Ushauri kwa Serikali: Ajira za mkataba ndiyo suluhisho pekee la uhaba wa ajira nchini

Top Management waende Ulaya wakafanye kazi huko! Bongo mfumo ubadilike ili kuondoa vilaza kwenye system tuna top management mbovu kuwahi kutokea ambayo inazurura tu kwenye midege!
anyway ni mawazo yenu ila kwenye utekelezaji ngumu sana job circle lazima iwepo popote hata kwenye familia
 
Sasa mantiki mbona ni ile ile! Weka pesa ifikie kiwango cha mtaji uwekeze na kusimamia biashara yako!

Inategemea na risk appetite ya mtu. Mwengine atawekeza hio hio million 1 wengine watawekeza 10M so kulingana na utakavyo kama uta manage kusimamia hela yako na kazini unaweza kuanza kuwekeza toka mshahara wa kwanzaπŸ˜…

Kukwambia ku save ifike 60M sio kana kwamba aanze kuila hio pesa bali afanye utekelezaji wa mpango wa muda mrefu!
 
Mshahara mtamu mkuu, mtu huyo huyo akiambiwa aitafute hio laki 5 akiwa hana hata thumni huku mtaani anaweza kuishia kufa na stress ama depression!

Hizo ajira wanaozing’ang’ania wala siwashangai mtaa huku ni mziki mnene!
 
Hoja ya kwanza inaweza kujadilika ndani na nje ya bunge
Hoja namba mbili itazungumzika nje ya bunge lakini hakuna atakayeiingiza kwenye mlango wa bunge.
Kwakweli mawazo yako ninayaona ni chanya
 
Ushaambiwa kwenye hio mshahara ukitoa mahitaji muhimu, you are left with nothing or little to save, hio mil 60 utaitolea wapi? Halafu sio kila mtu ni mfanyabiashara, halafu watu wata misuse ajira/position zao wakiona wanatolewa soon,lastly job security is important, it goes everywhere even home baba akiwa stressed or depressed athari zinaenda hadi kwa familia, wote tutafakari njia ambazo ziko more practical, we understand how hard it is but sio kuja na solutions zitakazo athiri wengine
 
Mshahara mtamu mkuu, mtu huyo huyo akiambiwa aitafute hio laki 5 akiwa hana hata thumni huku mtaani anaweza kuishia kufa na stress ama depression!

Hizo ajira wanaozing’ang’ania wala siwashangai mtaa huku ni mziki mnene!
kweli kabisa mkuu ndio maana watu hadi wanlogana kazini kupata vyeo na kubaki kazini alafu leo uwambie arudi mtaani
 
Yani ulipwe 5M per month ushindwe ku save 1M my friend? Kumbuka sizungumzii mishahara mbuzi ya 300K to 1M ile.., unless uwe unaishi maisha ya kifahari sana!

Uko sahihi kwa ishu ya job security ni muhimu ila hali ilivyo ni fedhea kwa kweli tunapoenda vijana wengi watashindwa hata kuoa sababu ya ishu hio hio ya kukosa mshahara!

Peace of mind ni haki ya kila mtanzania sio wachache ambao wamebahatika kupata nafasi!
 
Bila shaka
 
Yani ulipwe 5M per month ushindwe ku save 1M my friend? Kumbuka sizungumzii mishahara mbuzi ya 300K to 1M ile..,
Hahaaaaa mkuu siku Tanzania itakapoanza kulipa watu million 5 kwa mwezi ujue ni muujiza, kama wakiweza kulipa hela yote hio kwa mtu mmoja kwa nini wasi igawanye badala yake wakatoa kidogo lakini kwa kila mtu na kwa muda mrefu?????
 
Kwa mfano Prof kama aliyefariki wiki hii (Prof. Luhanga) unaweza ukamtengeneza ndani ya miaka mitano ?

Daktari bingwa anayefanya surgery za kufa mtu halafu unamtoa chap chap ...sio ndio tunatengeneza bomu lingine ?
Uko sahihi... Inahitaji muda na vipaji vingine ni exceptional! Itafutwe namna nyingine ya kuongeza fursa za ajira.
 
Hahaaaaa mkuu siku Tanzania itakapoanza kulipa watu million 5 kwa mwezi ujue ni muujiza, kama wakiweza kulipa hela yote hio kwa mtu mmoja kwa nini wasi igawanye badala yake wakatoa kidogo lakini kwa kila mtu na kwa muda mrefu?????
Hela inayopotea kwa wizi na ufisadi ni nyingi kuliko ambayo ingetosha kulipa watu 5M kwa mwezi! Kwa sasa tuna tozo pia mbona linawezekana!

Sasa kumbuka hapa tunazungumzia mpango maalumu ili kunusuru janga la ajira kwa graduates! Yani lengo ni upewe hela nyingi kwa muda mfupi ili upishe wenzio! Mbona hili swala liko practical sana.

Ambaye ataonekana hatoshi pia ataondolewa kupisha wengine, ili kulinda ufanisi! Cycle ya ajira inakuwa ya muda mfupi tu.
 
wataajiriwa wale wanaojitolea au wapiga tempo kwenye taasisi ili tayari wawe na uzoefu wa kazi!!PLAN INA WEZEKANA KABISA KAMA WADAU WAKIKAA NA KUTUNGA KANUNI NA SHERIA ZA KAZI NA AJIRA NCHINI!!!
 
Kwa mfano Prof kama aliyefariki wiki hii (Prof. Luhanga) unaweza ukamtengeneza ndani ya miaka mitano ?

Daktari bingwa anayefanya surgery za kufa mtu halafu unamtoa chap chap ...sio ndio tunatengeneza bomu lingine ?
Kwa hao wa afya huko wana exception mkuu! Hao wasiguswe nazungumzia huku kwa Cadre nyingine mkuu.
 
Sasa kumbuka hapa tunazungumzia mpango maalumu ili kunusuru janga la ajira kwa graduates!
Mkuu ndio maana nikasema tuwe practical, I understand the situation, ila siku ambayo Tanzania inaweza kumpa kila graduate mshahara wa million tano haipo!be realistic, na siku hio ikifika ujue matatizo mengi Tanzania yatakua yameshaisha ikiwepo Ajira, again tubuni njia nyingine, mimi kusema ukweli sio nakupinga tu bali ni ukweli hili jambo haliwezekani
 
Ila jamaa wawili kuiba billion 50 serikalini inawezekanaπŸ˜…?
 
Hata Flyover tuliambiwa haiwezekani na SGR haziwezekani kwa bongo ila zitawezekana tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…