Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Kwahiyo unatushauri tuwe kama Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo ili ajiskie always Right.
Huyo Mungu uliemuomba ambariki huyo mvunja katiba ungeanza kwa herufi ndogo jina lake isomeke 'mungu' na sio "Mungu"

Tena tuliosema atakua one term president tulikosea hata term moja hatamaliza kama tutashikilia msimamo wetu Septemba mosi na tunaweza kuigeuza ajenda ikawa ya kumng'oa ikulu.
He should be careful of what he wish for!

Ajenda ikawa ya kumng'oa Ikulu? Ben huyo? Halafu nchi umpe nani? Are you serious, ulifikiri kweli ulipoyaandika haya? Ben, may be you should be hospitalized, what happened to your thinking?
 
Hainitishi, naiunga mkono na ndio maana nimejitolea kuhamasisha watu tujitokeze kwa wingi siku hiyo ikifika!.
Kufuatia Umuhimu wa Maandamano ya UKUTA: Nimehamasika, Nitashiriki ...
Pasco

Pasco hii kaandika nani kama si woga , Tizama umezidiwa na woga mpaka umechanganyikiwa ???

Haya kaandika nani ??? au Pasco si mtu mmoja ni watu wengi ??? PASCO & CO.LTD

Wanabodi,

Kama kawaida yangu kutoa ushauri wa bure, huu ni ushauri wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba, nawashauri kwa dhati kabisa, tafadhalini sana msiandamane, na kusitisha hiyo Operesheni UKUTA, ili kuutumia ule msemo wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, na sio tuu ana nguvu zaidi yako, na tayari, umeishajua ni dikiteta, bali ndio mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.
 
1.Pasco nilifikiri wewe ni great thinker kumbe ni wale watu wa maskani.
2.Mimi sijamtishia mtu , Mbona pasco unatishika kumbe wewe ni muoga kiasi hiki ????
3.Unamfanya magufuli naye awe mwoga kama wewe ????
4.Hivi unapoongoza kwa haki na uadilifu unaogopa kitu gani ???
5.Wa kuogopwa ni Mungu anayeweza kuangamiza mwili na roho au hujui hilo ???
6.Mimi ninawakumbusha muelewe hilo kwa kuwa ninawapenda
7.kwani niliyotamka ni uongo ???
8.Pasco tuko karne nyengine hii
9.Kumbe Pasco wewe ni kada wa vijiweni ???
10.Kumbe wewe siye Great thinker ?
11.Hivi ulifika darasa la ngapi ???
12.Kwani hayo niliyosema , nimesema uongo hapo ??? nani asiyejua kuwa Karume kauliwa na askari
13.Nani asiyejua kuwa Kabila kauliwa na askari
14.unamtishia nani hapa
15.Ukitaka id yangu sio siri nitakupa usimtishie mtu hapa
16.Ogopa yule anayeweza kuangamiza mwili na roho
17.Huyo Magufuli anaogopa kitu gani kama anajiamini anafuata haki . Mungu hamtoshi kuwa mlinzi wake ???
18.Wacha kumtisha mtu , hivi unafikiri hapa uko maskani??? HAPA UPO JF KWA GREAT THINKERS
Mkuu Gavana,
1. Mimi sio GT ila pia sio mtu wa maskani, mimi ni free thinker ambaye sina chama chochote!, tukiunda maskani za ukweli mtupu, niajiunga!.
2. Mimi kweli ni muoga kuliko hata kunguru!, kwa ulichokisema, nimetishika, kwa sababu hata Hamudu alikisema kitu kama hicho, akapuuzwa!, na siku ya siku, akakitekeleza!, hapa nimewapa tuu angalizo, wale 'jamaa zetu' ili kama uu mmoja wao, wakuweke mahala salama!.
3. Magufuli ni muoga kuliko hata mimi, hata kelele tuu za mikutano ya hadhara zinamtisha, na kuhusu UKUTA, ameishatoa onyo, mwenye masikio na asikiye!.
4. Nikikutana naye nitakuulizia hili!.
5. Ni kweli wa kuogopwa ni Mungu tuu, ila vitabu vitakatifu, vimetufunza tutii mamlaka halali!.
6. Asante kwa upendo wa mshumaa, kuwamulikia wengine huku kwaklo kunateketea!.
7. Ni ukweli mtupu, ila kuna tofauti kati ya kutamka na ku anticipate uliyotamka, yatokee!.
8. Ni kweli tuko karne nyingine, zamani kujificha nyuma ya keyboard kwa kutumia penname, kulitosha, sasa tuko kwenye ip, kwa kutumia GPS, hadi uvunguni mtu unaonekana!.
9. kama jibu no.2
10. Kama jibu no.1
11. Niliishia darasa la 7.
12. Kama jibu no.7
13. Kama jibu no.7
14.Simtishi mtu, bali nimetoa tuu angalizo, angalia usije ukamponza Invicible.
15. Sio mimi wa kuitaka ID yako, bale ni wale "jamaa zetu" iwapo nao watatishika kama mimi!.
16. Kama jibu no 5
17. Kama jibu no 4
18. Kama jibu no 14.

