BlackPanther
JF-Expert Member
- Nov 25, 2015
- 9,185
- 8,715
Hata mondi ana views nyingi kuliko wizkid kwahyo sio ishu...
Sawa...watu kama wewe hawakosekani..Muhimu walioafiki mpaka sasa ni wengi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata mondi ana views nyingi kuliko wizkid kwahyo sio ishu...
Ni wangapi kati ya milioni 60Sawa...watu kama wewe hawakosekani..Muhimu walioafiki mpaka sasa ni wengi.
Hoja ili ionekana ni yenye Manufaa lazima ilindwe na Hoja, lazima ilijibu changamoto Kaza wa kaza, lazima iangaliwe kwa mitazamo yote miwili i mean Hasi na Chanya na ulinganifu uwepo ili kufanya maamuzi , Sasa hili swala Uraia pacha Diaspora members wanataka tu huo urai uwepo bila hata kuleta Fact zikafanyiwa screening ! Mushaona wapi hii.
Tatizo mtu akishaenda tu inje anawaona alowaacha huko nyumbani ni Ngumbaru kuliko Maelezo ! None sense
Mambo ya Uraia pacha hatutaki...
Mkuu sio iwe ya kibaguzi. Kwa wale waliopoteza uraia baada kuchukua uraia wa nchi nyingine, serikali itaamua kama warudishiwe haki zao za uraia. Tunazungumzia wale ambao bado hawajuchukua uraia wa nchi nyingine kwa kuogopa kupoteza uraia wa Tanzania na baadae.Naanza kuelewa - kwamba uraia pacha uwe wa kiubaguzi fulani hivi yaani Mtanzania aliyepoteza utanzania wake kwa kuukana alipotaka kufanikiwa akiwa nje ya Tanzania, aruhusiwe ku-reclaim uraia wake wa awali bila kupoteza uraia wake wa nchi ya pili; na iwe kwa kesi hizo tu na si vinginevyo.
Pili tusichanganye diaspora na uraia pacha maana diaspora kusaidia ndugu zake hakulazimishi mpaka awe na uraia pacha, au?
Najua hilo, ndio maana nasema hakuna sababu ya muhimu zaidi ya kuendesha nchi kwa fikra za kichawi badala ya kisomi.Mkuu, imesemwa hapo juu Membe akiwa Waziri wa Mambo ya Nje alilifanyia utafiti sana, na kukutana na viongozi wa Afrika na nchi za Magharibi kuelewa undani wake, na uzoefu wao baada ya kuruhusu uraia pacha. Ndio maana akatoa tamko kwamba akiwa raisi hilo ni jambo ataruhusu mara moja. Na kumbuka Membe alikuwa Mkurugenzi wa TISS, kwa hiyo hili suala la usalama wa nchi yeye aliliona kwa mapana kuliko hawa mabulikoko humu ndani wanaodai kwamba uraia pacha utaathiri usalama wa nchi
Ni wangapi kati ya milioni 60
Wanataka tusichakate pisi za kimalikia mpaka tunakufa ,it's not fair [emoji1787][emoji1787]Mkuu Smart911, vipi tena kamanda wangu! Tushukuru Mungu hili swala likipitishwa, lina faida kubwa sana.. Nchi nyingi za afrika zimeruhusu uraia pacha, na zimeendelea.
Mambo ya Uraia pacha hatutaki...
Wivu na roho mbaya itakumaliza ndugu...kwani wakiruhusu utahasirika nini!
Hapo umenichanganya. Dual cizitenship na uraia pacha si kitu kilekile? So how come India does not allow holding Indian citizenship and citizenship of a foreign country, but allows dual citizenship at the same time? So what is dual citizenship to India?
| Overseas Citizen of India | |
|---|---|
Front Cover of an OCI card | |
| First issued | 2 December 2005 |
| Purpose | Visa, Identification |
| Eligibility | see eligibility |
| Cost | ₹15000 (In India) US $275 (abroad) Renewal ₹1400 (In India) Renewal US $25 (abroad) |
Membe akiwa Foreign Affairs alisafiri nchi nyingi za Africa na Caribbean kukusanya maoni ya faida na hasara kutoka nchi hizo ambazo zote zinaruhusu uraia pacha na hitimisho lake lilikuwa kwamba faida ni nyingi mno kuliko hasara na hakukuwa na hasara zozote. Yule mnafiki Kikwete baada ya kuona maccm wanapinga uraia pacha kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu akamruka Membe. Hizo FACTS ziletwe mara ngapi? Unadhani nchi nyingi za Africa ambazo zimeamua kuruhusu uraia pacha ZIMEKURUPUKA bila kufanya TATHMINI ya kina?
