Watu humu naona wanajadili bila kuelewa jinsi mfumo wa hisa unavyofanya kazi.
Wengine naona wanadai kuwa ukiwa na hisa nyingi ndio unakuwa na nguvu ya kufanya maamuzi(sio siku zote iko hivyo)
Kampuni inayomilikiwa kwa mfumo wa hisa huwa inakuwa na bodi ya directors ambao ndio wanahisa.
Kitendo cha kumiliki hisa nyingi ama kuwa mwanzilishi haimanishi kuwa ndio utakuwa unaingilia utendaji wa kampuni moja kwa moja.
Kwa sababu wanahisa huajili CEO ambaye ndio atashughulika na utendaji wa manbo yote ya kampuni.
Mnaweza pitia hapa
historia ya kampun ya apple inc jinsi
steve jobs alivyopoteza nguvu kwa kampuni aliyoianzisha na kisha kujiuzulu.
Wanahisa watampa malengo wanayoyataka ya kampuni hivyo CEO atajua mwenyewe jinsi ya kufanya.
Kwa mujibu wa page ya instagram ya
diamondplutnumz inaonyesha kuwa diamond ndio CEO na MD wa wasafitv na radio.
Maana yake wanahisa wamemchagua yeye kwenye hilo jukumu hivyo operations zote za tv na radio yeye ndio anasimamia na sio mtu mwenye hisa nyingi.
Lakini wanahisa wanaweza wakamuondoa kwenye hiyo nafasi iwapo malengo hayajafikiwa ila hisa ataendelea kuwa nazo.
Nguvu ya maamuzi inategemea na kiasi cha hisa ambacho wanabodi wamelewana.
Inaweza ikawa kwa mfumo wa kula kwa kuangalia watu gani wana hisa nyingi.
Au inaweza ikawa mtu mwenye 55% ya hisa ndio mfanya maamuzi yaani final say.
Ila bado diamond ni mmiliki pia wa wasafi kwa 45% japokuwa huyu mwenye 53% nafasi ya ku-control ni kubwa ila tu jinsi wanahisa walivyoelewana kwenye hilo swala.