Ushauri kwa manufaa ya jamii nzima

Ushauri kwa manufaa ya jamii nzima

LIKIZO TIME YAKUPASAYO KUFANYA MZAZI WAKATI WA LIKIZO UKIWA NA WATOTO WAKO

(1) Mshukuru Mungu
[emoji117]Shukrani kwa Mungu kwa watoto wako kurudi salama,na kumaliza mhula wa shule salama, wako watoto wengine hawakuweza waliuugua,walifariki nk

(2)Wape muda watoto
[emoji117]Najua kweli mzazi upo bize kutafuta ridhiki ya kila siku,lakini wape muda watoto wako kipindi Cha likizo,kaa nao,angalia Kama Kuna mabadiliko yoyote ya kiroho au kimwili. Wape muda punguza ubize.

(3) Wasikilize
[emoji117]Jamani wazazi tuwe na tabia ya kusikiliza watoto wetu,wana mengi wamepitia wakiwa mbali na wewe,hebu wape muda wa kuwasikiliza basi,wanatamani kusema Ila hawana pa kusemea wape mudaa..

(4)Usiwajibu kwa ukali
[emoji117] inawezekana umengua kitu,ambacho sio kizuri,usiwakalipie,usifoke ovyooo,hata Ni kosa ongea kwa utulivu,Jifunze kutuliza hasira yako,mfano unakuta binti yako au kijana ameeanza mahusiano ya kimapenzi,so wewe unatakiwa umwambie madhara ya kufanya sex kabla ya wakati,ataelewa zaidi kuliko kumpiga...ongea na kwa upole.

(5)Watoe watoto wako outing[emoji1787]
[emoji117]
Kipindi hata sikumoja watoe watoto wako mahali wakatembeee,wacheze wafurahi,wale chakula pia nje ya nyumbani itakuwa furaha sanaa kwao.

(6)Hakikisha wanashiriki kazi za nyumbani
[emoji117] Kweli watoto walikuwa shule Sasa wamerudi,basi sio vibaya wakishiriki kazi za nyumbani ikiwa ni kupika,kuosha vyombo,kupanga sebule, vyumba vyao kuwa safi,kuosha vyombo nk wasimuachie dada wa kazi, kumbuka huu muda ndio mzuri wao kujifunza,usiwaache .

(7) Kuwa Makini kwa wanachoaangalia
[emoji117]Kweli likizo watakuwa na muda wa kuangalia sanaa tv,Ila kuwa Makini na carton,move nk wanazoangalia,zingine hazina maadili mazuri,jilizishe kwa kile wanachoaangalia.

(8)Watembelee ndugu,jamaa na marafiki
[emoji117] kipindi hiki Kama muda upo wapeleke wasalimie ndugu,Kuna familia watoto hawajui kabisa ndugu zao,hii hatari sababu hao watoto ujue wanakua na watakuwa na tabia ya kutowatembelea ndugu Wala kuwajali.

(9)Angalia mabegi yao,kabati zao.
[emoji117]Kama mzazi lazima mtoto anaporudi uangalie vizuri bag ambalo amerudi nalo,je amerudi na vitu vyake,? Wengine wanaanza tabia ya wizi au kuazimana anarudi na vitu sio vyake,Ila ktk kupekua bag Kuna vitu unaweza Kukutana navyo pia,Kuna watoto ambao wameaanza mahusiano utawakuta na vidonge vya majira, condoms nk so check up muhimu sanaa.

(10)Wahimize ibada
[emoji117]Ibada muhimu sanaa , hakikisha unaomba nao,pia kila mmoja mwambie akuandikie kwenye karatasi ombi ambalo anataka Mungu amtendeee nk omba nao wafundishe neno la Mungu nk wekeza vitu vyema kwa watoto wako...

#Watoto wetu furaha yetu
#uzao wetu mzuri
#Malezi sahihi ya watoto
 
UTAPELI UMERUDI KWA KASI

Kwa wakazi wa Dar es Salaam, chukueni tafadhari.

Hii imenitokea leo, kwenye mataa ya mtaa wa Lindi na Msimbazi. Nilifanya kosa pale (nilitakiwa kunyoosha moja kwa moja kutoka Kkoo kuja Karume, mie nikapinda kulia kuyafuata mataa ya Uhuru na Msimbazi). Nilipofika mataa ya Uhuru, mara wakatokea vijana wawili watanashati, wakiwa na pikipiki. Wakazuia gari kwa mbele; wakatoa vitambulisho, mmoja ni mfanyakazi wa UDART na mwingine ni askari wa Usalama barabarani. Kisha wakasema umefanya kosa kwa mujibu wa sheria za UDART. Hivyo unapaswa kwenda kizuizini kwa siku 14 kisha utalipa faini tsh 850,000 ndipo utakuwa huru. Haya ongoza Yadi. Kijana mmoja akapanda garini, yule mwingine akawa anatufuata nyuma na pikipiki. Nikatumia muda huo kuomba msamaha na kuomba kupunguziwa faini ili tumalizane yaishe. Lakini afisa yule alikuwa mkali, King'ang'anizi. Mara akapiga boss wake, akiagiza nipelekwe haraka Yadi, nikaomba kuongea na boss. Sasa ikabidi nipaki maeneo ya jirani na uwanja wa Karume (TFF). Katika maongezi yetu boss yule alitaka nilipe fine ya tsh laki 6 badala ya 860,000/=