Tatizo hiyo ajenda ya roho mbaya ndio mmeishikilia na ndio inayowakwamisha! Badala kushawishi kwa hoja mnawasema wenye mamlaka wana roho mbaya unadhani watawasaidia kweli... Sasa mimi nikuonee roho mbaya ya nini wakati sina na sitamani uraia wa aina hiyo maana hustle zangu zote ni hapa hapa na natoboa hapa hapa!Wivu na roho mbaya itakumaliza ndugu...kwani wakiruhusu utahasirika nini!
Mkuu BAK, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia pacha.
Sisi tunasubiri nini! Aise hii nchi basi tu!! Mungu asaidie kwakweli.
Tatizo hiyo ajenda ya roho mbaya ndio mmeishikilia na ndio inayowakwamisha! Badala kushawishi kwa hoja mnawasema wenye mamlaka wana roho mbaya unadhani watawasaidia kweli... Sasa mimi nikuonee roho mbaya ya nini wakati sina na sitamani uraia wa aina hiyo maana hustle zangu zote ni hapa hapa na natoboa hapa hapa!
NTIMA NYONGO Mkuu! Watu wanakuja na sababu zisizo na kichwa wala miguu oh! Watatuletea majasusi! Oh! Watakuja kufanya wizi wa kutisha kisha wakimbilie kwao wakati majizi ya nchi hii yanaishi hapa hapa nchini na wala hayana uDC na yanakwiba trillions za walipa kodi. Sitashangaa Mkuu Tanzania kama itakuwa nchi ya mwisho katika Afrika kuruhusu uraia pacha.
Okay nimekuelewa Mkuu! Hiyo haina maana, kwa kuwa ni permanent residency ambayo wao wameamua kuiita citizenship. Ona wanavyoichezea;The OCI scheme was introduced by The Citizenship (Amendment) Act, 2005 in response to demands for dual citizenship by the Indian diaspora. It provides Overseas citizens many of the rights available to resident citizens. However, in a notification issued in March 2021, the government of India has dramatically curtailed those rights.[4]
OCI status is not available to anyone who has ever been a Pakistani or Bangladeshi citizen, or who is a child, grandchild, or great-grandchild of such a person.
Hapa wame curtail kwa sababu za mambo yao ya uhasama wa tamaduni zao India vs Pakistan na Bangladesh. Sisi so far hatuna hizo tofauti au sijategemea kuwa zitawekwaOkay nimekuelewa Mkuu! Hiyo haina maana, kwa kuwa ni permanent residency ambayo wao wameamua kuiita citizenship. Ona wanavyoichezea;
March 2021, the government of India has dramatically curtailed those rights. OCI status is not available to anyone who has ever been a Pakistani or Bangladeshi citizen, or who is a child, grandchild, or great-grandchild of such a person.
Bila shaka Mheshimiwa Balozi anajua hili, alikuwa Marekani:Balozi Malamula hivi karibuni ametooa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.
Nilishaziponda sana point za Watanzania ambao wanadai kuwa tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa watu watakaochukua uraia pacha sio wazalendo. Niliuliza uzalendo katika mambo gani hasa? Ni kitu gani ambacho watu wanaona mtu mwenye uraia pacha atafanya kwa nchi hii ambacho kitakuwa ni ukosefu wa uzalendo?
