Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Kwa hiyo uraia pacha utakuwa wa kiubaguzi? Yaani Mhindi akitaka na uraia wa Tanzania akataliwe, ila Mtanzania akitaka na uraia wa India akubaliwe!
Hoja ya Dangote ilizaliwa na hoja kuwa watanzania walio nje (walioukana uraia) wanashindwa kuja kuwekeza Tanzania kwa kuwa si watanzania tena.
Ndiyo, inatakiwa iwe ya kiubaguzi. Haki ya uraia wa kuzaliwa siyo ndogo kama unatumia akili.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tunawaonea wivu nyinyi diaspora ?

Sasa kwa nini tuhangaike kubadilisha sheria kuwasapoti watu ambao wanatukashfu tuliopo hapa nchini wakisema wao wako njema mpaka tunawaonea wivu ?

Hoja nyepesi za wana diaspora ndio hizi maskini ya Mungu.
Hoja yako ya kukataa uraia pacha ni ipi?
Maana mtoa mada kaelezea kwa nini uraia pacha uruhusiwe.

Wewe hoja yako ni kuwa usiruhusiwe kwa sababu hamna wivu?
 
Mkuu Ingawa sina Hoja kali kama Zako ila Uraia Pacha utatuua...wahinndiu watachukua kila tuu kuanzia ajira...
Hapa Tuu sasa hivi wao ndio wanaongoza kwa Uraia Pacha wa Uingereza,Canada na India na hapa Bongo wamebadilisha sana Visa/Permit to work Wengine wanaishi zaidi ya Miaka 10
Kufanya Kazi eti ya Expert anabadilisha tuu cheo,Leo hiki kesho kile ili isibumbuluke...Uhamiaji ni sheeedah,Wahindi Shikamooni...
Mmewakomoa sana migration hadi Wameshiba tena wanawasaidia namna ya Kuishi
Uraia pacha si lazima uwe kwa watu wote. Tunaweza kuruhusu wazawa wa Tanzania peke yao au wao na vizazi vyao nakadhalika.
 
Udungaembe maana yake ni Nini??.
Kwa nini unatenga Afrika tu? Nji zifuatazo DUNIANI haziruhusu uraia pacha:

INDIA ISRAEL USA UK PAKISTAN SAUDI CANADA URUGUAY SOUTH AFRICA ETC ETC

Issue si "kuruhusu", isyu ni kwamba, mathalani, USA watakuruhusu tu kama utaitema hiyo inji ingine. In other words, dual citizenship ni ONE WAY TRAFFIC, ALLEGIANCE KWA NABEVERY KWANZA, Nadhani tu dulussu ni dualcitizen na Ubelgoji, anakuja huku anakunta, anaenda kule anakula. Like I said, Marekani wabaruhusu dual citizenship kwa magarti kwambavuape na kutekeleza anri hii ifuatayo:

"I hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state, or sovereignty, of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America ...".

Yaani the United Republic of Tanzania, ya Nyerere, na Karume, na Mirambo, na Kinjiketile, ni FOREIGN POTENTATE. Halafu anategemea twende Yanga pamoja? Over me dead body!
 
bila uraia pacha hayo hayawezi kufanyika? Mimi naona linaweza kuwa jambo zuri ila mnaotoa mada bado mko too brief.
Kufafanua kwa ufupi:
Uraia pacha unampa Mtanzania fursa ya kupata haki za raia wa nchi nyingine pia. Kwa mfano, kwenye swala la ajira. Kuna nchi zinazotoa ajira za aina au ngazi fulani kwa kutegemea uraia. Mtanzania mwenye uwezo wa kupata ajira hiyo, tayari anakosa nafasi hiyo kwasababu hana uraia wa nchi hiyo. Hii ni pamoja aina ya contracts ambazo angeweza kupata au unzishwaji wa miradi au kampuni katika nchi nyingine. Gharama huwa kubwa au nafasi chache, hata aishi huko miaka mingapi (ikitegemea pia nchi aliyoko).

