Ndiyo, inatakiwa iwe ya kiubaguzi. Haki ya uraia wa kuzaliwa siyo ndogo kama unatumia akili.Kwa hiyo uraia pacha utakuwa wa kiubaguzi? Yaani Mhindi akitaka na uraia wa Tanzania akataliwe, ila Mtanzania akitaka na uraia wa India akubaliwe!
Hoja ya Dangote ilizaliwa na hoja kuwa watanzania walio nje (walioukana uraia) wanashindwa kuja kuwekeza Tanzania kwa kuwa si watanzania tena.
Hoja yako ya kukataa uraia pacha ni ipi?Tunawaonea wivu nyinyi diaspora ?
Sasa kwa nini tuhangaike kubadilisha sheria kuwasapoti watu ambao wanatukashfu tuliopo hapa nchini wakisema wao wako njema mpaka tunawaonea wivu ?
Hoja nyepesi za wana diaspora ndio hizi maskini ya Mungu.
Uraia pacha si lazima uwe kwa watu wote. Tunaweza kuruhusu wazawa wa Tanzania peke yao au wao na vizazi vyao nakadhalika.Mkuu Ingawa sina Hoja kali kama Zako ila Uraia Pacha utatuua...wahinndiu watachukua kila tuu kuanzia ajira...
Hapa Tuu sasa hivi wao ndio wanaongoza kwa Uraia Pacha wa Uingereza,Canada na India na hapa Bongo wamebadilisha sana Visa/Permit to work Wengine wanaishi zaidi ya Miaka 10
Kufanya Kazi eti ya Expert anabadilisha tuu cheo,Leo hiki kesho kile ili isibumbuluke...Uhamiaji ni sheeedah,Wahindi Shikamooni...
Mmewakomoa sana migration hadi Wameshiba tena wanawasaidia namna ya Kuishi
Kwa nini unatenga Afrika tu? Nji zifuatazo DUNIANI haziruhusu uraia pacha:Udungaembe maana yake ni Nini??.
Kufafanua kwa ufupi:bila uraia pacha hayo hayawezi kufanyika? Mimi naona linaweza kuwa jambo zuri ila mnaotoa mada bado mko too brief.
Kufafanua kwa ufupi:
Uraia pacha unampa Mtanzania fursa ya kupata haki za raia wa nchi nyingine pia. Kwa mfano, kwenye swala la ajira. Kuna nchi zinazotoa ajira za aina au ngazi fulani kwa kutegemea uraia. Mtanzania mwenye uwezo wa kupata ajira hiyo, tayari anakosa nafasi hiyo kwasababu hana uraia wa nchi hiyo. Hii ni pamoja aina ya contracts ambazo angeweza kupata au unzishwaji wa miradi au kampuni katika nchi nyingine. Gharama huwa kubwa au nafasi chache, hata aishi huko miaka mingapi (ikitegemea pia nchi aliyoko).
Ina maana kwamba, mtanzania anayepata fursa nchi nyingine anapata ushawishi mkubwa wakubadili uraia hasa kama fursa hizo ni nzuri sana. Uraia pacha unampa ushawishi wa kubaki na uraia wake wa Tanzania na hivyo kumpa hamasa yakuendelea kuwekeza nyumbani (Tanzania). Mfano mzuri ni Nigeria. Ifikapo 2023, Wanaijerea waishiyo nje watakuwa wanatuma zaidi ya $35 billioni kwa mwaka, sawa na asilimia 6.1 ya GDP yao. (The New CBN Regulations: Impact on Remittances to Nigeria - AZA)
Nani anaukana uraia wa Tanzania kwa ajili ya kuwavimbia watu?Kwani shida ni ya nani? Ni watanzania kutaka uraia wa nchi zingine au wa nchi zingine kutaka uraia wa TZ? Shida ni kwamba kuna wa-TZ walioamua kuukana uraia wao na kuchota uraia wa nchi zingine wakiamini wameukata. Sasa kihoro kinawasumbua wanataka waruhusiwe kuwa tena wa TZ.
Ndo maana unasikia maneno kama kuonea wivu. Ni kwa kuamini kwamba walipopata uraia wa nje waliukata: BAlozi Mula mula huyo muonee huruma tu! NI bahati mbaya leo hii ni waziri labda naye anataka uraia wa Rwanda.
