Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Pasco mwaka 2025 jamaa akiamua atagombea tena kwa mabavu na kuvunja katiba,tutulie tu!Akishindwa akajitangaza mshindi tutulie tu kisa mkubwa ana jeshi?

PASCO ANASAHAU KUWA HILO JESHI ANALORINGIA MAGUFULI PAMOJA NA POLISI NA VYOMBO VYA USALAMA SIO ROBOTS HAO NI BINADAMU

KARUME MKUBWA KAONDOSHA NA HAO ALIOWAAMINI

KABILA MKUBWA YALIMFIKA HAYO HAYO
 
MA kuna karata ambayo wapinzani waliicheza vizuri hasa baada ya uchaguzi mkuu wa 2005 na 2010 ni kile kinachoitwa kama ajenda ya ufisadi. Ajenda hii iliwapa nafasi kubwa mbele ya wananchi wa Tanzania kiasi kwamba iliwafungua macho Watanzania kuelewa jinsi gani ufisadi ni tatizo nchini na ni kwa nini ni lazima udhibitiwe na ikiwezekana ukomeshwe kabisa ili taifa letu lijipe nafasi ya maendeleo ya haraka.

Ajenda hii ilieleweka, ilipendwa na ikakubalika. Hata watu ambao hawakuwa mashabiki wa upinzani waliweza kutafakari na kuona ukweli wa hoja zao kiasi kwamba wakaamua kuwaunga mkono. Na Watanzania hawakufanya utani; walielewa ajenda hii na ikasababisha taifa ligawanyike kifikra; wale ambao wanapinga ufisadi wazi wazi na wale ambao wanajaribu kufafanua ufisadi kwa namna ya kuutetea kiasi kwamba, mtu aliyekuwa CCM alionekana kama ni mtetezi wa ufisadi na yeyote aliyejitaja kuwa yeye ni Chadema basi alikubalika kuwa ni mpinga ufisadi.

Ajenda hii ilikuwa nzuri na iliwaletea matokeo mazuri sana hadi kwenye uchaguzi wa 2010. Ulipokuja uchaguzi wa mwaka jana kama wengi tulivyoshuhudia ajenda hii ilikufa kifo kisicho cha kawaida. Hakuna mtu yeyote ndani ya Chadema ambaye ameweza kuelezea vizuri ni kwa nini waliivuruga ajenda hii nzuri iliyokuwa na mashiko na kuchukua ajenda hewaya ‘mabadiliko ni Lowassa’. Naamini siku moja kuna watu watatoka ndani ya Chadema na watakuwa na ujasiri wa kusema “tulichemsha tulipobadili gia angani”.

Baada ya kuiiua ajenda hii ya ufisadi baadhi yetu hatukujua watakuja na ajenda gani ya kuwapa namna ya kutokea tena mbele ya mtu mashuhuri na anayeonekana kukubalika kama John Magufuli; mtu ambaye wao wenyewe walimsababisha aletwe. Ukweli ni kuwa Magufuli hakuletwa na CCM; CCM ilimsimamisha tu kwa sababu hakukuwa na jinsi; lakini ujio wa Magufuli CCM ni matokeo ya yaliyotokea ndani ya Chadema.

Hata hivyo imeonekana kuwa wamepata ajenda ambayo wanaamini itakubalika na Watanzania. Wanaamini kuwa ajenda hii ikikubalika kama ilivyokuwa ile ajenda waliyoivuruga ya ufisadi basi watakuwa na mahali pa kutokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na ule wa rais na wabunge wa 2010. Ajenda hii mpya ni ile ya kusema kuwa serikali ya sasa ni ya kidikteta na kuwa inaongoza kwa ubabe.

Sasa ajenda hii ni nzuri sana kwenye masikio ya wanasheria na watetezi wa haki za binadamu na watu wanaojali sana mambo ya demokrasia kama mimi. Naweza kuona baadhi ya mantiki ya hoja zao na hata kuwaonea huruma.

Hata hivyo, ajenda hii itakuwa mtego kwao na wasipoangalia watajikuta wamenasa kama yule sungura aliyenasa kwenye kinyago chenye ulimbo. Wameamua kumuita na kuendelea kutangaza kuwa Magufuli ni dikteta tena wengine wanasema ni dikteta uchwara. Na inaonekana wako tayari kabisa kuendeleza mpambano huu wakiamini wanafanya hivyo wakitetea demokrasia.

