soine
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 2,113
- 2,329
Marekani na ujanja wake wote inaingiliwa sembuse sisi, kwa sasa in uhakika gani kwamba hawapo?Mnataka mtuletee majasusi kijanja, bakini huko huko
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Marekani na ujanja wake wote inaingiliwa sembuse sisi, kwa sasa in uhakika gani kwamba hawapo?Mnataka mtuletee majasusi kijanja, bakini huko huko
Diaspora kusaidia huleta kuona fursa, wanapoona fursa huja kuwekeza...inanoga zaidi ninapokuja kuwekeza kama raia mzawaNaanza kuelewa - kwamba uraia pacha uwe wa kiubaguzi fulani hivi yaani Mtanzania aliyepoteza utanzania wake kwa kuukana alipotaka kufanikiwa akiwa nje ya Tanzania, aruhusiwe ku-reclaim uraia wake wa awali bila kupoteza uraia wake wa nchi ya pili; na iwe kwa kesi hizo tu na si vinginevyo.
Pili tusichanganye diaspora na uraia pacha maana diaspora kusaidia ndugu zake hakulazimishi mpaka awe na uraia pacha, au?
Nchi pekee zilizobaki Afrika kuruhusu uraia pacha ni
Sasa kama huu sio udungaembe ni nini?
- Tanzania
- Equatorial Guinea
- DRC
- Lesotho
- Malawi
- Zambia
- Cameroon (nadhani hawa wameruhusu sasa)
- Ethiopia (nadhani wameruhusu sasa)
- Liberia (Sielwi ilikuwaje walikuwa na raisi mwenye uraia wa wa nchi nyingine, Ellen Johnson Sirleaf)
- Eritrea
Ndio, kama sababu zenu ni zile za Mbwa mwitu kumwambia mwanakondoo aliyezaliwa mwaka huu kwamba wewe mwaka jana ulinitukana, kama sio wivu unawasumbua ni kitu gani? La sivyo sababu zenu za uzalendo na usalama ni za kitoto sana. Angalia hiyo ramani hapo juu. Tutakuwa madungaembe hadi lini?
Kwa taarifa yako mie sio Diaspora lakini naona umuhimu wa uraia pacha.
Wekeza huko ulipoDiaspora kusaidia huleta kuona fursa, wanapoona fursa huja kuwekeza...inanoga zaidi ninapokuja kuwekeza kama raia mzawa
Maskini mwenyewe, ukome kuita Tanzania ni maskini, endelea kutawaza wazee huko uliko kwa matajiri, huna akili kabisaOna sasa nchi zilizobaki ni masikini wa kutupwa,
Mkuu Ingawa sina Hoja kali kama Zako ila Uraia Pacha utatuua...wahinndiu watachukua kila tuu kuanzia ajira...
Hapa Tuu sasa hivi wao ndio wanaongoza kwa Uraia Pacha wa Uingereza,Canada na India na hapa Bongo wamebadilisha sana Visa/Permit to work Wengine wanaishi zaidi ya Miaka 10
Kufanya Kazi eti ya Expert anabadilisha tuu cheo,Leo hiki kesho kile ili isibumbuluke...Uhamiaji ni sheeedah,Wahindi Shikamooni...
Mmewakomoa sana migration hadi Wameshiba tena wanawasaidia namna ya Kuishi
Nyie ma raia pacha uchwara someni hiyoKuwa na Uraia pacha ni Uoga , Wapigaji akipiga Bongo akimbilie Marekani , utamfanya nini wakati yeye ni Mu USA !
Maskini mwenyewe, ukome kuita Tanzania ni maskini, endelea kutawaza wazee huko uliko kwa matajiri, huna akili kabisa
Don't follow majority.......... fata akili yako, Tanzania tunafata akili zetuAcha hivyo ndugu yangu, ebu tuwe kitu kimoja kuunga mkono hii kitu, ina manufaa makubwa sana kwetu. Nchi 44 kama sio 46 za afrika zimeruhusu uraia pacha, sasa kwanini na sisi tusifanye hivyo!!! Ni hayo tu mkuu ikigijo
Tunawaonea wivu nyinyi diaspora ?
Sasa kwa nini tuhangaike kubadilisha sheria kuwasapoti watu ambao wanatukashfu tuliopo hapa nchini wakisema wao wako njema mpaka tunawaonea wivu ?
Hoja nyepesi za wana diaspora ndio hizi maskini ya Mungu.
Wa adopt system ya IndiaBalozi Malamula hivi karibuni ametooa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.
Nilishaziponda sana point za Watanzania ambao wanadai kuwa tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa watu watakaochukua uraia pacha sio wazalendo. Niliuliza uzalendo katika mambo gani hasa? Ni kitu gani ambacho watu wanaona mtu mwenye uraia pacha atafanya kwa nchi hii ambacho kitakuwa ni ukosefu wa uzalendo?
Hata nilisema kuna nafasi kubwa ya mtu asiye na uraia pacha kukosa uzalendo kuliko hao watakaokuwa na uraia pacha. Mnaweza kuniambia hawa mafisadi wanaoipiga sana hii nchi, wanaoiba mafuta kigamboni, watu kama kina Ole Sabaya, watu wanaokula fedha za miradi ya serikali, wanafanya hivyo kwa sababu wana uraia pacha?
Hiyo nafasi ya raia pacha kuifanyia Tanzania matendo ya kukosa uzalendo itakuwa katika mambo gani? Hebu tuangalie baadhi ya nchi hapa Afrika zenye uraia pacha, na tuwaulize wameathirika vipi na ukosefu wa uzalendo kwa raia pacha wao; South Afrika, Kenya, Ghana, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda nk? Hivi kuna mtu makini mambo ya uzalendo kama Kagame? Kwamba hakutafakari hadi kuruhusu uraia pacha kwa Rwanda? Isitoshe, kwani nani alisema tutaruhusu uraia pacha bila kuweka vigezo kama ukiwa raia pacha huruhusiwi kuwa labda raisi au waziri wa Tanzania? Huo unabaki kuwa uamuzi wetu.