Pasco
 
Pasco hii kaandika nani kama si woga , Tizama umezidiwa na woga mpaka umechanganyikiwa ???

Haya kaandika nani ??? au Pasco si mtu mmoja ni watu wengi ??? PASCO & CO.LTD
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kutoa ushauri wa bure, huu ni ushauri wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba, nawashauri kwa dhati kabisa, tafadhalini sana msiandamane, na kusitisha hiyo Operesheni UKUTA, ili kuutumia ule msemo wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, na sio tuu ana nguvu zaidi yako, na tayari, umeishajua ni dikiteta, bali ndio mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.
Mkuu Gavana, huu sio uoga bali ni angalizo tuu!. Na baada ya kutoa angalizo hili, si nimerejea jf nikasema
Kufuatia Umuhimu wa Maandamano ya UKUTA: Nimehamasika, Nitashiriki Kikamilifu...

Pasco
 
Mkuu Gavana,

1. Mimi sio GT ila pia sio mtu wa maskani, mimi ni free thinker ambaye sina chama chochote!, tukiunda maskani za ukweli mtupu, niajiunga!.
2. Mimi kweli ni muoga kuliko hata kunguru!, kwa ulichokisema, nimetishika, kwa sababu hata Hamudu alikisema kitu kama hicho, akapuuzwa!, na siku ya siku, akakitekeleza!, hapa nimewapa tuu angalizo, wale 'jamaa zetu' ili kama uu mmoja wao, wakuweke mahala salama!.
3. Magufuli ni muoga kuliko hata mimi, hata kelele tuu za mikutano ya hadhara zinamtisha, na kuhusu UKUTA, ameishatoa onyo, mwenye masikio na asikiye!.
4. Nikikutana naye nitakuulizia hili!.
5. Ni kweli wa kuogopwa ni Mungu tuu, ila vitabu vitakatifu, vimetufunza tutii mamlaka halali!.
6. Asante kwa upendo wa mshumaa, kuwamulikia wengine huku kwaklo kunateketea!.
7. Ni ukweli mtupu, ila kuna tofauti kati ya kutamka na ku anticipate uliyotamka, yatokee!.
8. Ni kweli tuko karne nyingine, zamani kujificha nyuma ya keyboard kwa kutumia penname, kulitosha, sasa tuko kwenye ip, kwa kutumia GPS, hadi uvunguni mtu unaonekana!.
9. kama jibu no.2
10. Kama jibu no.1
11. Niliishia darasa la 7.
12. Kama jibu no.7
13. Kama jibu no.7
14.Simtishi mtu, bali nimetoa tuu angalizo, angalia usije ukamponza Invicible.
15. Sio mimi wa kuitaka ID yako, bale ni wale "jamaa zetu" iwapo nao watatishika kama mimi!.
16. Kama jibu no 5
17. Kama jibu no 4
18. Kama jibu no 14.