Ina maana kwamba, mtanzania anayepata fursa nchi nyingine anapata ushawishi mkubwa wakubadili uraia hasa kama fursa hizo ni nzuri sana. Uraia pacha unampa ushawishi wa kubaki na uraia wake wa Tanzania na hivyo kumpa hamasa yakuendelea kuwekeza nyumbani (Tanzania). Mfano mzuri ni Nigeria. Ifikapo 2023, Wanaijerea waishiyo nje watakuwa wanatuma zaidi ya $35 billioni kwa mwaka, sawa na asilimia 6.1 ya GDP yao. (The New CBN Regulations: Impact on Remittances to Nigeria - AZA)
 
🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾 Uko vizuri Mkuu 👍🏽

Kwani shida ni ya nani? Ni watanzania kutaka uraia wa nchi zingine au wa nchi zingine kutaka uraia wa TZ? Shida ni kwamba kuna wa-TZ walioamua kuukana uraia wao na kuchota uraia wa nchi zingine wakiamini wameukata. Sasa kihoro kinawasumbua wanataka waruhusiwe kuwa tena wa TZ.

Ndo maana unasikia maneno kama kuonea wivu. Ni kwa kuamini kwamba walipopata uraia wa nje waliukata: BAlozi Mula mula huyo muonee huruma tu! NI bahati mbaya leo hii ni waziri labda naye anataka uraia wa Rwanda.
Nani anaukana uraia wa Tanzania kwa ajili ya kuwavimbia watu?

Watu wanachukua uraia wa mataifa mengine kwa ajili ya kupata fursa mbalimbali katika mataifa hayo, sio for show off.

Mentality kama hii ya kudhani watu wanachukua uraia mwingine kwa ajili ya kujikweza ndio wivu wenyewe.

Pia wengine waonataka uraia pacha bado ni watanzania na wanataka kupata uraia wa mataifa mengine ili fursa fulani ziwafungukie. Hivyo tukiruhusu uraia pacha tunaweza kusaidia vijana wengi wenye sifa hapa tz wakapata ajira na fursa nyingine za elimu na biashara huko nje.
 
Kwa nini unatenga Afrika tu? Nji zifuatazo DUNIANI haziruhusu uraia pacha:

INDIA ISRAEL USA UK PAKISTAN SAUDI CANADA URUGUAY SOUTH AFRICA ETC ETC

Issue si "kuruhusu", isyu ni kwamba, mathalani, USA watakuruhusu tu kama utaitema hiyo inji ingine. In other words, dual citizenship ni ONE WAY TRAFFIC, ALLEGIANCE KWA NABEVERY KWANZA, Nadhani tu dulussu ni dualcitizen na Ubelgoji, anakuja huku anakunta, anaenda kule anakula. Like I said, Marekani wabaruhusu dual citizenship kwa magarti kwambavuape na kutekeleza anri hii ifuatayo:

"I hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state, or sovereignty, of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America ...".

Yaani the United Republic of Tanzania, ya Nyerere, na Karume, na Mirambo, na Kinjiketile, ni FOREIGN POTENTATE. Halafu anategemea twende Yanga pamoja? Over me dead body!
Mkuu, sidhani kama uko sahihi.

Japo Katiba au sheria ya Marekani haitaji "dual citizenship", haimkatazi raia wake kuwa na uraia pacha au raia wa nchi nyingine kupata uraia wa Marekani, kwa mujibu wa sheria wa nchi zote mbili. ILA kuingia Marekani lazima utumia pasi ya Marekani kama Mmarekani na katika shughuli nyingine zinazohitaji pasi.

1623161322307.png

Hilo ndiyo lilikuwa pendekezo la Membe kama sikosei pia wale walioolewa na Watanzania na waliooa Watanzania kama wanautaka uraia wa Watanzania. Sasa hivi Ghana imeruhusu Wamarekani weusi wote wanaoutaka uraia wa Ghana wafuate taratibu husika ili wapate uraia wa Ghana.
Uraia pacha si lazima uwe kwa watu wote. Tunaweza kuruhusu wazawa wa Tanzania peke yao au wao na vizazi vyao nakadhalika.
 
