Ushauri Kwa BAVICHA na CHADEMA; Someni Historia ya Nchi hii, mnajidhalilisha kwa wenye akili

Ushauri Kwa BAVICHA na CHADEMA; Someni Historia ya Nchi hii, mnajidhalilisha kwa wenye akili

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Habarini Bavicha na Chadema kwa Ujumla

Leo napenda kuwashauri jambo la kuwasaidia kutokana na trend yenu ya kuanzisha vi thread humu kuongelea kesi ya Mbowe na kuleta nadharia zenu kuhusu watu waliokuwa Wanajeshi ambao wamedhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama

Napenda kuwashauri hivi;

Embu jitahidini kusoma na kujua angalau kidogo historia ya nchi hii na nadhani itawasaidia kidogo

Wanajeshi wa kesi ya Mbowe si watu wa kwanza nchini kudhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama vya Tanzania baada ya kufanya Jinai.

Mwaka 1981, Wanajeshi kadhaa akiwemo Komando Tamimu, Kapteni Kadego,Kapteni Maganga, Luteni Zacharia Hanspope, Kapteni Maghee na wenzako walifanya mpango wa kutaka kuiangusha Serikali ya Awamu ya kwanza.

Kwenye mipango iyo Walishirikiana na Wanajeshi wenzao akiwemo Luteni Ndejembi( Ambaye alikuja kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma- Ni baba Mzazi wa Naibu Waziri Ndejembi, Mbunge wa Chamwino)

Wakati wanapanga mipango yao Ndejembi na wenzake waliwaripoti kwa Mkuu wa Usalama Jeshini . Enzi izo alikuwa Luteni Kanali Davis Mwamunyange ( Ambaye Kwa sasa ni CDF Mstaafu )

Baada ya mipango iyo kusanuliwa Vikosi vya ulinzi na Usalama ( JWTZ, TISS na Polisi) walifanya operesheni maalumu iliyowezesha wanajeshi hao wote kukamatwa na kuuwawa kwa Komando Tamimu ambaye aliuliwa akijaribu kutoroka. Wanajeshi hawa ukisoma kesi hii walipitia msoto wa uhakika ikiwemo torture ili kupata kiundani mipango yao

Kesi ilienda Mahakamani na watuhumiwa wote walihukumiwa vifungo gerezani! Kesi iyo iliendeshwa na Wakili wa Serikali matata aliyejulikana kama Sekule ambaye alikuwa DPP na baadae akaja kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Kwa maelezo haya napenda leo kuwahusia Bavicha na Chadema, acheni kuanzisha vi thread vyenu uchwara ambayo vinaonesha hamjui historia ya hii nchi. Kama mnadhani mnaleta uchonganishi basi jueni mnakosea sana. Vyombo vya dola vya Tanzania vinafanya kazi kwa utaratibu maalum na ndo mana nchi iko salama miaka yote hii tangu Uhuru

Poleni sana Bavicha na Chadema!

Mbowe haponi!
 
Habarini Bavicha na Chadema kwa Ujumla

Leo napenda kuwashauri jambo la kuwasaidia kutokana na trend yenu ya kuanzisha vi thread humu kuongelea kesi ya Mbowe na kuleta nadharia zenu kuhusu watu waliokuwa Wanajeshi ambao wamedhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama
Mama anaupiga mwingi siyo? 😁😁😁😁
 
Ulipaswa kukumbusha historia hiyo bila kuwa na upande unaoelemea. Kwa kuandika Mbowe haponi umefuta kila ulichoandika na kusababisha watu wengi wapuuze wito wako.
Puuzia wewe unaruhusiwa! Ila message sent and delivered
 
Wewe mwenyewe umeandika mada uchwara.kwani hizo kesi za hao uliowataja zinafanana na kesi ya mbowe?
Vi thread vinazungumzia wanajeshi waliodhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama!

Mada inasema hao wanajeshi si watu wa kwanza kudhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama hapa Tanzania
 
Tujadili mada sio mtoa mada (kwangu mtoa mada ni spoiled child aliyekulia na kuishi in a system's)mada imetoa maelezo mengi lakini kwangu nina summarise kuwa ile treason case aliyotolewa mfano hapo juu kuwa kwenye nchi zenye demokrasi na uhuru wa kimahakama ile case ingefutwa straight maana ushahidi uliopatikana kutokana na kuteswa haukubaliki mahakamani!(mada hii imethibitisha kuwa suspects waliteswa kabla ya kupelekwa mahakamani)na hao wote waliotajwa hapo ambao walishughulikia hii case wote walikua ni political redeployed cardes wa chama dola.
 
Habarini Bavicha na Chadema kwa Ujumla

Leo napenda kuwashauri jambo la kuwasaidia kutokana na trend yenu ya kuanzisha vi thread humu kuongelea kesi ya Mbowe na kuleta nadharia zenu kuhusu watu waliokuwa Wanajeshi ambao wamedhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama

Napenda kuwashauri hivi;
Nyie mnaonufaika na utawala dhalimu lazima muutetee tu bila kujali watu wanateseka na kufa ili mradi matumbo yenu yajae.
 