Mkuu, sidhani kama uko sahihi.Kwa nini unatenga Afrika tu? Nji zifuatazo DUNIANI haziruhusu uraia pacha:
INDIA ISRAEL USA UK PAKISTAN SAUDI CANADA URUGUAY SOUTH AFRICA ETC ETC
Issue si "kuruhusu", isyu ni kwamba, mathalani, USA watakuruhusu tu kama utaitema hiyo inji ingine. In other words, dual citizenship ni ONE WAY TRAFFIC, ALLEGIANCE KWA NABEVERY KWANZA, Nadhani tu dulussu ni dualcitizen na Ubelgoji, anakuja huku anakunta, anaenda kule anakula. Like I said, Marekani wabaruhusu dual citizenship kwa magarti kwambavuape na kutekeleza anri hii ifuatayo:
"I hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state, or sovereignty, of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America ...".
Yaani the United Republic of Tanzania, ya Nyerere, na Karume, na Mirambo, na Kinjiketile, ni FOREIGN POTENTATE. Halafu anategemea twende Yanga pamoja? Over me dead body!
Uraia pacha si lazima uwe kwa watu wote. Tunaweza kuruhusu wazawa wa Tanzania peke yao au wao na vizazi vyao nakadhalika.
Hujagundua kwamba presha ya walio nje kutaka uraia wao wa TZ ni kubwa kuliko walioko ndani kutaka uraia wa nje? Wengi wenye kazi za maana nje ya nchi, hawakuhitaji na hawahitaji kuchukuwa uraia wa huko, tatizo ni wale waliojiripua!Nani anaukana uraia wa Tanzania kwa ajili ya kuwavimbia watu?
Watu wanachukua uraia wa mataifa mengine kwa ajili ya kupata fursa mbalimbali katika mataifa hayo, sio for show off.
Mentality kama hii ya kudhani watu wanachukua uraia mwingine kwa ajili ya kujikweza ndio wivu wenyewe.
Pia wengine waonataka uraia pacha bado ni watanzania na wanataka kupata uraia wa mataifa mengine ili fursa fulani ziwafungukie. Hivyo tukiruhusu uraia pacha tunaweza kusaidia vijana wengi wenye sifa hapa tz wakapata ajira na fursa nyingine za elimu na biashara huko nje.
Hivi unafikiri tatizo la hao wanaoweka roho ngumu ni kushawishiwa? Watashaiwishiwa kwa point zipi za ziada juu ya suala hili? faida zote wameshaambiwa, mifano yote wameshapewa, ndio maana tumefikia kuamini kwamba issue sio uzalendo wala usalama wa taifa, ni selfishness na wivu sio na maana.Tatizo hiyo ajenda ya roho mbaya ndio mmeishikilia na ndio inayowakwamisha! Badala kushawishi kwa hoja mnawasema wenye mamlaka wana roho mbaya unadhani watawasaidia kweli... Sasa mimi nikuonee roho mbaya ya nini wakati sina na sitamani uraia wa aina hiyo maana hustle zangu zote ni hapa hapa na natoboa hapa hapa!
Sio kweli Mkuu; USA, UK, SOUTH AFRICA, CANADA wanaruhusu dual citizenship. Fanya tafiti yako vizuriKwa nini unatenga Afrika tu? Nji zifuatazo DUNIANI haziruhusu uraia pacha:
INDIA ISRAEL USA UK PAKISTAN SAUDI CANADA URUGUAY SOUTH AFRICA ETC ETC
Issue si "kuruhusu", isyu ni kwamba, mathalani, USA watakuruhusu tu kama utaitema hiyo inji ingine. In other words, dual citizenship ni ONE WAY TRAFFIC, ALLEGIANCE KWA NABEVERY KWANZA, Nadhani tu dulussu ni dualcitizen na Ubelgoji, anakuja huku anakunta, anaenda kule anakula. Like I said, Marekani wabaruhusu dual citizenship kwa magarti kwambavuape na kutekeleza anri hii ifuatayo:
"I hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state, or sovereignty, of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America ...".
Yaani the United Republic of Tanzania, ya Nyerere, na Karume, na Mirambo, na Kinjiketile, ni FOREIGN POTENTATE. Halafu anategemea twende Yanga pamoja? Over me dead body!
Yeye mwenyewe ni diaspora lakini kawa waziri, au yeye ana urai pacha? mimi sidhani uraia pacha ni tatizo la mtu kutoweza kuwekeza au kupata ajira huku nyumbani.hizo ni sababu tu, kwani watu wengi walio nje wamewekeza huku Tanzania pasi huo uraia pacha,watu waache visingizio kuwa eti wanashindwa kuwekeza au wanakosa fursa sababu ya uraia pacha semeni tu huko majuu maisha magumu.Balozi Malamula hivi karibuni ametooa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.
