Habarini Bavicha na Chadema kwa Ujumla
Leo napenda kuwashauri jambo la kuwasaidia kutokana na trend yenu ya kuanzisha vi thread humu kuongelea kesi ya Mbowe na kuleta nadharia zenu kuhusu watu waliokuwa Wanajeshi ambao wamedhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama
Napenda kuwashauri hivi;
Embu jitahidini kusoma na kujua angalau kidogo historia ya nchi hii na nadhani itawasaidia kidogo
Wanajeshi wa kesi ya Mbowe si watu wa kwanza nchini kudhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama vya Tanzania baada ya kufanya Jinai.
Mwaka 1981, Wanajeshi kadhaa akiwemo Komando Tamimu, Kapteni Kadego,Kapteni Maganga, Luteni Zacharia Hanspope, Kapteni Maghee na wenzako walifanya mpango wa kutaka kuiangusha Serikali ya Awamu ya kwanza.
Kwenye mipango iyo Walishirikiana na Wanajeshi wenzao akiwemo Luteni Ndejembi( Ambaye alikuja kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma- Ni baba Mzazi wa Naibu Waziri Ndejembi, Mbunge wa Chamwino)
Wakati wanapanga mipango yao Ndejembi na wenzake waliwaripoti kwa Mkuu wa Usalama Jeshini . Enzi izo alikuwa Luteni Kanali Davis Mwamunyange ( Ambaye Kwa sasa ni CDF Mstaafu )
Baada ya mipango iyo kusanuliwa Vikosi vya ulinzi na Usalama ( JWTZ, TISS na Polisi) walifanya operesheni maalumu iliyowezesha wanajeshi hao wote kukamatwa na kuuwawa kwa Komando Tamimu ambaye aliuliwa akijaribu kutoroka. Wanajeshi hawa ukisoma kesi hii walipitia msoto wa uhakika ikiwemo torture ili kupata kiundani mipango yao
Kesi ilienda Mahakamani na watuhumiwa wote walihukumiwa vifungo gerezani! Kesi iyo iliendeshwa na Wakili wa Serikali matata aliyejulikana kama Sekule ambaye alikuwa DPP na baadae akaja kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kwa maelezo haya napenda leo kuwahusia Bavicha na Chadema, acheni kuanzisha vi thread vyenu uchwara ambayo vinaonesha hamjui historia ya hii nchi. Kama mnadhani mnaleta uchonganishi basi jueni mnakosea sana. Vyombo vya dola vya Tanzania vinafanya kazi kwa utaratibu maalum na ndo mana nchi iko salama miaka yote hii tangu Uhuru
Poleni sana Bavicha na Chadema!
Mbowe haponi!