Ushauri kwa mdogo wangu: Alioa akiwa na umri wa miaka 23 sasa anamkataa mkewe akidai yeye bado mdogo

Ushauri kwa mdogo wangu: Alioa akiwa na umri wa miaka 23 sasa anamkataa mkewe akidai yeye bado mdogo

Jibu lake la hajui ilikuaje akaoa, pengine shemeji alimuekea dawa amuoe, tuambie unamuonaje huyo mke wake, labda dawa imeisha nguvu anaanza kuwaza kwa akili zake timamu
 
Mlitakiwa mumpe fact kabla ya kuoa mpe uelewa ili akioa na yakibadilika asidhubutu kurudi. Miaka 23 huyo alitakiwa awe chuoni ajifunze zaidi na zaidi
 
Anachekesha kweli kweli yeye alifikiri ndoa ni kuvaa Suti tu? mwambie aache ujinga.
 
Nina wasiwasi dogo kaonja nje kapagawishwa sasa anatafuta namna ya kukimbia nyumba yake.
 
Kuna mmoja hapa anapaparika kisa alioa mdogo(umri 21) majukumu yamemzidi na ndoa haina hata mwaka anajuta,ajira ya maana hana
 
Mwambie atulie tu huyo ni chaguo lake
Kilichomfanya awahi kuoa ni nini au na yeye alitaka kuoa sababu rafiki zake wameoa
 
Oa mkuu hawa hawa mafundi cherehani wauza mboga niwashamba, mpaka aje kuwa mjanja ana 40 au 45 hapo ashazaa watoto 3 sasa jifanye unataka wale wa viatu virefu uone, yaani hawa wa kitaa akija gheto haruki
Ha ha noted mkuu
 
Wachunguzeni marafiki zake, kama ana marafiki vijana kama yeye na hawana ndoa hiyo ndo sababu. Pia mke wake afanyiwe training kuwa wao bado vijana hivyo ndoa iwarahisishie kufurahia ujana na si vinginevyo.

Wasijifanye wao ni watu wazima wafanye maujinga yote ya ujanani bila kuvunja sheria za nchi na kwa kiasi. Wasimsahau MUNGU pia.

Mwisho mkumbushe kuwa kama ni ndoa ya kikatoliki kuvunjika ni ngumu kama kumeza wembe bila kuchanika.
 
Mwanaume 23 years anaoa? Alikua anawahi nini labda... Kwakweli hiyo ni sawa na kuondoka night club saa tatu usiku.

Alidhani ndoa ni kufanya tu matusi! Mwambie aendelee tu na mke wake, kama anajiona bado mdogo atakulia tu humo humo ndoani
I wonder pia
 
Wachunguzeni marafiki zake, kama ana marafiki vijana kama yeye na hawana ndoa hiyo ndo sababu. Pia mke wake afanyiwe training kuwa wao bado vijana hivyo ndoa iwarahisishie kufurahia ujana na si vinginevyo.

Wasijifanye wao ni watu wazima wafanye maujinga yote ya ujanani bila kuvunja sheria za nchi na kwa kiasi. Wasimsahau MUNGU pia.

Mwisho mkumbushe kuwa kama ni ndoa ya kikatoliki kuvunjika ni ngumu kama kumeza wembe bila kuchanika.
Hyo siyo ya kikatoliki haiwezi kuwa ya haraka kama hivyo.
 
Hyo siyo ya kikatoliki haiwezi kuwa ya haraka kama hivyo.
Kama si ya kikatoliki inavunjika tu. Ila awe na uhakika kuwa anataka ivunja, isiwe ni mihemuko maana kupata mwanmke wa kuoa ni rahisi ila kupata mke bora si rahisi.
 
Dogo kazidiwa akili na mchepuko baada ya kuonjeshwa mafiiiii anaona wife hafai.
 
Back
Top Bottom