Nani anaukana uraia wa Tanzania kwa ajili ya kuwavimbia watu?

Watu wanachukua uraia wa mataifa mengine kwa ajili ya kupata fursa mbalimbali katika mataifa hayo, sio for show off.

Mentality kama hii ya kudhani watu wanachukua uraia mwingine kwa ajili ya kujikweza ndio wivu wenyewe.

Pia wengine waonataka uraia pacha bado ni watanzania na wanataka kupata uraia wa mataifa mengine ili fursa fulani ziwafungukie. Hivyo tukiruhusu uraia pacha tunaweza kusaidia vijana wengi wenye sifa hapa tz wakapata ajira na fursa nyingine za elimu na biashara huko nje.
Hujagundua kwamba presha ya walio nje kutaka uraia wao wa TZ ni kubwa kuliko walioko ndani kutaka uraia wa nje? Wengi wenye kazi za maana nje ya nchi, hawakuhitaji na hawahitaji kuchukuwa uraia wa huko, tatizo ni wale waliojiripua!
 
Miaka ya nyuma Watanzania wengi waliobahatika kwenda kusoma nchi za nje na wengine kuwa na bahati hata ya kuombwa wabaki katika nchi hizo kwa jinsi walivyofaulu vizuri na pia kuahidiwa kazi za maana na mishahara minono walihofia kupoteza uraia wao wa Tanzania halafu na ile mentality ya kwamba akirudi hapa nyumbani atakuwa big boss Serikalini. shirika la umma au University hivyo wengi walikataa offers walizopewa siku hizi Watanzania hawalazi damu wanachakarika kivyao na kuchangamkia makaratasi na hata uraia ili wasikose ajira ambazo huwezi kuzipata kama si raia wa nchi husika.
 
Tatizo hiyo ajenda ya roho mbaya ndio mmeishikilia na ndio inayowakwamisha! Badala kushawishi kwa hoja mnawasema wenye mamlaka wana roho mbaya unadhani watawasaidia kweli... Sasa mimi nikuonee roho mbaya ya nini wakati sina na sitamani uraia wa aina hiyo maana hustle zangu zote ni hapa hapa na natoboa hapa hapa!
Hivi unafikiri tatizo la hao wanaoweka roho ngumu ni kushawishiwa? Watashaiwishiwa kwa point zipi za ziada juu ya suala hili? faida zote wameshaambiwa, mifano yote wameshapewa, ndio maana tumefikia kuamini kwamba issue sio uzalendo wala usalama wa taifa, ni selfishness na wivu sio na maana.
 
Kwa nini unatenga Afrika tu? Nji zifuatazo DUNIANI haziruhusu uraia pacha:

INDIA ISRAEL USA UK PAKISTAN SAUDI CANADA URUGUAY SOUTH AFRICA ETC ETC

Issue si "kuruhusu", isyu ni kwamba, mathalani, USA watakuruhusu tu kama utaitema hiyo inji ingine. In other words, dual citizenship ni ONE WAY TRAFFIC, ALLEGIANCE KWA NABEVERY KWANZA, Nadhani tu dulussu ni dualcitizen na Ubelgoji, anakuja huku anakunta, anaenda kule anakula. Like I said, Marekani wabaruhusu dual citizenship kwa magarti kwambavuape na kutekeleza anri hii ifuatayo:

"I hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state, or sovereignty, of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America ...".

Yaani the United Republic of Tanzania, ya Nyerere, na Karume, na Mirambo, na Kinjiketile, ni FOREIGN POTENTATE. Halafu anategemea twende Yanga pamoja? Over me dead body!
Sio kweli Mkuu; USA, UK, SOUTH AFRICA, CANADA wanaruhusu dual citizenship. Fanya tafiti yako vizuri

Nchi za nje ya Afrika zinazoruhusu dual citizenship ni hizi hapa; hizi ndizo tukiruhusu uraia pacha baadhi ya wenzetu watakuwa na uraia wa Tanzania na wa hizi nchi, ukiacha zile za Afrika