Kwa sasa ni nchi nyingi za Afika zinazoruhusu uraia pacha ni nyingi kuliko zisizoruhusu uraia pacha (angalia ramani hapo chini). Kuna nchi kama Somalia, Liberia, ambao wamekuwa na maraisi waliokuwa na uraia pacha, waliharibu kitu gani? Mnafikiri ni kwa nini?
Balozi Malamula, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia pacha.
Tatizo ni kwamba watu wanaopinga uraia pacha Tanzania wanafanya hivyo kwa sababu za wivu na ubinafsi tu, wala sio uzalendo. Wengi wao hawajawahi hata kutoka nje ya Tanzania. Na wengi wao hata chembe ya huo uzalendo hawana. Isitoshe, wengi wa wanaopinga uraia pacha wala hawaelewi kanuni na utaratibu wa mtu kupata uraia pacha. Watu wanadhani mtu anaenda tu kujiandikisha mahali apewe uraia pacha, kwa hiyo labda tukiruhusu uraia pacha labda nusu ya Watanzania wataomba uraia pacha!
Kuwa raia pacha sio jambo rahisi, linahitaji uwe umeishi nchi ya pili kama mkazi kwa muda mrefu mara nyingi zaidi ya miaka mitano. Tunaposema Tanzania iruhusu uraia pacha, kimsingi sio Tanzania inayoruhusu, bali ni nchi ya uraia wa pili kama itamrughusu huyo Mtanzania kuwa raia wake. Na sio suala la kusema mie nataka kuwa raia pacha na USA wakati hata USA hujawahi kufika, achilia mbali kuishi!
Kwa hiyo Balozi Malamula, suala la uraia pacha lisisubiri Katiba mpya. Mswaada wa uraia pacha upelekwe tena Bungeni, au ufufuliwe ule uliokuwa umepelekwa. Kuna wakati lilipelekwa Bungeni likapitishwa, na Kikwete ndio alishauri kwamba kwa kuwa tuna mchakato wa Katiba mpya, badala ya kulipitisha kama Sheria mpya basi liingizwe kwenye katiba mpya - na hapo ndipo tulipokosea. Tuliwapa nafasi watu wenye ubishi wa kitoto kuleta hoja zao zisizo na mshiko nyuma ya ajenda zao za wivu usio na maana. Na karibu wote wanaobisha au kupinga uraia pacha hawajui maana ya uraia pacha na taratibu za mtu kuwa raia pacha. Si watu wa kusikilizwa katika msingi huu, waelimishwe kwanza, kutia ndani na wabunge.
View attachment 1808843
Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:
Ni aibu kuona Wabunge wa CCM na wengineo wakibisha bila kujua maana ya uraia pacha au mtu anakuwaje raia pacha!
Wakati Tanzania imezama katika mawazo mgando ya mwaka 47 kuwakatalia raia zake uraia pacha, nchi nyingine sasa zinatoa uraia kukaribisha wawekezaji!
Wengi wanaopinga uraia pacha, wanajua hawana nafasi ya kuja kuwa raia pacha
Na wengine:
Wabeba mabox wana pesa kukukushinda, na wana ujuzi,uzoefu, kusinda weweTuonyesheni vya maana mlivyofanya huko mlipo wehu nyie, mabox yakubeba yameisha mnataka kurudi
Si uwe tu raia wa huko kama unaona uraia wa tz hauna faida kwako 😂😂
Ukiangalia faida zingine kama direct investment, kuongeza biashara kati ya nchi hizo mbili, transfer of knowledge, ubunifu, investment in elimu, kilimo, afya, utalii, technology.
Pia work ethics and their self confidence will rub off others. (Wanafanya kazi kwa bidii na kujiamini itasaidia wengine. Sababu USA na EU Lazima ufanye kazi kwa bidii, ujiamini,uthubutu, uwe vizuri zaidi ya wazungu wengi, mvumilivu na uwezo kusoma vitu, mazingira haraka. Otherwise hutoboi.
Hapo umenichanganya. Dual cizitenship na uraia pacha si kitu kilekile? So how come India does not allow holding Indian citizenship and citizenship of a foreign country, but allows dual citizenship at the same time? So what is dual citizenship to India?Wa adopt system ya India
The Constitution of India does not allow holding Indian citizenship and citizenship of a foreign country simultaneously. Based on the recommendation of the High Level committee on Indian Diaspora, the Government of India decided to grant Overseas Citizenship of India (OCI) commonly known as 'dual citizenship
Marekani ni tajiri na inadumu na hali nzuri kwa sababu ya mchanganyiko wa watu, kuna wahindi, wachina, waarabu mpaka wamasai wapo kule.
South Africa ni nchi yenye uchumi mkubwa kwa sababu ya mchanganyiko mkubwa wa watu wa rangi mbalimbali wanaoishi pamoja.
Watanzania wenzetu ambao wapo nje wanao mchango mkubwa sana wa kuipeleka Tanzania mbali kiuchumi, wanao uzoefu (exposure) wa hali ya juu kwenye masuala mengi. Sisi wenyewe kwa kubagua wenzetu hatuwezi kufika mbali.
Hata mondi ana views nyingi kuliko wizkid kwahyo sio ishu...Na ndio maana umepata like moja, ndio utambue uraia pacha unapendwa na wengi, ukiona kitu kinakubalika ujue kina faida na manufaa