Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

ni kweli,

kuna changamoto mbali mbali kwetu Tanzania...............wangekuja na alternative solutions,tungewaheshimu more...........

its time, kuwork with government,not to work against.....

maandamano haya achieve chochote,
 
Pasco bwana!
Sasa Chadema wakisikiliza Ushauri wako si kitakoma kuwa chama cha siasa, maana ground za kufanyia siasa zote zinapigwa libiti!
Grounds zipi za kufanya siasa? Si wanatakiwa kumuandikia ocd tu na akiridhia wanafanya tu! Acha kushikishwa UKUTA.
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kutoa ushauri wa bure, huu ni ushauri wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba, nawashauri kwa dhati kabisa, tafadhalini sana msiandamane, na kusitisha hiyo Operesheni UKUTA, ili kuutumia ule msemo wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, na sio tuu ana nguvu zaidi yako, na tayari, umeishajua ni dikiteta, bali ndio mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.

Misingi ya Katiba na The Rule of Law
Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya katiba na sheria, (the rule of law) ambapo inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na sio kwa matamko ya viongozi yanayokwenda kinyume cha katiba!.

The Separation of Powers & Check and Balance .
Nchi yetu ina mihimili mikuu mitatu, Serikali, (the executive), Bunge (The Legislature) na Mahakama (The Judiciary). Mihimili hii mitatu, ilipaswa kufanya kazi kwa kujitegemea bila mhimili mmoja kuingilia mhimili mwingine (independence), huki kila mhimili uki act as a watchdog wa muhimili mwingine usivuke mipaka ya madaraka au mamlaka yake yaani (The sepaation of powers check and balance).

Serikali yenye Nguvu, Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo!.
Mihimili hii, inaongozwa na viongozi ambao wana mamlaka kuu kuhusu mihimili yao. President ndio mkuu wa the executive, Spika ndio mkuu wa The Legistlatue, na Jaji Mkuu, ndie mkuu wa The Judiciary, lakini pamoja na nia njema kuwa mihimili yote inamamlaka na hakuna mhimili wowote uliokuwa unapaswa kuwa na mamlaka kuliko mhimili mwingine, lakini kiukweli, mhimili wa the executive ndio mhimili mkuu unaomiliki vyombo vya dola na kuitawala mihimili mingine yote!, hivyo mkuu wa the executive, yaani rais, ndio kila kitu!, akisema!, amesema!.

Rais Magufuli na Uvunjaji wa Katiba.
Tuambiane ukweli, tangu rais Magufuli ameingia madarakani, sio mara moja au mbili amekuwa akitoa kauli tata, zinazokwenda kinyume cha katiba, mhimili wa Bunge na Mahakama ilipaswa kuingilia kati kwa kumcheck mkuu wa the executive, lakini vyombo hivyo vimekaa kimya hivyo kumfanya rais ajisikie kuwa he is always right! kwa kanuni ya "the boss is always right!".

Udikiteta wa Magufuli.
Hoja kama Magufuli ni dikiteta au la, haina mjadala, Magufuli ni dikiteta wa ukweli ambaye hana msalie mtume, na alipoingia tuu madarakani, alianza kuonyesha udikiteta wake right away kwa kuliingilia bunge na mahakama kuziweka chini ya amri zake!. Lile katazo lake la watumishi wa umma hawaruhusiwi kusafiri safari za nje bila kibali chake kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, liliwahusu watumishi wote wa serikali, likiwemo bunge na mahakama!, just imagine Jaji Mkuu na Spika wa bunge wakapige magoti kwa rais kuomba kutimiza wajibu wao!.

Baada ya katazo lile, checks and balance zingepaswa kuanzia hapo kwa Jaji Mkuu kumweleza rais huko ni kuingilia uhuru wa mahakama (the independence of the judiciary) hivyo muhimili wa mahakama haukupaswa kujisubmit chini ya the executuve, bali mamlaka hayo ya kuzuia safari za nje, Spika alipaswa kuwa nayo kudhibiti safari za mhimili wa bunge, na Jaji Mkuu alipaswa kuwana nayo kudhibiti safari za mhimili wa mahakama, lakini mihimili hii ilikaa kimya kwa kujisubmit chini ya the executive, hivyo kumfanya rais ndio kila kitu!.