Lakini wakati hayo yanafanyika kichwani nilikuwa nawaza "Hawa jamaa wanaweza kuwa matapeli". Sasa nikazima gari. Nikawaomba hawa jamaa wawili nishuke nikatafute pesa kwa ndugu yangu ambaye anafanya biashara hapo jirani ( kwenye kituo cha daladala cha karume). Jamaa wakakubali. Tukaongozana; nilipomkuta dada nikamsimulia tukio hili kwa kifupi, kisha nikamwambia aende pale kituo cha polisi (jirani) aulize uhalali hii operation ya maafisa wa UDART. Wale jamaa walipoona dada anaenda kituoni wakanifuata, wakasema niwape hela yoyote niliyonayo ili mambo yaishe.. tukiwa bado tunabishana mara akatoka askari mmoja namimi nikaitwa kituoni. Wale jamaa walipoona hayo wakakimbia kwa kasi. Kumbe walikuwa Matapeli tu, sio UDART wala sio askari, ni Matapeli.

Basi nikawashukuru wale askari kisha nikaondoka.

Mtaarifu na mwingine, asije akaibiwa kizembe.

Copy & Paste as received
 
YAH: SHAMBULIO LA KIMTANDAO (CYBER ATTACK) INAYOENDELEA KWENYE WHATSAPP PLATFORMS
Ndugu Wanaumoja
Kumetokea shambulio la kimtandao katika baadhi ya platforms nilizomo ambapo mvamizi amekuwa akiwatumia link zenye whatsapp code baadhi ya watu ili waweza kuhakiki(verify) account zao. Baada ya mhusika kuclick hiyo link anakuwa amejikabidhi mikononi mwa mvamizi ambaye atateka (hack) groups zote ambazo mhusika yupo.

Akishafanikiwa kuingia atawaondolea uadmin admins wote kisha group litakuwa chini yake. Baada ya hapo atabadili settings za group. Na kuendelea kushambulia members wengine wote kwa kudukua akaunti zao.

Tafadhali usibonyeze link yoyote unayotumiwa ambayo haieleweki eleweki, ikiwemo inayojinadi kuwa shindano la Cocacola. Utauza group letu wote tutachukuliwa mateka.

Tafadhali tuzingatie haya

IKITOKEA HACKERS WAMEFANIKIWA KUTUTEKA TUFANYEJE?

1). Angalia Adimins ni Nani. ukikuta siyo Mwanaumoja, toa rai ya kuwataka Wanaumoja wajiondoe kwenye group mara moja kabla hawajadukuliwa account zao. Wadukuzi wanaweza kupata password ulizohifadhi kwenye simu na taarifa mbalimbali; wanaweza wakatumia namba yako ya simu wakaomba watumiwe Fedha na watu ambao mnafahamiana n.k
 
Furaha inatoka wapi kama unaandika mambo ya uhalifu kuongezeka kwa kasi!???

Hii si ni dalili ya kuanza kuishi kwa hofu

Mbona unajikanganya kwenye maelezo mkuu
wakati wa magufuli ndio tuliishi sana kwa hofu,ya kutekwa,kupewa kesi ukikosoa, na mauchafu kibao
 
UTAPELI UMERUDI KWA KASI

Kwa wakazi wa Dar es Salaam, chukueni tafadhari.

Hii imenitokea leo, kwenye mataa ya mtaa wa Lindi na Msimbazi. Nilifanya kosa pale (nilitakiwa kunyoosha moja kwa moja kutoka Kkoo kuja Karume, mie nikapinda kulia kuyafuata mataa ya Uhuru na Msimbazi). Nilipofika mataa ya Uhuru, mara wakatokea vijana wawili watanashati, wakiwa na pikipiki. Wakazuia gari kwa mbele; wakatoa vitambulisho, mmoja ni mfanyakazi wa UDART na mwingine ni askari wa Usalama barabarani. Kisha wakasema umefanya kosa kwa mujibu wa sheria za UDART. Hivyo unapaswa kwenda kizuizini kwa siku 14 kisha utalipa faini tsh 850,000 ndipo utakuwa huru. Haya ongoza Yadi. Kijana mmoja akapanda garini, yule mwingine akawa anatufuata nyuma na pikipiki. Nikatumia muda huo kuomba msamaha na kuomba kupunguziwa faini ili tumalizane yaishe. Lakini afisa yule alikuwa mkali, King'ang'anizi. Mara akapiga boss wake, akiagiza nipelekwe haraka Yadi, nikaomba kuongea na boss. Sasa ikabidi nipaki maeneo ya jirani na uwanja wa Karume (TFF). Katika maongezi yetu boss yule alitaka nilipe fine ya tsh laki 6 badala ya 860,000/=

