Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Siku hao wazee wakifikiwa wataanza nawao kitoa matamko kama kwa maveterani wa Mugabe.Udikteta sio mchezo tutalia machozi ya damu.

QUOTE="king's lawyer, post: 17026535, member: 287834"]Lile BARAZA LA WAZEE LA CHAMA KILEEEEEE[emoji117],huwa linafanya kazi saa ngapi?wako macho?wanaona upepo mkali ukivuma?wanaona mwelekeo wa jahazi?kwakuwa sisi si wazoefu,tunatamani watuhakikishie safari.[/QUOTE]
 
"Hakuna dhambi mbaya kama uoga" Godbless Lema

Acha tuandamane tutapambana barabarani na polisi.

Makamanda tujiandae kuingia barabarani nawaomba Mbowe na Lowassa pamoja na Sumaye tuwe pamoja kwenye maandamano.
Wacha kujifanya kutabiri jua wakati wa kiangazi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hapo kwenye rangi pataanza kupata umaarufu mkubwa nchini kama hali nchini itaendelea kuelekea siko. Tusikubali kukaa kimya huku tukiona nchi inapelekwa gizani na huyu dikteta na vitisho dhidi ya raia, viongozi wa upinzani kila kukicha na kutoheshimu katiba ya nchi.

Kwahiyo unatushauri tuwe kama Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo ili ajiskie always Right.

Huyo Mungu uliemuomba ambariki huyo mvunja katiba ungeanza kwa herufi ndogo jina lake isomeke 'mungu' na sio "Mungu"


Tena tuliosema atakua one term president tulikosea hata term moja hatamaliza kama tutashikilia msimamo wetu Septemba mosi na tunaweza kuigeuza ajenda ikawa ya kumng'oa ikulu.

He should be careful of what he wish for!
 
Kwani Katiba inasemaje.Katiba haisemi ni lazima amalize miaka 5. Hata maandamano yanaweza kumng'oa kupitia shinikizo kwa bunge .Nashangaa kuna watu wanatoa povu hapa
 
Kwani Katiba inasemaje.Katiba haisemi ni lazima amalize miaka 5. Hata maandamano yanaweza kumng'oa kupitia shinikizo kwa bunge .Nashangaa kuna watu wanatoa povu hapa
Kumbe lengo lenu ni kumng, oa Rais wetu.. Hakika tunasubiri hiyo tarehe 1
 
Pasco alikuwa ni wa miaka hiyo lkn huyu wa sasa ni Pasco karatasi
Pasco wewe tayari tumesha kustukia kuwa unatumika sasa na watawala hivyo ushauri wako peleka huko huko kwenu lumumba
Mkuu Mmawia, Pasco ni yule yule wa juzi, jana na leo kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Mimi sina kabisa chama, sio mshabiki wala mfuasi ila ni mzalendo na siku zote Natanguliza uzalendo wangu kwa taifa langu! .

Fuatilia threads humu jf uangalie ni mwana jf gani amekomalia udikiteta wa Magufuli kama Pasco wa JF, hivyo kitendo cha kuniita mimi ni wa Lumumba ni kama kunitukana, hata hivyo I'm coming up of an age na the most favourite past time ya retirees ni politics hivyo msishangae mwakani wakati wa mikutano Mkuu wa CCCM nami nikajiunge nikajilie pensheni nono huko kuliko kuendelea kufa njaa huku juani nilipo sasa kwa sababu kujiunga chama chochote sio dhambi.

Pasco
 
Mkuu Mmawia, Pasco ni yule yule wa juzi, jana na leo kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Mimi sina kabisa chama, sio mshabiki wala mfuasi ila ni mzalendo na siku zote Natanguliza uzalendo wangu kwa taifa langu! .

Fuatilia threads humu jf uangalie ni mwana jf gani amekomalia udikiteta wa Magufuli kama Pasco wa JF, hivyo kitendo cha kuniita mimi ni wa Lumumba ni kama kunitukana, hata hivyo I'm coming up of an age na the most favourite past time ya retirees ni politics hivyo msishangae mwakani wakati wa mikutano Mkuu wa CCCM nami nikajiunge nikajilie pensheni nono huko kuliko kuendelea kufa njaa huku juani nilipo sasa kwa sababu kujiunga chama chochote sio dhambi.

Pasco
Mkuu kawadanganye wasiyo kufahamu au inaelekea wewe ndiye hunijui kwa sababu ya hii ID yangu lkn ni watu tulio wahi kufanya kazi kwa pamoja
 
Hakuna habari ya mwenye nguvu mpishe ingelikuwa hivyo wazee wetu na mwl nyerere wasingetuletea uhuru maana mkoloni mwingereza alikuwa na kila kitu.Kikubwa tunatumia HAKI YA MNYONGE HIARI YA MWENYE NGUVU,hapa ni kutumia maneno kama silaha na ushindi utakao patikana ni ushindi wa nguvu za maneno ndo maana ya kufanya mikutano,lazima kuhakikisha kuwa nguvu ya maneno zinafaulu kupenya ktk masikio yanayotambua na kukiri madai ya maneno hayo wala hajaribiwi mtu,pale mtu mwenye nguvu anapo mpuuza mnyonge.je huyu atafanya nn?
 
