Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Asante nishafahamu sasa turudi kwenye mada iliyo mezani.
Nitamuomba mode jukwaa la dini liwe public ili hawa wafia dini wamalize hasira zao huko.
Pasco

Umefahamu kitu gani mbona unataka kuwaomba mods wapeleke mambo ya siasa kwenye ukumbi wa dini?? Hivi kuna aya yeyote ya biblia au quran hapo ??
 
Tatizo ni levels tuu za uwezo wa kusoma in between the lines, ukinisoma umetulia level yako ya uelewa itapanda na utanielewa, bandiko hili na lile la nitaandamana is the same! , ila ni kwa watu wa levels tofauti za uelewa, moja ni direct, jingine indirect but it is the same thing! .

Vivyo hivyo kwa Magufuli ni dikiteta ila ni benevolent dictator ambaye ni dikiteta mzalendo mwenye anayekerwa na rushwa na ufisadi toka ndani ya nafsi yake hivyo anaufanya huu udikiteta wake kwa nia njema na dhamira safi ya kulikomboa taifa hili toka kwenye lindi la umasikini uliotopea uliogubikwa na rushwa na ufisadi.

Pasco
 
Umefahamu kitu gani mbona unataka kuwaomba mods wapeleke mambo ya siasa kwenye ukumbi wa dini?? Hivi kuna aya yeyote ya biblia au quran hapo ??
umesehau kule ulikonielekeza kwa yule mfia dini? .

Pasco
 
umesehau kule ulikonielekeza kwa yule mfia dini? .

Pasco


KWA MFIA DINI GANI ?? WEWE HUNA DINI ??

Hakuna hata sehemu moja nimekuletea kunakozungumziwa biblia au qurani

mote mna siasa za Nyerere na kanisa dhidi ya waislamu.

Naona umechanganyikiwa
 



ETI Anakerwa na rushwa na ufisadi tehtehtehhhh , na huku unajitia unamuunga mkono na hapohapo unajifanya unaenda kumpinga . Njaa kitu hatari , Kazi ipo opportunist

Hapa nakuwekea mstari


Mathayo 6:24

"Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Maana atamchukia mmoja na kumpenda huyo wa pili; au ataambatana na mmoja na kumdharau huyo mwingine.

Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.
 
Du! ,kumbe we jamaa ni muhubiri? !.

Nimepandisha nyuzi kibao humu kuhusu udikiteta wa Magufuli ambao nchi hii iliuhitaji ila pia naunga mkono UKUTA ili kuuzuia udikiteta huu usivuke mpaka, yaani udikiteta uishie kwenye kupambana na rushwa, uzembe, ufisadi na kuchochea Maendeleo lakini wakati huo huo akiiacha demokrasia ishamiri.

Pasco
 
Gavan/Pasco,
Katika hayo aliyoweka Gavana rejea si mimi.
Soma tena uone waliofanyiwa rejea ni kina nani.

Waliofanyiwa rejea ni Bergen na Sivalon na hawa wala si Waislam.

Gavana hakuishia hapo kaweka na maelezo kuweka wazi yote yale
yaliyotokea.

Hakika mimi nimesoma shule za misheni lakini elimu yangu haikuanzia
hapo.

Nimeisoma na dini yangu na hii ndiyo ilikuwa ya kwanza kutangulia kabla
ya kitu chochote kuingia katika ubongo wangu na naendelea kusoma
hadi sasa uzeeni.

Na ukipenda kufahamu hii elimu ya majadiliano haitokani na elimu ya
sekula hii nimesoma kwa Sheikh Haruna na siku zote huwaambieni.

Unaandika umeghadhibika.
Unaghadhibika kwa kuwa huna kitu.

Mimi nina mengi ya kusomessha hapa kwa hiyo hasira haina upenyo
katika fikra yangu.

Hii ndiyo tofauti kuu baina yangu na Pasco.
 
Swadakta.
Pasco
 
we unaongea kama nani kibaraka mbwabwaji tu,inawezekana hata kwenye hayo maandamano hutakuwepo.nani asiyejua km nyie ni watetea tumbo tu,hamna lolote
 
Umefahamu kitu gani mbona unataka kuwaomba mods wapeleke mambo ya siasa kwenye ukumbi wa dini?? Hivi kuna aya yeyote ya biblia au quran hapo ??

Duh Gavana Wewe si mchezo maana umemfanya Pasco akimbilie Kwa marefa.
Unanikumbusha Mwandishi wa Kimerekani
James Baldwin alipofanya hoja Na William Buckley (Mwenye siasa kali za kibaguzi USA)
Huko Cambridge union society 1965.
Hongera tu Mkuu
 

Maalim Mohamed Said huwa nafarijika sana kusoma hoja zako Na kujifunza sana juu ya elmu Na hekma zako.Mwenye Ez Mungu akuzidishie sana Nuru ili tupate mwangaza toka kwenye Nuru yako.
 
Kijana kama unampango wakuandamana hakikisha umepata sababu kumi kwanini unataka kuandamana kama hazifiki kumi kitulize kwenu au kwako usitie watu kwenye gharama za kukupeleka hospital wakati hujui unatetea nini. Usifananishe Tanzania na huko kwa wenzetu nje hii ni Africa utapigwa halafu kiongozi alikujaza upepo uandamane aseme makamanda walipigana vyema wakati huo yuko uingereza umeshampa KIKI
 
Elites hawana tabia ya kubadilikabadilika kama kinyonga! Pasco kuna kitu kinakuondoa taratibu kwenye kundi la elites.

CHADEMA Wakiamua kutokuandamana maana take Ni kwamba tumeamua kuwa kama Bunge,Au kuwa kama vyombo Vya habari Tanzania.Tutaandamana! Tena tutaandamana bila kikomo. Jumatatu hadi jumamosi,Septemba yote mpaka kieleweke.
 
Asanteni Chadema kuuchukua ushauri huu na kuufanyia kazi! .

Pasco
 
Pasco bwana!
Sasa Chadema wakisikiliza Ushauri wako si kitakoma kuwa chama cha siasa, maana ground za kufanyia siasa zote zinapigwa libiti!
Ushauri umesikilizwa, jee sasa kimekoma kuwa chama cha siasa? .

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…