Lakini wakati hayo yanafanyika kichwani nilikuwa nawaza "Hawa jamaa wanaweza kuwa matapeli". Sasa nikazima gari. Nikawaomba hawa jamaa wawili nishuke nikatafute pesa kwa ndugu yangu ambaye anafanya biashara hapo jirani ( kwenye kituo cha daladala cha karume). Jamaa wakakubali. Tukaongozana; nilipomkuta dada nikamsimulia tukio hili kwa kifupi, kisha nikamwambia aende pale kituo cha polisi (jirani) aulize uhalali hii operation ya maafisa wa UDART. Wale jamaa walipoona dada anaenda kituoni wakanifuata, wakasema niwape hela yoyote niliyonayo ili mambo yaishe.. tukiwa bado tunabishana mara akatoka askari mmoja namimi nikaitwa kituoni. Wale jamaa walipoona hayo wakakimbia kwa kasi. Kumbe walikuwa Matapeli tu, sio UDART wala sio askari, ni Matapeli.

Basi nikawashukuru wale askari kisha nikaondoka.

Mtaarifu na mwingine, asije akaibiwa kizembe.

Copy & Paste as received
dah,basi inaonyesha washawapiga wengi kwa style iyo
 
[emoji569]️NENO LA LEO,2021[emoji569]️

[emoji363]Alhamisi,July 01

[emoji860]Tunaitwa kutenda [emoji3539]haki na huruma[emoji885]

[emoji353]️Kutoka 23:1-5

[1]Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu.
[2]Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;
[3]wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake.
[4]Ukimwona ng’ombe wa adui wako, au punda wake, amepotea, sharti umrudishie mwenyewe tena.
[5]Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye hali ameanguka chini ya mzigo wake, nawe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.

[emoji848]TAFAKURI;

[emoji1614]Tunatakiwa kutenda haki na huruma, na wala si kutenda mambo ya ukatili na udhalimu hata dhidi ya wanyama, mifugo wasio na hatia.
_[emoji1006]Somo la leo linatukataza kutenda uovu wa kupotoa hukumu.Tunatakiwa kutenda haki wala tusifanye upendeleo.Tukiona ng'ombe au punda wa mtu amepotea au amepata shida tumsaidie na tumrudishe salama nyumbani kwake. _
[emoji1006][emoji1006]Jamani Wapendwa wana wa Mungu tusaidiane, tusifanyiane mambo ya hiana na udhalimu bali tutende haki na huruma sisi kwa sisi, lakini pia kwa viumbe wasio na hatia.

SALA [emoji992]

[emoji915]Bwana Yesu Kristo, asante kwa kunihurumia mimi mwenye dhambi.Unisaidie mimi na msomaji Huyu tutende haki na huruma kwa jirani zetu katika jina lako takatifu[emoji915]

[emoji973]AMINA[emoji973]
 
Kwa wale wasiokuwa na cheti cha kuzaliwa pale sabasaba jengo la Rita nenda na barua ya serikali ya mtaa au kitamburisho cha mpiga kura na elfu 10000 unapata cheti chako hapo hapo waambie na watu wengine[emoji1666] ni ofa
 
Nazir Karamagi na Yogesh Manek watafanikiwa kuendelea kuinyonya Tanzania kupitia bandari ya DSM?

Na Juma Kambi, Kuli Bandarini DSM

Wawili hawa ni wamiliki wa kampuni ya kusimamia makontena katika bandari ya Dar (TICTS).Kwa miaka mingi wamekuwa wakipokea mabilioni ya fedha huku utendaji wa kampuni hiyo na bandari kwa ujumla ukisuasua na kusababisha wateja wengi kuhamia Mombasa Kenya, wakikosesha nchi mabilioni ya mapato huku wao wakinufaika.Manek ni mfanyabiashara nyingi kubwa nchini ikiwemo Benki ya Exim huku Karamagi akiwa Waziri wa zamani wa Nishati na Madini mwenye kashfa ya kusaini mkataba wa madini wa Tanzania mwaka 2007 hotelini Jijini London na mmoja ya wanufaika katika kashfa ya Richmond.

Chini ya utawala wa hayati Rais Magufuli ikafanyika jitihada ya kuanza kuwaondoa na kuboresha utendaji wa bandari, baada ya Magufuli kufariki Rais Samia akaendeleza jitihada hizo. Hivi sasa wawili hao wamejipanga kupambana na Rais Samia ili wapate mkataba mpya kuendelea kubaki bandarini hapo.Swali ni kwamba je watafanikiwa.? Ni suala la kusubiri kuona.
Screenshot_20220726-190118.jpg
 
Back
Top Bottom