Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Mkuu umeandika GAZETI hata sijui ulikuwa unataka nini.....!
 

Pascongojaa historia iandikwe. AUE KWA MAMILIONI
 
Ben ccm ina vibaraka wake kwenye vyama vya upinzani kama Mrema, cheyo, Dovutwa and likes.

Hivi hakuna mabingwa wa mikakati huko kwenye UKAWA mkawa na chama chenu cha kimkakati kwa mfano labda UMD kiandae matembezi ya mshikamano kuunga mkono kauli ya Rais?

Kuna wakati inabidi kumtwisti tu mtu mpenda sifa then mwisho anajiona yeye ndio hana busara.

Kwa upeo wangu taasisi ikiomba kibali Polisi cha matembezi ya mshikamano kumuunga mkono Rais hakuna Polisi wa kuzuiya.

Nadhani ifike wakati akili za watu fulani uende nazo kama zilivyo then mwisho wa siku mjinga anajurikana.

Mfano mimi Matola na wenzangu leo tukitaka kuanzisha chama cha siasa msajili atatukatalia? Na kama atakubali tutaweza vipi kukijenga chama chetu kipya bila kuwafata wananchi na kuwaeleza sera zetu?

Nadhani sasa ni muda muhafaka wa kupractice Umkotho we Sizwe.
 

Dogo we andamana tu hiyo September 1 uone
 
Bado hawajawai kuonja moto wa jiwe

Watu wanao kuita dikteta ikiwa wewe siyo dikteta
Nibora uwape moto wa udikteta
Ili liwe findisho .

HAWA JK KAWALEA SANA

WALI MTUKANA SANA
WALI MZONGA SANA
WACHA WAKIONE.



"Nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao halafu wataona cha mtemakuni’"
 

Mbona mlisema mnaenda ICC kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Magufuli imefikia wapi?
 
Pasco bwana!
Sasa Chadema wakisikiliza Ushauri wako si kitakoma kuwa chama cha siasa, maana ground za kufanyia siasa zote zinapigwa libiti!
Ushauri wangu ni kwa Chadema kuachana na siasa za uanaharakati, the politics of confrontation, na badala yake wafanye real politics of development, Magufuli ni dikiteta mzalendo mwenye no sense ya busara zozote when it comes kwenye kumjaribu, Huyu ni mwenye nguvu akisema jambo fulani ni hapana na iwe hapana kweli hataki mchezo.

The right thing to do kwa Chadema ni kwenda mahakamani kuiomba mahakama kutoa tafsiri sahihi ya haki ya mikutano, freedom of lawful assembly, freedom of expression, na political activities hivyo kuonyesha tamko la rais ni batili na kinyume cha katiba na sheria lakini sio kumpinga rais kwa mikutano ya hadhara na matamko ya kutishana na kutunishiana misuli! .

Pasco
 
Dogo we andamana tu hiyo September 1 uone
Chadema wametangulia akili sana, ungejiuliza ni kwa nini mikutano imewekwa mwezi mmoja mbele?
Kuna mabingwa wa mikakati wanazijuwa akili zenu mtalipuka mapovu yote kabla hata tarehe waliotangaza Chadema haijafika Dunia nzima itakuwa inajuwa kwamba kuna tatizo Magogoni.

Mimi ningelikuwa Rais ningewaambia wapinzani anaetaka kuandamana hata kila siku ruksa tu na aandamane.
Hii ndio best medicine aliitumia Nyerere kwa Mrema, aliwaambia Polisi wamwache Mrema tena tu si kwa wanaosukuma gari lake bali wambembe kabisa.

Bado sielewi kama ccm mpaka leo kama wanakumbuka sawasawa misingi ya mwalimu ilikuwa ni ipi!
Ili kuweka kumbukumbu sawa, nchi hii mtu wa kwanza kushtakiwa kwa kosa la uchochezi ni Baba wa Taifa.
 

Asante kwa ufafanuzi wa kumsaidia huyo ndugu kuelewa
Yeye anafikiri Tanzania anayoingoza ni exceptional na iko ktk ulimwengu mwingine wa kwake!
He's wrong na wanaomshangalia kama majuha hawampendi asilani!!
Aaambiwe huyu asije akatuingiza ktk matatizo bureee
 
Sawa Ben,
You should also be careful what you wish for.
Kuna wengi ambao walikwisha andamana na kukesha na mabango hadi rais akasepa.
Faida iliyopatikana baada ya hapo ni kidogo sana.
Na matatizo yalizalishwa baada ya hapo ni makubwa na mabaya mara 1000 zaidi ya yule rais walieyemuandamania.
 