Albania, Armenia, Austria, Australia, Bangladesh, Belgium, Brazil Bulgaria Canada Chile Colombia Cyprus Denmark Dominica Ecuador El Salvador Fiji Finland France Germany Georgia Greece Grenada Hungary Iceland Iraq Ireland Israel Italy Jordan Kosovo Latvia Lebanon Lithuania Luxembourg Macedonia Malta Mexico Moldova Montenegro New Zealand Pakistan Peru Philippines Poland Portugal Romania Russia Serbia Slovenia Spain Sri Lanka St. Kitts and Nevis Sweden Switzerland Syria Thailand Turkey United Kingdom United States of America Vietnam Western Samoa
 
Balozi Malamula hivi karibuni ametooa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.

Nilishaziponda sana point za Watanzania ambao wanadai kuwa tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa watu watakaochukua uraia pacha sio wazalendo. Niliuliza uzalendo katika mambo gani hasa? Ni kitu gani ambacho watu wanaona mtu mwenye uraia pacha atafanya kwa nchi hii ambacho kitakuwa ni ukosefu wa uzalendo?

Hata nilisema kuna nafasi kubwa ya mtu asiye na uraia pacha kukosa uzalendo kuliko hao watakaokuwa na uraia pacha. Mnaweza kuniambia hawa mafisadi wanaoipiga sana hii nchi, wanaoiba mafuta kigamboni, watu kama kina Ole Sabaya, watu wanaokula fedha za miradi ya serikali, wanafanya hivyo kwa sababu wana uraia pacha?

Hiyo nafasi ya raia pacha kuifanyia Tanzania matendo ya kukosa uzalendo itakuwa katika mambo gani? Hebu tuangalie baadhi ya nchi hapa Afrika zenye uraia pacha, na tuwaulize wameathirika vipi na ukosefu wa uzalendo kwa raia pacha wao; South Afrika, Kenya, Ghana, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda nk? Hivi kuna mtu makini mambo ya uzalendo kama Kagame? Kwamba hakutafakari hadi kuruhusu uraia pacha kwa Rwanda? Isitoshe, kwani nani alisema tutaruhusu uraia pacha bila kuweka vigezo kama ukiwa raia pacha huruhusiwi kuwa labda raisi au waziri wa Tanzania? Huo unabaki kuwa uamuzi wetu.

Kwa sasa ni nchi nyingi za Afika zinazoruhusu uraia pacha ni nyingi kuliko zisizoruhusu uraia pacha (angalia ramani hapo chini). Kuna nchi kama Somalia, Liberia, ambao wamekuwa na maraisi waliokuwa na uraia pacha, waliharibu kitu gani? Mnafikiri ni kwa nini?

Balozi Malamula, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia pacha.

Tatizo ni kwamba watu wanaopinga uraia pacha Tanzania wanafanya hivyo kwa sababu za wivu na ubinafsi tu, wala sio uzalendo. Wengi wao hawajawahi hata kutoka nje ya Tanzania. Na wengi wao hata chembe ya huo uzalendo hawana. Isitoshe, wengi wa wanaopinga uraia pacha wala hawaelewi kanuni na utaratibu wa mtu kupata uraia pacha. Watu wanadhani mtu anaenda tu kujiandikisha mahali apewe uraia pacha, kwa hiyo labda tukiruhusu uraia pacha labda nusu ya Watanzania wataomba uraia pacha!

Kuwa raia pacha sio jambo rahisi, linahitaji uwe umeishi nchi ya pili kama mkazi kwa muda mrefu mara nyingi zaidi ya miaka mitano. Tunaposema Tanzania iruhusu uraia pacha, kimsingi sio Tanzania inayoruhusu, bali ni nchi ya uraia wa pili kama itamrughusu huyo Mtanzania kuwa raia wake. Na sio suala la kusema mie nataka kuwa raia pacha na USA wakati hata USA hujawahi kufika, achilia mbali kuishi!