Binafsi nitaandamana bila kumuogopa mpuuzi yeyote.. nitakuwa mstali wa mbele.. kama wananiua kama mwangosi na kamanda mawazo waniue..
lakini nikitoka bila kufa nao wajiandae kuuwawa
 
Pasco bana! UKUTA na wengine wote wanaomlalamikia Rais Magufuli wajaribu kukumbuka hali ya nchi ilivyokuwa. Kwa kweli inahitaji kuwa na kiongozi kama Magufuli kuweza kuirejesha nchi katika mstari. Magufuli ni msomi anayejua fika umuhimu wa Katiba. Je tunategemea aendelee kufuata mtindo wa uongozi ulioifikisha nchi hapo ilipokuwa kabla ya yeye kuingia madarakani? Ana miaka 5, mwacheni msaidieni!
Hivi mnafanya makusudi au ni ukweli upeo wenu ndio umeishia hapo?

Mimi namuunga mkono Rais kwenye vita dhidi ya ufisadi, uzembe kwenye ofisi za umma na kurudisha uwajibikaji.

Ila nitampinga kwa nguvu zote kuingilia haki za raia kujumuika hili halikubaliki hata chembe, hakuna mtu yeyote aliyemzuia Rais asifanye kazi yake.

Otherwise labda unishawishi upya kwamba ilani ya ccm ilisema wakishinda urais watapiga marufuku shughuli za kisiasa.
 
Ushauri wangu ni kwa Chadema kuachana na siasa za uanaharakati, the politics of confrontation, na badala yake wafanye real politics of development, Magufuli ni dikiteta mzalendo mwenye no sense ya busara zozote when it comes kwenye kumjaribu, Huyu ni mwenye nguvu akisema jambo fulani ni hapana na iwe hapana kweli hataki mchezo.

The right thing to do kwa Chadema ni kwenda mahakamani kuiomba mahakama kutoa tafsiri sahihi ya haki ya mikutano, freedom of lawful assembly, freedom of expression, na political activities hivyo kuonyesha tamko la rais ni batili na kinyume cha katiba na sheria lakini sio kumpinga rais kwa mikutano ya hadhara na matamko ya kutishana na kutunishiana misuli! .

Pasco
Hiiiiii hapa iko poaaa zaidi
 
Tanzania itaendelea kuwa maskini hivi hivi kwa sababu ina watu wengi waoga! Mfikilie Mandela, J. K. Nyerere, Nkurumah na wengine wengi. Wangeogopa kusimamia hoja zao kwa kuwaogopa waliokuwa na dola, ingekuwaje!?
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kutoa ushauri wa bure, huu ni ushauri wa bure kwa Chadema, japo kuandamana na mikutano ya kisiasa ni haki iliyotolewa kihalali ndani ya katiba, nawashauri kwa dhati kabisa, tafadhalini sana msiandamane, na kusitisha hiyo Operesheni UKUTA, ili kuutumia ule msemo wa Kiswahili "Mwenye nguvu mpishe", hata kama una haki, usitake kujipima nguvu kwa kutunishiana misuli na mtu mwenye nguvu zaidi yako, na sio tuu ana nguvu zaidi yako, na tayari, umeishajua ni dikiteta, bali ndio mwenye nguvu ya dola mikononi mwake!.

Misingi ya Katiba na The Rule of Law
Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya katiba na sheria, (the rule of law) ambapo inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, na sio kwa matamko ya viongozi yanayokwenda kinyume cha katiba!.

The Separation of Powers & Check and Balance .
Nchi yetu ina mihimili mikuu mitatu, Serikali, (the executive), Bunge (The Legislature) na Mahakama (The Judiciary). Mihimili hii mitatu, ilipaswa kufanya kazi kwa kujitegemea bila mhimili mmoja kuingilia mhimili mwingine (independence), huki kila mhimili uki act as a watchdog wa muhimili mwingine usivuke mipaka ya madaraka au mamlaka yake yaani (The sepaation of powers check and balance).

Serikali yenye Nguvu, Bunge Butu na Mahakama Kibogoyo!.
Mihimili hii, inaongozwa na viongozi ambao wana mamlaka kuu kuhusu mihimili yao. President ndio mkuu wa the executive, Spika ndio mkuu wa The Legistlatue, na Jaji Mkuu, ndie mkuu wa The Judiciary, lakini pamoja na nia njema kuwa mihimili yote inamamlaka na hakuna mhimili wowote uliokuwa unapaswa kuwa na mamlaka kuliko mhimili mwingine, lakini kiukweli, mhimili wa the executive ndio mhimili mkuu unaomiliki vyombo vya dola na kuitawala mihimili mingine yote!, hivyo mkuu wa the executive, yaani rais, ndio kila kitu!, akisema!, amesema!.