Nilitegemea uwashauri pia wachukue hatua gani ili dikteta aache udikteta kama andiko langu yenye ushauri. Dikteta hatazamwi tu na kusema shauri yake bali anazuiwa na wasiopenda huo udikteta. Udikteta ukikomaa madhara yake ni makubwa mno anaweza akamwita hata kampeni manaja wake akamchinja. Wenye ujasiri lazima wapambane ili kumdhibiti akaleta madhara makubwa na yeye kuendelea kujifunza kufuata katiba aliyotumia Kuapa kuwa atalinda. Kwa wale tuliowahi kuangalia vita ya Vietnam wanasema FOR OTHERS TO SURVIVE OTHERS MUST DIE. Pasco tumia taaluma yako kutoa maandiko mengi ya viongozi wetu kufuata katiba na kutii sheria kama wazee wetu walivyoasisi. CCM walipa kura zaidi ya million nane, Wapinzani wana kura zaidi ya million sita. Kuna kura zaidi million tisa hazijapiga kura hivyo bado kazi ni kubwa kushindana na wapinzani.
 
Mkuu Ben kiukweli mimi huwa nina wa admire watu mashujaa kama wewe wenye nia thabiti mioyoni mwao, kauli thabiti midomoni, mwao kama hizi kauli zako humu za one term lakini reality ni nyingine kabisa! .

Hili la one term hamalizi nililisikia kwa yule yule mhubiri ili tuu kuendelea kumdanganya 'jamaa yetu' kuwa ni yeye ndiye aliyeandikiwa, kiukweli hakuna kitu kama hicho na kwa kasi ya udikiteta ninavyoiona hata hiyo 2020 sijui kama tutahitaji uchaguzi wa rais na sisi wananchi tunaolitakia mema taifa hili tutaandamana nchi nzima ili kile kipengele cha ukomo wa two terms kiondolewe Magufuli aendelee tuu kama Nyerere mpaka achoke mwenyewe! .

Nimemuombea kwa Mungu na sio kwa mungu kwa sababu ni Mungu ndie aliyesema tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari na tumpe Mungu yaliyo ya Mungu.

Tembelea ule uzi wangu wa rais wa Tanzania ni yule tuu aliyepangwa na Mungu, maadam ni Magufuli, then ndiye aliyepangwa na Mungu, tuendelee kumuombea

Pasco
 


Mr Pasco, please hebu naomba nijuze kidogo, inawezekana mimi sielewi.

Hivi hizi "politics of development" ni zipi hizo na zinafanywaje mkubwa?

Na ukimaliza kueleza hebu dadavua na "politics of confrontation" ni zipi hizo na zinafanywaje eti?

Nimeona na kimsikia mkulu wetu mara nyingi naye akisema "watanzania wanataka siasa za maendeleo"... it is a little bit confuses me ninaposikia na kusoma vitu kama hivi!

It is either you and Mr president don't understand the meaning of politics in relationship with development or you purposely try to manipulate people with your own defenition of politics!

That's what I can comment about these fallaciuos statements from you guys!!

Namkumbuka sana Dr Wilbroad Peter Slaa katibu mkuu wa CHADEMA aliyepita aliyeongoza harakati kabambe wakati wa Kikwete hata kuiweka CHADEMA ktk chati ya juu na pengine kuifanya serikali iamke na kufanya kazi ya ziada ktk kutekeleza ahadi zake za kuwahudumia wananchi kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo japo kasoro za hapa na pale haziwezi kukosekana.

Tell me. CHADEMA ya wakati wa Dr Slaa ilikuwa inafanya siasa za namna gani kati ya hizo ulizozitaja.....development or confrontation politics.........or both?
 
Mkuu mahakama kibogoyo ndio hizi zilizo wapa ushindi wabunge wa chadema kwenye case zao za uchaguzi. Hakika umenichekesha....
 
ushauri hewa kwa cdm huu. chadema wakumbuke haki haiombwi bali hudaiwa....
Naunga mkono kwa asilimia 100 % chini ya 100% haki haiombwI au kuletewa kwenye kisahani cha chai bali haki hudaiwa, kupiganiwa na ikibidi hata kufia lakini sio kwa mikutano ya hadhara matamko na maandamano, mwenye nchi tuliyempa dhamana hataki hivyo msilazimishe, tumieni sheria, taratibu na kanuni rasmi za kudai haki ikiwemo kumshitaki rais lakini mshishindane na
mwenye nguvu mtaumia bure na hiyo haki inayopiganiwa isipatikane! .

Nawashauri waandishi wa Arusha wakazitembelee zile familia za wahanga wa yale maandamano ya Arusha kuona jinsi mashujaa wale wanavyoenziwa ndipo wajitokeze hiyo September 1. Mtu ukiishakijua kitakachokupata ukifanya jambo fulani na wewe ukafanya na hicho cha kukupata kikakupata, sisi tunasema umejitakia kwa vile ulijua.

Pasco
 
Hizo sababu ulizozisema ndio chadema isimame badala ya wananchi wakatae kabisa na wananchi tuwaunge mkono marufuku mtu mmoja kutumia vyombo vya dola kuvuruga amani ya nchi lazima asimamishwe sasa na sio wakakti mwingine wowote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…