Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!


Sawa. Maneno mengi ya nini? Tunasubiri tuone mkwara wenu hapo September 1.
 
Tehe tehe tehe umeamka na faida leo [emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]
 
Umeongea vizuri sana wote tungekuwa tunafikiria hivyo tungefika mbali.
 
Mkuu Pasco, kufa ni mara moja tu.
Ni kweli kufa ni mara moja tuu, ila sio mtu umeona moto halafu unakwenda kucheza na moto, ukiungua usilie! . Wafuasi wa Chadema sio watoto wa kuambiwa wacheze na wembe! , ushujaa ni kufa katika kupigania haki na kifo kikakukuta katika mapambano kama vitani lakini sio unakiona kifo kile kisha unakifuata mwenyewe kama walivyokufa Wafuasi wa Kibwetere au wale wa David Koresh wa Camp Davidians! .
Pasco
 

Nitasimama na kuitetea nchi yangu,siwezi kuona mtu mmoja akiangamiza nchi.
 
Pasco huyo mtu wako ni PAPER TIGER na ni mharibifu toka eneo la waharibifu Dikteta Uchwara
Mkuu Magelemwa, uchwara ni isiyo halisi yaani yule anayejifanyisha tuu kama walivyo the barking dogs seldom bite! , mbwa koko hubwekwa sana ila ukimkaribia kimya na kuufyata mkia! .

Magufuli sio dikiteta uchwala ni dikiteta halisi kwa maneno na matendo ,ila tofautI na madikiteta wengine huyu ni dikiteta mzalendo anayefanya udikiteta kwa nia njema na dhamira safi ya kulikomboa taifa hili kwa sababu demokrasia, uhuru uliopitiliza, haki na utawala wa sharia ndio vimetufikisha hapa. Anachofanya ni kutumia udikiteta kidogo kwa kuiweka kando kidogo katiba na kuinyoosha kwanza nchi, maana kiukweli nchi ilikuwa imepinda sana, serikali ilikuwa imewekwa mifukoni na mafisadi, nchi ikiisha nyooka na kukaa kwenye mstari sasa ndipo tutazungumzia demokrasia na haki za binaadamu.

Pasco
 
Mbowe aliwakataza Bavicha wasiende dodoma watatumia njia za kimahakama kudai haki zao. Sasa nini kimebadili msimamo wao na Lowasa aliyewashauri kuwa maandamano hayasaidii? Hivi hawa ndugu zetu wanajua wanasimamia nini?
Mkuu Mtazamo, kama hata baada ya yote yanayozungumzwa na bado kuna wafuasi watajitokeza, nitaamini kweli hawa jamaa ni nyumbu! .

Naunga mkono haki ya kuandamana na haki ya kukusanyika ila mkiisha katazwa na mamlaka husika, hakuna sababu za kutunishiana misuli na mwenye nguvu, mwenye nguvu mpishe!.

Pasco
 
Sheria iko wazi, kimsingi washauri wa raisi kama si kuwa wanamwogopa kuna jambo mkuu wetu haliko sawa. Kudhihilisha hilo hata msajili wa vyama vya siasa amekwepa vifungu vya sheria vinavyotoa haki za kidemokrasia kwa vyama vya siasa imelalia kipengele cha zuio bila kuweka bayana vipengele vyote vinavyotoa haki ya hayo maandamano na mikutano. Hii tafakari ya mhariri wa gazeti la mwananchi inatosha kutoa rejea kwa wanaopinga tamko la CHADEMA bila kuleta rejea za kisheria. Ukifuatilia michango ya wadau wa upande wa pili, hawana hoja ya msingi bali wanasimamia maneno ya raisi anayoendelea kutoa bila kuakisi ni wapi amekosea. #Kuna watu wanamwabudu rais hata kwenye makosa.
 
Pasco bana! UKUTA na wengine wote wanaomlalamikia Rais Magufuli wajaribu kukumbuka hali ya nchi ilivyokuwa. Kwa kweli inahitaji kuwa na kiongozi kama Magufuli kuweza kuirejesha nchi katika mstari. Magufuli ni msomi anayejua fika umuhimu wa Katiba. Je tunategemea aendelee kufuata mtindo wa uongozi ulioifikisha nchi hapo ilipokuwa kabla ya yeye kuingia madarakani? Ana miaka 5, mwacheni msaidieni!
 
