Ushauri kwa manufaa ya jamii nzima

Pia tusiwaamini sana housekeepers
 
11.Punguza Ulevi au acha pombe kabisa.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mi nimeamua kuacha
Last time nimeibiwa nilitoka kupombeka

Sasa Hivi nawaangalia tu wanywaji
Mie nakunywa Bavaria au fresh juice
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kamanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wapendwa habarini za leo? kwa walioangalia taarifa ya habari jana nadhani wamesikia kuwa kuna kikundi cha watu kinawateka watoto hata kama akiwa anaenda dukani au wakiwa wanacheza mazingira ya nyumbani. Wakishawateka wanawapigia wazazi simu au ndugu na kuwatajia kiasi cha pesa wanachotaka bila hivyo watamuua mtoto yaani wanatoa vitisho huku wakidai pesa, na mpaka sasa watoto waliopotea huko arusha leo siku ya nne bado hawafanikiwa kuwapata japo idadi yao haikutajwa. Ndugu wazazi naombeni tuwe makink na watoto wetu pindi wanapocheza mazingira ya nyumbani na dukani watumeni watu wazima sio watoto pia ikiwezekana ujumbe huu tumeni pia kwenye shule ambazo watoto wanasoma ili walimu nao wajue kinachoendelea kwa sasa so sad. Hali ya maisha imekuwa ngumu hivyo kila mtu anabuni mbinu ya kupata pesa.

Ukiondoka nyumbani asubuhi kama mtoto amefunga shule au hajaanza shule msisitize dada awe makini na watoto kwa wale wenye mageti basi waambie ni akina dada sio kila mgeni anaekuja ni mtu mwema wengine wana nia zao binafsi. Asante sana wazazi tutimize wajibu wetu wa kuwatunza na kuwalea watoto wetu bila kusahau maombi ya familia na Tanzania kwa ujumla.
 
TANGAZO MAALUMU:
Kwenye Sherehe Za arusi na mikusanyiko ya jamii, vibaka sasa wanakwenda kwa Mshehereshaji kutangaza matangazo kama vile "gari yenye usajili namba fulani imezuia njia" Unapotoka kwenda nje ya gari lako unakuta watu wenye bunduki wakijua kuwa Una funguo za gari, wanakuamrisha kuendesha gari nje ya eneo la kuegeshea wakiwa ndani ya gari pamoja na wewe.
Tafadhali fanya yafuatayo namba ya gari lako inapotajwa kwenye sherehe za kijamii.
1. Chukua muda kabla hujaenda nje
2. Usiende peke yako angalau watu wawili au zaidi.
3. Usiende mojakwamoja mahali gari lako lilipo hakikisha kama kweli yupo mtu uliyemzuia.
4. Angalia mazingira kwa makini kabla hujakaribia gari lako.
Tafadhali nakili na changia na wengine hata kama huna gari,
Okoa watu wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msisahau kulala na panga chini ya kitanda..
Umejuaje...!!!! Mi kulala geto bila panga uvunguni sipati amani kabisa....babu alinipa mkuki nimeuacha Tukuyu, kila siku naukumbuka,yaani sina amani kabisa huku niliko....
 

basi huelewi maana ya neno furaha.

furaha ni hali unayokuwa nayo unapokuwa na amani,ukiona huna amani na unajihisi kufurahi,jua unaigiza furaha.

hakuna wasi wasi kwamba kwa sasa uhalifu umeamka tena,Mama mwenye nchi anakiri wazi wazi.
kitendo ch wewe kutoa vijihera kwa wakala halafu huna uhakika kama utafika navyo nyumbani ni tatizo kubwa sana,huwezi sema una fulaha kwa mazingira hayo.
 
Ahaaaa, binafsi nimeelewa kwamba furaha ipo kwa watenda ubalifu, maana sasa Wana uhuru.
 
Kwa kuongezea kwa hao wanaobaki Nyumbani, pia waambiwe Wasikubali kumuingiza mtu yeyote ndani ambae hawamjui, kwa madai yeye ametumwa kuja kuchukua ama kutengeneza kifaa chochote ndani kwa madai tayari amewasiliana na mwenye nyumba.
 
Nina furaha kwakuwa hakuna kutekana tena . hilo ni kubwa sana na watekaji sasa wanadondoka mmojammoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo namba 5 ina matatizo kidogo boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…