Pasco

2. Mimi kweli ni muoga kuliko hata kunguru!, kwa ulichokisema, nimetishika, kwa sababu hata Hamudu alikisema kitu kama hicho, akapuuzwa!, na siku ya siku, akakitekeleza!, hapa nimewapa tuu angalizo, wale 'jamaa zetu' ili kama uu mmoja wao, wakuweke mahala salama!.

MAJIBU

Hamuud alisema nini na mimi nimesema nini ??? Aliyemuua Kabila alisema nini ?? mbona unajichanganya ??? Na kujaribu kutisha watu ukitumia nyuso tofauti ??? huu si unafiki ni kitu gani ???

hichi ulichokiandika ni kitu gani ??

Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

6. Asante kwa upendo wa mshumaa, kuwamulikia wengine huku kwaklo kunateketea!.

MAJIBU

Kumbe una ajenda yako nyengine na ndio ukawa ni mtu mwenye nyuso nyingi ???

7. Ni ukweli mtupu, ila kuna tofauti kati ya kutamka na ku anticipate uliyotamka, yatokee!.

MAJIBU

Soma vizuri nimeandika kitu gani ??? ni wapi nime anticipate yatokee ???

8. Ni kweli tuko karne nyingine, zamani kujificha nyuma ya keyboard kwa kutumia penname, kulitosha, sasa tuko kwenye ip, kwa kutumia GPS, hadi uvunguni mtu unaonekana!.

MAJIBU

Kama ndio hivyo yanini kutishana kuhusu id na kumtisha invicible na wakati GPS zipo ???
 
Mimi ni yule yule juzi, jana na leo!. Nimeanzisha threads 973 na kuchangia mara 18,330.
Kama ni hoja ya udikiteta, nimeizungumza sana humu, tofauti na wengi, kwao ikiwa ni nyeusi basi lazima iwe ni nyeusi tii, hata kama ina madoa madoa meupe, hawakubali kusema, ina madao, watang'ang'ania nyeusi tii!.

Mimi ni mtu mkweli daima na siku zote husema ukweli daima na sio kuwafurahisha watu humu na wala sifungamani na chama chochote, katika hizo post zote angalia kitu kinachoitwa central theme ni moja na imesimama kuwa Magufuli ni dikiteta, ila pia Tanzania, tulipofikia, tunahitaji mtu kama huyu ili mambo yaende!.

Nakuona kama una panic, usipanic, nimesisitiza sikutishi, wala sitishi mtu, bali nimetoa tuu angalizo, next time chunga sana hizi kauli za ma prophets of the doom!, likitokea la kutokea, kunakuwa hakuna pa kutokea, hata kama ulijisemea tuu, na wala huhusiki, ila by the time inakuja kuwa proved huhusiki, it might be too little too late!.

Nashauri kwa hapa tulipofika, inatosha, sasa nenda na nyuzi nyingine!.

Pasco
 
Haya usemayo ni kweli, kwa watetezi wa demokrasia ya kweli wanaotaka kuiona Tanzania ikishamiri kwenye mfumo imara wa vyama vingi, kwa huku bara, wataisupport Chadema, lakini hawatakuwa tayari kuinga mkono inapofanya maamuzi ya kitoto kama ya ya bungeni, na hili sasa la kutaka kumchezea simba sharubu!.

Chadema needs serious help rather than sympathy!, wekiendelea na mipango hii ya kutunushiana misuli badala ya kufuata the right cause of action, hata hao wenye busara wake wataishia kuonekana ni wajinga tuu!.