Hata nilisema kuna nafasi kubwa ya mtu asiye na uraia pacha kukosa uzalendo kuliko hao watakaokuwa na uraia pacha. Mnaweza kuniambia hawa mafisadi wanaoipiga sana hii nchi, wanaoiba mafuta kigamboni, watu kama kina Ole Sabaya, watu wanaokula fedha za miradi ya serikali, wanafanya hivyo kwa sababu wana uraia pacha?
Hiyo nafasi ya raia pacha kuifanyia Tanzania matendo ya kukosa uzalendo itakuwa katika mambo gani? Hebu tuangalie baadhi ya nchi hapa Afrika zenye uraia pacha, na tuwaulize wameathirika vipi na ukosefu wa uzalendo kwa raia pacha wao; South Afrika, Kenya, Ghana, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda nk? Hivi kuna mtu makini mambo ya uzalendo kama Kagame? Kwamba hakutafakari hadi kuruhusu uraia pacha kwa Rwanda? Isitoshe, kwani nani alisema tutaruhusu uraia pacha bila kuweka vigezo kama ukiwa raia pacha huruhusiwi kuwa labda raisi au waziri wa Tanzania? Huo unabaki kuwa uamuzi wetu.
Kwa sasa ni nchi nyingi za Afika zinazoruhusu uraia pacha ni nyingi kuliko zisizoruhusu uraia pacha (angalia ramani hapo chini). Kuna nchi kama Somalia, Liberia, ambao wamekuwa na maraisi waliokuwa na uraia pacha, waliharibu kitu gani? Mnafikiri ni kwa nini?
Balozi Malamula, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia pacha.
Tatizo ni kwamba watu wanaopinga uraia pacha Tanzania wanafanya hivyo kwa sababu za wivu na ubinafsi tu, wala sio uzalendo. Wengi wao hawajawahi hata kutoka nje ya Tanzania. Na wengi wao hata chembe ya huo uzalendo hawana. Isitoshe, wengi wa wanaopinga uraia pacha wala hawaelewi kanuni na utaratibu wa mtu kupata uraia pacha. Watu wanadhani mtu anaenda tu kujiandikisha mahali apewe uraia pacha, kwa hiyo labda tukiruhusu uraia pacha labda nusu ya Watanzania wataomba uraia pacha!
Kuwa raia pacha sio jambo rahisi, linahitaji uwe umeishi nchi ya pili kama mkazi kwa muda mrefu mara nyingi zaidi ya miaka mitano. Tunaposema Tanzania iruhusu uraia pacha, kimsingi sio Tanzania inayoruhusu, bali ni nchi ya uraia wa pili kama itamrughusu huyo Mtanzania kuwa raia wake. Na sio suala la kusema mie nataka kuwa raia pacha na USA wakati hata USA hujawahi kufika, achilia mbali kuishi!
Kwa hiyo Balozi Malamula, suala la uraia pacha lisisubiri Katiba mpya. Mswaada wa uraia pacha upelekwe tena Bungeni, au ufufuliwe ule uliokuwa umepelekwa. Kuna wakati lilipelekwa Bungeni likapitishwa, na Kikwete ndio alishauri kwamba kwa kuwa tuna mchakato wa Katiba mpya, badala ya kulipitisha kama Sheria mpya basi liingizwe kwenye katiba mpya - na hapo ndipo tulipokosea. Tuliwapa nafasi watu wenye ubishi wa kitoto kuleta hoja zao zisizo na mshiko nyuma ya ajenda zao za wivu usio na maana. Na karibu wote wanaobisha au kupinga uraia pacha hawajui maana ya uraia pacha na taratibu za mtu kuwa raia pacha. Si watu wa kusikilizwa katika msingi huu, waelimishwe kwanza, kutia ndani na wabunge.
View attachment 1808843
Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:
Ni aibu kuona Wabunge wa CCM na wengineo wakibisha bila kujua maana ya uraia pacha au mtu anakuwaje raia pacha!
Wakati Tanzania imezama katika mawazo mgando ya mwaka 47 kuwakatalia raia zake uraia pacha, nchi nyingine sasa zinatoa uraia kukaribisha wawekezaji!
Wengi wanaopinga uraia pacha, wanajua hawana nafasi ya kuja kuwa raia pacha
Na wengine: