Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Nadhani wengi humu hamjamuelewa Pasco, mimi nimemuelewa vizuri sana, inahitaji uwe ni mtu wa tafakuri ya kina ili kumuelewa Pasco.

Msiomuelewa Pasco iko hivi, IGP Omary Mahita, CDF Robert Mboma, Tiss DG Hans Kitine na Apson Mwang'onda na chief Judge Augustino Ramadhani hawa wote ni ccm na licha ya hizo nafasi kutokuwaruhusu kuwa kwenye siasa lakini waligombea.

Ila katika hao wote mwenye dhambi kuu ni Jaji/Padre Augustino Ramadhani ambaye ameinajisi mahakama kwa kitendo chake cha kukatwa jina tano bora na majina ya wahuni tu wengine yakapelekwa kupigiwa kura Nec.

Sina maneno mazuri ya kuwataka huyu mtu mumuelewe kivingine ila hata lugha ya picha hufikisha ujumbe pia.

1469891750858.jpg

1469891787317.jpg
1469891798814.jpg

Mapinduzi si lazima yawe ya kijeshi tu yapo ya kiraia pia tena kupitia sanduku la kura ili jumuiya za kimataifa zisikutenge.
 
Huyo unayesema ana nguvu una uhakika kwamba hizo nguvu anazo ? Hakuna binadamu aliyeumbwa kwa udongo mwenye nguvu ya kuwazidi wengine .
 
Great words....

Mm nilizani IPTL ingetaifishwa na serekali kama bunge lilivyo adhimia....

Mm nilizan waliochukuwa Mapesa ya escrow thru Stanbank kwa marumbesa wangekuwa Jela sasahivi...lakin wapi?
Mi nilidhani cdm mngetupa mzoga ili msifuatwe na nzi
 
Mkuu Gamba la Nyoka, atakachofanya Magufuli, ni kuwatumia the best of his snipers, wadunguaji wazuri, kwenye maandamano Kikwete alikuwa akishoot randomly ili kuogofya tuu, na waliokuwa wakiuwawa ni akina kaja.. nani!, kiukweli Magufuli, atawashikisha adabu kiukweli kweli haswa, kazi ya wadunguaji ni ku target vinara!, mkuu wa nchi hawezi kufikishwa the Hague kwa ku clear the mess ya kifo kimoja au viwili, na amini usiamini, wakiandamana tuu, watadunguliwa kwa risasi za moto, lakini taarifa ya polisi itasema walitumia rubber bullets, postmortem report itathibitisha hilo na mchezo, utakwisha.

Pasco
Unadanganya kushauri lakini kumbe umekuja kutisha ! Very poor !
 
Uko sahihi 100% mwenye nguvu mpishe, after all cdm ilishapoteza watu wengi, mawazo, mwangosi, arusha, morogoro, iringa, etc etc, na hakuna aliyewajibika, majority of people in remote rural areas of Tz conspicuously displayed big ignorance of an irresponsible country
 
Mkuu Magelemwa, uchwara ni isiyo halisi yaani yule anayejifanyisha tuu kama walivyo the barking dogs seldom bite! , mbwa koko hubwekwa sana ila ukimkaribia kimya na kuufyata mkia! .

Magufuli sio dikiteta uchwala ni dikiteta halisi kwa maneno na matendo ,ila tofautI na madikiteta wengine huyu ni dikiteta mzalendo anayefanya udikiteta kwa nia njema na dhamira safi ya kulikomboa taifa hili kwa sababu demokrasia, uhuru uliopitiliza, haki na utawala wa sharia ndio vimetufikisha hapa. Anachofanya ni kutumia udikiteta kidogo kwa kuiweka kando kidogo katiba na kuinyoosha kwanza nchi, maana kiukweli nchi ilikuwa imepinda sana, serikali ilikuwa imewekwa mifukoni na mafisadi, nchi ikiisha nyooka na kukaa kwenye mstari sasa ndipo tutazungumzia demokrasia na haki za binaadamu.

Pasco
Not Sustainable
 
Chadema walijichimbia kaburi July 2015. Sasa hivi wanajifukia wenyewe, mwaka mmoja baadae.