Hivyo sasa rais Magufuli ndio kila kitu, hakuna cha bunge, mahakama, wala katiba, amri ya rais ndio kila kitu na ndio sheria kuu!, hivyo nawashauri Chadema kwa dhati kabisa, wasitishe maandamano yao, wasifanye kabisa mchezo wa kumjaribu Ngosha, wataumia bure!.

Hili la udikiteta wa rais Magufuli, tumeisha lizungumza sana humu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa ...

Ila kitu kimoja kuzuri kuhusu udikiteta wa rais wetu, ni Rais Magufuli ni dikiteta mzalendo!, mwenye uchungu na umasikini wa nchi hii, mwenye nia njema ya kusafisha uozo wote wa uzembe, rushwa na ufisadi, na kulikomboa taifa letu toka kwenye lindi la umasikini uliotopea na kuwa nchi ya maziwa na asali kupitia uchumi wa gesi na viwanda.

Mungu mbariki Magufuli!.

Mungu ibariki Tanzania.

Wasalaam.

Pasco
Rejea za shauri za bure
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa ...
Ushauri wa Bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared for ...
Ushauri wa Bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako ...
Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep ...
Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)-Kwa Hili la ...
Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report: Please Keep Quite ...
Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Magufuli, Futilia Mbali Utawala wa Sheria ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Usikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
Ushauri wa Bure kwa Dr. Shein: Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ...
Ushauri wa Bure kwa Magufuli, DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...

MLAPUNDA soma hii
 
Na alaaniwe alaniye marehemu! . Badala ya appreciation kwa Baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere, wewe ndio unamuita hivyo?!. Wenzio tuko kwenye process ya kuutangaza Mwenye Heri, one step kabla hajatangazwa Mtakatifu! .

Mtakatifu mtarajiwa Julius Kambarage Nyerere, Muombee mdhambi Gavana asamehewe dhambi zake kwa maana hajui atendalo! .

Pasco

SOMA HAPA KWENYE LINK UTAMJUA NYERERE NI NANI Mohamed Said: MWL. JULIUS K. NYERERE, KANISA KATOLIKI NA UISLAM: DOLA NA TATIZO LA UDINI TANZANIA
 
Kama reference yako ni huyu mdini Mkuu humu jf, endelea, jamaa kasomeshwa na misheni lakini Shukrani hana! . Kwa kukusaidia tuu, misheni ndio kila kitu na akiwa Mkristu ni lazima awe Mkatoliki, alianza Juliasi, akaja Benyamini na sasa nI Yohana, ni chaguo la Kurasini japo muungwana alimtaka Benado pia wakamleta Petiro ili kumtumia kama kichinjio cha kumchinjia Eduadi.

Tena Nyerere ni wa kumshukuru sana maana asingeifutilia mbali ile jumuiya ya mujahidina, saa hizi na sisi tungekuwa kama Somalia! .

Katika kitabu chake Bw. Bergen, kiitwacho Development and Religion in Tanzania, katika Ukurasa wake wa 98 mwanadishi huyo anasema:- “Catholic Missionaries came to East Africa to find not new churches, but new provinces of the Roman Church” Kwa mujibu wa tafsiri yangu “Wamishionari wa Kikatoliki hawakuja hapa Afrika ya Mashariki kwa minaajili ya kuasisi Makanisa mapya, bali walikuja kuunda majimbo mapya ya Kanisa la Roma”. Ni kwamba, Tanzania (Tanganyika) ipo Afrika Mashariki, na kwa mujibu wa mwandishi Bergen, Tanzania nayo ni moja ya majimbo ya Kanisa la Roma, au kwa lugha nyepesi tuseme Tanzania ni Koloni la Vatican! Je, ni kweli Tanzania (Tanganyika) ni Koloni la Vatican? Padri. Dk. Sivalon, naye katika kitabu chake Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania Bara (1953-1985) anaeleza bayana kuwa Mwalimu Julius Nyerere Rais wa Kwanza wa nchi yetu, alikuwa kiungo pekee kati ya Chama (CCM), Serikali na Kanisa Katoliki.