Nilishaziponda sana point za Watanzania ambao wanadai kuwa tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa watu watakaochukua uraia pacha sio wazalendo. Niliuliza uzalendo katika mambo gani hasa? Ni kitu gani ambacho watu wanaona mtu mwenye uraia pacha atafanya kwa nchi hii ambacho kitakuwa ni ukosefu wa uzalendo?
Hata nilisema kuna nafasi kubwa ya mtu asiye na uraia pacha kukosa uzalendo kuliko hao watakaokuwa na uraia pacha. Mnaweza kuniambia hawa mafisadi wanaoipiga sana hii nchi, wanaoiba mafuta kigamboni, watu kama kina Ole Sabaya, watu wanaokula fedha za miradi ya serikali, wanafanya hivyo kwa sababu wana uraia pacha?
Hiyo nafasi ya raia pacha kuifanyia Tanzania matendo ya kukosa uzalendo itakuwa katika mambo gani? Hebu tuangalie baadhi ya nchi hapa Afrika zenye uraia pacha, na tuwaulize wameathirika vipi na ukosefu wa uzalendo kwa raia pacha wao; South Afrika, Kenya, Ghana, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda nk? Hivi kuna mtu makini mambo ya uzalendo kama Kagame? Kwamba hakutafakari hadi kuruhusu uraia pacha kwa Rwanda? Isitoshe, kwani nani alisema tutaruhusu uraia pacha bila kuweka vigezo kama ukiwa raia pacha huruhusiwi kuwa labda raisi au waziri wa Tanzania? Huo unabaki kuwa uamuzi wetu.
Kwa sasa ni nchi nyingi za Afika zinazoruhusu uraia pacha ni nyingi kuliko zisizoruhusu uraia pacha (angalia ramani hapo chini). Kuna nchi kama Somalia, Liberia, ambao wamekuwa na maraisi waliokuwa na uraia pacha, waliharibu kitu gani? Mnafikiri ni kwa nini?
Balozi Malamula, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia pacha.
Tatizo ni kwamba watu wanaopinga uraia pacha Tanzania wanafanya hivyo kwa sababu za wivu na ubinafsi tu, wala sio uzalendo. Wengi wao hawajawahi hata kutoka nje ya Tanzania. Na wengi wao hata chembe ya huo uzalendo hawana. Isitoshe, wengi wa wanaopinga uraia pacha wala hawaelewi kanuni na utaratibu wa mtu kupata uraia pacha. Watu wanadhani mtu anaenda tu kujiandikisha mahali apewe uraia pacha, kwa hiyo labda tukiruhusu uraia pacha labda nusu ya Watanzania wataomba uraia pacha!
Kuwa raia pacha sio jambo rahisi, linahitaji uwe umeishi nchi ya pili kama mkazi kwa muda mrefu mara nyingi zaidi ya miaka mitano. Tunaposema Tanzania iruhusu uraia pacha, kimsingi sio Tanzania inayoruhusu, bali ni nchi ya uraia wa pili kama itamrughusu huyo Mtanzania kuwa raia wake. Na sio suala la kusema mie nataka kuwa raia pacha na USA wakati hata USA hujawahi kufika, achilia mbali kuishi!
Kwa hiyo Balozi Malamula, suala la uraia pacha lisisubiri Katiba mpya. Mswaada wa uraia pacha upelekwe tena Bungeni, au ufufuliwe ule uliokuwa umepelekwa. Kuna wakati lilipelekwa Bungeni likapitishwa, na Kikwete ndio alishauri kwamba kwa kuwa tuna mchakato wa Katiba mpya, badala ya kulipitisha kama Sheria mpya basi liingizwe kwenye katiba mpya - na hapo ndipo tulipokosea. Tuliwapa nafasi watu wenye ubishi wa kitoto kuleta hoja zao zisizo na mshiko nyuma ya ajenda zao za wivu usio na maana. Na karibu wote wanaobisha au kupinga uraia pacha hawajui maana ya uraia pacha na taratibu za mtu kuwa raia pacha. Si watu wa kusikilizwa katika msingi huu, waelimishwe kwanza, kutia ndani na wabunge.
View attachment 1808843
Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:
Ni aibu kuona Wabunge wa CCM na wengineo wakibisha bila kujua maana ya uraia pacha au mtu anakuwaje raia pacha!
Wakati Tanzania imezama katika mawazo mgando ya mwaka 47 kuwakatalia raia zake uraia pacha, nchi nyingine sasa zinatoa uraia kukaribisha wawekezaji!