Kwa hiyo Balozi Malamula, suala la uraia pacha lisisubiri Katiba mpya. Mswaada wa uraia pacha upelekwe tena Bungeni, au ufufuliwe ule uliokuwa umepelekwa. Kuna wakati lilipelekwa Bungeni likapitishwa, na Kikwete ndio alishauri kwamba kwa kuwa tuna mchakato wa Katiba mpya, badala ya kulipitisha kama Sheria mpya basi liingizwe kwenye katiba mpya - na hapo ndipo tulipokosea. Tuliwapa nafasi watu wenye ubishi wa kitoto kuleta hoja zao zisizo na mshiko nyuma ya ajenda zao za wivu usio na maana. Na karibu wote wanaobisha au kupinga uraia pacha hawajui maana ya uraia pacha na taratibu za mtu kuwa raia pacha. Si watu wa kusikilizwa katika msingi huu, waelimishwe kwanza, kutia ndani na wabunge.

View attachment 1808843

Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:

Na wengine:​

Yeye mwenyewe ni diaspora lakini kawa waziri, au yeye ana urai pacha? mimi sidhani uraia pacha ni tatizo la mtu kutoweza kuwekeza au kupata ajira huku nyumbani.hizo ni sababu tu, kwani watu wengi walio nje wamewekeza huku Tanzania pasi huo uraia pacha,watu waache visingizio kuwa eti wanashindwa kuwekeza au wanakosa fursa sababu ya uraia pacha semeni tu huko majuu maisha magumu.
 
Mkuu acha kuongea bila kuingia ndani. Hebu jaribu uende Bank Kuu waambie wewe ni Mtanzania unataka kutuma dola 2000 kwenda Uganda usikie watakuambiaje. Halafu waambie wewe ni raia wa Uganda unataka kutuma hizo dola Uganda. Hiyo itaanza kukuonyesha tofauti.
 
Balozi Malamula hivi karibuni ametooa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.

Nilishaziponda sana point za Watanzania ambao wanadai kuwa tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa watu watakaochukua uraia pacha sio wazalendo. Niliuliza uzalendo katika mambo gani hasa? Ni kitu gani ambacho watu wanaona mtu mwenye uraia pacha atafanya kwa nchi hii ambacho kitakuwa ni ukosefu wa uzalendo?

Hata nilisema kuna nafasi kubwa ya mtu asiye na uraia pacha kukosa uzalendo kuliko hao watakaokuwa na uraia pacha. Mnaweza kuniambia hawa mafisadi wanaoipiga sana hii nchi, wanaoiba mafuta kigamboni, watu kama kina Ole Sabaya, watu wanaokula fedha za miradi ya serikali, wanafanya hivyo kwa sababu wana uraia pacha?

Hiyo nafasi ya raia pacha kuifanyia Tanzania matendo ya kukosa uzalendo itakuwa katika mambo gani? Hebu tuangalie baadhi ya nchi hapa Afrika zenye uraia pacha, na tuwaulize wameathirika vipi na ukosefu wa uzalendo kwa raia pacha wao; South Afrika, Kenya, Ghana, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda nk? Hivi kuna mtu makini mambo ya uzalendo kama Kagame? Kwamba hakutafakari hadi kuruhusu uraia pacha kwa Rwanda? Isitoshe, kwani nani alisema tutaruhusu uraia pacha bila kuweka vigezo kama ukiwa raia pacha huruhusiwi kuwa labda raisi au waziri wa Tanzania? Huo unabaki kuwa uamuzi wetu.

Kwa sasa ni nchi nyingi za Afika zinazoruhusu uraia pacha ni nyingi kuliko zisizoruhusu uraia pacha (angalia ramani hapo chini). Kuna nchi kama Somalia, Liberia, ambao wamekuwa na maraisi waliokuwa na uraia pacha, waliharibu kitu gani? Mnafikiri ni kwa nini?

Balozi Malamula, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia pacha.

Tatizo ni kwamba watu wanaopinga uraia pacha Tanzania wanafanya hivyo kwa sababu za wivu na ubinafsi tu, wala sio uzalendo. Wengi wao hawajawahi hata kutoka nje ya Tanzania. Na wengi wao hata chembe ya huo uzalendo hawana. Isitoshe, wengi wa wanaopinga uraia pacha wala hawaelewi kanuni na utaratibu wa mtu kupata uraia pacha. Watu wanadhani mtu anaenda tu kujiandikisha mahali apewe uraia pacha, kwa hiyo labda tukiruhusu uraia pacha labda nusu ya Watanzania wataomba uraia pacha!