Na kwa msingi huo viongozi wa Kanisa wamekuja kuwa na nafasi ya pekee kuelekeza hisia, mitazamo na siasa ya Tanzania, na wamefanya hivyo wakipania pia kuwa kuhujumu Uislamu. (Msomoe Sivalon Uk. 5-6,
katika kitabu chake hicho). Naye m mwandishi Bergen katika kitabu chake amemnukuu Mwalimu Nyerere akisema kamwe hawezi kwenda kinyume na kanisa lake. (Bergen Uk. 335). Agosti 3, 1970 Mwalimu Nyerere, alimwita Ikulu Padri Rweyemamu katika mazungumzo maalum ambapo Nyerere alimuahidi Rweyemamu kuwa, hivi sasa Kanisa ndilo lililoshika hatamu za kuongoza dola naye atahakikisha hali inaendelea kuwa hivyo. “Tanzania is not Catholic country, but Catholics is strong, I want to give the church a better chance here”. Akiwa na maana kwamba:- japo “Tanzania si nchi ya Kikatoliki, lakini Ukatoliki una nguvu, hivyo nataka kulipa Kanisa nafasi ya pekee hapa nchini” (Msome, Bergen Uk. 335). Na hali hii ya Kanisa kuwa na nafasi kubwa Serikalini iko wazi.

Waandishi wote hawa wanatuthibitishia kuwa, kuna ukweli fulani kwamba yapo mafungamano ya dhati kati ya Kanisa Katoliki na Serikali ya Tanzania. Ni mafungamano hayo hayo ndiyo yameendelea kuwapa uweza viongozi wa Kanisa Katoliki kutoa maelekezo, maagizo na vilio vyao Serikalini na wakasikilizwa pamoja na kutekelezwa yale wanayoyahitaji hata kama yamelenga kuleta maafa kwa Waislamu. Mfano, mwaka 1998, Padri Lwambano, ambaye ni Paroko wa Kanisa Katoliki Mburahati Jijini Dar es Salaam, alisema kuiambia Serikali:- “Lazima Serikali ichukue hatua kali sana kwa Waislamu wanaoendesha Mihadhara, sababu ni watu wabaya kabisa, nimepita Sinza na Mwembechai, nimekuta Waislamu hao wanamtukana Yesu wanasema Yesu si Mungu”, alisema Paroko huyo na kuongeza; “Kama Serikali imeshindwa kuchukua hatua kali kukomesha Mihadhara ya Waislamu na kuendelea kutupaka matope kwa mgongo wa chupa, Serikali hii ijue sisi tutalishughulikia jambo hilo kwa nguvu zetu zote”.

Kauli hii ya Padri Lwambano, ilirushwa hewani na Kituo cha Radio Tumaini kinachomilikiwa na Kanisa hilo hapa nchini, Februari 13, 1998. Padri Lwambano bila kujali kuwa imani yake inaamini ‘Yesu ni Mungu’ na Waislamu imani yao inaamini ‘Yesu si Mungu’, aliinyooshea kidole Serikali nayo ilifuata bila kujali yenyewe (Serikali) haina dini na raia wake wana dini, kwa imani tofauti.

Katika utekelezaji wa agizo hilo bila shaka kila mtu anakumbuka kilichotokea. Ama kwa wale ambao walikuwa ni wadogo kipindi hicho ni kwamba Jeshi la Polisi lilifika Msikiti wa Mwembechai na kuuwa Waislamu kwa risasi na kikumbukumbu ni maarufu kwa ‘Mauaji ya Mwembechai’. Kufuatia madai hayo ya Padri Lwambano, viongozi kadhaa wa nchi walifikia hatua ya kuliomba radhi Kanisa Katoliki na Wakristo kwa ujumla. Majina na vyeo vya viongozi hao wakuu wa Serikali yanafahamika.

Baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Jeshi la Polisi, kazi ya kukatili maisha ya Waislamu na kubaka haki zao, kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini Polycarp Kadinali Pengo, aliipongeza Serikali kwa upande mmoja na Polisi kwa upande wa pili kufuatia mauaji hayo hayo ya Waislamu, Mwembechai. Pongezi hizo alizitoa April 12, 1998 wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Dar es Salaam (DTV). Kanisa likionekana kuuchukukia vilivyo Uislamu, liliongeza harakati za siri na za wazi na kwa kutumia nguvu za dola ili kupunguza kwa upande mwingine nguvu ya Uislamu, maana kuuzima kabisa ni jambo lisilowezekana.

Askofu Mkuu Pengo alitoa taarifa ya kuenea Uislamu hapa Tanzania huku akihitaji msaada wa hali na mali katika kuhidhibiti hali hiyo. Na kwa kweli, Serikali ilitekeleza kudhibiti Mihadhara na Wahadhiri, ambapo wahadhiri maarufu nchini wakiongozwa na Habib Mazinge, walitiwa mbaroni na kutupwa Magerezani. Aidha sehemu ya taarifa yake ilisema hivi; “Uislamu umekuwa tishio kubwa sana kwa imani ya Kikristo nchini Tanzania, iwapo mihadhara ya Waislamu itaachwa iendelee, Kanisa litegemee kukimbiwa na waumini wake na kusilimu, kwa hiyo juhudi lazima zifanywe kuzuia Mihadhara hiyo.

“Tunashindwa kujibu hoja zao Waislamu sababu zina ukweli ndani yake”, maelezo haya yanapatikana katika kitabu cha Askofu Pengo kiitwacho Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwenye vijilia Sinodi ya Maaskofu wa Afrika kwa ajili ya Afrika.
 
S
I represent nobody but the truth!. Ushauri wa bure ni sadakalawe tuu, you take it or leave it, tutakapokuta tena ni kwenye mrejesho tuu!.

Hi unajua kuwa Chadema ilikuwa wachukue nchi, 2015!, nini kilishindikana?, angalia hapa nilisema nini,
Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM ...

na nini kilitokea!, sisi wengine wenzenu hatuna vyama lakini tunakereka na wacheza makida makida, au wachezea shilingi chooni!, na kazi yetu ni kusema tuu!.

Hiyo siku ikifika andamaneni, ila kama maandamano hayo hayana kibali, hakuna mwenye akili timamu ataandamana!.

Pasco
Sheria ipi inayohitaji maandamano yawe na kibali, hususan kibali cha polisi?
 
S
Sheria ipi inayohitaji maandamano yawe na kibali, hususan kibali cha polisi?
Kila sheria inatungiwa kanuni za utekelezaji, kwenye kanuni ndipo lilipo hitaji la kumwarifu OCD kwa maandishi na OCD atoe kibali kwa maandishi kuwa atapawatia Usalama.

Ikitokea siku hiyo ndio siku ya seminar elekezi kwa askari, hivyo kukawa hakuna askari wa kutosha, au wakipokea taarifa za kiinteligensia za uvunjifu wa amani na Usalama, then OCD atawajibu kwa maandishi kuwa hakuna kibali cha kuandamana wala mikutano!, kwa hoja ya kutokuwepo askari wa kutosha kulinda amani, ila mkiandamana bila kibali askari wa kutosha kuzuia maandamano watapatikana.

Circuses
 
Nimesoma hiyo link na hiki ndicho nilichokupa comment kwenye linki hiyo.

Leo nimeelekezwa na mtu kule jamiiforums kuja bandiko hili. Niliposoma tuu Chapter 1 na kukutana na urongo, nimeishiwa nguvu kuendelea kusoma! . Mwandishi anasema Wamishenari walikuja Africa Mashariki ili kuutokomeza Uislamu!. Huu ni uwongo mkubwa wa mchana kweupe wenye nia ovu, "the ill motives behind ". Wamishenari walikuja kueneza dini na walioenda mahala pengi hata kule ambako hakuna Uislamu kabisa! .

Ukiishaweka urongo mmoja tuu, hata kama kuna ukweli 99, ule ukweli wote unakuwa dismissed na urongo mmoja tuu! .