Wengi wanaopinga uraia pacha, wanajua hawana nafasi ya kuja kuwa raia pacha
Na wengine:
Mkuu acha kuongea bila kuingia ndani. Hebu jaribu uende Bank Kuu waambie wewe ni Mtanzania unataka kutuma dola 2000 kwenda Uganda usikie watakuambiaje. Halafu waambie wewe ni raia wa Uganda unataka kutuma hizo dola Uganda. Hiyo itaanza kukuonyesha tofauti.Yeye mwenyewe ni diaspora lakini kawa waziri, au yeye ana urai pacha? mimi sidhani uraia pacha ni tatizo la mtu kutoweza kuwekeza au kupata ajira huku nyumbani.hizo ni sababu tu, kwani watu wengi walio nje wamewekeza huku Tanzania pasi huo uraia pacha,watu waache visingizio kuwa eti wanashindwa kuwekeza au wanakosa fursa sababu ya uraia pacha semeni tu huko majuu maisha magumu.
Balozi Malamula hivi karibuni ametooa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.
Nilishaziponda sana point za Watanzania ambao wanadai kuwa tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa watu watakaochukua uraia pacha sio wazalendo. Niliuliza uzalendo katika mambo gani hasa? Ni kitu gani ambacho watu wanaona mtu mwenye uraia pacha atafanya kwa nchi hii ambacho kitakuwa ni ukosefu wa uzalendo?
Hata nilisema kuna nafasi kubwa ya mtu asiye na uraia pacha kukosa uzalendo kuliko hao watakaokuwa na uraia pacha. Mnaweza kuniambia hawa mafisadi wanaoipiga sana hii nchi, wanaoiba mafuta kigamboni, watu kama kina Ole Sabaya, watu wanaokula fedha za miradi ya serikali, wanafanya hivyo kwa sababu wana uraia pacha?
Hiyo nafasi ya raia pacha kuifanyia Tanzania matendo ya kukosa uzalendo itakuwa katika mambo gani? Hebu tuangalie baadhi ya nchi hapa Afrika zenye uraia pacha, na tuwaulize wameathirika vipi na ukosefu wa uzalendo kwa raia pacha wao; South Afrika, Kenya, Ghana, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda nk? Hivi kuna mtu makini mambo ya uzalendo kama Kagame? Kwamba hakutafakari hadi kuruhusu uraia pacha kwa Rwanda? Isitoshe, kwani nani alisema tutaruhusu uraia pacha bila kuweka vigezo kama ukiwa raia pacha huruhusiwi kuwa labda raisi au waziri wa Tanzania? Huo unabaki kuwa uamuzi wetu.
Kwa sasa ni nchi nyingi za Afika zinazoruhusu uraia pacha ni nyingi kuliko zisizoruhusu uraia pacha (angalia ramani hapo chini). Kuna nchi kama Somalia, Liberia, ambao wamekuwa na maraisi waliokuwa na uraia pacha, waliharibu kitu gani? Mnafikiri ni kwa nini?
Balozi Malamula, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia pacha.
Tatizo ni kwamba watu wanaopinga uraia pacha Tanzania wanafanya hivyo kwa sababu za wivu na ubinafsi tu, wala sio uzalendo. Wengi wao hawajawahi hata kutoka nje ya Tanzania. Na wengi wao hata chembe ya huo uzalendo hawana. Isitoshe, wengi wa wanaopinga uraia pacha wala hawaelewi kanuni na utaratibu wa mtu kupata uraia pacha. Watu wanadhani mtu anaenda tu kujiandikisha mahali apewe uraia pacha, kwa hiyo labda tukiruhusu uraia pacha labda nusu ya Watanzania wataomba uraia pacha!
Kuwa raia pacha sio jambo rahisi, linahitaji uwe umeishi nchi ya pili kama mkazi kwa muda mrefu mara nyingi zaidi ya miaka mitano. Tunaposema Tanzania iruhusu uraia pacha, kimsingi sio Tanzania inayoruhusu, bali ni nchi ya uraia wa pili kama itamrughusu huyo Mtanzania kuwa raia wake. Na sio suala la kusema mie nataka kuwa raia pacha na USA wakati hata USA hujawahi kufika, achilia mbali kuishi!