Hili linaweza kuwa kweli. Tatizo na mtego wenyewe upo kwenye mwitikio wa Watanzania. Mwitikio huu wa Watanzania utategemea kwa kiasi kikubwa kuona ni jinsi gani Magufuli na serikali yake wameweza kwanza kabisa kudhibiti ufisadi, kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mafisadi hasa baada ya kuanza kwa Mahakama ya Wahujumu Uchumi naUfisadi. Je, watumishi wa umma wataanza kuwa na hofu na fedha za umma? Je, watendaji wataanza kuogopa kutumia madaraka yao vibaya kujinufaisha au kunufaisha watu wa karibu yao? Je, fedha za umma ambazo ziliibwa na kufichwa nje ya nchi zitaanza kurudishwa? Je, Magufuli hatawafumbia macho “vigogo” ambao walikuwa hawagusiki miaka nenda rudi?

Kwa kiasi majibu ya hili yameanza kuonekana. Hadi sasa watu wameanza kupata matumaini ya kuona kuwa nchi haiendi kama ilivyokuwa inaenda. Watu wameanza kuamini maneno ya Magufuli kuwa anataka Tanzania isonge mbele.

Na hili litatengeneza jambo la pili. Je, Watanzania wataona mabadiliko katika maisha yao? Je, watoto wao watasoma bure kama ilivyosemwa? Je, shule zitakuwa na madawati na watoto wao hawatokaa chini tena? Je, kutajengwa majengo ya kisasa hata kama ni kwa kutumia makontena ambapo watoto wetu wataweza kusoma kama watoto wa binadamu katika karne ya ishirini na moja? Je, barabara zitakuwa zinapitika misimu yote? Je, kutakuwa na hali ya usalama mitaani?

Majibu ya haya yote yataamua kama “dikteta uchwara” anaweza kuwa ni “dikteta mzalendo”? Au wanayemuita “dikteta uchwara” kumbe siyo bali ni “kiongozi asiye na masikhara”? Kama ni kiongozi ambaye hataki utani kwenye maneno yake, kama ni kiongozi ambaye analosema ndilo analofanya na kuwa hana wa kumwogopa au kumwonea aibu; basi kitambaa chenye maneno “dikteta” ambacho wapinzani wanafikiri wanaweza kukinyanyua kila anakopita Magufuli kinaweza kikaonekana kama ni kituko.

Hatari yake ni kuwa Watanzania ambao walikuwa wanasubiri kiongozi anayesema akamaanisha, asiyecheka na nyani shambani watawaona kuwa wapinzani wanataka kulirudisha taifa kule ambako tumetoka.

Na somo zuri hapa ni kuwa wapo wapinzani ambao wao wenyewe wanamsema Baba waTaifa kuwa alikuwa ni Dikteta; wanasahau – na labda hawajifunzi kabisa kuwa – mamilioni ya Watanzania walimkubali, walimpenda na hadi leo ameacha alama ya mtu aliyelipenda taifa lake kuliko. Kama alikuwa dikteta au la hilo haliwahusu; wanachojua ni kuwa aliwafanya Watanzania wajisikie kuwa wanaheshimika hata katika umaskini wao, hakuogopa kuchukua uamuzi mgumu ambao wakati mwingine haukuwa na matokeo aliyotarajia, lakini hakuna mtu yeyote aliyehoji kama Nyerere alikuwa anawapenda Watanzania. Na wengi wanakumbuka salamu zake za mwisho akiwa hospitalini St. Mary kule Uingereza ni kuwa Watanzania waambiwe kuwa “anawapenda sana”.

Kama Magufuli atakuwa “dikteta” kwa mfano wa Nyerere; kama atawafanya Watanzania watembee vifua mbele, na waone heshima na hadhi ya wao kuwa binadamu, basi kazi ya upinzani itakuwa ngumu mno. Kwani mwisho wa siku wanaweza kujikuta wao tu na wasomi wengine wachache wakilia “dikteta dikteta” wakati mwenzao anawawashia indiketa ya mabadiliko kwa taifa lake.

Mtego wa namna hiyo sijui mtu atajinasuaje. Unaweza kujikuta umenasa hubanduki

Raia Mwema
 
nimesoma hii nakala aisee ni nzuri sana ongera.Japokuwa wapo ambao hawatakuelewa kwa upande wangu nina mambo yafuatayo
1)Turudi nyuma kidogo miaka ya 1995s chama kikubwa cha upinzani kilikuwa ni c.u.f kilipata umarufu lkn kupitia kufanya maandamano walipata kichapo na kupoteza mvuto kwa wanatanzania.
2)kuanzia miaka ya 2000s ndipo chadema ilichukua nafasi ya cuf.Upinzani wa chadema ulikuwa juu sana mara baada ya kusimama na hoja ya ufisadi ambayo iliwapa nguvu sn.Watanzani walipenda kuwasikia wakisema kuhusu ufisadi na misimamo yao ktk jambo hili baya.Lakini kumalizila kwa uchaguzi mkuu nazani mtakubaliana na mimi kuwa chadema hawaimbi hata nyimbo moja ya kukemea ufisadi jambo ambalo linawashangaza wananchi.kitendo cha mh rais kupinga kwa vitendo ufisadi na kuchukua hatua mblmbl zimerudisha imani kwa wananchi.
3)hoja ya udikteta uchwara hii ni hoja ya wanasheria lkn wananchi hajui kbs upuuzi huo.kwani sisi tunataka kuona tunapata huduma nzuri.
my take 1/9/2016 chadema hii ni siku ambayo mtapuuzwa sana kwa kukosa nguvu ya wananchi km mlivyozoea na kuanguka kama cuf
 
"Hakuna dhambi mbaya kama uoga" Godbless Lema

Acha tuandamane tutapambana barabarani na polisi.

