Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
- #241
Mkuu Maono Makuu, kwanza asante kwa mchango huu, na kweli wewe ni maono makuu!, nimeguswa sana na mchango wako, haswa ulipozungumzia Vietnam, hili neno "for others to survive, others must die!", kitaaluma mimi ni mtangazaji, uandishi ni kwa kujitolea tuu for the love of it!, kama ni kuandika humu, nimeandika sana, wenye macho wameona na amini usiamini hao viongozi tunaowaandika humu wanaona na wanasoma, wengine wana change for the better kutokana na michango ya jf, lakini hawana ujasiri wa kusema asante!, hivyo we are doing something!.Nilitegemea uwashauri pia wachukue hatua gani ili dikteta aache udikteta kama andiko langu yenye ushauri. Dikteta hatazamwi tu na kusema shauri yake bali anazuiwa na wasiopenda huo udikteta. Udikteta ukikomaa madhara yake ni makubwa mno anaweza akamwita hata kampeni manaja wake akamchinja. Wenye ujasiri lazima wapambane ili kumdhibiti akaleta madhara makubwa na yeye kuendelea kujifunza kufuata katiba aliyotumia Kuapa kuwa atalinda. Kwa wale tuliowahi kuangalia vita ya Vietnam wanasema FOR OTHERS TO SURVIVE OTHERS MUST DIE. Pasco tumia taaluma yako kutoa maandiko mengi ya viongozi wetu kufuata katiba na kutii sheria kama wazee wetu walivyoasisi. CCM walipa kura zaidi ya million nane, Wapinzani wana kura zaidi ya million sita. Kuna kura zaidi million tisa hazijapiga kura hivyo bado kazi ni kubwa kushindana na wapinzani.
Kwa vile mimi ni mtangazaji, bado najipanga kuzivurumisha hoja zangu kwenye talk show program, kitu cha kwanza ni kujenga kwanza mazingira bora ya familia, kuhakikisha whatever happens to you, usimtese mke na watoto by dying for others to survive, nakaribia kusimama imara, na baada ya kusimama, kiukweli nitawalipua vilivyo ili kuhakikisha Tanzania ni nchi ya katiba inayoheshimiwa inayofuata the rule of law na sio utashi wa viongozi wenye viashiria vyote vya udikiteta na utawala wa kiimla!.
Pasco