

Yakifanyika hayo, wote tutakuwa sawa mbele ya Sheria na tulipe Kodi na wote tuhisi uchungu wa kulipa Kodi Ili pia tuzisimamie vizuri.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Hapo kwa Rais tunaweza kuacha, kuna mawaziri, wabunge, majaji etc hawa walipe kodi kwa mafao wanayapata. Haileti maana mtu wa kawaida hata ukilipwa laki tatu unapaswa kulipwa kodi huku watajwa hapo juu wakibeba mafurushi ya fedha bila kulipa hata mia.
 
Hii ni poverty mentality. Si kazi ya mbunge kututua changamoto za kifedha za wananchi. Mbunge anaweza kuhamasisha na kuchangia fedha katika miradi jimboni kwake. Jamii ielimishwe kuwa si kazi ya mbunge kugawa hela
Wabunge wana fedha za mfuko wa jimbo, wazitumie ipasavyo kuleta maendeleo katika maeneo yao ya ubunge.
 
Si namba pekee,

Ni muhimu iwe inclusive, isibague baadhi walipe wengine wale laini!!
Sasa hapa mada inataja wabunge kama ndio ushauri.
Labda aweke hivi....kila mwanasiasa akipokea pato akatwe X% itakayohudumia shughuli za siasa na maendeleo.hiyo ndio significant number in taxation.yaani unaanzia mjumbe wa serikali ya mtaa hadi kada wa chama...that is number!!that is inclusion.
 
Back
Top Bottom