Tujadili mada sio mtoa mada (kwangu mtoa mada ni spoiled child aliyekulia na kuishi in a system's)mada imetoa maelezo mengi lakini kwangu nina summarise kuwa ile treason case aliyotolewa mfano hapo juu kuwa kwenye nchi zenye demokrasi na uhuru wa kimahakama ile case ingefutwa straight maana ushahidi uliopatikana kutokana na kuteswa haukubaliki mahakamani!(mada hii imethibitisha kuwa suspects waliteswa kabla ya kupelekwa mahakamani)na hao wote waliotajwa hapo ambao walishughulikia hii case wote walikua ni political redeployed cardes wa chama dola.
Mtu mwenye miaka 46 aliyetoka kwenye familia ya Mkulima akasoma Sheria na sasa anafanya kilimo Mkoa wa RUVUMA anakuwaje spoiled Child na anakuliaje kwenye system?

Unasema usijadili mtoa hoja wakati na wewe unaleta nadharia zako juu ya mtoa hoja

You are a wasted sperm Kwa kweli
 
Bahati mbaya sana zama zimebadilika!

Mnajidanganya sana kama mnalenga kuihukumu kesi hii kama mlivyohukumu hiyo kesi ya miaka 40 iliyopita!
Wakili matata hayupo tena upande wa serikali! Na hii kesi mmeipeleka mahakamani kama kesi ya ugaidi siyo ya mapinduzi!
Rudi ulishwe matangopori!

Shame on you!
 
Vi thread vinazungumzia wanajeshi waliodhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama!

Mada inasema hao wanajeshi si watu wa kwanza kudhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama hapa Tanzania
Umeshindwa kuelewa kuhusu SHERIA na UHUNI. Tanzania hakuna sheria inaruhusu mtuhumiwa kuteswa, kunyanyaswa au kufanyiwa vitendo VIOVU katika kupata ushahidi (confession).

Ndiyo maana kuna sheria zimewekwa kuhusu haya mambo, ukiona zimekiukwa unayo HAKI ya kushughurikia kwa mujibu wa sheria,ndicho wanafanya washtakiwa (Mbowe na wenzake).

Wewe umeandika kuhalalisha UHUNI ambao wakina Kingai & Co unaona wanaukwepa pale Mahakamani kwa ushahidi (wa kutunga) kwamba hawakuwatesa wala kuwanyanyasa kwa wakati wote.

Ifike muda tuwe na utaratibu wa kuhimiza utawala wa sheria, kuna watu wamepata vilema na wengine kupoteza maisha kabisa kutokana na mateso ya Jeshi la polisi.

Leo unatoa KEJELI kwa sababu tu hili linamuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA, kuna watanzania wengi wasio na hatia wamepitia mateso kwenye mikono ya Jeshi la polisi hata kuwa vilema na kupoteza maisha kabisa.

Yesu alidhihakiwa, alinyanyaswa, aliteswa na hadi kufa siyo kwamba alikuwa na hatia ya kweli bali Mungu alitaka kutimiza mapenzi yake kwetu.

Ubarikiwe.
 
Mtu mwenye miaka 46 aliyetoka kwenye familia ya Mkulima akasoma Sheria na sasa anafanya kilimo Mkoa wa RUVUMA anakuwaje spoiled Child na anakuliaje kwenye system?

Unasema usijadili mtoa hoja wakati na wewe unaleta nadharia zako juu ya mtoa hoja

You are a wasted sperm Kwa kweli
Tatizo liko kwenye watu kama wewe middle class ambao wanajiona wapo above level,uliyoyaongea hapo juu sio maongezi ya msomi wa kawaida anayejua hali halisi ipo vipi on the ground?after all karibu sana HukuLingusenguse naona hapo Matarawe kunakufanya ujione upo first world,njoo huku uone hali halisi za maisha na pitia Litola,Lwegu,Kumbara,Njalamatata,then ufanye tathimini ya maisha ipo vipi.wastage sperm hi ni No No nimeishi maisha bora baada ya hard work na never sitasahau reality iliyopo nchini.
 
jiwe wako alitamba kwa data za kihistoria kua.

waliomtangulia ote walimaliza miaka 10,kwanini yeye asimalize miaka 10.

kalazimisha kilichomkuta ote mnajua.
hivyo zama zile sio hizi.

wewe unafikili ni kwanini watu wana picha hadi za ushahidi walivyokua wanateswa.
ujue hata humo kuna baadhi ya askali wenye hofu ya mungu wanaumia juu ya haya yanayotendeka.
 
Umeshindwa kuelewa kuhusu SHERIA na UHUNI. Tanzania hakuna sheria inaruhusu mtuhumiwa kuteswa, kunyanyaswa au kufanyiwa vitendo VIOVU katika kupata ushahidi (confession).
Umeandika vyema, ila hapo kwenye habari za Yesu umeharibu, Yesu ni kweli aliishi miaka hiyo, lakini Yesu halisi ni tofauti na aliyesimuliwa kwenye biblia (Stories nyingi za kwenye biblia ni za kutunga na zimejaa chai za kiwango cha SGR).
 
Back
Top Bottom