Waziri kwako unamuona ni Mungu. Hata huyo waziri angeniandikia mambo wakati namba siijui nisingemjibu. Go straight to the point. Kaka kwema. Kuna abcdefg
Rafiki waziri kwangu si Mungu ila najaribu kuonesha kuwa kuna muda inabidi kuishi na watu vile walivyo .
Actually na mimi nilikuwa kama wewe sikupenda mtu aanze na bla bla badala yake anyooke kwenye point .
Ila sasa tuko kwenye kizazi cha Generation Z vijana hawaelewi hata useme nini hivyo kuna muda unaishi nao kulingana na hulka na silka zao as long as haupungukiwi na chochote mkuu .
Nakupa mfano , nimewahi kuwa napogiwa simu na mtu simjui na yeye ana shida kwaangu kichekesho anapiga simu napokea anasema habari mkuu nasema salama , alafu ananiambia niambie 🤔 kiukweli nilikuwa najawa na hasira sana ila mwisho ikabidi nikubali mazingira na watu wa dunia yangu ya Tanzania kuwa sina namna zaidi ya kuendana nao .
Kataa kubali sio kila anayetuma meseji za salamu hataki kwenda direct kwenye point anaomba hela au msaada wowote wengine wanakuwa ni wema kwako kwa baadhi ya either taarifa utakazopewa ndugu .
Ni hayo tu kaka mkubwa ila nimetaja mawaziri sio kwakuwa ni lolote wala chochote ila ni kwakuwa hulka na silka ya watanzania wengi ni kuwa wajivuni hivyo kwa hizi tabia ninhetegemea hata wao wajivune wasiwe wanajibu meseji zetu hata usiku wa manane .
Note: Sio mawaziri wote ndugu yangu .
Karibu Keko _ Akida ni wikiendi imeanza kaka , njoo tufurahi maisha ni haya haya , kwani yuko wapi mama yangu ? Baba yangu ? Je Magufuli yupo ?
Basi tuishi kwa amani na furaha sie ni wapitaji .