Pasco
Now I know which side of your arguments represent. Repression of justice and cowardice; you are not alone; but leave us WE DO NOT WANT HELP FROM YOU OR THOSE YOU YOU REPRESENT.
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kutoa ushauri wa bure, huu ni ushauri wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba, nawashauri kwa dhati kabisa, tafadhalini sana msiandamane, na kusitisha hiyo Operesheni UKUTA, ili kuutumia ule msemo wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, na sio tuu ana nguvu zaidi yako, na tayari, umeishajua ni dikiteta, bali ndio mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.

Misingi ya Katiba na The Rule of Law
Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya katiba na sheria, (the rule of law) ambapo inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na sio kwa matamko ya viongozi yanayokwenda kinyume cha katiba!.

The Separation of Powers & Check and Balance .
Nchi yetu ina mihimili mikuu mitatu, Serikali, (the executive), Bunge (The Legislature) na Mahakama (The Judiciary). Mihimili hii mitatu, ilipaswa kufanya kazi kwa kujitegemea bila mhimili mmoja kuingilia mhimili mwingine (independence), huki kila mhimili uki act as a watchdog wa muhimili mwingine usivuke mipaka ya madaraka au mamlaka yake yaani (The sepaation of powers check and balance).

Serikali yenye Nguvu, Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo!.
Mihimili hii, inaongozwa na viongozi ambao wana mamlaka kuu kuhusu mihimili yao. President ndio mkuu wa the executive, Spika ndio mkuu wa The Legistlatue, na Jaji Mkuu, ndie mkuu wa The Judiciary, lakini pamoja na nia njema kuwa mihimili yote inamamlaka na hakuna mhimili wowote uliokuwa unapaswa kuwa na mamlaka kuliko mhimili mwingine, lakini kiukweli, mhimili wa the executive ndio mhimili mkuu unaomiliki vyombo vya dola na kuitawala mihimili mingine yote!, hivyo mkuu wa the executive, yaani rais, ndio kila kitu!, akisema!, amesema!.

Rais Magufuli na Uvunjaji wa Katiba.
Tuambiane ukweli, tangu rais Magufuli ameingia madarakani, sio mara moja au mbili amekuwa akitoa kauli tata, zinazokwenda kinyume cha katiba, mhimili wa Bunge na Mahakama ilipaswa kuingilia kati kwa kumcheck mkuu wa the executive, lakini vyombo hivyo vimekaa kimya hivyo kumfanya rais ajisikie kuwa he is always right! kwa kanuni ya "the boss is always right!".

Udikiteta wa Magufuli.
Hoja kama Magufuli ni dikiteta au la, haina mjadala, Magufuli ni dikiteta wa ukweli ambaye hana msalie mtume, na alipoingia tuu madarakani, alianza kuonyesha udikiteta wake right away kwa kuliingilia bunge na mahakama kuziweka chini ya amri zake!. Lile katazo lake la watumishi wa umma hawaruhusiwi kusafiri safari za nje bila kibali chake kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, liliwahusu watumishi wote wa serikali, likiwemo bunge na mahakama!, just imagine Jaji Mkuu na Spika wa bunge wakapige magoti kwa rais kuomba kutimiza wajibu wao!.

Baada ya katazo lile, checks and balance zingepaswa kuanzia hapo kwa Jaji Mkuu kumweleza rais huko ni kuingilia uhuru wa mahakama (the independence of the judiciary) hivyo muhimili wa mahakama haukupaswa kujisubmit chini ya the executuve, bali mamlaka hayo ya kuzuia safari za nje, Spika alipaswa kuwa nayo kudhibiti safari za mhimili wa bunge, na Jaji Mkuu alipaswa kuwana nayo kudhibiti safari za mhimili wa mahakama, lakini mihimili hii ilikaa kimya kwa kujisubmit chini ya the executive, hivyo kumfanya rais ndio kila kitu!.

