Mr Pasco, please hebu naomba nijuze kidogo, inawezekana mimi sielewi.
Hivi hizi "politics of development" ni zipi hizo na zinafanywaje mkubwa?
Na ukimaliza kueleza hebu dadavua na "politics of confrontation" ni zipi hizo na zinafanywaje eti?
Nimeona na kimsikia mkulu wetu mara nyingi naye akisema "watanzania wanataka siasa za maendeleo"... it is a little bit confuses me ninaposikia na kusoma vitu kama hivi!
It is either you and Mr president don't understand the meaning of politics in relationship with development or you purposely try to manipulate people with your own defenition of politics!
That's what I can comment about these fallaciuos statements from you guys!!
Namkumbuka sana Dr Wilbroad Peter Slaa katibu mkuu wa CHADEMA aliyepita aliyeongoza harakati kabambe wakati wa Kikwete hata kuiweka CHADEMA ktk chati ya juu na pengine kuifanya serikali iamke na kufanya kazi ya ziada ktk kutekeleza ahadi zake za kuwahudumia wananchi kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo japo kasoro za hapa na pale haziwezi kukosekana.
Tell me. CHADEMA ya wakati wa Dr Slaa ilikuwa inafanya siasa za namna gani kati ya hizo ulizozitaja.....development or confrontation politics.........or both?
Mkuu Kitaturu, kuna siasa za aina tatu, siasa za maendeleo, (developmental politics), siasa za kujifurahisha (politics of politiking), na kuna siasa za migogoro, (politics of confrontation).
1. Siasa za Maendeleo.
Hizi ni siasa zenye malengo ya kuleta mabadiliko chanya, changing for the better. Kila political move unayofanya, ila malengo chanya ya kuleta mabadiliko, siasa hizi zimefundishwa sana na Mwalimu Nyerere katika kitabu chake cha Binadamu na Maendeleo. Siasa hizi ni siasa zenye sera, ilani, malengo, mikakati na time frame, hizi mimi naziita SMART Politics, ni siasa zenye
S - specific, significant, stretching
M - measurable, meaningful, motivational
A - agreed upon, attainable, achievable, acceptable, action-oriented
R - realistic, relevant, reasonable, rewarding, results-oriented
T - time-based, time-bound, timely, tangible, trackable
2. Siasa za Kujifurahisha.
Hizi ni kauli za kisiasa kwa ajili ya kujifurahisha tuu to gain political mileage lakini hakuna chochote kinachofanyika, hizi zinajumlisha ahadi zisizotekeleka, hizi ni politiking, mtu unazungumza ili tuu uonekane na wewe upo upo. Kwenye kundi hili, zile siasa za bendera fuata upepo pia zimo kwenye kundi hili. Hizi ni siasa ambazo hazina maana yoyote kwa maendeleo!, huku ndiko siasa za fitna, majungu, uongo, zengwe etc, etc.
3. Siasa na Migogoro
Hizi naziita ni siasa za attention seeking, yaani kupinga tuu kila kitu ili tuu kuonekana na kutafuta public sympathy, lakini hizo moves hazina faida yoyote wala manufaa yoyote ya maana!. Hapa ndio pale watu wanapinga kila kitu hata kile chenye manufaa kwao kwa lengo la kutafuta tuu mgogoro. Siasa hizi hufanywa sana kwa mikutano ya hadhaa na maandamano ambayo hayana manufaa yoyote!.
Mfano hai ni hii kampeni ya UKUTA!, Rais Magufuli ambaye kweli ni dikiteta, amevunja katiba kwa kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kinyume cha katiba!. Chadema wanasema wao wataandamana na kufanya mikutano nchi nzima!. Lengo la mikutano hii na maandamano wameiita kupinga udikiteta nchini!. Sasa kitakachofanyika kwenye mikutano hiyo na maandamano ni mabango na kauli chonganishi kuupinga udikiteta ili wananchi waone Chadema inapinga udikiteta wa Magufuli!. Kupinga huku ni kwa kujifurahisha tuu, kwa sababu hakutabadilisha lolote wala chochote katika udikiteta wa Magufuli, sana sana Magufuli atawatandika tena kwa kutumia "za moto" japo taarifa ya polisi itasema ni rubber bullets, na miili ya baadhi ya wataotandikwa, itachukuliwa na polisi na ku vanish into thin air!, hakuna atakayejua nini kiliwasibu!.
SMART politics kwenye kuupinga udikiteta wa Magufuli, ni kwa kutumia katiba na sheria, imeeleza wazi nini kinachotakiwa kufanywa pale kiongozi aliyeapa kuilinda katiba, akawa ndie wa kwanza kuivunja hiyo katiba!. Mikutano ya hadharra na maandamano sio njia sahihi ya kudeal na udikiteta wa mkuu wa nchi, haswa ukizingatia dikiteta mwenyewe, ni dikiteta mzalendo!, hicho anachofanya rais Magufuli, ndicho wananchi wanachotaka na ndicho kinachoweza kufanyika kututoa hapa tulipo, na kutufikisha kule tunakotaka kwenda!.
Kama ulifuatilia ule mkutano wa Chadema wa Mwembe Yanga, ulioitangaza list of shame, Katibu Mkuu wa Chadema na viongozi wote walikuwa wakali sana kuhusu rushwa na ufisadi, huku wakiendesha siasa za uanaharakati. Miongoni mwa sala za wanahaakati ni kumuomba Mungu, atupatie rais dikiteta mwenye uwezo wa kudeal na rushwa na ufisadi!. Mungu katusikia sala zetu, katupatia rais dikitate kweli, John Pombe Magufuli!, sasa wale wale waliokuwa wakipinga rushwa na ufisadi, sasa ndio wamewakumbatia mafisadi wale wale wa kwenye list of shame na sasa ndio wanaopiga kelele kulaani rais dikiteta!.
Pasco