Kuwa raia pacha sio jambo rahisi, linahitaji uwe umeishi nchi ya pili kama mkazi kwa muda mrefu mara nyingi zaidi ya miaka mitano. Tunaposema Tanzania iruhusu uraia pacha, kimsingi sio Tanzania inayoruhusu, bali ni nchi ya uraia wa pili kama itamrughusu huyo Mtanzania kuwa raia wake. Na sio suala la kusema mie nataka kuwa raia pacha na USA wakati hata USA hujawahi kufika, achilia mbali kuishi!

Kwa hiyo Balozi Malamula, suala la uraia pacha lisisubiri Katiba mpya. Mswaada wa uraia pacha upelekwe tena Bungeni, au ufufuliwe ule uliokuwa umepelekwa. Kuna wakati lilipelekwa Bungeni likapitishwa, na Kikwete ndio alishauri kwamba kwa kuwa tuna mchakato wa Katiba mpya, badala ya kulipitisha kama Sheria mpya basi liingizwe kwenye katiba mpya - na hapo ndipo tulipokosea. Tuliwapa nafasi watu wenye ubishi wa kitoto kuleta hoja zao zisizo na mshiko nyuma ya ajenda zao za wivu usio na maana. Na karibu wote wanaobisha au kupinga uraia pacha hawajui maana ya uraia pacha na taratibu za mtu kuwa raia pacha. Si watu wa kusikilizwa katika msingi huu, waelimishwe kwanza, kutia ndani na wabunge.

View attachment 1808843

Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:

Na wengine:​

Kuna uraia na utaifa. Mimi ni Mtanzania na hilo siwezi kulibadilisha ila uraia ni suala la makaratasi na kufukuzia fursa zitokanazo na nchi husika.

Kuwa na gamba la bongo halikuongezi chochote katika dunia ya leo zaidi ya kumfunga mtu kama ng’ombe ambaye amefungwa kamba kwenye mti hawezi kufaidi malisho ya mbali.

Mimi kwa kweli baada ya kupima faida na hasara za kuwa na uraia wa nchi nyingine (nchi moaj hapa ulaya) nimeamua kuukana uraia wa bongo.

Kuna njia nyingi za kufaidi fursa za Tanzania hata nikipoteza uraia. Hivi navyoandika nilishapata uraia w nchi nyingine na nachosuburi kufanya ni kuukana utanzania kwa maandishi na kurejesha hati yangu ya kusafiria.

Hati nayotumia kwa sasa inaniruhusu kwenda hata Marekani bila visa kwa miezi mitatu na nina access ya dunia kwa kuwa na ile gamba tu, ya nini ni ng’ang’anie ya Tanzania yenye kuhitaji visa kila kona wakati nina fursa ya kupata hii inayonifungulia dunia?

Serikali ya Tanzania lazima itafakari upya. Kuwadhibiti wananchi kunaendeleza tu umasikini. Hakuna zaidi ya hapo.
 
Mkuu acha kuongea bila kuingia ndani. Hebu jaribu uende Bank Kuu waambie wewe ni Mtanzania unataka kutuma dola 2000 kwenda Uganda usikie watakuambiaje. Halafu waambie wewe ni raia wa Uganda unataka kutuma hizo dola Uganda. Hiyo itaanza kukuonyesha tofauti.
Mkuu acha uongo nini hizo usd 2000 mimi mwenyewe natuma au na kupokea zaidi ya hizo USD kutoka nchi mbalimbali kwa kupitia akaunti ya kigeni , cha muhimu ni kuweka bayana kuwa unafanya shughuli gani ili kuepusha utakatishaji pesa .Na nikuuliza toka lini Benki Kuu inafanya miamala ya watu binafsi? Benki Kuu niende kufanya nini wakati benki hizi za biashara ndio hufanya miamala ya pesa za kigeni. Kifupi nadhani hujui unachoongea bali umefuata tu mkumbo.
 