Makamanda tujiandae kuingia barabarani nawaomba Mbowe na Lowassa pamoja na Sumaye tuwe pamoja kwenye maandamano.
lowasa huwa anapanda daladala na wananchi nategemea atakuwa front line ktk maandamano pia
 
"Hakuna dhambi mbaya kama uoga" Godbless Lema

Acha tuandamane tutapambana barabarani na polisi.

Makamanda tujiandae kuingia barabarani nawaomba Mbowe na Lowassa pamoja na Sumaye tuwe pamoja kwenye maandamano.
lowasa huwa anapanda daladala na wananchi nategemea atakuwa front line ktk maandamano pia
 
PASCO ANASAHAU KUWA HILO JESHI ANALORINGIA MAGUFULI PAMOJA NA POLISI NA VYOMBO VYA USALAMA SIO ROBOTS HAO NI BINADAMU

KARUME MKUBWA KAONDOSHA NA HAO ALIOWAAMINI

KABILA MKUBWA YALIMFIKA HAYO HAYO
Angalia usimponze Invisible kutakiwa kwa lazima kuwasilisha jina la mmiliki wa title ya Gavana humu jf , na kuliwasilishwa kunahusika ili kufanyiwa uchunguzi asije kuwa ni member wa vikosi vyetu, pia kutafutwa kwa kufanyiwa mahojiano marefu kuhusu posti aliyoipost jf kumtishia Magufuli kuwa asiringie majeshi , na kwamba kunauwezekano kumkuta kilichomkuta Karume Snr na Kabila Snr kwa kuondoshwa na anaowaamini!. Hivyo wakati tukisubiria wale 'jamaa zetu' kumjua Gavana ni nani, tunashauri rais Magufuli afanye pangua pangua ya mabadiliko ya haraka ya vile vikosi vyake vya ulinzi mapema, kwa kuwa weka pembeni walinzi wote waliopo, kama Gavana ni mmoja wao, au type ya hao Gavana aliyowazungumzia, kama wapo ili wasiweze kuleta madhara yoyote, na badala yake, sasa rais wetu alindwe na kikosi maalum cha sungusungu wa Ng'wana Ngosha kutoka Chato?!.

Pasco
 
nimesoma hii nakala aisee ni nzuri sana ongera.Japokuwa wapo ambao hawatakuelewa kwa upande wangu nina mambo yafuatayo
1)Turudi nyuma kidogo miaka ya 1995s chama kikubwa cha upinzani kilikuwa ni c.u.f kilipata umarufu lkn kupitia kufanya maandamano walipata kichapo na kupoteza mvuto kwa wanatanzania.
2)kuanzia miaka ya 2000s ndipo chadema ilichukua nafasi ya cuf.Upinzani wa chadema ulikuwa juu sana mara baada ya kusimama na hoja ya ufisadi ambayo iliwapa nguvu sn.Watanzani walipenda kuwasikia wakisema kuhusu ufisadi na misimamo yao ktk jambo hili baya.Lakini kumalizila kwa uchaguzi mkuu nazani mtakubaliana na mimi kuwa chadema hawaimbi hata nyimbo moja ya kukemea ufisadi jambo ambalo linawashangaza wananchi.kitendo cha mh rais kupinga kwa vitendo ufisadi na kuchukua hatua mblmbl zimerudisha imani kwa wananchi.
3)hoja ya udikteta uchwara hii ni hoja ya wanasheria lkn wananchi hajui kbs upuuzi huo.kwani sisi tunataka kuona tunapata huduma nzuri.
my take 1/9/2016 chadema hii ni siku ambayo mtapuuzwa sana kwa kukosa nguvu ya wananchi km mlivyozoea na kuanguka kama cuf
kumbuka majipu yote ccm na wananchi wanalitambua hilo na UKAWA haina haja tena ya kuwaambia wananchi.tunakwenda kuzuia UDIKTETA TAREHE 1 HILO LIKO WAZI
subiria mziki wake tu.

swissme
 
Sasa ndio ufurahi kupuuzwa kwa chadema ili ccm iendelee kuongoza badala ya kujifanya unashauri kumbe ni mnafiki tu kwa kuleta propaganda uchwara.
 
