Pia serikali iache kununua magari ya kifahari, samani za ofisini za kifahari, ziara za kwenda Dodoma makao makuu zisitishwe watumie zoom, email na mitandao, nyumba za serikali za wakubwa viuzwe, watendaji wa serikali kuu na za tawala za mikoa wajipangie nyumba wenyewe kwa kulipa kodi au kukopa mikopo ya muda mrefu NHC mortgages n.k
Listi ni ndefu sana ya jinsi ambavyo serikali inaweza kupunguza matumizi na hii siyo kubana bali kuondokana na matumizi haya ya anasa. Ukienda ofisi ya serikali Denmark, Ufaransa, Ubelgiji utaona ofisi zina samani / fenicha zisizo ghali wala za kifahari na hawa ndiyo wanaotupa misaada au kuitwa wawe wadau wa maendeleo Tanzania lakini hawa wadau wana nidhamu kubwa ya matumizi ya kodi kwa kutojinunulia fanicha za ofisi, magari n.k ya kifahari.