Hivyo sasa rais Magufuli ndio kila kitu, hakuna cha bunge, mahakama, wala katiba, amri ya rais ndio kila kitu na ndio sheria kuu!, hivyo nawashauri Chadema kwa dhati kabisa, wasitishe maandamano yao, wasifanye kabisa mchezo wa kumjaribu Ngosha, wataumia bure!.

Hili la udikiteta wa rais Magufuli, tumeisha lizungumza sana humu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa ...

Ila kitu kimoja kuzuri kuhusu udikiteta wa rais wetu, ni Rais Magufuli ni dikiteta mzalendo!, mwenye uchungu na umasikini wa nchi hii, mwenye nia njema ya kusafisha uozo wote wa uzembe, rushwa na ufisadi, na kulikomboa taifa letu toka kwenye lindi la umasikini uliotopea na kuwa nchi ya maziwa na asali kupitia uchumi wa gesi na viwanda.

Mungu mbariki Magufuli!.

Mungu ibariki Tanzania.

Wasalaam.

Pasco
Rejea za shauri za bure
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa ...
Ushauri wa Bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared for ...
Ushauri wa Bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako ...
Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep ...
Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)-Kwa Hili la ...
Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report: Please Keep Quite ...
Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Magufuli, Futilia Mbali Utawala wa Sheria ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Usikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
Ushauri wa Bure kwa Dr. Shein: Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ...
Ushauri wa Bure kwa Magufuli, DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...

Is it true that Tanzania the MOST PASSIVE SOCIETY IN THE WORLD? No I can not believe this!!
That we must say YES to dictatorship. Be ware
The negative effects of dictatorship is not only for opposition parties or northern tribes or coastal areas or central Tanzania or the southerners or the westerners or easterners. Dictatorship has no History of boundaries I tell you. It is for all
Even the ruling party leaders and members are suffering in their hearts!! Come out before it is too late.
The check of sanity must be a must for all Tanzanians!! if you can not see this!!
 
Now I know which side of your arguments represent. Repression of justice and cowardice; you are not alone; but leave us WE DO NOT WANT HELP FROM YOU OR THOSE YOU YOU REPRESENT.
I represent nobody but the truth!. Ushauri wa bure ni sadakalawe tuu, you take it or leave it, tutakapokuta tena ni kwenye mrejesho tuu!.

Hi unajua kuwa Chadema ilikuwa wachukue nchi, 2015!, nini kilishindikana?, angalia hapa nilisema nini,
Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM ...

na nini kilitokea!, sisi wengine wenzenu hatuna vyama lakini tunakereka na wacheza makida makida, au wachezea shilingi chooni!, na kazi yetu ni kusema tuu!.

Hiyo siku ikifika andamaneni, ila kama maandamano hayo hayana kibali, hakuna mwenye akili timamu ataandamana!.

Pasco
 
Nakuona kama una panic, usipanic, nimesisitiza sikutishi, wala sitishi mtu, bali nimetoa tuu angalizo, next time chunga sana hizi kauli za ma prophets of the doom!, likitokea la kutokea, kunakuwa hakuna pa kutokea, hata kama ulijisemea tuu, na wala huhusiki, ila by the time inakuja kuwa proved huhusiki, it might be too little too late!.

Nashauri kwa hapa tulipofika, inatosha, sasa nenda na nyuzi nyingine!.

Pasco

Unakimbia kistyle. Mimi simkimbii mtu wala simwogopi mtu huko ndani tumeshakaa tena wakati wa dikteta nyerere .Aliyepanic ni wewe ambye una njaa yako unajaribu kujipendekeza huku na huku uonekanwe ni mtaalamu kumbe njaa inakusumbua. Au namba zimekuwia nyingi umechanganyikiwa kuzisoma
 
I represent nobody but the truth!. Ushauri wa bure ni sadakalawe tuu, you take it or leave it, tutakapokuta tena ni kwenye mrejesho tuu!.