Kwa hiyo Balozi Malamula, suala la uraia pacha lisisubiri Katiba mpya. Mswaada wa uraia pacha upelekwe tena Bungeni, au ufufuliwe ule uliokuwa umepelekwa. Kuna wakati lilipelekwa Bungeni likapitishwa, na Kikwete ndio alishauri kwamba kwa kuwa tuna mchakato wa Katiba mpya, badala ya kulipitisha kama Sheria mpya basi liingizwe kwenye katiba mpya - na hapo ndipo tulipokosea. Tuliwapa nafasi watu wenye ubishi wa kitoto kuleta hoja zao zisizo na mshiko nyuma ya ajenda zao za wivu usio na maana. Na karibu wote wanaobisha au kupinga uraia pacha hawajui maana ya uraia pacha na taratibu za mtu kuwa raia pacha. Si watu wa kusikilizwa katika msingi huu, waelimishwe kwanza, kutia ndani na wabunge.
View attachment 1808843
Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:
Ni aibu kuona Wabunge wa CCM na wengineo wakibisha bila kujua maana ya uraia pacha au mtu anakuwaje raia pacha!
Wakati Tanzania imezama katika mawazo mgando ya mwaka 47 kuwakatalia raia zake uraia pacha, nchi nyingine sasa zinatoa uraia kukaribisha wawekezaji!
Wengi wanaopinga uraia pacha, wanajua hawana nafasi ya kuja kuwa raia pacha
Na wengine:
Mkuu acha uongo nini hizo usd 2000 mimi mwenyewe natuma au na kupokea zaidi ya hizo USD kutoka nchi mbalimbali kwa kupitia akaunti ya kigeni , cha muhimu ni kuweka bayana kuwa unafanya shughuli gani ili kuepusha utakatishaji pesa .Na nikuuliza toka lini Benki Kuu inafanya miamala ya watu binafsi? Benki Kuu niende kufanya nini wakati benki hizi za biashara ndio hufanya miamala ya pesa za kigeni. Kifupi nadhani hujui unachoongea bali umefuata tu mkumbo.Mkuu acha kuongea bila kuingia ndani. Hebu jaribu uende Bank Kuu waambie wewe ni Mtanzania unataka kutuma dola 2000 kwenda Uganda usikie watakuambiaje. Halafu waambie wewe ni raia wa Uganda unataka kutuma hizo dola Uganda. Hiyo itaanza kukuonyesha tofauti.
Okay tunapishana. Kwa taarifa yako kuna watu wana account BOT. Lakini nilitaka kusema nenda banki yako kutuma hizo dola usikie utaambiwaje. Si kweli unatuma dola nje kutumia benki, hapo unadanganya. Na sio tu suala la kueleza kwa nini unataka kutuma. Lazima uonyeshe invoice, sijui nini, sijui nini. Ndio maana hakuna internet banking Tanzania inayokuruhusu kutuma hela nje ya nchi, au hata dola ndani ya nchi. Na hao wanaokutumia dola toka nje wanapitia hayo hayo. Sio kwamba wanatuma kirahisi tu kila nchi. Hata South Africa hapa inabidi raia wajieleze wakitaka kutuma fedha nje kupitia benki. Sema angalau siku hizi ni nafuu kuna vitu kama Mpesa. Angalia masharti haya, halafu wewe unasema unatuma tu kirahisiMkuu acha uongo nini hizo usd 2000 mimi mwenyewe natuma au na kupokea zaidi ya hizo USD kutoka nchi mbalimbali kwa kupitia akaunti ya kigeni , cha muhimu ni kuweka bayana kuwa unafanya shughuli gani ili kuepusha utakatishaji pesa .Na nikuuliza toka lini Benki Kuu inafanya miamala ya watu binafsi? Benki Kuu niende kufanya nini wakati benki hizi za biashara ndio hufanya miamala ya pesa za kigeni. Kifupi nadhani hujui unachoongea bali umefuata tu mkumbo.
Sio kweli Mkuu; USA, UK, SOUTH AFRICA, CANADA wanaruhusu dual citizenship. Fanya tafiti yako vizuri
Nchi za nje ya Afrika zinazoruhusu dual citizenship ni hizi hapa; hizi ndizo tukiruhusu uraia pacha baadhi ya wenzetu watakuwa na uraia wa Tanzania na wa hizi nchi, ukiacha zile za Afrika
Albania, Armenia, Austria, Australia, Bangladesh, Belgium, Brazil Bulgaria Canada Chile Colombia Cyprus Denmark Dominica Ecuador El Salvador Fiji Finland France Germany Georgia Greece Grenada Hungary Iceland Iraq Ireland Israel Italy Jordan Kosovo Latvia Lebanon Lithuania Luxembourg Macedonia Malta Mexico Moldova Montenegro New Zealand Pakistan Peru Philippines Poland Portugal Romania Russia Serbia Slovenia Spain Sri Lanka St. Kitts and Nevis Sweden Switzerland Syria Thailand Turkey United Kingdom United States of America Vietnam Western Samoa