Ushauri kwa Serikali: Ajira za mkataba ndiyo suluhisho pekee la uhaba wa ajira nchini

Ushauri kwa Serikali: Ajira za mkataba ndiyo suluhisho pekee la uhaba wa ajira nchini

Miaka ya kustaafu ipunguzwe 45 mwisho mtu aachie ngazi sasa wazee wamekaza eti mpaka miaka 60 ni mingi sana 45 tu astaafu akiwa a nguvu zake akaanzishe mradi ili awaajir wengine na wengine warithi nafasi yake. pia ajira za mkataba n sawa sasa sirikali inaangaika mbowe tu

Why the limit?!?

Binafsi nadhani, if possible ajira ilingane na output.

Kama uko ofisini for more than 5 years iwe na maana mchango wako ni dhahabu, even at the retirement age uwe na faida sio tu ilimradi uliwahi kuhudumu serikalini.

Otherwise even in two years of your service to the nation ukionekana huna msaada kitaifa utolewe tu!
 
Hela inayopotea kwa wizi na ufisadi ni nyingi kuliko ambayo ingetosha kulipa watu 5M kwa mwezi! Kwa sasa tuna tozo pia mbona linawezekana!

Sasa kumbuka hapa tunazungumzia mpango maalumu ili kunusuru janga la ajira kwa graduates! Yani lengo ni upewe hela nyingi kwa muda mfupi ili upishe wenzio! Mbona hili swala liko practical sana.

Ambaye ataonekana hatoshi pia ataondolewa kupisha wengine, ili kulinda ufanisi! Cycle ya ajira inakuwa ya muda mfupi tu.
No haliko practical mkuu, kama ishu ni mitaji kwa nini badala ya kuwaongezea mishahara waajiriwa kwa nini wasiwape graduates hio pesa wafanye mitaji??
 
Hapo Kuna Kitu utasaidia Ila Kuna Mambo Utaharibu Kabisa. Naona Umeangalia Kwa Upande mmoja Kwamba Unawasaidia Wasio na Ajira Pekee

Kumbuka Makazini Kunahitaji Uzoefu Pia Wa Kazi huwezi Kuingiza Watu na Kutoa Tu na Kuweka Wasio na Uzoefu

Uzoefu unapatikana aje Chief?

Mleta mada kalenga panapostahili!
 
Uko sahihi, kazi za serikali ziwe za mikataba na zisizidi miaka 10
 
RAISI AJAE

Tanzania kuna watu wengi ukiwaambia katiba mpya ni kitu muhimu sana watasema siyo muhimu lakini akigeuka analalamikia mambo yanasababishwa na katiba mbovu. Kwa kifupi wengi hawaoni correlation kati ya vitu kama ulivyoandika na katiba.
Watu wengi uwezo wao kufikiri kwa mantiki uko chini.
 
Mmeanza roho mbaya
Roho mbaya ipi? Hii nchi si ya watanzania wote? Kwa nini wengine wafe wakiwa vikongwe kwenye ajira za umma ambazo ni kodi za watanzania wote huku wengine wakionekana hawastahili?

Watu wanachotaka ni Watanzania wote wawe na fursa ya ku enjoy hiyo keki ndogo ya taifa kidogo kidogo.
 
Hii haina tija. Unawaajiri watu ná kuwapa training yenye gharama kubwa katika utendaji wa kazi zao za kila siku. Baada ya miaka mitatu wakati tayari wana experience ya kutosha katika utendaji wa kazi zao unawaondoa na kuwaleta wapya ambao hawajui chochote na zoezi la kutoa training upya linaanza tena!!!. Kuna wizi, ufisadi na ubadhirifu mkubwa sana Serikalini kama mianya hii ikiondolewa basi Serikali inaweza ikatoa ajira nyingine kati ya laki 5 mpaka milioni bila matatizo yoyote yale.

RAISI AJAE
Hiyo training waliyoipata na uzoefu kazini wataenda kuutumia kwenye sekta binafsi, hicho ndicho kinachofanyika Marekani ndio maana unaona watu wengi sana kwenye siasa na sekta binafsi ya Marekani ni wanajeshi wastaafu ila bado ni vijana.
 
Sio kusaga rumba! Unapewa miaka 5 ya kulipwa vizuri tu hili wazo nilishakujaga nalo jamaa ameamua kulianzishia uzi pia too good kumbe kuna mtu alikuwa na maono sawa na mimi tu!

Chukulia mfano mtumishi alipwe 5M kila mwezi bila kujali cadre! Kuwe na kiwango fixed kwamba kulingana na uchumi wa sasa we need to pay atleast 5M itampa nafasi ya kila mtumishi kuishi na ku save kiasi flani kila mwezi nje ya pension yake anayokatwa na NSSF! Chukulia mfano una save million kila mwezi tu..after 12 months utakuwa na million 12...after 5 years una million 60! Ukijumlisha na yale makato ya NSSF hamna hamna una 85M hivi kwa hii pesa mtu hajapata pa kuanzia tu?

Ikifika miaka mitano mkataba unaisha unaondoka na mtaji wa kutosha kabisa usiopungua 50M! Utashindwa kujiajiri kweli?
Miaka mitano mtu anakuwa bado hajaiva kiutumishi hivyo taasisi zitayumba
 
Ni kweli mkuu kazi nyingi zina value experience ya mtu,kwa kampuni the cost ya kusubiri new graduates wapate uzoefu wa kazi sio sawa na ku retain employees ambao wana uzoefu.

Plus hii HAITAPUNGUZA TATIZO LA AJIRA since kila mwaka kuna wahitimu wengi wanashushwa mtaani, jibu ni kutafuta njia za kuongeza ajira na sio njia za kutafuta kugawana hicho kidogo kilichopo
Itapunguza sana tatizo la ajira kila mwaka kunaweza kuwa na watu wapya zaidi ya laki watakoukuwa wanaingia kwenye mfumo wa ajira wa serikali huku wengine wengi wanaotoka serikalini wakiwa wanaingia kwenye mfumo wa wa sekta binafsi kupitia mafao yao kama mitaji.
 
Mkuu Marekani baadhi ya ajira ni kweli ni za mikataba lakini si nyingi sana lakini mishahara yake ni mikubwa sana lakini wengi hurenew hiyo mikataba pale pale sun hutafuta mkataba mwingine sehemu nyingine lakini kazi kama hizo ni chache sana.

Hiyo training waliyoipata na uzoefu kazini wataenda kuutumia kwenye sekta binafsi, hicho ndicho kinachofanyika Marekani ndio maana unaona watu wengi sana kwenye siasa na sekta binafsi ya Marekani ni wanajeshi wastaafu ila bado ni vijana.
 
Back
Top Bottom