LOoo, mkuu 'aloycious',
Unawakumbusha shuka wakati kumekucha tayari?
Wakati huu ndio wawaendee wananchi kwa kazi waliyotakiwa kuifanya kwa uendelevu miaka mitano iliyopita?.
Ninakubaliana na baadhi ya uliyowashauri, lakini hata wewe mwenyewe umechelewa kutoa ushauri waufanyie kazi kungali mapema.
Nadhani kuna sababu wasizotaka kuzieleza CHADEMA kuhusu sera zao, maanake ni nadra sana kusikia viongozi wakizungumzia mambo yanayosimamiwa na chama chao ili wananchi wayaelewe.
Haya mambo siyo ya kusubiri kuyaelezea wakati wa kampeni peke yake. Wakati wa kampeni ni kutoa ufafanuzi sehemu zinazohitaji kufafanuliwa, au zinazopindishwa na wapinzani wao.
Safari hii Magufuli katika miaka yake mitano hii amekwishawatengenezea ajenda nzito mno za kuwapelekea wananchi.
Wakishindwa kuzieleza kwa wananchi wajilaumu tu wao wenyewe kwa kukosa uwezo wa kuzijengea hoja.
Kwa mfano: Ni mwananchi gani asiyeweza kusimama na kusikiliza maelezo ya umhimu wa utawala bora kwa nchi yetu!
Ni mwananchi yupi asiyependa haki zake zilindwe, kama haki ya kupiga kura na kuchagua viongozi anaotaka yeye bila ya kuwa na shaka ya kura yake kuharibiwa au kutohesabiwa kabisa.
Ni mwananchi gani asiyetaka kupata na kutoa habari bila ya hofu ya kudhaniwa kuwa anavunja sheria.
Ni mwananchi gani asiyependa kuona wawakilishi wake bungeni wakifanya kazi kwa niaba yake bila ya kuingiliwa na/au kufichwa kinachotakiwa kuonekana kinafanyika wakati akifanya kazi hiyo.
Umoja wetu wa kitaifa na mshikamano wetu haujawahi kutetereka kama ulivyofikia wakati wa miaka hii mitano. Wewe unadhani wapinzani wakilieleza hili kwa wananchi, bado wananchi watakuwa hawaelewi kitu?
Ajenda kazitengeneza nyingi mno Magufuli, kiasi kwamba itawawia vigumu wapinzani wachague zipi za kuwaeleza wananchi katika muda mfupi wa kampeni.
Kwa maoni yangu 'agenda' ulizopendekeza ni nzuri sana lakini si mtaji kwa siasa za Africa hasa Tanzania, si kipaumbele cha watanzania wengi wanaopiga kura.
Suala ambalo linaweza kuwa mtaji mkubwa kwa wapinzani ni suala la ajira, mfumo wa biashara ya mazao kama ufuta, korosho, pamba na pamoja na mfumo wa bidhaa za wanyama kama ngozi,n.k.
Suala la serikali kuhusu namna inavyo shughulika na sera ya viwanda kwa kulazimisha vitu haraka kisha kuleta shida ya mfumuko wa bei kwenye bidhaa kama sukari.
Namna serikali ilivyoingilia biashara ya mazao na uagizaji sukari toka nje ya nchi imesababisha shida kubwa sana kwenye masoko na bei ya hizo bidhaa.
Hapa masuala ya kibiashara yameshughulikiwa kisiasa kitu ambacho si sahihi na mara nyingi hakuna matokeo chanya.
Mfumo wa masoko, wa kibiashara sio kama kuhamia Dodoma ambako unaweza kubadili mambo kwa amri kwa haraka.
Biashara inahitaji utulivu, maafikiano, utayari wa pande zote sababu ni suala la kiushindani. Mahitaji (demands) ndiyo huamua utaratibu sahihi kwa muda husika. Ukitaka kubadili huo utaratibu basi lazima kuwe na mabadiliko ya taratibu ya hatua kwa hatua (a gradual change).
You can't just wake up one morning and issue a decree (order) which instructs how to conduct business in a new norm.
Your decree can work within your borders and not otherwise. Na ndiyo maana ili uweze kufanikiwa kusikilizwa, kuheshimiwa na kutimizwa baadhi ya matakwa yako na wafanyabiashara wa nje inabidi kuwe na mikataba ya kibiashara na wadau wa nje au na nchi zao.
Hizo hoja za uhuru wa utoaji habari, demokrasia na kurusha shughuli za bunge mubashara hazigusi sana hisia na maisha ya wapiga kura wengi wa huko mikoani hasa vijijini, au huku mijini kwa watu wazima ambao wengi ndiyo wapiga kura watiifu .
Unafikiri mwanakijiji na mzee wa mjini ambaye si mwandishi au mwanasiasa anaona umuhimu wa kusambaza habari mitandaoni au kwenye magazeti au redioni?
Tuachane na siasa za kukariri ajenda za nchi zilizo endelea, wao wamesha endelea hivyo hawashughuliki sana na shida tunazosumbuka nazo sisi nchi maskini. Tunashirikiana tatizo moja tu la ajira lakini hayo mengine kwetu siyo kipaumbele chetu watanzania ambao bado tunapigania uhakika wa matibabu , mavazi na chakula.