Ushauri Kwa kijana yeyote anayetaka Kuingia kwenye mahusiano ya Ndoa.

Ushauri Kwa kijana yeyote anayetaka Kuingia kwenye mahusiano ya Ndoa.

Kilenzi _Jr

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2021
Posts
301
Reaction score
1,110
Mpendwa rafiki yangu,

Zama ambazo vijana wengi wanahangaika kumpata mtu sahihi ni zama hizi kwa sababu watu wengi wanakuwa wanavaa barakoi yaani mask katika nyuzo zao hivyo ni ngumu kumjua yupi ni mtu sahihi kwako kama ukiingia kichwa kichwa. Watu wamekuwa ni wa kufanya maamuzi kwenye eneo la mahusiano kwa kutumia hisia badala ya kutumia akili.

Huwa watu wanafanya maamuzi kwa hisia halafu baadaye wanakuja kuamua kwa akili baada ya kufanya maamuzi. Tunakuwa na kesi nyingi ambazo ukizichunguza utagundua ni watu wanafanya maamuzi bila kufikiri, fikra zinakuwa chini pale wanapofanya maamuzi yao na wanajikuta wanakosea sana katika maamuzi kwa sababu hakuna anayeweza kubaki salama kama akiwa ni mtu wa kufanya maamuzi pale fikra zake zinapokuwa chini na hisia ziko juu.


KAA IJUE NJAA YA WANANDOA

Vijana wengi wanajikuta wanatumia muda mwingi kumtafuta mtu sahihi kwao ambae wanaweza kuwa pamoja katika maisha ya wito wa ndoa. Tunasahau ile falsafa ya kuwa huwezi kumpata mtu sahihi katika maisha yako kama wewe siyo mtu sahihi. Mtu ni mlevi wa kupindukia halafu anamtafuta mtu ambaye amatulia ni mchaMungu kwa hali kama hiyo ni sawa na kusubiri meli uwanja wa ndege, na utasubiri bila mafanikio miaka yako yote.

Kama unataka kumpata mtu sahihi kwanza unatakiwa kuwa mtu sahihi wewe mwenyewe, yaani sifa za yule unayemtaka kuwa naye anza kuwa nazo wewe na kama unajua sheria ya nguvu ya uvutanao itakukutanisha na yule anayeendana na tabia zako.

Kwa kijana yeyote anayetaka kuingia katika wito wa ndoa anatakiwa kufanya yafuatayo; kwanza kuwa na vigezo kabisa unataka kuwa na mtu wa namna gani? wengi wanatafuta wenza wa kuishi nao lakini changamoto kubwa wanatafuta wakiwa hawana vigezo hivyo kama unavyojua unapotafuta bila vigezo ni rahisi kupata hata kile usichostahili hivyo yoyote anayekujia mbele yako kwa sababu umri umeenda wazazi, marafiki wanakusema sana kwanini hauoi basi unajikuta unafanya maamuzi ya fasta unaoa hata usimyetarajia ili kuwafurahisha watu ambao hata hawataenda kuishi naye.
Hivyo basi, kama wewe uko kwenye ndoa au unataka kuingia kwenye ndoa nimekuandalia maarifa sahihi ya kukuwezesha wewe kukufanikiwa katika eneo la mahusiano kwa ujumla. Nimekuandalia kitabu ambacho kipo tayari kinachoitwa Ijue Njaa Ya Wanandoa.
 
Sijui nipo sayari ipi? Maana hii niliyomo vijana wanatazama wo wo wo na shepu, wakati mabinti wanatazama pesa maana ndio future ilipohamia...
 
Wewe ni Nesi wa wapi ambae ni Mmbadi jamani.
 
Unaweza pata mcha mungu na wife material lakin hujavutiwa nae!!!!Tunavutiwa na madem wenye mvuto na wowo la haja bila kujali tabia!!!
 
Unaweza pata mcha mungu na wife material lakin hujavutiwa nae!!!!Tunavutiwa na madem wenye mvuto na wowo la haja bila kujali tabia!!!
 
1. Karibu sana jamii forums Baddest Nurse.
2. Hongera kwa kuandika kitabu.
3. Tupe bei ya kitabu, mawasiliano yako na namna ya kukipata.
 
Back
Top Bottom