Rais Magufuli na Uvunjaji wa Katiba.
Tuambiane ukweli, tangu rais Magufuli ameingia madarakani, sio mara moja au mbili amekuwa akitoa kauli tata, zinazokwenda kinyume cha katiba, mhimili wa Bunge na Mahakama ilipaswa kuingilia kati kwa kumcheck mkuu wa the executive, lakini vyombo hivyo vimekaa kimya hivyo kumfanya rais ajisikie kuwa he is always right! kwa kanuni ya "the boss is always right!".

Udikiteta wa Magufuli.
Hoja kama Magufuli ni dikiteta au la, haina mjadala, Magufuli ni dikiteta wa ukweli ambaye hana msalie mtume, na alipoingia tuu madarakani, alianza kuonyesha udikiteta wake right away kwa kuliingilia bunge na mahakama kuziweka chini ya amri zake!. Lile katazo lake la watumishi wa umma hawaruhusiwi kusafiri safari za nje bila kibali chake kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, liliwahusu watumishi wote wa serikali, likiwemo bunge na mahakama!, just imagine Jaji Mkuu na Spika wa bunge wakapige magoti kwa rais kuomba kutimiza wajibu wao!.

Baada ya katazo lile, checks and balance zingepaswa kuanzia hapo kwa Jaji Mkuu kumweleza rais huko ni kuingilia uhuru wa mahakama (the independence of the judiciary) hivyo muhimili wa mahakama haukupaswa kujisubmit chini ya the executuve, bali mamlaka hayo ya kuzuia safari za nje, Spika alipaswa kuwa nayo kudhibiti safari za mhimili wa bunge, na Jaji Mkuu alipaswa kuwana nayo kudhibiti safari za mhimili wa mahakama, lakini mihimili hii ilikaa kimya kwa kujisubmit chini ya the executive, hivyo kumfanya rais ndio kila kitu!.

Hivyo sasa rais Magufuli ndio kila kitu, hakuna cha bunge, mahakama, wala katiba, amri ya rais ndio kila kitu na ndio sheria kuu!, hivyo nawashauri Chadema kwa dhati kabisa, wasitishe maandamano yao, wasifanye kabisa mchezo wa kumjaribu Ngosha, wataumia bure!.

Hili la udikiteta wa rais Magufuli, tumeisha lizungumza sana humu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa ...

Ila kitu kimoja kuzuri kuhusu udikiteta wa rais wetu, ni Rais Magufuli ni dikiteta mzalendo!, mwenye uchungu na umasikini wa nchi hii, mwenye nia njema ya kusafisha uozo wote wa uzembe, rushwa na ufisadi, na kulikomboa taifa letu toka kwenye lindi la umasikini uliotopea na kuwa nchi ya maziwa na asali kupitia uchumi wa gesi na viwanda.

Mungu mbariki Magufuli!.

Mungu ibariki Tanzania.

Wasalaam.

Pasco
Rejea za shauri za bure
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa ...
Ushauri wa Bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared for ...
Ushauri wa Bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako ...
Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep ...
Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb)-Kwa Hili la ...
Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report: Please Keep Quite ...
Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Magufuli, Futilia Mbali Utawala wa Sheria ...
Ushauri wa Bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya ...
Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Usikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!.
Ushauri wa Bure kwa Dr. Shein: Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ...
Ushauri wa Bure kwa Magufuli, DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...
masikini wee muda wa mdanganyika umepotea bure
 
Naisikitikia serikali kwa kujiingiza katika confrontation zisizo za lazima, kwa sababu katiba na sheria za nchi zinaruhusu mikutano ya kisiasa ya chama chochote chenye usajili nchini kufanya mikutano ktk mikoa yote ya nchi!. Hili liko wazi na wala siyo hisani ya mtu yoyote kuguarantee haki hii

Sheria haijasema walioshinda peke yake ndo wafanye mikutano katika majimbo yao.

Kwa jinsi ninavyoona, iwapo Watu wataandamana na ikatokea nguvu kutumika hadi kupoteza maisha ya wananchi, basi kuna hatari watu kupelekwa katika vyombo vya kimataifa kama the Hague kujibu mashtaka, kwa maana wananchi hao wanadai kilicho haki kwa mujibu wa sheria za vyama vya siasa kuhusu haki ya kufanya mikutano!
Mkuu Gamba la Nyoka, atakachofanya Magufuli, ni kuwatumia the best of his snipers, wadunguaji wazuri, kwenye maandamano Kikwete alikuwa akishoot randomly ili kuogofya tuu, na waliokuwa wakiuwawa ni akina kaja.. nani!, kiukweli Magufuli, atawashikisha adabu kiukweli kweli haswa, kazi ya wadunguaji ni ku target vinara!, mkuu wa nchi hawezi kufikishwa the Hague kwa ku clear the mess ya kifo kimoja au viwili, na amini usiamini, wakiandamana tuu, watadunguliwa kwa risasi za moto, lakini taarifa ya polisi itasema walitumia rubber bullets, postmortem report itathibitisha hilo na mchezo, utakwisha.

Pasco
 
Back
Top Bottom