Ushauri kwa Adamu Mchomvu (Baba Jonii) na game ya mziki


Hebu Watanzani tuache kuwa wachonganishi! Adam mchovu huwa hapeleki nyimbo zake vituo vingine..hata TBC sijawai kuuona ukichezwa! The man is not serious in music! Recho,mwasiti,Barnaba, linah wote zinachezwa na wako chini ya kituo cha Clouds..!
 

kama hasambazi mziki wake bas hayupo serious!
 
kama hasambazi mziki wake bas hayupo serious!

Elewa kuwa Adam hafanyi mziki pesa bali anafanya mziki burudani kwendana na aina ya kazi zake. Ni kama swaga kazini au kachumbari kwenye pilau. Wala huwezi kumuweka kwenye list ya wanamziki hapa bongo. Ni vizuri tumjadili kama mtangazaji badala ya kumjadili kama mwanamziki.
 

Jamaa ni mtangazaji mzuri sana,na ukitaka kujua hilo waskilize watangazaji vijana wengi wa kibongo bongo wanao tangaza vipindi vya burudani wanavyo iga swaga za kuongea za mchomvu ndio utajua msela ni noma.
 

Mkuu ni kweli Mchonvu hafanyi muziki kama kazi ni hobi yake na afanya just for fun

Ni mtangazaji mzuri sana tu kibongo bongo lakini ukisikiliza nyimbo zake zinafurahisha sana
, si unajua jamaa kwa ukomedi

Wala huna haja ya kumshauri aache kuimba aongeZe nguvu kwenye utangazaji maana ukimuona anavyoimbaga kwenye mafiesta yao na manyimbo yake ya kikomedi its very fun
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…