tena wakilipwa mishahara minono
Kuwalipa mishahara minono inaweza isiwe suluhisho kwa sababu tatizo sio ajira chache,tatizo ni kuwa serikali pemgine bajeti ya kuajiri watu wengine haitoshi.
Mfano una watu 10 unawalipa laki kila mtu manake kila mwezi serikali itatoa milioni moja kulipa mishahara,wakati huo kuna watu mtaani hawana ajira pengine pesa haitoshi serikalini.
Sasa ukija wewe ukasema hawa watu 10 wafanye kazi mwezi kisha wapishwe wengine kumi,lakini ukataka hawa 10 walipwe laki mbili kila mtu,hii maana yake kwa mwezi serikali itatoa 2M kulipa mishahara yaani gharama itakuwa kubwa kuliko mwanzo.
Sasa kama ghharama ni kubwa kuliko mwanzo na pale mwanzo serikali iloshindwa kuajiri kwa sababu ya bajeti haitoshi hapo itakuwa hakuna tulishoishauri serikali zaidi ya kuiongezea gharama tu.
Kwa sababu tunaasuume kwamba serikali haiajiri kwa sababu ya pesa ya kuwalipa waajiriwa wapya hakuna,hivyo kuongeza mishahara kwa watu wa idadi ile ile huku wakibadilishana hao gharama ambayo serikali ikiikimbia ndio itakuwa mara mbili.
Ingekuwa bora kwa upande wangu useme kwamba serikali iajiri kwa mkataba kwa mishahara ile ile,au ipunguze mishahara kama mtu anapokea laki tatu apewe laki na nusu ili aajiriwe mwingine,SINA MAANA KWWMBA HAYA NDIO MAAMUZI BORA YA KUTATUA CHANGAMOTO YA AJIRA,ILA TU NIMESHAURI KWA MUJIBU WA UZI WAKO.