Wewe mwandishi mwenyewe hiyo elimu yako umeponea shule ya misheni, wasingekuwepo saa hizi ungekuwa wapi? !.

Pasco
 
Katika kitabu chake Bw. Bergen, kiitwacho Development and Religion in Tanzania, katika Ukurasa wake wa 98 mwanadishi huyo anasema:- “Catholic Missionaries came to East Africa to find not new churches, but new provinces of the Roman Church” Kwa mujibu wa tafsiri yangu “Wamishionari wa Kikatoliki hawakuja hapa Afrika ya Mashariki kwa minaajili ya kuasisi Makanisa mapya, bali walikuja kuunda majimbo mapya ya Kanisa la Roma”. Ni kwamba, Tanzania (Tanganyika) ipo Afrika Mashariki, na kwa mujibu wa mwandishi Bergen, Tanzania nayo ni moja ya majimbo ya Kanisa la Roma, au kwa lugha nyepesi tuseme Tanzania ni Koloni la Vatican! Je, ni kweli Tanzania (Tanganyika) ni Koloni la Vatican? Padri. Dk. Sivalon, naye katika kitabu chake Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania Bara (1953-1985) anaeleza bayana kuwa Mwalimu Julius Nyerere Rais wa Kwanza wa nchi yetu, alikuwa kiungo pekee kati ya Chama (CCM), Serikali na Kanisa Katoliki.

N a k w a m s i n g i h u o viongozi wa Kanisa wamekuja kuwa na nafasi ya pekee kuelekeza hisia, mitazamo na siasa ya Tanzania, na wamefanya hivyo wakipania pia kuwa kuhujumu Uislamu. (Msomoe Sivalon Uk. 5-6,
katika kitabu chake hicho). N a y e m w a n d i s h i Bergen katika kitabu chake a m e m n u k u u M w a l i m u Nyerere akisema kamwe hawezi kwenda kinyume na kanisa lake. (Bergen Uk. 335). Agosti 3, 1970 Mwalimu
Nyerere, alimwita Ikulu Padri Rweyemamu katika mazungumzo maalum ambapo Nyerere alimuahidi Rweyemamu kuwa, hivi sasa Kanisa ndilo lililoshika hatamu za kuongoza dola naye atahakikisha hali inaendelea kuwa hivyo. “Tanzania is not Catholic country, but Catholics is strong, I want to give the church a better chance here”. Akiwa na maana kwamba:- japo “Tanzania si nchi ya Kikatoliki, lakini Ukatoliki una nguvu, hivyo nataka kulipa Kanisa nafasi ya pekee hapa nchini” (Msome, Bergen Uk. 335). Na hali hii ya Kanisa kuwa na nafasi kubwa Serikalini iko wazi.

Waandishi wote hawa wanatuthibitishia kuwa, kuna ukweli fulani kwamba yapo mafungamano ya dhati kati ya Kanisa Katoliki na Serikali ya Tanzania. Ni mafungamano hayo hayo ndiyo yameendelea kuwapa uweza viongozi wa Kanisa Katoliki kutoa maelekezo, maagizo na vilio vyao Serikalini na wakasikilizwa pamoja na kutekelezwa yale wanayoyahitaji hata kama yamelenga kuleta maafa kwa Waislamu. Mfano, mwaka 1998, Padri Lwambano, ambaye ni Paroko wa Kanisa Katoliki Mburahati Jijini Dar es Salaam, alisema kuiambia Serikali:- “Lazima Serikali ichukue hatua kali sana kwa Waislamu wanaoendesha Mihadhara, sababu ni watu wabaya kabisa, nimepita Sinza na Mwembechai, n i m e k u t a Wa i s l a m u hao wanamtukana Yesu wanasema Yesu si Mungu”, alisema Paroko huyo na kuongeza; “ K a m a S e r i k a l i imeshindwa kuchukua hatua kali kukomesha Mihadhara ya Waislamu na kuendelea k u t u p a k a m a t o p e k w a mgongo wa chupa, Serikali hii ijue sisi tutalishughulikia jambo hilo kwa nguvu zetu zote”.