Miaka mitano baadae wataibuka kama wafu?
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kutoa ushauri wa bure, huu ni ushauri wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba, nawashauri kwa dhati kabisa, tafadhalini sana msiandamane, na kusitisha hiyo Operesheni UKUTA, ili kuutumia ule msemo wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, na sio tuu ana nguvu zaidi yako, na tayari, umeishajua ni dikiteta, bali ndio mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.

Misingi ya Katiba na The Rule of Law
Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya katiba na sheria, (the rule of law) ambapo inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na sio kwa matamko ya viongozi yanayokwenda kinyume cha katiba!.

The Separation of Powers & Check and Balance .
Nchi yetu ina mihimili mikuu mitatu, Serikali, (the executive), Bunge (The Legislature) na Mahakama (The Judiciary). Mihimili hii mitatu, ilipaswa kufanya kazi kwa kujitegemea bila mhimili mmoja kuingilia mhimili mwingine (independence), huki kila mhimili uki act as a watchdog wa muhimili mwingine usivuke mipaka ya madaraka au mamlaka yake yaani (The sepaation of powers check and balance).

Serikali yenye Nguvu, Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo!.
Mihimili hii, inaongozwa na viongozi ambao wana mamlaka kuu kuhusu mihimili yao. President ndio mkuu wa the executive, Spika ndio mkuu wa The Legistlatue, na Jaji Mkuu, ndie mkuu wa The Judiciary, lakini pamoja na nia njema kuwa mihimili yote inamamlaka na hakuna mhimili wowote uliokuwa unapaswa kuwa na mamlaka kuliko mhimili mwingine, lakini kiukweli, mhimili wa the executive ndio mhimili mkuu unaomiliki vyombo vya dola na kuitawala mihimili mingine yote!, hivyo mkuu wa the executive, yaani rais, ndio kila kitu!, akisema!, amesema!.

Rais Magufuli na Uvunjaji wa Katiba.
Tuambiane ukweli, tangu rais Magufuli ameingia madarakani, sio mara moja au mbili amekuwa akitoa kauli tata, zinazokwenda kinyume cha katiba, mhimili wa Bunge na Mahakama ilipaswa kuingilia kati kwa kumcheck mkuu wa the executive, lakini vyombo hivyo vimekaa kimya hivyo kumfanya rais ajisikie kuwa he is always right! kwa kanuni ya "the boss is always right!".

Udikiteta wa Magufuli.
Hoja kama Magufuli ni dikiteta au la, haina mjadala, Magufuli ni dikiteta wa ukweli ambaye hana msalie mtume, na alipoingia tuu madarakani, alianza kuonyesha udikiteta wake right away kwa kuliingilia bunge na mahakama kuziweka chini ya amri zake!. Lile katazo lake la watumishi wa umma hawaruhusiwi kusafiri safari za nje bila kibali chake kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, liliwahusu watumishi wote wa serikali, likiwemo bunge na mahakama!, just imagine Jaji Mkuu na Spika wa bunge wakapige magoti kwa rais kuomba kutimiza wajibu wao!.

Baada ya katazo lile, checks and balance zingepaswa kuanzia hapo kwa Jaji Mkuu kumweleza rais huko ni kuingilia uhuru wa mahakama (the independence of the judiciary) hivyo muhimili wa mahakama haukupaswa kujisubmit chini ya the executuve, bali mamlaka hayo ya kuzuia safari za nje, Spika alipaswa kuwa nayo kudhibiti safari za mhimili wa bunge, na Jaji Mkuu alipaswa kuwana nayo kudhibiti safari za mhimili wa mahakama, lakini mihimili hii ilikaa kimya kwa kujisubmit chini ya the executive, hivyo kumfanya rais ndio kila kitu!.

Hivyo sasa rais Magufuli ndio kila kitu, hakuna cha bunge, mahakama, wala katiba, amri ya rais ndio kila kitu na ndio sheria kuu!, hivyo nawashauri Chadema kwa dhati kabisa, wasitishe maandamano yao, wasifanye kabisa mchezo wa kumjaribu Ngosha, wataumia bure!.

