LIKIZO TIME YAKUPASAYO KUFANYA MZAZI WAKATI WA LIKIZO UKIWA NA WATOTO WAKO
(1) Mshukuru Mungu
[emoji117]Shukrani kwa Mungu kwa watoto wako kurudi salama,na kumaliza mhula wa shule salama, wako watoto wengine hawakuweza waliuugua,walifariki nk
(2)Wape muda watoto
[emoji117]Najua kweli mzazi upo bize kutafuta ridhiki ya kila siku,lakini wape muda watoto wako kipindi Cha likizo,kaa nao,angalia Kama Kuna mabadiliko yoyote ya kiroho au kimwili. Wape muda punguza ubize.
(3) Wasikilize
[emoji117]Jamani wazazi tuwe na tabia ya kusikiliza watoto wetu,wana mengi wamepitia wakiwa mbali na wewe,hebu wape muda wa kuwasikiliza basi,wanatamani kusema Ila hawana pa kusemea wape mudaa..
(4)Usiwajibu kwa ukali
[emoji117] inawezekana umengua kitu,ambacho sio kizuri,usiwakalipie,usifoke ovyooo,hata Ni kosa ongea kwa utulivu,Jifunze kutuliza hasira yako,mfano unakuta binti yako au kijana ameeanza mahusiano ya kimapenzi,so wewe unatakiwa umwambie madhara ya kufanya sex kabla ya wakati,ataelewa zaidi kuliko kumpiga...ongea na kwa upole.
(5)Watoe watoto wako outing[emoji1787]
[emoji117]
Kipindi hata sikumoja watoe watoto wako mahali wakatembeee,wacheze wafurahi,wale chakula pia nje ya nyumbani itakuwa furaha sanaa kwao.
(6)Hakikisha wanashiriki kazi za nyumbani
[emoji117] Kweli watoto walikuwa shule Sasa wamerudi,basi sio vibaya wakishiriki kazi za nyumbani ikiwa ni kupika,kuosha vyombo,kupanga sebule, vyumba vyao kuwa safi,kuosha vyombo nk wasimuachie dada wa kazi, kumbuka huu muda ndio mzuri wao kujifunza,usiwaache .
(7) Kuwa Makini kwa wanachoaangalia
[emoji117]Kweli likizo watakuwa na muda wa kuangalia sanaa tv,Ila kuwa Makini na carton,move nk wanazoangalia,zingine hazina maadili mazuri,jilizishe kwa kile wanachoaangalia.
(8)Watembelee ndugu,jamaa na marafiki
[emoji117] kipindi hiki Kama muda upo wapeleke wasalimie ndugu,Kuna familia watoto hawajui kabisa ndugu zao,hii hatari sababu hao watoto ujue wanakua na watakuwa na tabia ya kutowatembelea ndugu Wala kuwajali.
(9)Angalia mabegi yao,kabati zao.
[emoji117]Kama mzazi lazima mtoto anaporudi uangalie vizuri bag ambalo amerudi nalo,je amerudi na vitu vyake,? Wengine wanaanza tabia ya wizi au kuazimana anarudi na vitu sio vyake,Ila ktk kupekua bag Kuna vitu unaweza Kukutana navyo pia,Kuna watoto ambao wameaanza mahusiano utawakuta na vidonge vya majira, condoms nk so check up muhimu sanaa.
(10)Wahimize ibada
[emoji117]Ibada muhimu sanaa , hakikisha unaomba nao,pia kila mmoja mwambie akuandikie kwenye karatasi ombi ambalo anataka Mungu amtendeee nk omba nao wafundishe neno la Mungu nk wekeza vitu vyema kwa watoto wako...
#Watoto wetu furaha yetu
#uzao wetu mzuri
#Malezi sahihi ya watoto