Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,313
- 4,751
Hii sarakasi aliyofanya Msajili wa vyama vya siasa nchini la kumkata mgombea uraisi wa ACT Wazalendo kwa kutumia katiba na kanuni za chama hicho, mbona ni rahisi tu kwa wao ACT Wazalendo nao kuicheza hiyo sarakasi.
Katiba na kanuni za chama ni mwongozo wa mkutano mkuu wa chama husika kwa watenda kazi wa chama. Hivyo wamiliki wa hizo kanuni na katiba ni mkutano mkuu wa chama na siyo msajili wa vyama. Mkutano mkuu una mamlaka ya ya kuzibadili wakati wo wote. Hivi majuzi mkutano mkuu wa ccm kwa njia ya mtandao uliamua kuipa madaraka kamati kuu kufyeka mgombea ubunge yeyot hata kama alishinda kwa kishindo kwenye kura za maoni.
Hivyo ACT wazalendo waitishe mkutano mkuu wa chama haraka hata kwa njia ya Mtandao wa kubadili hizo kanuni ya siku 7 au sijui mwezi mmoja zinazomtaka mwanachama mpya kuwa kwenye chama kabla ya kuruhusiwa kuwa mgombea wa nafasi ya udiwani, ubunge au uraisi. Kanuni hii ndiyo kaitumia msajili kumwengua Mpina na Tume Huru ya Uchaguzi kuafiki.
Wamepewa kuja na alternative hadi jumatatu ijayo. Hivyo katika kucheza hii sarakasi, waitishe mkutano mkuu ambao utamteua tena Mpina kuwa mgombea wao. Kwanza hadi sasa ameshamaliza hicho kipindi cha mwezi mmoja hadi ajiunge na chama. Wafanye hiyo sarakasi huku wakiendelea na hizo hatua mahakamani. This might solve the problem in the easiest manner.