Okay tunapishana. Kwa taarifa yako kuna watu wana account BOT. Lakini nilitaka kusema nenda banki yako kutuma hizo dola usikie utaambiwaje. Si kweli unatuma dola nje kutumia benki, hapo unadanganya. Na sio tu suala la kueleza kwa nini unataka kutuma. Lazima uonyeshe invoice, sijui nini, sijui nini. Ndio maana hakuna internet banking Tanzania inayokuruhusu kutuma hela nje ya nchi, au hata dola ndani ya nchi. Na hao wanaokutumia dola toka nje wanapitia hayo hayo. Sio kwamba wanatuma kirahisi tu kila nchi. Hata South Africa hapa inabidi raia wajieleze wakitaka kutuma fedha nje kupitia benki. Sema angalau siku hizi ni nafuu kuna vitu kama Mpesa. Angalia masharti haya, halafu wewe unasema unatuma tu kirahisi

Prerequisites for International Money Transfers
  1. Relevant invoice, in the case of importation;
  2. Letter or invoice from respective educational or medical institution, in the case of medical or education expenses;
  3. Employment contract, in the case of expatriate proceeds;
  4. Pension award letter and employment contract, in the case of retirement benefits;
  5. Contractual documents, invoices or fee note and certification of settlement of tax obligations in case of consultancy management or royalty agreements;
  6. In the case of dividends and profits to foreign shareholders, audited reports indicating declared dividends or profits to be repatriated and documents confirming payments of all relevant taxes; or
  7. Any other relevant document depending on the nature of the request.
Conclusion
Transfer of foreign currency in Tanzania is increasing its usage now as opposed to the time of centralized economy. This is due to adoption of the liberalized economic policies which have led to an increase of commercial banks and financial institutions. Above all, the liberalized economy has led to an influx of foreign direct investments in Tanzania, thus necessitating the need for having an efficient payment, clearing and settlement system involving foreign currency.

Laws and respective regulations have been enacted to regulate and monitor foreign currency transfers. The procedures and limitations on foreign currency transfers have been highlighted above.

The enactment of the national payment system has been aligned to cater for foreign currency transfers. The challenges related to foreign transfers have been addressed through enactment of legislation such as the Anti-Money Laundering Act, 2006, the Foreign Exchange Act, 1992 and Foreign Exchange Exposure Limits Regulations, 2015 and other legislation as highlighted above.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Sio kweli Mkuu; USA, UK, SOUTH AFRICA, CANADA wanaruhusu dual citizenship. Fanya tafiti yako vizuri

Nchi za nje ya Afrika zinazoruhusu dual citizenship ni hizi hapa; hizi ndizo tukiruhusu uraia pacha baadhi ya wenzetu watakuwa na uraia wa Tanzania na wa hizi nchi, ukiacha zile za Afrika

Albania, Armenia, Austria, Australia, Bangladesh, Belgium, Brazil Bulgaria Canada Chile Colombia Cyprus Denmark Dominica Ecuador El Salvador Fiji Finland France Germany Georgia Greece Grenada Hungary Iceland Iraq Ireland Israel Italy Jordan Kosovo Latvia Lebanon Lithuania Luxembourg Macedonia Malta Mexico Moldova Montenegro New Zealand Pakistan Peru Philippines Poland Portugal Romania Russia Serbia Slovenia Spain Sri Lanka St. Kitts and Nevis Sweden Switzerland Syria Thailand Turkey United Kingdom United States of America Vietnam Western Samoa

Shukrani mkuu, uko vizuri mno!
 
Ni kweli mkuu huu ni wakati wa kuwa na mawazo chanya Ili kukuza uchumi na kutafutia vijana fursa

Akina Mwendazake na genge lake walikuwa na uzalendo gani zaidi ya wivu na kupiga propaganda uchwara?

Hata taasisi za serikali ni vyema zikawa facilitators badala ya kuwa za udhibiti
 
Back
Top Bottom