Hili la udikiteta wa rais Magufuli, tumeisha lizungumza sana humu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa ...

Ila kitu kimoja kuzuri kuhusu udikiteta wa rais wetu, ni Rais Magufuli ni dikiteta mzalendo!, mwenye uchungu na umasikini wa nchi hii, mwenye nia njema ya kusafisha uozo wote wa uzembe, rushwa na ufisadi, na kulikomboa taifa letu toka kwenye lindi la umasikini uliotopea na kuwa nchi ya maziwa na asali kupitia uchumi wa gesi na viwanda.

Mungu mbariki Magufuli!.

Mungu ibariki Tanzania.

Wasalaam.

Pasco
Rejea za shauri za bure
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa ...
Ushauri wa Bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared for ...
Ushauri wa Bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako ...
Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep ...
Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)-Kwa Hili la ...
Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report: Please Keep Quite ...
Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Magufuli, Futilia Mbali Utawala wa Sheria ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Usikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
Ushauri wa Bure kwa Dr. Shein: Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ...
Ushauri wa Bure kwa Magufuli, DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...
Kimsingi hakuna dikiteta mzalendo, dikiteta ni dikiteta tu. Hivi dikiteta wa wapi umemsikia akisema yeye sio mzalendo?. Dalili ya kwanza ya udikiteta ni kuwaona wengine sio wazalendo.

Issue ya kusafisha uozo uliopo ndio kazi raisi aliyo-omba na wengi wanamuunga mkono.

Nisichokielewa ni yeye kutaka kufanya siasa za kitaifa peke yake. Waliwaita vyama vya upinzani vyama vya musimu (JK et al), sasa wanasema 2020. Sasa vyama vitajijenga vipi kama havifanyi siasa? Hili JK alilizungumzia juzi-Kinana alifanya hivyo kuipandisha chati CCM.

Sisi waoga tutajifungia na kusema nyuma ya key boards, wenye uwezo watasema mchana kweupe na walio na uthubutu watatenda. Tuki-surrender atakavyo PASCO hujui kipi kitafuata. Na hapa siongelei strategy ya CDM-ninachosema ni kuwa hii hali inahitaji concerted effort ili tuwe na siasa huru vinginevyo tuzike democrasia ya vyama ving turudi kule tulikotoka. Hawa jamaa wanataka tueleweke tuna demokrasia wakati hawapractice hiyo kitu.
 
Huu mchezo hauhitaji hasira!
Ili tuendelee tunahitaji siasa safi, ardhi, uongozi bora na ......... Mwl. Nyerere.
 
Ushauri umefika!!
Inabidi tujifunze juu ya mfuma wa uongozi wa nchi tulionao.Raisi ni mkuu wa nchi na mkuu wa serikali, yeye ni tofauti na wakuu wa mihimili mingine nchini.
Mwajiri mkuu wa watumishi wa umma ni Rais.
JPM amekuja na mpango wa kubana matumizi ya serikali- hata mahakama na bunge kwenye maumizi yanayofadhiliwa na serikali lazima wahusikie.
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kutoa ushauri wa bure, huu ni ushauri wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba, nawashauri kwa dhati kabisa, tafadhalini sana msiandamane, na kusitisha hiyo Operesheni UKUTA, ili kuutumia ule msemo wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, na sio tuu ana nguvu zaidi yako, na tayari, umeishajua ni dikiteta, bali ndio mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.

Misingi ya Katiba na The Rule of Law
Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya katiba na sheria, (the rule of law) ambapo inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na sio kwa matamko ya viongozi yanayokwenda kinyume cha katiba!.

The Separation of Powers & Check and Balance .
Nchi yetu ina mihimili mikuu mitatu, Serikali, (the executive), Bunge (The Legislature) na Mahakama (The Judiciary). Mihimili hii mitatu, ilipaswa kufanya kazi kwa kujitegemea bila mhimili mmoja kuingilia mhimili mwingine (independence), huki kila mhimili uki act as a watchdog wa muhimili mwingine usivuke mipaka ya madaraka au mamlaka yake yaani (The sepaation of powers check and balance).