K auli hii y a Padri Lwambano, ilirushwa hewani na Kituo cha Radio Tumaini kinachomilikiwa na Kanisa hilo hapa nchini, Februari 13, 1998. Padri Lwambano bila kujali kuwa imani yake inaamini ‘Yesu ni Mungu’ na Waislamu imani yao inaamini ‘Yesu si Mungu’, aliinyooshea kidole Serikali nayo ilifuata bila kujali yenyewe (Serikali) haina dini na raia wake wana dini, kwa imani tofauti.

K a t i k a u t e k e l e z a j i wa agizo hilo bila shaka k i l a m t u a n a k u m b u k a kilichotokea. Ama kwa wale ambao walikuwa ni wadogo kipindi hicho ni kwamba Jeshi la Polisi lilifika Msikiti wa Mwembechai na kuuwa Waislamu kwa risasi na kikumbukumbu ni maarufu kwa ‘Mauaji ya Mwembechai’. Kufuatia madai hayo ya Padri Lwambano, viongozi kadhaa wa nchi walifikia hatua ya kuliomba radhi Kanisa Katoliki na Wakristo kwa ujumla. Majina na vyeo vya viongozi hao wakuu wa Serikali yanafahamika.

Baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Jeshi la Polisi, kazi ya kukatili maisha ya Waislamu na kubaka haki zao, kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini Polycarp Kadinali Pengo, aliipongeza Serikali kwa upande mmoja na Polisi kwa upande wa pili kufuatia mauaji hayo hayo ya Waislamu, Mwembechai. Pongezi hizo alizitoa April 12, 1998 wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Dar es Salaam (DTV). Kanisa likionekana kuuchukukia vilivyo Uislamu, liliongeza harakati za siri na za wazi na kwa kutumia nguvu za dola ili kupunguza kwa upande mwingine nguvu ya Uislamu, maana kuuzima kabisa ni jambo lisilowezekana.

Askofu Mkuu Pengo alitoa taarifa ya kuenea Uislamu hapa Tanzania huku akihitaji msaada wa hali na mali katika kuhidhibiti hali hiyo. Na kwa kweli, Serikali ilitekeleza kudhibiti Mihadhara na Wahadhiri, ambapo wahadhiri maarufu nchini wakiongozwa na Habib Mazinge, walitiwa mbaroni na kutupwa Magerezani. Aidha sehemu ya taarifa yake ilisema hivi; “Uislamu umekuwa tishio kubwa sana kwa imani ya Kikristo nchini Tanzania, iwapo mihadhara ya Waislamu itaachwa iendelee, Kanisa litegemee kukimbiwa na waumini wake na kusilimu, kwa hiyo juhudi lazima zifanywe kuzuia Mihadhara hiyo.

“Tunashindwa kujibu hoja zao Waislamu sababu zina ukweli ndani yake”, maelezo haya yanapatikana katika kitabu cha Askofu Pengo kiitwacho Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwenye vijilia Sinodi ya Maaskofu wa Afrika kwa ajili ya Afrika.
Asante, tumekuelewa, sasa turudi kwenye mada iliyoko mezani.

Kuleta hoja za udini ni dalili ya kuwa mufslisi wa hoja, udini huu peleka huko kunakohusika.

Hapo tuendelee kukata issue iliyomo mezani.

Pasco
 
Nimesoma hiyo link na hiki ndicho nilichokupa comment kwenye linki hiyo.

Leo nimeelekezwa na mtu kule jamiiforums kuja bandiko hili. Niliposoma tuu Chapter 1 na kukutana na urongo, nimeishiwa nguvu kuendelea kusoma! . Mwandishi anasema Wamishenari walikuja Africa Mashariki ili kuutokomeza Uislamu!. Huu ni uwongo mkubwa wa mchana kweupe wenye nia ovu, "the ill motives behind ". Wamishenari walikuja kueneza dini na walioenda mahala pengi hata kule ambako hakuna Uislamu kabisa! .

Ukiishaweka urongo mmoja tuu, hata kama kuna ukweli 99, ule ukweli wote unakuwa dismissed na urongo mmoja tuu! .

