dolevaby
JF-Expert Member
- Aug 25, 2013
- 12,958
- 9,516
Mkuu umeandika GAZETI hata sijui ulikuwa unataka nini.....!Unajua kwa tanzania elimu ya siasa na uraia kuna mapungufu sana........
Kiukweli wapinzani pamoja na serikali wote wanamaeneo wanakosea pia wanapatia.........
Nikianza na wapinzani........hawa mlengo wa hoja zao zimekaa kukosoa serikali sio kwa lengo la kuijenga bali kuiharibia ili nao wapate ridhaa ya wananchi katika kuliongoza taifa.....hili si jambo zuri hata kidogo.......huu ni usanii kabisa....
Nitawapa mfano wa inshu ya sukari.........wabunge wengi wa upinzani walichachamaa sana kwa kuwaambia wananchi kuwa serikali haiwatakii mema kwa kuzia uagizaji wa sukari usio fuata taratibu za kisheria za biashara katika manunuzi........nakumbuka walituhadaa wananchi kuwa sukari haitokuja kushuka maana serikali inakosea......leo hapa mimi nipo kilimanjaro nimetoka kununua sukari kilo 1800. Tokea ilipokuwa 3000. Sasa najiuliza huwa wapinzani wakiongea wanatumia taarifa za wapi.......maana ni kama wanapotosha uma.........mimi naona ni kama wanaweka jitihada nyingi kubeza jitihada zinazofanywa na kupotosha uma wa watanzania.......na asilimia kubwa ya watanzania si wafuatiliahi huwa wanajiridhisha na story za kusadikika ama za mtaani au post za facebook ambazo huwa wanaozipost hawajulikani ni akina nani plus wanamalengo gani.......
Swala la elimu......wanabeza sana maamuzi ya kuweka vigezo ambavyo vitarejesha thamani ya elimu sio kama sasa kila mtu anadegree uchwara halafu uwezo zero kazi kupiga domo tu.....wapinzani wanakazana kuropoka tu ili wapate hii popularity kama ya akina wema na diamond kwa kuropoka.......
Me nasema mh.raisi yupo sahihi kukataza hizi kelele zisizo na tija yeyote ........hawa wapinzani si muda wote.wapo sahihi......wanayohaki ya kuikanya......kuirekebisha na kuikosoa serikali.......ila sio kwa staili hii wanavyofanya ya kuibeza na kuikejeli badala ya kuishauri.............wapinzani hawaongei jipya kazi yao ni kubeza .Unapomkosoa mtu......toa suggestion ......au wazo mbadala ila sio unangojea mwenzako akosee ndipo povu likutoke........tena unatoa kauli za kuhatarisha amani na usalama wa raia........
serikali ni kweli inakosea kuwazuia wapinzani kuongea na uma lakini ni kwasababu wamegundua mnaitumia fursa hiyo kuongea vijembe.....na kukejeli serikali ndio maana wanawabana kwa kila namna .......hata ningekuwa mimi nisingeruhusu mtu ambaye hauna ridhaa ya kuendesha nchi uongee maneno ya uchochezi badala ya kutoa ushauri.......hii kitu alishaifanyaga mbatia mara moja tu......aliishauri serikali kuhusu kuhamisha maofisi yao maeneo ya posta na kuyasambaza maeneo mengine ili kupunguza msongamano wa foleni za magari asubuhi watu wanapokwenda makazini maana msongamano huu unaitia serikali hasara kila siku ya mabilioni......na ndio maana kikwete akamkubali sana akampa nafasi ubunge viti maalumu.........mrema huyo hapo amepewa nafasi anashirikiana na serikali......huo ndio upinzani wa ukweli unatakiwa kuwa sio hawa wakina zitto wanakwenda kusoma vitabu na notes za shule wanakuja kutuletea theory za utabiri hapa.....wanaboa sana......