THEN KWA KIFUPI PASCO HAKUNA HAJA YA VYAMA VINGI UNTIL 2020
 


Siyo kweli kwamba Raisi wa JMTZ ana Mamlaka sawa Spika au Jaji Mkuu huo ni upotoshaji mkubwa, Raisi wa JMTZ ndiyo kila kitu na hii ni kulingana na madaraka makubwa aliyo nayo Raisi wa JMTZ, kwani Raisi anaweza kuvunja Bunge muda wowote ule kama wakimzingua na hii ni Kikatiba kabisa ukija kwenye Mahakama raisi ndiyo anayetuea Majaji wote mpaka Jaji Mkuu hivyo indirectly ni kwamba ana nguvu juu yao whether unataka au hautaki kwa maana anayekuteua yuko juu yako hiyo ni common sense ya kawaida kabisa na kama hiyo haitoshi Raisi wa JMTZ ndiyo Mwenyekiti wa CCM Chama ambacho ndicho kilichotoa Spika na Naibu Spika na chenye Wabunge wengi klk vyote, hivyo kwa kuwa Spika ni Mbunge wa CCM ina maana Bosi wake ni Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Raisi wa JMTZ, hivyo basi ina maana Mwenyekiti wa CCM ana uwezo wa kusitisha Uanachama wa Mwanachama yoyote ikiwa pmj na Mbunge ambaye ndiye Spika wa Bunge la JMTZ, hivyo kwa kuzingatia hayo kusema kwamba Raisi kwa mujibu wa Katiba yetu ana madaraka sawa na Jaji Mkuu au Spika siyo kweli kwani,


Raisi wa JMTZ yuko juu ya Sheria ndani ya JMTZ!
 
Idd Amin dadaa alianzaga kidogo matamko,mbwembwe za ngoma,kutukana wapinzani wake na baadae akaanza kuua,kutesa na kula nyama za waganda.Watanzania tujenge UKUTA kabla mbo hayajawa magumu na uncontrollable
 
Lile BARAZA LA WAZEE LA CHAMA KILEEEEEE[emoji117],huwa linafanya kazi saa ngapi?wako macho?wanaona upepo mkali ukivuma?wanaona mwelekeo wa jahazi?kwakuwa sisi si wazoefu,tunatamani watuhakikishie safari.
 
Pasco wewe tayari tumesha kustukia kuwa unatumika sasa na watawala hivyo ushauri wako peleka huko huko kwenu lumumba
 
Mkuu Sophist, kwanza nimefarijika sana kwa mchango wako kwa sababu wewe ndio mtu wa kwanza kuchangia kuhusu the separation of powers tena kwa kupangua hoja kwa hoja japo you are not right but you've tried.

Lengo la the principal of the separation of powers and checks and balance ni ili kuuzuia mhimili mmoja usijiinue kupitiliza. Bunge ni mtunga sheria, mahakama mfasiri na serikali mtekelezaji, serikali inapotunga a draconian law na Bunge likaipitisha Mahakama inauwezo wa kuifutilia mbali. Serikali ikitenda kwa kukiuka, kutokutenda au kukandamiza, mahakama kupitia powers zake inatoa executive orders, au writs za prohibition, certiorary na mandamus kuiamuru serikali itake isitake! .

Kitendo cha the executive kuingilia freedom of movement kwa mhimili ya Bunge na Mahakama ni kuingilia the independence ya mihimili hii.

Haki ya vyama vya siasa kukutana na kufanya mikutano ni haki iliyomo kwenye katiba, haki hii sio territorial lakini rais ameingilia haki hii kinyume cha katiba kama ilivyo rais hana mamlaka yoyote ya kupunguza mshahara wa mtumishi yoyote.

Rais Magufuli ametoa kauli kibao za uvunjaji wa katiba Bunge na Mahakama vinaangalia tuu.

Pale kunapotokea kauli za uvunjaji wa katiba au kinyume cha haki za binaadamu kama zilivyoainishwa kwenye katiba, Mahakama ina mamlaka ya ku act kwa mtindo unaoitwa act on suo motto, ni acting on it's own volition na kutoa tafsiri ya katiba ili maandishi nini bila hata kumsubiri yoyote kufungua shauri.

Bunge linapoona rais anatenda ndiyo sivyo lina mamlaka kujadili kauli za rais na kuzitolea azimio la Bunge.

Lakini hebu tusemezane ukweli, Jaji Chande na Spika Ndungai na Naibu Dr. Tulia ni watu wa kutengemewa kumfanyia checks Magufuli huku wengine wamefanywa kubebwa na wengine ni wastaafu siku nyingi wanaendelea na kazi kwa hisani tuu ya Magufuli.

Tanzania tunafuata mfumo wa presidential ambao rais ndio kila kitu, Bunge ni Butu na Mahakama ni Kibogoyo haina meno ya kuingata serikali, ndio maana nawashauri Chadema Mkuu wa the executive akisema hiki usifanye, hata kama wewe ndio mwenye haki, usifanye kwa sababu kauli hiyo ni final na conclusive! . Japo katiba yetu inasisitiza no one's is above the law, rais wetu is over and above the law! . Yeye ndio katiba, ndio Bunge, ndio mahakama na ndiye the law kubali kataa. Mtu wa namna hii akisema hapana ni hapana.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…