Wewe mwandishi mwenyewe hiyo elimu yako umeponea shule ya misheni, wasingekuwepo saa hizi ungekuwa wapi? !.

Pasco

Hiyo elimu yako ya misheni imekusaidia kitu gani ?? Zaidi ya kuhesabu namba na kutapatapa kujipendekeza huku na kule ?? Hufahamiki mara unawaonya chadema mara unataka kwenda kwenye maandamano , umekuwa hufahamiki unataka kitu gani ?

Mara ujipendekeze kwa Magufuli , mara Magufuli ni Dikteta mara Magufuli anahitajika kuwa dikteta

Ni vizuri ukamwona psychiatric NAMBA UNAZISOMA KINYUME NYUME
 
Asante, tumekuelewa, sasa turudi kwenye mada iliyoko mezani.

Kuleta hoja za udini ni dalili ya kuwa mufslisi wa hoja, udini huu peleka huko kunakohusika.

Hapo tuendelee kukata issue iliyomo mezani.

Pasco

NILIKUWA NAKUFAHAMISHA HUO UDIKTETA WA NYERERE LAKINI NJAA INAKUSUMBUA UNAJIFANYA HUTAKI KUSIKIA

SIKILIZA VITABU VYA KIKATOLIKI VINAVYOSEMA au navyo ni kama unavyosema ni

"the ill motives behind ". ???????

Asante nishafahamu sasa turudi kwenye mada iliyo mezani.
Nitamuomba mode jukwaa la dini liwe public ili hawa wafia dini wamalize hasira zao huko.
Pasco
 
Hiyo elimu yako ya misheni imekusaidia kitu gani ?? Zaidi ya kuhesabu namba na kutapatapa kujipendekeza huku na kule ?? Hufahamiki mara unawaonya chadema mara unataka kwenda kwenye maandamano , umekuwa hufahamiki unataka kitu gani ?

Mara ujipendekeze kwa Magufuli , mara Magufuli ni Dikteta mara Magufuli anahitajika kuwa dikteta

Ni vizuri ukamwona psychiatric NAMBA UNAZISOMA KINYUME NYUME
Unaniona kama sina msimamo kwa sababu sina kabisa upande niliiegemea, mimi niko kwenye total neutrality ndio maana Ufipa naenda, Lumumba naenda na Buguruni Mnyamani pia naenda! .

Sifungamani na chama chochote cha siasa bali ukweli pekee.

Pasco
 
Big up Pasco!! ushauri mzur sana...Wahenga walisema asiye sikia la mkuu huvunjika guu...wasipokusikia shauri yao
....yetu macho hyo sinema ya tar moja sept.
 
Kwahiyo unatushauri tuwe kama Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo ili ajiskie always Right.
Huyo Mungu uliemuomba ambariki huyo mvunja katiba ungeanza kwa herufi ndogo jina lake isomeke 'mungu' na sio "Mungu"

Tena tuliosema atakua one term president tulikosea hata term moja hatamaliza kama tutashikilia msimamo wetu Septemba mosi na tunaweza kuigeuza ajenda ikawa ya kumng'oa ikulu.
He should be careful of what he wish for!
Uonekane hiyo tarehe moja, sio unatoa maneno kwenye mitandao alafu tar 1 ujifiche.
 
Unaniona kama sina msimamo kwa sababu sina kabisa upande niliiegemea, mimi niko kwenye total neutrality ndio maana Ufipa naenda, Lumumba naenda na Buguruni Mnyamani pia naenda! .

Sifungamani na chama chochote cha siasa bali ukweli pekee.

Pasco

Usijidanganye nafsi yako wewe ni mtu unayeganga njaa na ndio ukajifanya eti uko neutral . Njaa kitu hatari . Umekua kama paka lenye mikia 9 .Opportunist kinoma. Mara umgeukie magufuli dikteta mzuri. Mara uwageukie chadema msiandamane mara unawaambia chadema nitakuja kuandamana kupinga udikteta . Unafiki mtupu
 
Back
Top Bottom