Serikali yenye Nguvu, Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo!.
Mihimili hii, inaongozwa na viongozi ambao wana mamlaka kuu kuhusu mihimili yao. President ndio mkuu wa the executive, Spika ndio mkuu wa The Legistlatue, na Jaji Mkuu, ndie mkuu wa The Judiciary, lakini pamoja na nia njema kuwa mihimili yote inamamlaka na hakuna mhimili wowote uliokuwa unapaswa kuwa na mamlaka kuliko mhimili mwingine, lakini kiukweli, mhimili wa the executive ndio mhimili mkuu unaomiliki vyombo vya dola na kuitawala mihimili mingine yote!, hivyo mkuu wa the executive, yaani rais, ndio kila kitu!, akisema!, amesema!.

Rais Magufuli na Uvunjaji wa Katiba.
Tuambiane ukweli, tangu rais Magufuli ameingia madarakani, sio mara moja au mbili amekuwa akitoa kauli tata, zinazokwenda kinyume cha katiba, mhimili wa Bunge na Mahakama ilipaswa kuingilia kati kwa kumcheck mkuu wa the executive, lakini vyombo hivyo vimekaa kimya hivyo kumfanya rais ajisikie kuwa he is always right! kwa kanuni ya "the boss is always right!".

Udikiteta wa Magufuli.
Hoja kama Magufuli ni dikiteta au la, haina mjadala, Magufuli ni dikiteta wa ukweli ambaye hana msalie mtume, na alipoingia tuu madarakani, alianza kuonyesha udikiteta wake right away kwa kuliingilia bunge na mahakama kuziweka chini ya amri zake!. Lile katazo lake la watumishi wa umma hawaruhusiwi kusafiri safari za nje bila kibali chake kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, liliwahusu watumishi wote wa serikali, likiwemo bunge na mahakama!, just imagine Jaji Mkuu na Spika wa bunge wakapige magoti kwa rais kuomba kutimiza wajibu wao!.

Baada ya katazo lile, checks and balance zingepaswa kuanzia hapo kwa Jaji Mkuu kumweleza rais huko ni kuingilia uhuru wa mahakama (the independence of the judiciary) hivyo muhimili wa mahakama haukupaswa kujisubmit chini ya the executuve, bali mamlaka hayo ya kuzuia safari za nje, Spika alipaswa kuwa nayo kudhibiti safari za mhimili wa bunge, na Jaji Mkuu alipaswa kuwana nayo kudhibiti safari za mhimili wa mahakama, lakini mihimili hii ilikaa kimya kwa kujisubmit chini ya the executive, hivyo kumfanya rais ndio kila kitu!.

Hivyo sasa rais Magufuli ndio kila kitu, hakuna cha bunge, mahakama, wala katiba, amri ya rais ndio kila kitu na ndio sheria kuu!, hivyo nawashauri Chadema kwa dhati kabisa, wasitishe maandamano yao, wasifanye kabisa mchezo wa kumjaribu Ngosha, wataumia bure!.

Hili la udikiteta wa rais Magufuli, tumeisha lizungumza sana humu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa ...

Ila kitu kimoja kuzuri kuhusu udikiteta wa rais wetu, ni Rais Magufuli ni dikiteta mzalendo!, mwenye uchungu na umasikini wa nchi hii, mwenye nia njema ya kusafisha uozo wote wa uzembe, rushwa na ufisadi, na kulikomboa taifa letu toka kwenye lindi la umasikini uliotopea na kuwa nchi ya maziwa na asali kupitia uchumi wa gesi na viwanda.

Mungu mbariki Magufuli!.

Mungu ibariki Tanzania.

Wasalaam.

Pasco
Rejea za shauri za bure
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa ...
Ushauri wa Bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared for ...
Ushauri wa Bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako ...
Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep ...
Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)-Kwa Hili la ...
Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report: Please Keep Quite ...
Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Magufuli, Futilia Mbali Utawala wa Sheria ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Usikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
Ushauri wa Bure kwa Dr. Shein: Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ...
Ushauri wa Bure kwa Magufuli, DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...
granted Pasco.

kwa hiyo wapinzani waendelee kusubiri kushushiwa "mana toka mbinguni", siyo?
 
Back
Top Bottom