Ushauri kwa Diamond: Unatia aibu, achana na Makonda anakuharibia sana

Ushauri kwa Diamond: Unatia aibu, achana na Makonda anakuharibia sana

Msimchagulie Diamond marafiki ni haki yake kuwana marafiki anaowapenda vyeti vya makonda vinamahusiano gani na urafiki wao...ina maana Makonda awe na.maadui tuuu.achaneni na fikira za kitoto.
Msanii ni kioo cha jamii!!! Kuwa na uswahiba na mtu anayeshukiwa kuwa na tuhuma kibao unageuka kuwa Mchafuzi wa jamii!!!
 
Diamond amekosa shule..!! Hata wanaomvunguka hawajielewi sana
 
Brother acha chuki binafsi suala mnalo lishadàdia ni kosa la jinai na siku zote makosa ya jinai mlalamikaji ni Jamuhuri muacheni jamuhuri aamue kama ataana kuna ushahidi atachukua hatua lakini siyo kwa shinikizo eti kwasababu kazuia madawa ya kulevya kawabana wabadhilifu nk kesi za jinai hazihitaji ushabiki na chuki kama mnavyo jichukulia sheria mikononi kwa kuwaua watu wasio na hatia kwa kisingizio cha mob justice!
 
Nimetokea kukuchukia sana sister coco ingawa sikufahamu kutokana na uandishi wako wa kujipendekeza badilika swaiba .
 
Hahaha
Aiwezekani, diamond anatembelewa na mawaziri kwake,iweje ashangae call ya rais!!
Watamfilisi mtoto wa watu.

Kwa yeye ni kitu kidogo lakini kwa mashabiki ni kikubwa hasa ukizingatia amewasemea wasanii wenzake.
 
Watanzania sijui tutapona lini, huku JF nako tunajiita GT lakini mambo tunayoshabikia hayaendani na sifa yenyewe.

GT kwa kipi hasa??.

Jaribu kuwa msomaji wa mada na maoni ya watu humu JF kwa wiki nzima bila kuchangia chochote, utapata majibu kwanini nasema hivi..

Bwana GT kwani hili jukwaa linaitwaje?
 
Diamond umehangaika kujenga brand yako sana.kitendo ulichofanya juzi kutokea kwenye sherehe ya makonda ya kutimiza mwaka mmoja wa Makonda umejishusha sana. Makonda ni mchafu sana kwa aliyoyafanya. Usidhani anapingwa na chadema tu..hata sisi CCM tunataka aondolewe.

Diamond umekosa nn? Unamashabiki wengi sana..!! Usipende kujihusisha na chama hasa na watu km makonda ambao wameshafuka. Unamashabiki wengi sana waliopo ccm, ukawa, na wasio na vyama. Acha kujipendekeza kijana jiamini..!! Makonda anakuzidi nini cha ziada..!! Makonda hakufikii kwa chochote. Makonda ni liability kwako ..not asset km unavyodhani.

Makonda acha kutumia mgongo wa wasanii kujisaficha hauwezi ukawa msafi tena. Kwanza umedanganya umma kuhusu jina lako, unatumia Cheti siyo chako. Chama kinapitia wakati mgumu kwa sababu yako. Umemfanya Rais anaonekana ana double standard kisa wewe.

Suala siyo ziro..suala ni kitumia Cheti cha MTU.

Diamond achana na makonda na mambo ya vyama. Makonda huyu ambaye akifika hata marekani anapiga picha..ushamba mzigo..!! Diomomd wewe siyo tid, wewe siyo yule mzee kijana mtoto wa malechela ambaye hajielewi.

Diamond kuwa mjanja basi. makonda anakutia aibu. Punguza kujifanya wewe ccm..wewe siyo ccm ..wenye ccm hawana makeke hivyo, wametulia kimya..!! Watakutumia tu. Hata juma nature na marlaw walikuwa ccm. Wewe ni asset..

Diamond unakuwa km bashite na wewe.
Ngoja na Mimi nimwambie shoga yangu mke wa Makonda aachane na Makonda. Anayeishi naye ni Bashite siyo Makonda. Paul Christian M. ni muhaya wakati yeye anabeba dushe la Msukuma Daudi Albert Bashite.
 
Usingemtaja huyo sijui.



Diamond kwa kweli pale ali kera kweli, hivi zile akili alizo zionesha kwenye kuizima bifu yake na Kiba zilimfanya aonekane ana maana, halafu akaja kuharibu kabisaaaa kwa kuonekana na Bashite.
Kwanza yeye ina muongezeaa nini aki kaa jirani na Bashite?, angekaa home ingempungua nini?, hajui kuwa RC alikuwa ana mtumia kwa aijili tu ya kutaka vijisifa vyake mwenyewe.
Namkubali sana Domo ila kwa Bashite kaonesha u pompompo wa hali ya juu.
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Nisinge ntaja huyo ni sawa na kuimba wimbo bila koras.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji115] mwache Kiba.
Hapa tumjadili Mondi kwanini alishiriki katika mwaka mmoja wa Makonda Bashite

Kumbuka kwenye kampeni pia alikuwepo
 
Back
Top Bottom