MANENO HAYO UNAYAPATA KWENYE KATIKA IPI ??
Hayo sio maneno ya katiba bali ni maneno ya yule tuliyempa dhamana ya kuilinda katiba yetu, kwa ridhaa yetu wenyewe, kupitia uchaguzi huru na wa haki, ametutangazia kuwa uchaguzi umekwisha, muda wa kupiga siasa ulikuwa ni wakati wa uchaguzi, baada ya uchaguzi kumalizika pia muda wa kupiga siasa nao umemalizika sasa ni wakati wa kuchapa kazi kulinganisha taifa na sio kukalia kupiga siasa domo, ndio maana kwa kauli mbiu yake ni "sasa kazi, hapa kazi tuu ".

Na katiba inasema kitu gani kuhusu kufanya siasa ??? Tafadhali nisaidie
 
Angalia usimponze Invisible kutakiwa kwa lazima kuwasilisha jina la mmiliki wa title ya Gavana humu jf , na kuliwasilishwa kunahusika ili kufanyiwa uchunguzi asije kuwa ni member wa vikosi vyetu, pia kutafutwa kwa kufanyiwa mahojiano marefu kuhusu posti aliyoipost jf kumtishia Magufuli kuwa asiringie majeshi , na kwamba kunauwezekano kumkuta kilichomkuta Karume Snr na Kabila Snr kwa kuondoshwa na anaowaamini!. Hivyo wakati tukisubiria wale 'jamaa zetu' kumjua Gavana ni nani, tunashauri rais Magufuli afanye pangua pangua ya mabadiliko ya haraka ya vile vikosi vyake vya ulinzi mapema, kwa kuwa weka pembeni walinzi wote waliopo, kama Gavana ni mmoja wao, au type ya hao Gavana aliyowazungumzia, kama wapo ili wasiweze kuleta madhara yoyote, na badala yake, sasa rais wetu alindwe na kikosi maalum cha sungusungu wa Ng'wana Ngosha kutoka Chato?!.

Pasco

Pasco nilifikiri wewe ni great thinker kumbe ni wale watu wa maskani.

Mimi sijamtishia mtu , Mbona pasco unatishika kumbe wewe ni muoga kiasi hiki ????

Unamfanya magufuli naye awe mwoga kama wewe ????

Hivi unapoongoza kwa haki na uadilifu unaogopa kitu gani ???

Wa kuogopwa ni Mungu anayeweza kuangamiza mwili na roho au hujui hilo ???

Mimi ninawakumbusha muelewe hilo kwa kuwa ninawapenda

kwani niliyotamka ni uongo ???

Pasco tuko karne nyengine hii
 
Angalia usimponze Invisible kutakiwa kwa lazima kuwasilisha jina la mmiliki wa title ya Gavana humu jf , na kuliwasilishwa kunahusika ili kufanyiwa uchunguzi asije kuwa ni member wa vikosi vyetu, pia kutafutwa kwa kufanyiwa mahojiano marefu kuhusu posti aliyoipost jf kumtishia Magufuli kuwa asiringie majeshi , na kwamba kunauwezekano kumkuta kilichomkuta Karume Snr na Kabila Snr kwa kuondoshwa na anaowaamini!. Hivyo wakati tukisubiria wale 'jamaa zetu' kumjua Gavana ni nani, tunashauri rais Magufuli afanye pangua pangua ya mabadiliko ya haraka ya vile vikosi vyake vya ulinzi mapema, kwa kuwa weka pembeni walinzi wote waliopo, kama Gavana ni mmoja wao, au type ya hao Gavana aliyowazungumzia, kama wapo ili wasiweze kuleta madhara yoyote, na badala yake, sasa rais wetu alindwe na kikosi maalum cha sungusungu wa Ng'wana Ngosha kutoka Chato?!.

Pasco

Kumbe Pasco wewe ni kada wa vijiweni ??? Kumbe wewe siye Great thinker ?

Hivi ulifika darasa la ngapi ???

Kwani hayo niliyosema , nimesema uongo hapo ??? nani asiyejua kuwa Karume kauliwa na askari

Nani asiyejua kuwa Kabila kauliwa na askari

unamtishia nani hapa

Ukitaka id yangu sio siri nitakupa usimtishie mtu hapa

Ogopa yule anayeweza kuangamiza mwili na roho

Huyo Magufuli anaogopa kitu gani kama anajiamini anafuata haki . Mungu hamtoshi kuwa mlinzi wake ???

Wacha kumtisha mtu , hivi unafikiri hapa uko maskani??? HAPA UPO JF KWA GREAT THINKERS
 
Back
Top Bottom