Mkuu Sophist, kwanza nimefarijika sana kwa mchango wako kwa sababu wewe ndio mtu wa kwanza kuchangia kuhusu the separation of powers tena kwa kupangua hoja kwa hoja japo you are not right but you've tried.
Lengo la the principal of the separation of powers and checks and balance ni ili kuuzuia mhimili mmoja usijiinue kupitiliza. Bunge ni mtunga sheria, mahakama mfasiri na serikali mtekelezaji, serikali inapotunga a draconian law na Bunge likaipitisha Mahakama inauwezo wa kuifutilia mbali. Serikali ikitenda kwa kukiuka, kutokutenda au kukandamiza, mahakama kupitia powers zake inatoa executive orders, au writs za prohibition, certiorary na mandamus kuiamuru serikali itake isitake! .
Kitendo cha the executive kuingilia freedom of movement kwa mhimili ya Bunge na Mahakama ni kuingilia the independence ya mihimili hii.
Haki ya vyama vya siasa kukutana na kufanya mikutano ni haki iliyomo kwenye katiba, haki hii sio territorial lakini rais ameingilia haki hii kinyume cha katiba kama ilivyo rais hana mamlaka yoyote ya kupunguza mshahara wa mtumishi yoyote.
Rais Magufuli ametoa kauli kibao za uvunjaji wa katiba Bunge na Mahakama vinaangalia tuu.
Pale kunapotokea kauli za uvunjaji wa katiba au kinyume cha haki za binaadamu kama zilivyoainishwa kwenye katiba, Mahakama ina mamlaka ya ku act kwa mtindo unaoitwa act on suo motto, ni acting on it's own volition na kutoa tafsiri ya katiba ili maandishi nini bila hata kumsubiri yoyote kufungua shauri.
Bunge linapoona rais anatenda ndiyo sivyo lina mamlaka kujadili kauli za rais na kuzitolea azimio la Bunge.
Lakini hebu tusemezane ukweli, Jaji Chande na Spika Ndungai na Naibu Dr. Tulia ni watu wa kutengemewa kumfanyia checks Magufuli huku wengine wamefanywa kubebwa na wengine ni wastaafu siku nyingi wanaendelea na kazi kwa hisani tuu ya Magufuli.
Tanzania tunafuata mfumo wa presidential ambao rais ndio kila kitu, Bunge ni Butu na Mahakama ni Kibogoyo haina meno ya kuingata serikali, ndio maana nawashauri Chadema Mkuu wa the executive akisema hiki usifanye, hata kama wewe ndio mwenye haki, usifanye kwa sababu kauli hiyo ni final na conclusive! . Japo katiba yetu inasisitiza no one's is above the law, rais wetu is over and above the law! . Yeye ndio katiba, ndio Bunge, ndio mahakama na ndiye the law kubali kataa. Mtu wa namna hii akisema hapana ni hapana.
Pasco