Hi unajua kuwa Chadema ilikuwa wachukue nchi, 2015!, nini kilishindikana?, angalia hapa nilisema nini,
Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM ...

na nini kilitokea!, sisi wengine wenzenu hatuna vyama lakini tunakereka na wacheza makida makida, au wachezea shilingi chooni!, na kazi yetu ni kusema tuu!.

Hiyo siku ikifika andamaneni, ila kama maandamano hayo hayana kibali, hakuna mwenye akili timamu ataandamana!.

Pasco

Unaingia kwa ngozi yako halisi . Umetumwa??? Au ulipewa buku ngapi na Lumumba kwa hii kazi ??
 
Is it true that Tanzania the MOST PASSIVE SOCIETY IN THE WORLD? No I can not believe this!!
That we must say YES to dictatorship. Be ware
The negative effects of dictatorship is not only for opposition parties or northern tribes or coastal areas or central Tanzania or the southerners or the westerners or easterners. Dictatorship has no History of boundaries I tell you. It is for all
Even the ruling party leaders and members are suffering in their hearts!! Come out before it is too late.
The check of sanity must be a must for all Tanzanians!! if you can not see this!!

Unamkatisha maini pasco &co. Ltd
 
Mimi ni yule yule juzi, jana na leo!. Nimeanzisha threads 973 na kuchangia mara 18,330.
Kama ni hoja ya udikiteta, nimeizungumza sana humu, tofauti na wengi, kwao ikiwa ni nyeusi basi lazima iwe ni nyeusi tii, hata kama ina madoa madoa meupe, hawakubali kusema, ina madao, watang'ang'ania nyeusi tii!.

Mimi ni mtu mkweli daima na siku zote husema ukweli daima na sio kuwafurahisha watu humu na wala sifungamani na chama chochote, katika hizo post zote angalia kitu kinachoitwa central theme ni moja na imesimama kuwa Magufuli ni dikiteta, ila pia Tanzania, tulipofikia, tunahitaji mtu kama huyu ili mambo yaende!.

Pasco

Tanzania haihitaji dikteta inahitaji mtu mkweli mwenye kufuata katiba ambayo ameiapia kuilinda na kuifuata pamoja na sheria za nchi.
 
Huku kufuata katiba, sheria, Taratibu na kanuni ndio kumetufikisha hapa tulipo. Tanzania ili hitaji dikiteta mzalendo anayefanya udikiteta kwa nia njema na dhamira safi ya kulikomboa taifa hili toka kwenye lindi la umasikini uliotopea uliogubikwa na rushwa na ufisadi.

Aliyeifikisha nchi hapa ni dictator Nyerere . Watu wakiburunga yeye akiwabadilisha wizara . Kama tunahitaji dictator unamdanganya nani?? wazungu na viumbe vyake kwa kuapa utailinda katiba?

Hao unaowaongoza sio robots na wala hao wataokulinda sio robots.

Angalia nini kinatokea Burundi, somalia na kwengineko kwenye madikteta. Mwisho wake ni maangamizo
 
Aliyeifikisha nchi hapa ni dictator Nyerere . Watu wakiburunga yeye akiwabadilisha wizara . Kama tunahitaji dictator unamdanganya Man who wasungu na viumbe vyake kwa kuapa utailinda katiba? Hao unaowaongoz sio robots na wala hao wataokulinda sio robots. Angalia nini kinatokeA urundi, somalia na kwengineko kwenye madikteta.wisho wake ni mAngamizo
Na alaaniwe alaniye marehemu! . Badala ya appreciation kwa Baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere, wewe ndio unamuita hivyo?!. Wenzio tuko kwenye process ya kuutangaza Mwenye Heri, one step kabla hajatangazwa Mtakatifu! .

Mtakatifu mtarajiwa Julius Kambarage Nyerere, Muombee mdhambi Gavana asamehewe dhambi zake kwa maana hajui atendalo! .

Pasco
 
Back
Top Bottom